Jerlamarel
JF-Expert Member
- Sep 14, 2021
- 843
- 2,525
Preamble:
=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×=×
Fikiria una nyumba 1000, zote zina huduma ya umeme na fiber. Zote zina matumizi ya kawaida ya umeme na fiber.
Kwa kawaida gharama ya umeme iko chini kushinda fiber. Nyumba moja inaweza kutumia 20,000/= kwa mwezi kwenye umeme. Kwenye fiber kifurushi cha 50,000/= unlimited kwa mwezi kiko affordable sana kwa kila familia hizi zenye maisha ya kawaida.
Hapo ukipiga hesabu obvious fiber itaingiza mapato makubwa kushinda umeme.
"Sasa hivi mapato mengi ya simu sio kwenye voice call [sauti] ni kwenye data [intaneti]."
Naibu Spika wa Bunge, Mussa Zungu juu ya namna Serikali inavyoweza kuongeza mapato kupitia intaneti.

Tulipolalamika kwamba gharama za internet ziko juu sana, waziri anayehusika pamoja na wanasiasa kadhaa walisimama wakasema Tanzania gharama za internet ziko chini sana ukilinganisha na nchi zingine.
Lakini jambo ambalo liko wazi ni kwamba ni ukweli usiopingika kwamba gharama ziko juu, sababu kubwa ni kwamba tunauziwa internet ya kupimiwa kwenye kibubu.
Na ni ukweli usiopingika kwamba wanaokwamisha mkongo wa taifa usianze kufanya kazi kwa kusupply fiber majumbani ni haya haya makampuni ya simu ambayo yanahonga baadhi ya watendaji ili mchakato huu usifanikiwe ili wao waendelee kutukamua wananchi kupitia hivyo vifurushi vya kupima kwenye kibubu.
Leo Naibu Spika mwenyewe amekubali kwamba serikali haipati kile inachostahili sababu ya hawa internet providers ambao wengi ni kutoka nje ya nchi, kuchukua almost mapato yote sababu wao ndiyo service provider.
Kwa sasa huduma ya internet ni moja ya sehemu ya basic need, huwezi kuishi bila internet kwa sasa kama unahitaji kuwa updated, na huduma karibu zote huko maofisini na majumbani zinahitaji internet. Dunia iko digitalized now, bila internet ya uhakika maisha hayataenda.
Serikali inatakiwa ijue kwa sasa internet ni kama umeme. Ina demand kubwa sana kama umeme. Sasa kitu chenye demand kubwa ina maana kinahitaji supply ya maana pia.
Mimi kwa mwezi mfano natumia elfu 70 kwenye data, ukiniletea fiber kwa elfu 50 ni wazi utakuwa umenisaidia na mapato ya serikali yataongezeka mara dufu sababu hakuna ambaye atanunu hizi internet za kupimiana kwenye vibubu tena.
JE, NI NANI ATAMFUNGA PAKA KENGELE?