CHE GUEVARA-II
JF-Expert Member
- Jun 17, 2010
- 571
- 156
Habari zenu wadau? Natafuta mkopo wa 25,000,000 Tshs. Nina nyumba yangu iliyokwishanigharimu si chini ya 45,000,000 Tshs. Iko PUGU VIWEGE. Imo ndani ya kiwanja chenye ukubwa wa 30X30m. Ina vyumba 3, kimoja masterbedroom. Imeshaezekwa bati. Imeshafanyiwa wiring na plumbing. Ina ukuta wa tofali na gate + grills zenye decorations Nguzo za umeme zipo umbali ambao hauzidi mita 100. Kiwanja na nyumba ni mali yangu halali (hati ni za serikali za mitaa) eneo halijapimwa lakini kuna watu wengi sana wamejenga majengo hata yenye thamani ya 100,000,000Tshs. Kuna dharura imejitokeza nahitaji kuitatua. Atakayenipatia hiyo pesa tutaandikishanahata kwa mwanasheria kwa sharti kuwa nitakuwa nampatia 750,000 Tshs kila mwezi hadi hapo nitakapomrudishia pesa yake hiyo 25,000,000 Tshs kwa sharti kwamba haitazidi miezi 12 (ikiisha miezi 12 hiyo nyumba iuzwe achukue pesa yake, au ikitokea hali yoyote ile kabla miezi 12 haijaisha nyumba iuzwe na kufidia hizo 750,000 Tshs ambazo hazijalipwa katika miezi husika). In fact haiwezi kuzidi miezi 6. Lkn pia aniruhusu niendelee kuijenga kwa sababu nataka nije niweke mpaka swimming pool na garden nzuri.