fagix
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 739
- 554
Naamini muwazima wa afya, awali ya yote niwapongeze wote mliobahatika kupata mkopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB).
Hiyo ni haki yenu kwani vigezo na sifa za kupata mkopo umevitimiza. Pia poleni kwa wote ambao hamjapata mkopo, pia nanyi vingezo na sifa naamini mnavyo ila bahati haikuwa kwenu. Msikate tamaa wala kurudi nyuma huo ni mwanzo wa mapambano ya maisha yako.
Niseme kwa maneno machache tu "mkopo sio zawadi". Mwaka wa kwanza walio wengi ambao wamepata mkopo akili yao wanahisi sasa maisha tayari yamekaa mguu sawa ni mwendo wa bata tu hadi boom likome.
Kama una mawazo hayo futa kabisa, siku zote pesa za mkopo hazitoshi kukidhi haja zako.
Unachotakiwa kufanya ni nini:
1. Tumia hela yako katika matumizi muhimu.
2. Usipende kuwa na rafiki asiye endena na bajeti yako.
3. Muda wote kumbuka maisha halisia ya familia yako.
4. Tambua familia hazilingani kipato, usipende kuiga vitu usivyo na uwezo navyo.
5. Wekeza hata kibanda cha nyanya nyumbani kwako, ili ukimaliza uwe na pakuanzia maisha.
6. Kumbuka mkopo ni deni na utaulipa kwa riba, haitajalisha kama umeajiriwa au hapana.
7. Acha ushamba wa kupapalikia mademu wa chuo wataku-cost. Kumbuka mwanamke hutumia boom lake tu kama boom la boyfriend wake limeisha.
8. Tumia mkopo kama nyenyo ya kupata elimu na sio kichocheo cha starehe.
9. Heshimu quiz, test, UE etc. kama unavyoheshimu sehemu zako za siri.
10. Usije ukakwaruzana na lecturer/instructor/tutor kisa demu kwa pesa zako za boom, utaumia wewe.