Mkopo wa mil 35

Mkopo wa mil 35

Wadau, habari zenu?

Naomba mnisaidie kunijulisha ni nani anaweza kunikopesha 35,000,000 nitamrudishia 1,500,000 kila mwezi kwa miezi 30.

Sina gari, sina nyumba, sina kiwanja.

Nina kazi kama permanent employee katika International company, napata take home 4,000,000/= Tshs.

Kazi nimeanza mwezi huu.

Natumia Standard Chartered Bank, wanaweza kunikopesha tu endapo kampuni yangu itakuwa ilishaweka mkataba nao (unfortunately kampuni yangu haitumii bank hii), japo kampuni yangu ilisema inaweza kuipatia details bank ninayopitishia mshahara kuwa mimi ni mwajiriwa wake.

Ni fanyeje? I need some money soon!

Nataka ninunue beach plot Mtwara.

Nenda barclays wana premier life banking. Hiyo inaruhusu mtu anayepata zaidi ya 1 million kama take home kukopa hadi 30 million tena ndani ya mwezi. Mwajiri hawi mdhamini wako. Ila anaji commit kwamba atakuwa akipeleka mshahara wako Barclays. Hata waweza badirisha ajira bila kuathiri ulipaji wa mkopo.
Vitu watakavyohitaji mwanzo ni salary slip za miezi mitatu, bank statement, kitambulisho cha kazi, na barua ya kutoka ofisini kwako ambayo ni utambulisho wa kukuruhusu ufungue account. Riba yao ni kubwa kiasi, ila haitafanana na utakayomlipa mtu binafsi kama utakopa kwa kipindi kirefu kama hicho.

Siyo hivyo kaka, kuna mfanyakazi wa SCB aliniambia siwezi kupata mkopo kama kampuni yangu haijafanya makubaliano na Bank - kwamba inabidi iingie contract kuwa wafanyakazi wake wanaweza kuwa wanakopeshwa na SCB (haikuniingia akilini), nd'o nikaona niwaulize GREAT THINKERS na if possible mnipatie alternative. Wadau mliochangia inaonesha mnawafahamu vizuri hawa SCB, mnaweza kunipatia contact za mmoja wa wafanyakazi wa SCB. Nataka next week niwazukie ofisini, if possible nionane na Branch Manager. Lakini nahitaji mchango wenu zaidi na hata alternatives zingine. (sikimbii riba, huoni nime-promise kutoa 45,000,000 in total). I salute you all!!!!!!!!!

next time ukitaka kupata maelezo ya mikopo bank nenda onana na meneja au Afsa mikopo wa bank. achana na hao cleaners hawajui watakupa chaka.

Tatizo moja linalofanywa na vijana wengi wa Kitanzania hasa miaka 10 hii, ni kuingia kichwa kichwa kwenye swala la mikopo bila kufanya cost to benefit ratio. Huwezi kukopa pesa ukaenda kuzizika kwenye depriciated asset kama gari unless unakopa at less than 7% Fixed Interest rate. Na kama unachukua pesa na kununua asset kama huyu jamaa ambae anaenda kununua beach plot in Mtwara, kwanza lazima utazame long term benefit ya beach plot ambayo unakopea leo.

When will the loan matured? Na jee kiwanja hicho unataka kukifanyia nini? Jiulize maswali mengi na drop all kind of WORSE Scenerio kuangalia kama kweli unaitaji kukupa at 18%.

Mwisho sio kila University Graduate ni mjasilimali, some of us belong to the cubicle and others belong to the world business class. Jipime mwenyewe upo upande gani.

return on investmen ya hiyo beach plot iko vipi

Vifuatavyo ni vitu vichache kati ya vingi vitakavyokuwa Mtwara in 2 years to come:
1. Barabara toka Dar-Mtwara itakuwa full mkeka (just 5-6hrs drive)
2. Kuna kampuni at least tatu ambazo zitakwepo Mtwara (ya mafuta, ya gas na ya cement)

Kuna plo mwaka juzi iliuzwa 5M, mwaka huu imeuzwa 20M.

Mimi nanunua kwa ajili ya mwanangu ambaye ana umri wa mwaka mmoja kwa sasa ili atakapofikia umri wa kuwa amemaliza University (at 22-25 yrs of age) atumie elimu yake kuajiri watu kupitia hiyo beach plot (atafanya fanyaje, ....... atakuta ameshakuwa na akili ya maisha na ya darasani - atajua atafanyaje).

