Ozzie
JF-Expert Member
- Oct 9, 2007
- 3,217
- 1,261

Wadau, habari zenu?

Naomba mnisaidie kunijulisha ni nani anaweza kunikopesha 35,000,000 nitamrudishia 1,500,000 kila mwezi kwa miezi 30.

Sina gari, sina nyumba, sina kiwanja.

Nina kazi kama permanent employee katika International company, napata take home 4,000,000/= Tshs.

Kazi nimeanza mwezi huu.

Natumia Standard Chartered Bank, wanaweza kunikopesha tu endapo kampuni yangu itakuwa ilishaweka mkataba nao (unfortunately kampuni yangu haitumii bank hii), japo kampuni yangu ilisema inaweza kuipatia details bank ninayopitishia mshahara kuwa mimi ni mwajiriwa wake.

Ni fanyeje? I need some money soon!

Nataka ninunue beach plot Mtwara.

Nenda barclays wana premier life banking. Hiyo inaruhusu mtu anayepata zaidi ya 1 million kama take home kukopa hadi 30 million tena ndani ya mwezi. Mwajiri hawi mdhamini wako. Ila anaji commit kwamba atakuwa akipeleka mshahara wako Barclays. Hata waweza badirisha ajira bila kuathiri ulipaji wa mkopo.
Vitu watakavyohitaji mwanzo ni salary slip za miezi mitatu, bank statement, kitambulisho cha kazi, na barua ya kutoka ofisini kwako ambayo ni utambulisho wa kukuruhusu ufungue account. Riba yao ni kubwa kiasi, ila haitafanana na utakayomlipa mtu binafsi kama utakopa kwa kipindi kirefu kama hicho.