Mkopo wa BMN wa Mshiko Faster, unaweza kukufanya ukadhalilika vibaya sana

Mkopo wa BMN wa Mshiko Faster, unaweza kukufanya ukadhalilika vibaya sana

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Wadau, nawapa tahadhari kuwa huu mkopo wa NMB wa Mshiko Faster, unapanda na kushuka utadhani bei ya hisa kwenye masoko ya hisa kwenye masoko ya hisa duniani. Kwahiyo, ukikopa, usitarajie kile kiwango ulichopewa mara ya kwanza, ndio utapewa tena baada ya kulipa deni na kuomba mkopo mwungine hata kama utakuwa umelipa kwa wakati.

Hivyo,usije ukafanya kosa la kukopa hela mahali ili ulipe kwa wakati halafu utarajie ukope tena wakupe kiwango kama cha mwanzo kwani unaweza kuumbuka.

Binafsi, kuna jamaa yangu nilimuongezea shilingi 100,000 ili alipe deni lake la awali, ila alichopata, hakika nilimuhurumia sana ikabidi tu niwe mvumilivu kwasababu ukweli naujua. Kiwango chake kilishuka sana kwani alipewa karibu thelethu moja ya mkopo wa awali tena sio tu baada ya kulipa, bali ilibidi tusubiri kwa masaa kadha mfumo umruhusu akope tena

Katika kufuatilia, majibu aliyopewe ni kuwa wao wanaangalia transcations zako unazofanya na ndio zinaamua mkopo wako uongezeke au upungue, bila shaka hivyo ndio vigezo na mashariti. Kwahiyo, kwa wale wanaopanga kuchukua huu mkopo au teyari wameshachukua, nawashauri wawe makini na wasitarajie mkopo wao utaongezeka kisa tu umelipa ndani ya muda ila wawe teyari kwa uwezekano wa kupata kiwango cha chini kuliko kile cha awali.

Mwisho, hii mikopo chukua kama una shida kweli kweli vinginevyo iepuke kabisa hasa kwa wafanyakazi wa serikali ambao baada ya mshahara kuingia na kutoka, hana transaction yoyote anayofanya ya kuweka na kutoa hela kwenye akaunti yake mpaka mwezi unaofuata mshahara mwingine uingie. Ni hatari sana na unaweza kudhalilika.
 
Back
Top Bottom