carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Aliyekuwa sajenti meja wa Jeshi la Rwanda na mkosoaji wa Rais Paul Kagame, Robert Kabera, amekutwa ameuawa na mwili wake kukatwa kichwa nchini Uganda, ambako alikuwa amekimbilia akidai kukabiliwa na mateso ya kisiasa nchini mwake.
Kabera, mwenye umri wa miaka 50, alikutwa amefariki dunia mjini Kampala mwishoni mwa wiki, huku polisi wakisema hadi jana Jumapili kichwa chake kilikuwa bado hakijapatikana.
Msemaji wa Polisi Uganda, Kituuma Rusoke, amesema uchunguzi kuhusu mauaji hayo unaendelea, ingawa hakutoa maelezo zaidi kuhusu waliohusika.
Kabera alikimbilia Uganda baada ya kushutumiwa kwa kosa la unyanyasaji wa kingono, tuhuma alizozikanusha. Aliomba hifadhi nchini humo akidai anakabiliwa na mateso ya kisiasa.
Kifo cha Kabera kimeongeza wasiwasi kuhusu usalama wa wakosoaji wa Kagame wanaoishi uhamishoni, kufuatia matukio mengine ya kuuawa kwa watu waliopinga utawala wake ndani na nje ya Rwanda.
Mjane wa Kabera, Jeanne d’Arc Rwigema Uwizeye, aliiambia BBC Great Lakes kupitia ujumbe wa maandishi kuwa ana hofu kuhusu usalama wake na wa familia yake.
Chanzo : Trt Swahili , Mwananchi official