Mkopo kukua zaidi ya mtaji

Mkopo kukua zaidi ya mtaji

card78

Member
Joined
Sep 22, 2018
Posts
49
Reaction score
48
Kumekuwa na ongezeko la uchukuaji wa mkopo kutoka taasisi mbalimbali lakini bado kusimama kiuchumi bila utegemezi wa mkopo umeshindikana.

Matarajio ya wengi katika mkopo ni kurudisha mkopo kwa wakati sahihi na kuongeza kiwango cha mkopo baada ya muda nadhani hii imekuwa ni kasumba ya wengi katika zana nzima ya mkopo.

Najiuliza kwa nn wengi waliokwisha chukua mkopo hawajasimama katika mtaji wao binafsi baada faida ya kwanza katika mkopo wa awali ila unakuta kiwango cha mkopo ndo kina panda na hatimaye mtu anaweza filisiwa hata baada ya miaka 15 kisa ya mkopo mmoja kati ya 5 aliokwisha kukopa hapo awali.

Ushauri wangu ni vema kuhakikisha baada ya mkopo unabaki na mtaji wako wa kuendesha biashara na sio kupanda kimkopo .
 
Somo zuri ila ukumbuke pesa haitoshi

Wengi wanavyo anza kuchukua mikopo huwa na mawazo kama yako ila baada ya kuchukua na kulipa hujikuta wakibaki katika kutafuta mkopo mkubwa zaidi

Sababu ni za wengi

Baada ya kuwa na pesa hujiingiza katika uwekezaji wa miradi mingi ambayo huwa haiwezi kurudisha hela kwa haraka kwa mfano watu hujikuta wanajenga nyumba za kupangisha ambazo haziwezi kukupa matokeo ya haraka na ukawa na mtaji tena

Wengi hujikuta wako katika kutafuta sifa kwa kuwa na biashara kubwa sasa ukimwambia abaki na mtaji wake halisi baada ya kulipa mkopo atajikuta amerudi nyuma km za kutosha hivyo itamlazimu kutafuta mkopo ili kubaki juu kibiashara

Lakin pia wapo wanao uza dhamana kwa lengo la kuhamisha makazi maana najua akiuza nyumba haiwezi kufika uhitaji wa pesa anayo taka hivyo anaingia benk na kuchukua mkopo mkubwa na kutelekeza dhamana wewe unao kafilisika kumbe kauza kwa njia nyingne

Pia wapo ambao kazi yao ni kuhamisha madeni hawa hujikuta hawapati hata faida zaidi hufaidisha benk na hawa ndio hufirisika kabisa

Kwa Leo nifikie hapa
 
Ni kweli kaka
 
Hivi kanuni za marejesho huwa zipoje boss ni kwa mwaka au mwezi?
 
Back
Top Bottom