Walionunua majaruba ya mpunga maeneo ya Mwenge/ Kijitonyama, Mbezi, e.t.c wasingefanya "ujinga" huo watoto/ wajukuu zao wasingeonekana wa maana. Kwa hiyo nami nataka nifanye ujinga huo ili watoto/ wajukuu waje wafaidi. Mimi sina shida (ninachokitaka ambacho ni cha MUHIMU na LAZIMA kwangu nakipata).

• Thanks
Reactions: LAT
Nitajaribu kuwa-check pia. N'shaonge na Stanbic wamesema wanaweza kunikopesha ndani ya miezi mitatu (sharti salary ipitie kwao for at least three months) na barua ya mwajiri kuthibitisha kuwa mimi ni mwajiriwa wake. Thanks for your advice.

Standard chattered salary ikishapita mara moja unapata mkopo na si miezi mitatu kama stanbic. kwa salary yako SCB riba ni 18%. wasiliana na hiyo contact uliyopewa. asipokusaidia mwone dada mmoja anaitwa Mary kipeja yupo international house!

Huyo Salmin nimeshaongea naye, naye anasema si rahisi kwa kuwa inabidi kampuni iingie makubaliano na bank kuwa wafanyakazi wake wawe wanakopeshwa na bank (kitu ambacho kwangu siyo hivyo kwa sababu mimi kampuni ilisema itaweza kuandika barua kuwa mimi kweli ni mfanyakazi wake). Nilishaenda Stanbic ninafanya mchakato wa kufungua Account, wao wanaweza kunikopesha kwa mtindo huo, by Nov/Dec I expect to get not more than but almost equal to 12X net salary or yearly income - sasa sijui na hao wafanyakazi wa Standard Chartered Bank nao ni kama day worker? Kwa nini wasijue? Mara huyu anasema inawezekana, mwingine anasema haiwezekani! Naomba namba ya simu ya Mary Kipeja nijaribu kuwasiliana naye nijue tena ili kabla sija-channel mshahara wang Stanbic nijue mbivu na mbichi. Kwa muda huu nipo Ruvuma (Tanganyika ambako kuna NMB ambayo nd'o mama, baba!); ningekuwa Dar ningemtafuta.

When will the loan matured? Na jee kiwanja hicho unataka kukifanyia nini? Jiulize maswali mengi na drop all kind of WORSE Scenerio kuangalia kama kweli unaitaji kukupa at 18%.

Mwisho sio kila University Graduate ni mjasilimali, some of us belong to the cubicle and others belong to the world business class. Jipime mwenyewe upo upande gani.

Mkuu Mtanganyika umeongea mambo muhimu sana ambayo watu wengi wanatatizo hilo hasa graduates wetu sasahivi ningefurahi sana kama ntapata profile yako

Wadau, habari zenu?
Naomba mnisaidie kunijulisha ni nani anaweza kunikopesha 35,000,000 nitamrudishia 1,500,000 kila mwezi kwa miezi 30.
Sina gari, sina nyumba, sina kiwanja.

Nina kazi kama permanent employee katika International company, napata take home 4,000,000/= Tshs.
Kazi nimeanza mwezi huu.
Natumia Standard Chartered Bank, wanaweza kunikopesha tu endapo kampuni yangu itakuwa ilishaweka mkataba nao (unfortunately kampuni yangu haitumii bank hii), japo kampuni yangu ilisema inaweza kuipatia details bank ninayopitishia mshahara kuwa mimi ni mwajiriwa wake.

Ni fanyeje? I need some money soon!

Nataka ninunue beach plot Mtwara.

we kama utapata mshahara wa 4m kwa mwezi kwa nini ofisi isikudhamini? unakimbilia wapi kaka? acheni tamaa bana ndizo zinapelekea kuwa mafisadi.

Unajua msijaribu kuingia ktk matatizo kirahisi hivi, wewe ndo kwanza umeanza kazi mwezi huu na unataka ukope milion 35, mi haiingii akilini kabisa! Una uhakika gani kama utafanya kazi na kampuni hiyo mpaka mwisho na ulipe deni lako? Kaa kwanza jipime mwenyewe. Mshara wa mil 4 unaweza ukasevu mil 3 kila mwezi na baada ya mwaka tu utakuwa umesave mil 36 sasa kwa nini ukimbilie kukopa? Tulia acha tamaa mbaya sana sio kila unachokiona unataka uwe nacho.

