Mkopo... Mkopo...mkopo wa pesa!

CHE GUEVARA-II

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2010
Posts
571
Reaction score
156
Habari zenu wadau? Natafuta mkopo wa 25,000,000 Tshs. Nina nyumba yangu iliyokwishanigharimu si chini ya 45,000,000 Tshs. Iko PUGU VIWEGE. Imo ndani ya kiwanja chenye ukubwa wa 30X30m. Ina vyumba 3, kimoja masterbedroom. Imeshaezekwa bati. Imeshafanyiwa wiring na plumbing. Ina ukuta wa tofali na gate + grills zenye decorations Nguzo za umeme zipo umbali ambao hauzidi mita 100. Kiwanja na nyumba ni mali yangu halali (hati ni za serikali za mitaa) eneo halijapimwa lakini kuna watu wengi sana wamejenga majengo hata yenye thamani ya 100,000,000Tshs. Kuna dharura imejitokeza nahitaji kuitatua. Atakayenipatia hiyo pesa tutaandikishanahata kwa mwanasheria kwa sharti kuwa nitakuwa nampatia 750,000 Tshs kila mwezi hadi hapo nitakapomrudishia pesa yake hiyo 25,000,000 Tshs kwa sharti kwamba haitazidi miezi 12 (ikiisha miezi 12 hiyo nyumba iuzwe achukue pesa yake, au ikitokea hali yoyote ile kabla miezi 12 haijaisha nyumba iuzwe na kufidia hizo 750,000 Tshs ambazo hazijalipwa katika miezi husika). In fact haiwezi kuzidi miezi 6. Lkn pia aniruhusu niendelee kuijenga kwa sababu nataka nije niweke mpaka swimming pool na garden nzuri.
 

Attachments

  • CLOSE APPEARANCE.jpg
    79.4 KB · Views: 188
  • 25 May-2012 - 1.jpg
    1 MB · Views: 148
  • BEFORE GRILLS & GATE.jpg
    61.4 KB · Views: 144
  • UKUTA & GATE.jpg
    60.4 KB · Views: 130
  • UKUTA & GATE-3.jpg
    78.8 KB · Views: 136
Reactions: BZA
Nenda benki kama CRDB,AKIBA na Barclays,hiyo pesa kwa dhamana yako unapata!
 
Hana hati ya kiwanja benk haiwezi kutoa mkopo kwa kiwanja/collateral ambayo haimiliki kisheria,wanahitaji uhakika wa collateral i.e security atakayoweka dhamana in exchange ya hyo loan
Nenda benki kama CRDB,AKIBA na Barclays,hiyo pesa kwa dhamana yako unapata!
 
Hana hati ya kiwanja benk haiwezi kutoa mkopo kwa kiwanja/collateral ambayo haimiliki kisheria,wanahitaji uhakika wa collateral i.e security atakayoweka dhamana in exchange ya hyo loan

Uko sahihi Latoya.
Nd'o maana nikakimbilia humu JF.
Lengo la kukopa bank kwa kutumia hako kakibanda lipo lkn hadi ifikapo 2016/2017.
Next yr nitafuatilia nipate title deed pamoja na kukamilisha estimates za building cost (~75-80M) then by 2015/2016 nianze mchakato wa kukopa bank, ili by 2016/2017 nivute mkopo.

Kwa sasa naimalizia kwanza kuijenga.
Tatizo nimepata dharura kidogo..
 


kweli jamani 750,000 x 12 = 25,000,000 + riba?

hapo inaonyesha ndani ya mwaka utarejesha mill 9 tu ndani ya mwaka tena hujazungumzia riba, sa unafkir nani atakulipia kiasi kilicho baki?! kuhusu riba ambayo hujaiongelea unamaanisha unataka mkopo wenye masharti ya kiisilamu?
 
Mkuu nenda Access bank wanachukua hati y, tena mauziano yenye baraka ya serikali ya mtaa kama dhamana,pia benki hii haichelewesh kutoa mkopo
 

Umeisoma post yangu vizuri lkn?
Hiyo 9M nd'o faida ndani ya miezi 12 (yaani ktk mwezi wa 12 unajikuta una 34M cumulatively) halafu unasema mkopo wa Kiislam?
Hiyo 25M at the end nitailipa CASH kwa sababu najiamini, nikishindwa unauza nyumba (hauoni hapo nimeji-sacrifice kuweka rehani Nyumba yenye thamani ya zaidi ya 45M kwa mkopo wa 25M?
 
Mkuu nenda Access bank wanachukua hati y, tena mauziano yenye baraka ya serikali ya mtaa kama dhamana,pia benki hii haichelewesh kutoa mkopo

Asante, ngoja ni-check nao hao Access bank.
Hofu yangu ni kwamba wanaweza wasikubali hizo hati za serikali za mitaa kwamba shahidi muuzaji, majirani na viongozi wa kata (japokuwa nina waraka tuliuandikisha kwa mwanasheria pia, nikiwa na muuzaji)
 

ok nimekupata mkuu kumbe unamaanisha mkopo utaurejesha mwishoni kwa kurudisha kiasi chote kwa mkupuo mmoja! Sorr bana nilidhano hiyo 750k ndo marejesho ya mkopo kumbe badala yake hiyo ni kama riba ya mkopo!
Asante!!
 
wenye pesa changamkieni hii kitu. pesa ya bure kabisa-riba ya zaidi ya 60% kwa mwaka!!!!
 
wenye pesa changamkieni hii kitu. pesa ya bure kabisa-riba ya zaidi ya 60% kwa mwaka!!!!

SIO 60% Huyu jamaa alishapiga hesabu nzuri kabisa hiyo ni 36% tu na ukiondoa inflation ya ki-TZ itabaki 20% tu kama anakubali hiyo 60% aje nimpe hiyo pesa maanake 25 mln x 60% + 25 mln = 40 mln kwa maelezo yake 15mln /12= 1,250,000 anapaswa kulipa kila mwezi na mwisho atalipa principal 25mln
 

Hiyo 60% mimi siwezi, kwa sababu pia kumbuka HATA hiyo miezi 12 inaweza isifike. Naweza kukurudishia P (yaani 25M) hata kabla ya miezi 4. Hiyo miezi 12 ni MAXIMUM.
Mi' natoa 750,000 kila mwezi.
Aliye tayari anijulishe.

Kwa yeyote mwenye namba za simu za mkononi za mfanyakazi wa Access Bank, Akiba Commercial Bank au na zingine zingine mnazojua wanaweza kunisaidia ni-PM au weka hapa jamvini niwasiliane nao vizuri.
Thanks!
 
Kumbe Acceess Bank wanakopesha hadi uwe na biashara?
Kwa hiyo kama unataka ununue kitu au unataka uitumie kumalizia jengo au kuongeza plot hawakopeshi hata ukiwa na nyumba au nyumba na kazi (permanent employment) yenye uhakika wa kuwalipa hayo marejesho kila mwezi bado hawataki, wanataka LAZIMA uwe na biashara!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…