Mkopo: Natafuta mkopo m5, nitalipa mchele Magunia 20 ya mpunga july.

Mkopo: Natafuta mkopo m5, nitalipa mchele Magunia 20 ya mpunga july.

Logo

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2011
Posts
588
Reaction score
48
Wadau,
nina mashamba ya mpunga Kyela, natafuta mkopo wa milion 5, nikivuna nitamlipa mchele magunia 20 au tunaweza kuelewana zaidi.

Nitafurahi sana ukiniPM.
 
Elezea vizuri mkuu.
Huo mpunga unalima kilimo cha umwagiliaji au ndo mambo ya kusubiri mvua?

Dhamana?

Nadhani maelezo hayajajitosheleza.
 
Wadau,
nina mashamba ya mpunga Kyela, natafuta mkopo wa milion 5, nikiivisha mchele wangu nitamlipa mpunga magunia 20 au tunaweza kuelewana zaidi.

Nitafurahi sana ukiniPM.

Mkuu, Gunia 20 za mpunga kwa 5M?!!!!...bado.
 
Mkuu, Gunia 20 za mpunga kwa 5M?!!!!...bado.
Ukichukua hiyo 5M ukagawanya kwa 20 (idadi ya magunia atakayolipa) unapata 250,000. Maana yake ni kuwa jamaa atachukua pesa yako 5M atakaa nayo kwa takribani miezi 4-5. Halafu mwisho wa siku atakuuzia gunia moja la mpunga kwa sh. 250,000/-.

Bei halali ya gunia la mpunga wakati wa mavuno haizidi 60,000/-. Hata bei ipande vipi gunia moja la mchele (sio mpunga) halitazidi 120,000 - 130,000.

So jamaa aendelee tu kutafuta atapata mtu wa kumkopesha hizo 5M!
 
Wadau,
nina mashamba ya mpunga Kyela, natafuta mkopo wa milion 5, nikiivisha mchele wangu nitamlipa mpunga magunia 20 au tunaweza kuelewana zaidi.

Nitafurahi sana ukiniPM.
acha utapeli sisi tunakopesha sh 40000 kwa gunia la mpunga debe 10 kulipa july!5m kwa just 20?ungesema 200 sawa
 
Ukichukua hiyo 5M ukagawanya kwa 20 (idadi ya magunia atakayolipa) unapata 250,000. Maana yake ni kuwa jamaa atachukua pesa yako 5M atakaa nayo kwa takribani miezi 4-5. Halafu mwisho wa siku atakuuzia gunia moja la mpunga kwa sh. 250,000/-.

Bei halali ya gunia la mpunga wakati wa mavuno haizidi 60,000/-. Hata bei ipande vipi gunia moja la mchele (sio mpunga) halitazidi 120,000 - 130,000.

So jamaa aendelee tu kutafuta atapata mtu wa kumkopesha hizo 5M!

Hahahaa, kumbe na wewe umeona ee? Hata kama amekosea hesabu, hafai kukopeshwa kwa sababu hayuko makini na hesabu zake!
 
kule mang'ula gunia la mpunga sh 50,000 kwa lugha nyingine ulipaswa ulipe magunia 100 hapa bado hujaweka interest
 
Watu wanao anzisha uzi kama wananifanya nijiulize maswali mengi! Na sijui nimuweke kundi gani?
 
Last edited by a moderator:
Watanzania hatukopesheki!!na sababu kuu ni kushindwa kuandika mchanganuo sahihi wa biashara.
 
BONGOLALA Amoeba BADILI TABIA CHAI CHUNGU nimesema magunia 20 ya mchele, hivi mnaelewa mchele na mpunga tofauti yake lakini?

hata kama ni mchele bado hailipi wewe sema ulichemka kama vipi jipange upya. Huwezi kuuza gunia moja la mchele kwa Tshs 250,000 kwa kuwa gunia moja la kilo mia la mpunga utoa kilo 60 za mchele kwa hiyo bei ni bora mtu asubirie kipindi cha mavuno ununue kwa wakulima at prevailing market price ambayo inakuwaga nafuu sana ukifananisha na hiyo. Mtu anapokupatia fedha inabidi umpe favourable terms ambazo zitamvutia maana kama ungekopa benki ungewekewa riba ambayo ungerudisha fedha nyingi zaidi. Nina uhakika milioni tano kipindi cha mavuno unaweza kupata mpunga gunia 100 au zaidi
 
BONGOLALA Amoeba BADILI TABIA CHAI CHUNGU nimesema magunia 20 ya mchele, hivi mnaelewa mchele na mpunga tofauti yake lakini?
Gunia la mchele kipindi hiki ambapo bei ipo juu ni sh. 120,000 - 130,000. Tena hapo ni Dar es Salaam, sio Ifakara wala Mang'ula wala sio Kyera.

Sasa wewe unataka kutuuzia gunia moja la mchele kwa sh. 250,000 tena kipindi cha mavuno halafu shambani. Hapo hatujaweka gharama ya usafiri na riba. Kwa bei yako hiyo unamaanisha unaweza kutuuzia gunia moja la mchele kwa sh. 300,000 kama tutaweka gharama zote.

Sasa hapo utakuwa umekopeshwa au umeongezewa mtaji!?
 
Wadau mnapombishia na kumpa facts jamaa ndiyo anafurahi maana anachotaka yeye ni hizo ni Facts ambazo wadau mnampa kwa kumshangaa juu ya hiyo bei yake. Huo ni ujanja wake wa kupata taarifa tu, ila siyo njia nzuri kuwafanya wenzio hamnazo!
 
Stakabadhi ghalani!!! Yaani utakuwa umenunua kijanja!!!!
 
Hahahahahaha raha ya BONGO huwezi kupata majibu mazuri kwa kuuliza swali kistaraabu weka madudu upate majibu mazuri! sihitaji mkopo nilihitaji kujua bei za Mchele na Mpunga kwa Dar, na mambo mengine. Asanteni kwa kushiriki
 
Utakuwa umekosea jukwaa mkuu, hii thread ungeipeleka jukwaa la udaku!
:bange::bange::bange::bange::bange::bange::bange:
 
kajipange kaka magunia 20 ya mpunga ili anayekukopesha akayafanyie nini!?
 
Back
Top Bottom