Mkristo anayekiri kuishiwa na kujiona masikini anaikosea heshima hii aya

Mkristo anayekiri kuishiwa na kujiona masikini anaikosea heshima hii aya

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Ukristo no taasisi ya imani sio ya kisayansi. Mambo ya kisayansi yanahitaji ushahidi wa kugusika.
Ila mambo ya imani yanahitaji uamini kauli za Mungu bila kujali uhalisia.

Sasa hii kauli ya Maandiko ukiishika na kuiamini itakupa ujasiri wa kuoata chochote popote wakati wowote.

Itakupa nguvu ya subira ukiamini hata usivyonavyo unavyo wakati unasubiri viwe halisi (manifestation).

Maandiko yanasema

Wafilipi 4:19
Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachokihitaji kwa kadiri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu.

Unapoamka asubuhi ingiq duniani ukiwa na plenty mentality. Yaani Mungu hatakupungukia. Umejazwa kila unachokihitaji bila kujali kinaonekana au hakionekani. Hii itakufanya usiwe na wasiwasi wa maisha, na itakupa utulivu wa kupangilia mambo yako.

Ni haya tu.
 
maisha yangekua marahisi hivyo kila mkristo angekua tajiri, hasa hawa wa afrika wanaosali ovyo😂

anajua unachotaka ila lazima uombe😂

haya bana
 
NI SAWA HATUKATAI ILA MWANDISHI KAELEZEA STRAIGHT FORWARD KAMA VILE NI RAHISI TU
Mambo ya imani yako straight.
Amini hata kama hakionekani. Ushahidi wako kuwa jambo litakuwa ni hiyo kauli ya Mungu.
 
Mambo ya imani yako straight.
Amini hata kama hakionekani. Ushahidi wako kuwa jambo litakuwa ni hiyo kauli ya Mungu.
sasa mbona watu wanaenda kwenye mikutano mikubwa tena kwa wachungaji maarufu na wanaomba utajiri lakini tuko nao vilevile?
 
sasa mbona watu wanaenda kwenye mikutano mikubwa tena kwa wachungaji maarufu na wanaomba utajiri lakini tuko nao vilevile?
Usiangalie watu angalia kauli ya Mungu.

Kulikuwa na wakoma wengi sana Israel lakini alipona mkoma mmoja tu wa syria naaman.
 
Usiangalie watu angalia kauli ya Mungu.

Kulikuwa na wakoma wengi sana Israel lakini alipona mkoma mmoja tu wa syria.
kwa hiyo hawa wachungaji wanaosema pokea gari pokea nyumba pokea utajiri ni WAPIGAJI?
 
kwa hiyo hawa wachungaji wanaosema pokea gari pokea nyumba pokea utajiri ni WAPIGAJI?
Siwezi kuwasemea.
Kikubwa tusiangalie kauli za wachungaji. Ni kujiuliza tu je hayo maneno wanayotamka wanamistari inayoyasupport kwenye maandiko?.

Mungu amesema leo hatakupungukia, atakujaza. Shika hiki, amini. Uwe na mentality hii ukiwa katika shughuli zako za mikono itakuwa halisi.
 
Back
Top Bottom