Kauli za watu ambao wamekosa haja hapa jamvini.
1. Badala ya kujibu hoja anakugeuza wewe hoja : "una hasira, mmeo/mkeo hivi, boyfriend/girlfriend wako vile, umeachwa " wakati hakujui.
2. Badala ya kujibu hoja anadiscredit ulichouliza kwa kusema hujui kitu wakati yeye ndie alieshindwa kukujibu.
3. Badala ya kujibu hoja anaanzisha mada nyingine mpya kabisa.
4. Badala ya kujibu hoja anaanzisha matusi.
5. Badala ya kujibu hoja anaanza kudai "unatoa povu" ili tu uulize povu gani na kupoteza mlichokua mnajadili.
6. Badala ya kujibu hoja anakuita mbishi.
7. Badala ya kujibu hoja anakwambia usingechangia "hukuombwa/lazimishwa kuchangia" .
8. Ukitaka kuelewa point yake kuhusu tabia fulani anakwambia "wewe utakua hivyo hivyo" badala ya kukuelewesha.
9. Ukimuelewesha/jaribu kumrudisha kwenye mada anasema unamlazimisha kufikiri kama wewe.
. . . . . .