Uchaguzi 2020 "Mkono mtupu haulambwi" Mbowe ajitenga na kampeni za Lissu

Uchaguzi 2020 "Mkono mtupu haulambwi" Mbowe ajitenga na kampeni za Lissu

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwenyekiti wa CHADEMA ndugu Freeman Mbowe ajitenga na kampeni za CHADEMA kuusaka Urais. Ikumbukwe mwaka 2015 Mbowe alishiriki kampeni za Lowassa kikamilifu hadi kufikia kupoteza fahamu katika kufurahia "nyomi" na michango ya kampeni toka kwa marafiki wa EL.

Inasemekana sababu nyingine ni hali tete ya Ubunge wa wilaya ya Hai kwani Mbowe yupo taabani kutokana na kukubalika kwa Mgombea Ubunge kupitia CCM ndugu Saashisha aka Mbunge anayesubmiri kuapishwa.
 
Mwaka huu CHADEMA itawafanye mvae boxer vicwani!!
Huyu jamaa asipoandika uzi wa Lissu ndani ya dakika tano anaugua. Sijui anafikiria saangapi maendeleo yake na familia yake.
Lissu akiongea anaandika uzi, akikaa kimya anaandika uzi, Lissu akisema CCM wako hivi anaandika uzi, akisema CHADEMA watafanya hili anaandika uzi, Mbowe akiongea anaandika uzi, asipoongea anachanganyikiwa. Ni wa kupuuza tu.
 
2015 Lowasa isingewezekana kuachwa peke yake. Pia ilikuwa ni liability yake kumnadi Lowasa baada ya kubadili gia angani. Leo kiko chuma cha pua, Lissu. Mwamba kapata fursa ya kufanya kampeni kwibgine pamoja na jimboni kwake. Subirieni maumivu
 
Safari hii mgombea Tundu Lissu ni ngangari hivyo mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu mkuu John Mnyika wamejikita katika kuratibu kwa ukaribu shughuli za uchaguzi mkuu wa wabunge na madiwani ikiwemo mtego wa CCM Mpya waliouweka kuengua wabunge na madiwani wakidhani mgombea Urais wa CHADEMA ataathirika mfano kwa Freeman kuvunjwa mguu n.k lakini wamekuta timu nzima ipo imara wale wa field yaani wagombea na wale wanaohitajita kuratibu shughuli za chama ofisini pia wanajimudu kiutendaji.
 
Ndugu zangu,

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mwenyekiti wa Chadema ndugu Freeman Mbowe ajitenga na kampeni za Chadema kuusaka Urais. Ikumbukwe mwaka 2015 Mbowe alishiriki kampeni za Lowassa kikamilifu hadi kufikia kupoteza fahamu katika kufurahia "nyomi" na michango ya kampeni toka kwa marafiki wa EL.

Inasemekana sababu nyingine ni hali tete ya ubunge wa wilaya ya Hai kwani kutoka kwa Mbunge anayesubiri kuapishwa ndiye.
Wakuvuavua;
Malizia basi Uzi wako maana hueleweki ulitaka kuandika nini?
Tunakusubiri umalizie tuchangie.
 
Hahaha hivi Mzee Mangula naye hajalipwa au ndio sumu bado inamsumbua mwilini, haonekani jukwaani au naye kasusa ?!
 
TL anajiweza jukwaani anamudu kusema kujibu chochote, acheni Mwenyekiti apunzike amesemwa Sana kuua upinzani, kochà haingii kucheza anaangalia utekelezwaji wa maelekezo,,
 
Mwambieni kuwa makaburu wa Afrika kusini waliijenga S.A kama ULAYA, lakini haikuwafanya "WASAUZI" wawapende makaburu kwa UKATILI wao.

Mnamo mwaka 1994 makaburu waliondolewa madarakani, kwahiyo TUDARAJA 'twake' tusimpe uhalali wa kulazimisha KUTAWALA watu kwa MKONO WA CHUMA.

Hujawai shuhudia utawala wa mkono wa chuma, afu unaleta dharau, eti tudaraja twake, wakati ni madaraja ya wa Tanzania.
Mtu kaamua kwa mamlaka alonayo hizo hela zikasaidie maskini, afu unasema tudaraja twake, as if ni daraja amejenga, aise.
 
Back
Top Bottom