Mkono bado unauma baada ya kuanguka mpirani

Penguin-1

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2012
Posts
406
Reaction score
65
Habari JF Dr,

Shida yangu ndogo ila sasa naona imeanza kunikwaza na ninakuwa na wasiwasi,
Nikiwa nacheza mpira nilianguka na kujizuia na mkono wa kushoto ,hivyo ukashituka(sina hakika ,ila nikapata maumivu) maeneo ya kwenye joint begani.

Nikajuwa nitapona tu ,tunaanguka mara nyingi tu ,zikapita wiki 2 ,mpaka mwezi bado nasikia maumizu kwa mbali ,au mkono ukiwa kwenye angles flan flan. Nikaenda hospitali nikachukua Xray(tena mdada wa xray aliniangalia akasema hujaumia wewe ,kisa nilikuwa nimebeba bag)

Xray ikasomwa ,report inasema sina fracture ,..kimsingi nipo pouwa.

Ila ukweli mimi bado mkono unaniuma ,tena nahisi maumizi yanaongezeka slowly with time ,mara nyingine siwezi vuta ,beba vitu kwa mkono huu..

Nini inaweza kuwa shida?,
Nipo najiandaa kurudi hospitali kesho.
 
Ni ngumu kupata jibu sahihi kupitia hapa maana inahitaji kuhojiwa vizuri mazingira ya ajari na kufanyiwa uchunguzi (clinical examination ) na pia uchunguzi wa kutumia vifaa....

Ila inakupasa kufahamu kuwa unapopata trauma sio wakati wote mifupa huumia...unaweza kuumiza pia misuli, ligaments, tendons nk...

Na pia Xray hainyoshi mara zote fracture za mifupa hasa zikiwa ndogo au utaalamu wa fundi radiologia ukiwa mdogo....kuna fracture zinaonekana kwenye scanner au vifaa vingine....

Nakushauri rudi hospitali mapema iwezekanavyo na jitahidi kuonana na specialist wa traumatology nadhani wapo MOI kwa bongo (sina uhakika)...

Mwisho ugua pole na usisite kuleta feedback ili na sisi tujifunze...
 
Back
Top Bottom