Mkono wa kushoto

Mkono wa kushoto

Mokoyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2010
Posts
15,145
Reaction score
5,566
Nini chanzo cha kuumwa mkono wa kushoto? hasa kwenye eneo la bega na mkono mzima kukosa raha? Je tiba yake ni nini?
 
nini chanzo cha kuumwa mkono wa kushoto? Hasa kwenye eneo la bega na mkono mzima kukosa raha? Je tiba yake ni nini?
inawezekana uliulalia usiku,mwone daktari.
 
your stree level could be high, punguza mawazo japo shida kwa mbongo ni kama CCM na ufisadi.
 
your stree level could be high, punguza mawazo japo shida kwa mbongo ni kama CCM na ufisadi.
kuna mtu aliniambia jambo kama hili tena lakini mwenyewe sijioni kuwa na mawazo kiasi hicho. Asante
 
UMEROGWA NDUGU YANGU.
NGOJA NlIKUCHEKIE HAPA KWENYE TV YANGU YA KIENYEJI KISHA NTAKUPA MKANDA KAMILI NA TIBA YA MATATIZO YAKO.
 
Pole sana. Jaribu kuangalia ni wakati na hali gani unakua nayo wakati unauma. Mfano mimi nikiwa stressed naumwa sana shingo na mabega. Otherwise jaribu kuangalia matumizi ya mkono wako pia (try to google ergonomics)
 
UMEROGWA NDUGU YANGU.
NGOJA NlIKUCHEKIE HAPA KWENYE TV YANGU YA KIENYEJI KISHA NTAKUPA MKANDA KAMILI NA TIBA YA MATATIZO YAKO.
Wewe ni agent wa sheikh yahya nini? Extra curricular activities....
 
Pole sana. Jaribu kuangalia ni wakati na hali gani unakua nayo wakati unauma. Mfano mimi nikiwa stressed naumwa sana shingo na mabega. Otherwise jaribu kuangalia matumizi ya mkono wako pia (try to google ergonomics)
Asante sana Mkuu, nimepata makala nzuri baada ya kugoogle ngoja nisome kama itanisaidia
 
jaribu pia kuufanyisha mazoesi mtu wangu yaweza kuwa may be wakati unadrive huwa uko idle sana na unakuwa wakati mwingi unadrive..nilikuwa na hilo tatizo pia wakati namwendesha mheshimiwa mmoja for long time..
 
UMEROGWA NDUGU YANGU.
NGOJA NlIKUCHEKIE HAPA KWENYE TV YANGU YA KIENYEJI KISHA NTAKUPA MKANDA KAMILI NA TIBA YA MATATIZO YAKO.

Umejuaje kama karogwa wakati hata hiyo TV yako hujaiangalia...mpe ushauri wa kisayansi hizi TV za kienyeji hatutafika
 
Kamwone cardiologist, maumivu hayo yanaweza kuwa na uhusiano na matatizo ya moyo.
 
Kamwone cardiologist, maumivu hayo yanaweza kuwa na uhusiano na matatizo ya moyo.
Asante Ama ila umenitisha sana Ndugu...Maradhi ya moyo nayaogopa kama nini. MUNGU nisaidie na kuniepusha na janga hili. Amen
 
Asante Ama ila umenitisha sana Ndugu...Maradhi ya moyo nayaogopa kama nini. MUNGU nisaidie na kuniepusha na janga hili. Amen

Ndugu usiogope, huwezi kuchagua ugonjwa....ila ni kweli kunakuwa na uhusiano wa kuuma mkono wa kushoto na Moyo. La msingi na ukweli nenda Hosipitali naamini watasaidia kiasi fulani....
 
Ndugu usiogope, huwezi kuchagua ugonjwa....ila ni kweli kunakuwa na uhusiano wa kuuma mkono wa kushoto na Moyo. La msingi na ukweli nenda Hosipitali naamini watasaidia kiasi fulani....
Ni kweli MwM
Ila nimekwenda hospitali mbali mbali nimepima mpaka kipimo cha ECHO, fullblood picture lakini hakuna kilichogundulika. Nisaidieni nikapime nini hasa?
 
Labda una pressure au pafu limejaa maji ndugu yangu.....nenda hospital
 
Back
Top Bottom