Mkopo Bank of Afrika (BOA)

Mkopo Bank of Afrika (BOA)

msomso

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2014
Posts
464
Reaction score
152
Mimi ni mtumishi serikalini nimeomba mkopo katika tawi moja la boa hapa Tanzania Kanda ya Ziwa sasa nimetimiza mwezi mmoja kila nikienda loan officer dada mmoja ananijibu approve ya mkopo wako bado.

Jamani hivi approve inakaa zaidi ya mwezi nateseka sana na nashida kubwa.Naomba wanajamvi mnisaidie kama mnayo idea na benki ya boa mnisaidie.
 
loan officers kawaida yao hua ni njaa sana, hapo anataka umlainishe mikono.........
 
Ndugu wanajamvi, Mimi ni Mtumishi serikalini, nimeomba mkopo Bank of Africa (BOA) katika tawi moja Kanda ya Ziwa. Nina mwezi na wiki sasa kila nikienda wanadai offer letter inayotoka Makao Makuu Dar es salaam bado.

Yaani wakuu, Mimi aiseee nashindwa kuwaelewa hawa BOA mbona hivyo?! Mimi sijawahi ona tangu nizaliwe. Naombeni wataalamu mnijuze hawa BOA wanahitaji nini, mbona hivyooo!?
 
Ndugu wanajamvi nimeumia sana Leo kunajamaa mmoja ni MWALIMU aliomba mkopo benki ya boa tawi moja kanda ya ziwa tangu Tarehe 13.01.2015 kila akienda anajibiwa offer letter inayotoka makao makuu bado.

Jana ijumaa anaenda uliza pale benk anajibiwa kuwa kaka naona kama ntakukwamisha mimi kila nikiwapigia cm makao makuu wabadai nisubiri afisa mikopo ndo anamuambia hivo aka conclude kuwa kaka angu naona kama ntakukwamisha find another alternative.

Imeniuma sana kupotezewa muda.

Hakika Benk Of Afrika (BOA) Kweli mnaboa.
 
msomso,

Hata lugha yetu ya taifa ni ngumu kiasi hiki? Kumbe ndio maana umekosa mkopo inawezekana barua uliandika kama ulivyoandika hapa.
 
Last edited by a moderator:
Aiseeee wewe umekalili kila mkopo mpaka uandike barua acha umburula
 
Kwanini asiende kukopa NMB au huko amekopa tena?
 
Mbona CRDB na NMB wanatoa mikopo tena kwa riba nafuu.
 
Ndugu zangu NMB alishakopa na CRDB walimuambia kuwa Kwa sasa wamesitisha kuwakopesha walimu ndo akaenda BENk of Afrikaans (boa) ndo wakawa kila siku akienda wanamuambia offer letter.

Bado ambayo inatoka makao makuu hivi hawa boa hawajui siku hizi kuna big result now Kwa nini wanamuweka MWALIMU wetu mwezi na wiki mbili halafu wanakuja muambia are find another alternative why wajameni inaniuma sana kupotezewa muda.
 
CRDB branch gan kaenda, maana ninao waalimu kibao wamepewa mikopo CRDB Karibun kabisa.

Hebu weka bayana hapa wap alienda?
 
Mbona unajifanya anaeomba mkopo sio wewe wakati ni wewe. Kwani ukisema nimekopa kunatatizo gani?
 
Hivi hela wanazokatwa walimu miaka nenda rudi hazitoshi mtaji kuanzisha Benk yao ambayo ingekuwa inawakopesha kwa masharti rahisi?
 
HAWA chama cha walimu (CWT) kiukweli wanatakiwa waanzishe benki waache viongozi kula hizo hela tu wanazokatwa walimu wetu na mishahara yao midogo kiukweli hamna mtu namuonea huruma kama MWL mshahara ni Mdogo sana ,

hana posho kifupi hana source nyingine zaidi ya kuusubiri mshahara wake ambao ni kiduchu
 
Kwanza amshukuru Mungu kwa kumuepusha na Makato ya mshahara wake. Hivi kwa mshahara wa ualimu ...ukipokea cash bila makato ya mkopo...unakuta mwalimu akifika tarehe 10 tu hata senti tano mfukoni hana, sasa unapolaumu unacheleweshewa mkopo...si majanga hayo??

Walimu lazima mjitambue....ni vema ukawa mwalimu pia ukawa mjasiria mali ili usiishi kwa kutegemea huo mshahara. Siku hizi fursa ni nyingi. Hata leo upate 10 Milioni mwalimu...then after one week...huna kitu.

Naomba msinirushie mawe walimu tafadhali..lakini najaribu tu kutoa tahadhari ili tuangalie njia mbadala ya kujikwamua badala ya kutegemea merely your monthly salary!

Mwalimu ndio mwanga....hata rais , waziri, daktari, Nurse, and others wamefundishwa na mwalimu. So be proud to be a teacher!
 
Back
Top Bottom