Mtego wa Noti
JF-Expert Member
- Nov 27, 2010
- 2,591
- 1,616
Hapo zamani mawasiliano ya Internet yalikuwa yanapita kwenye waya za simu na satellite, ndani ya nchi na africa. yalikuwa
Lakini kutoka Africa na kwenda Europe na Mabara mengine ilkuwa ni kwa njia ya Satellite pekee, sasa huu mkonga umeunganisha africa na Continent nyingine kwa njia ya huu mkonga
Sasa ni kwamba ni nini tofauti ya huu mkonga na zile njia za simu za zamani ? Huu mkonga ni Fibre Optic yaani signal inakuwa ni mwanga, kwa hiyo hii ina kasi zaidi ni kama badala ya kutumia barabara za uchochoro wa magari kupita sasa wamejenga Highway
Kwa hiyo mawasiliano yataendelea kupita kwa njia za satellite kama zamani pia na kwenye huu mkonga...,
Kwa mfano wa magari mkonga ni kama Highway kubwa imejengwa ambayo itafanya magari mengi yapite na kwa kasi.., pia tuseme zamani kwenda ulaya kulikuwa kuna usafiri wa meli peke yake lakini sasa kutakuwa na usafiri wa ndege.
Kwahio huu Mkonga ni kama barabara kubwa zinasambazwa nchi nzima ili magari yapite kwa urahisi na kwa kasi
Unajua internet ni (web) kama ile nyumba ya buibui au barabaraasante sana Voice OfReason, kwa hiyo hizo optic fibres zitaunganishwa kwenye hii minara au zitakuwa zinachukua signals zikwa ardhini hivohivo? au kutakuwa na station maalum ambayo hizo fibres zina chukua na kurusha signals?
Thanks for you kindness in elaborating this to me!
Unajua internet ni (web) kama ile nyumba ya buibui au barabara
Kwahiyo kutoka kwangu signal inaweza ikapita kwenye mkonga then satellite then mkonga then satellite then ndio inafika kwako.., inategemea na traffic jams (mfano wa magari kwenye barabara, Kufika Pugu kuna njia zaidi ya moja) kwahiyo hizi zote zitakuwa interconnected kama barabara zilivyo connected zote.., uzuri kwa sasa badala ya signal kutoka marekani kuja africa kutumia satellite peke yake, sasa kutakuwa na huu mkonga
Hata hiyo modem yako ya Zain/Zantel/Tigo..., signal inaweza ikatoka kwako kwa njia ya satellite mpaka huko kwa hao Zain/Zantel/Tigo (Gateway) ambapo hapo kutakuwa kuna barabara nyingi (Mikonga na Satellite) kupeleka signal yako inapokwenda.
Pia kumbuka hata ukituma Picha ili ifike kwangu hiyo picha inavunjwa vunjwa kwenye pcs ndogo ndogo alafu hizo pcs (pkts) zinatumwa kwa njia tofauti alafu zikifika kwangu browser yangu inazikusanya zote na kuziunganisha ili nipate full picha.., kwahiyo huenda pua ya picha ilipitia njia ya mkonga then satellite wakati sikio lilipita kwenye satellite peke yake.