Muone Jairo, Lowasa ama Rostam hata ukitaka mil 50 utapata

Wadau, habari zenu?
Naomba mnisaidie kunijulisha ni nani anaweza kunikopesha 35,000,000 nitamrudishia 1,500,000 kila mwezi kwa miezi 30.
Sina gari, sina nyumba, sina kiwanja.

Nina kazi kama permanent employee katika International company, napata take home 4,000,000/= Tshs.
Kazi nimeanza mwezi huu.
Natumia Standard Chartered Bank, wanaweza kunikopesha tu endapo kampuni yangu itakuwa ilishaweka mkataba nao (unfortunately kampuni yangu haitumii bank hii), japo kampuni yangu ilisema inaweza kuipatia details bank ninayopitishia mshahara kuwa mimi ni mwajiriwa wake.

Ni fanyeje? I need some money soon!

Nataka ninunue beach plot Mtwara.

Hii haraka ya nini mtu umeanza kazi mwezi mmoja uliopita na mara hii unataka kutimiza azima ya ndoto za kujenga magorofa? Ninyi ndo wale ndoto zisipotimia mnaamua kuwa mafisadi.

Vumilia uzoee kazi yako na bana matumizi baada ya miaka kama miwili hivi utajikuta una akiba ya kuanza kujenga magorofa, lakini kuanza kazi leo leo na leo leo ujenge magorofa hili ni gumu.

Hata mikopo bank watakuuliza uliajiriwa lini maana kuwa mfanya kazi kwa mwezi mmoja tu unaonekana bado upo katika majaribio na uthibitisho utafuata kutokana na utendaji wako wa sasa.

Tulia kwanza yakhe, usione watu wanajenga msingi na mwaka unaofuata anapandisha ukuta mmoja hadi nyumba ikammilike umri wa nyumba unalinga na umri wa mtoto analiye sekondari au chuo. Kazi kwelikweli.

Hizi njia za mkato zina athari zake bora kuwa na subira.

Stanbic 21% StanChart 18%

Sasa hii interest mpaka nimalize kulipa inaweza kujenga kibanda cha pili? Bora niuze vitunguu gengeni kuongeza kipato lakini haya ya bank balaa tu. Tujaribu hii michezo ya upatu inasaidia wengi.

Sasa hii interest mpaka nimalize kulipa inaweza kujenga kibanda cha pili? Bora niuze vitunguu gengeni kuongeza kipato lakini haya ya bank balaa tu. Tujaribu hii michezo ya upatu inasaidia wengi.

Kwa hiyo mnataka kusema huu mkopo tayari ambao na-process (nimeshakubaliwa), nisitishe? Au mnamaanisha nini?
Nichane makaratasi ambayo tayari nayajaza au nisiyarudishe bank ambako nilikaa nao tukaelewana na hatimaye kunipatia makaratasi ya kujaza - hii nchi ya ajabu kweli! Kuna watu na viatu!

Wadau, habari zenu?
Naomba mnisaidie kunijulisha ni nani anaweza kunikopesha 35,000,000 nitamrudishia 1,500,000 kila mwezi kwa miezi 30.
Sina gari, sina nyumba, sina kiwanja.

Nina kazi kama permanent employee katika International company, napata take home 4,000,000/= Tshs.
Kazi nimeanza mwezi huu.
Natumia Standard Chartered Bank, wanaweza kunikopesha tu endapo kampuni yangu itakuwa ilishaweka mkataba nao (unfortunately kampuni yangu haitumii bank hii), japo kampuni yangu ilisema inaweza kuipatia details bank ninayopitishia mshahara kuwa mimi ni mwajiriwa wake.

Ni fanyeje? I need some money soon!

Nataka ninunue beach plot Mtwara.

kaka, kipato chako kwa mwezi kinavutia sana, i mean una uhakika wa kuishi haya maisha magumu bila tatizo pia unakopesheka. Maana kwa sasa SCB wanatoa hadi times 19 ya net yako so mzee you can take up to 76m.

Cha msingi lazima kampuni unayoifanyika kazi iingie mkataba na SCB bila hivyo kaka unajisumbua bure.

Back
Top Bottom