Mkono wa Kulia na Mguu wa Kulia

Mkono wa Kulia na Mguu wa Kulia

Amavubi

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2010
Posts
30,156
Reaction score
13,258
Haya maneno hua yananitatiza sana, huenda ni sawa kusema mkono wa KULIA (Chakula) lakini napata shida kusema mguu wa KULIA (kwa asili ya yalikotoka)

wadau tusaidiane hapa mana najua SIKO peke yangu
 
Haya
maneno hua
yananitatiza sana, huenda ni sawa kusema mkono wa KULIA (Chakula)
lakini napata shida kusema mguu wa KULIA (kwa asili ya yalikotoka)

wadau tusaidiane hapa mana najua SIKO peke yangu

Kuna upande wa kulia,ktk khs viungo vya mwili upande wa kulia
unamaanishwa ni huu ambao moyo haupo,kwamba upande wa kushoto kfuan kuna
moyo,huu mwngne ndio wa kulia..MAANA NI HIYO MKUU
usije ukasema tena eti huu ni mkono au mguu wa kulia,kwani sio wote wanatumia mkono huo kwa kulia chakula..
 
Kuondoa utata ulionao, tumia lugha hii;
Mkono wa kuume au mguu wa kuume

Ila yakupasa utambue kuwa, neno kulia linaweza kutumika kama "Kitenzi" ambapo kitenzi mama hapo ni LIA, hali kadhalika hutumika kama "Kivumishi".
Sasa katika muundo wa sentensi za Kiswahili ni rahisi kung'amua matumizi ya neno husika kwa kuangalia sehemu lilipotumika na mantiki iliyobebwa.
 
umenigusa sana Y-N

Wanaharakati wa Kifeminist watakuja juu hapa
Kuondoa utata ulionao, tumia lugha hii;
Mkono wa kuume au mguu wa kuume

Ila yakupasa utambue kuwa, neno kulia linaweza kutumika kama "Kitenzi" ambapo kitenzi mama hapo ni LIA, hali kadhalika hutumika kama "Kivumishi".
Sasa katika muundo wa sentensi za Kiswahili ni rahisi kung'amua matumizi ya neno husika kwa kuangalia sehemu lilipotumika na mantiki iliyobebwa.
 
nimechunguza wenzetu wanaita Roght hand na left hand nayo pia sijui mantiki yake
 
Haya maneno hua yananitatiza sana, huenda ni sawa kusema mkono wa KULIA (Chakula) lakini napata shida kusema mguu wa KULIA (kwa asili ya yalikotoka)

wadau tusaidiane hapa mana najua SIKO peke yangu

Neno la kiswahili moja laweza kuwa na maana nyingi kulingana na wapi linatumika. mfano mbuzi, kaa na panda.
Hivyo neno kulia yaweza kuwa na maana tofauti kulingana na matumizi yake.
Mfano: Nitakulia chakula. - kula chakula kwa niaba
Nitaenda kulia msibani - Kutoa machozi
Amevaa shanga mguu wa kulia - amevaa shanga mguu wa kuume.
 
wamogori sijakusoma kabisa

Nilichokuwa nafafanua ni kuwa neno KULIA halina maana moja katika kiswahili, lina maana nyingi isipokuwa itategemea na namna gani limetumika katika sentensi.
mfano neno KULIA linaweza kuwa na maana zifuatazo.
a. Kitendo cha kutoa machozi
b. Upande wa kuume.
c. Kula kitu kwa niaba ya mtu mwingine.
d. Kitumizi cha kula mfano mkono, kijiko n.k

Hivyo kutoka neno KULIA na maana zako hapo juu unaweza kuwa na sentesi tatu tofauti zenye neno KULIA lakini zikawa na maana tofauti.
mfano:
a. Ukifika kwa mama yake anza KULIA. (Ikiwa na maana toa machozi)
b. Ukifika njia panda pinda KULIA. (Ikiwa na maana mkono wa kuume)
c Harambee ame-KULIA chakula. (ikiwa na maana amekula kwa niaba yako)
d. Hii sahani ni ya KULIA ugali. (Ikiwa na maana ya kitumizi)

Hivyo kusema mguu wa kulia ni sahihi kwani humaanisha mguu wa kuume na sio kitumizi cha kula.
 
hapa ndipo penye swali kwanini KUUME na si KUUKE?

Ukirejea kwenye fasili ya lugha utakuta ni lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kusemwa na watu kwa aliji ya mawasiliano. ukifafanua neno sauti za nasibu maana yake ni kwamba sauti hizo hazina uhusiano na kitu kinachowakilishwa pia ni sauti zilizozuka kwa bahati bila kikao chochote cha watu. hivyo neno kikombe halina uhusiano na kifaa kinachowakilishwa, hivyo kama lingekuwa na uhusiano basi dunia nzima kifaa hicho kingeitwa kikombe. hivyo basi hata neno kuume (kulia) ni sauti za nasibu ambazo zimezuka tu kwa ajili ya kuwakilisha upande husika, kuanza kutaka na kushoto kuitwe kikeni ni nje ya mfumo wa lugha, yaani ni sawa na kuanza kuhoji kwa nini sahani isiitwe pera?
 
Back
Top Bottom