Haya
maneno hua
yananitatiza sana, huenda ni sawa kusema mkono wa KULIA (Chakula)
lakini napata shida kusema mguu wa KULIA (kwa asili ya yalikotoka)
wadau tusaidiane hapa mana najua SIKO peke yangu
Kuna upande wa kulia,ktk khs viungo vya mwili upande wa kulia
unamaanishwa ni huu ambao moyo haupo,kwamba upande wa kushoto kfuan kuna
moyo,huu mwngne ndio wa kulia..MAANA NI HIYO MKUU
usije ukasema tena eti huu ni mkono au mguu wa kulia,kwani sio wote wanatumia mkono huo kwa kulia chakula..
Kuondoa utata ulionao, tumia lugha hii;
Mkono wa kuume au mguu wa kuume
Ila yakupasa utambue kuwa, neno kulia linaweza kutumika kama "Kitenzi" ambapo kitenzi mama hapo ni LIA, hali kadhalika hutumika kama "Kivumishi".
Sasa katika muundo wa sentensi za Kiswahili ni rahisi kung'amua matumizi ya neno husika kwa kuangalia sehemu lilipotumika na mantiki iliyobebwa.
umenigusa sana Y-N
Haya maneno hua yananitatiza sana, huenda ni sawa kusema mkono wa KULIA (Chakula) lakini napata shida kusema mguu wa KULIA (kwa asili ya yalikotoka)
wadau tusaidiane hapa mana najua SIKO peke yangu
Neno la kiswahili moja laweza kuwa na maana nyingi kulingana na wapi linatumika. mfano mbuzi, kaa na panda.
Hivyo neno kulia yaweza kuwa na maana tofauti kulingana na matumizi yake.
Mfano: Nitakulia chakula. - kula chakula kwa niaba
Nitaenda kulia msibani - Kutoa machozi
Amevaa shanga mguu wa kulia - amevaa shanga mguu wa kuume.
wamogori sijakusoma kabisa
Nilichokuwa nafafanua ni kuwa neno KULIA halina maana moja katika kiswahili, lina maana nyingi isipokuwa itategemea na namna gani limetumika katika sentensi.
mfano neno KULIA linaweza kuwa na maana zifuatazo.
a. Kitendo cha kutoa machozi
b. Upande wa kuume.
c. Kula kitu kwa niaba ya mtu mwingine.
d. Kitumizi cha kula mfano mkono, kijiko n.k
Hivyo kutoka neno KULIA na maana zako hapo juu unaweza kuwa na sentesi tatu tofauti zenye neno KULIA lakini zikawa na maana tofauti.
mfano:
a. Ukifika kwa mama yake anza KULIA. (Ikiwa na maana toa machozi)
b. Ukifika njia panda pinda KULIA. (Ikiwa na maana mkono wa kuume)
c Harambee ame-KULIA chakula. (ikiwa na maana amekula kwa niaba yako)
d. Hii sahani ni ya KULIA ugali. (Ikiwa na maana ya kitumizi)
Hivyo kusema mguu wa kulia ni sahihi kwani humaanisha mguu wa kuume na sio kitumizi cha kula.
hapa ndipo penye swali kwanini KUUME na si KUUKE?