Tetesi: Mkt CCM Simiyu kuteuliwa Mkuu wa Mkoa, Kihongosi akalia kuti kavu

Joined
Jan 30, 2023
Posts
16
Reaction score
14
MKUU wa Mkoa wa Simiyu, Kennan Kihongosi amekalia kuti kavu baada ya kushindwa kusimamia shughuli za Serikali ndani ya Mkoa huo na kutumia muda kujihusisha na makundi ya kisiasa ya kugombea ubunge katika Jimbo la Bariadi.

Tetesi zinazoenea ni kwamba mkuu huyo wa mkoa ameshagombana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Simiyu baada ya mwenyekiti huyo kumaliza mgomo wa madereva wa daladala huku yeye mkuu wa mkoa akishindwa kumaliza mgomo huo na ikidaiwa kuwa ameacha shughuli za serikali na muda mwingi anautumia kwenye makundi ya kisiasa ya ubunge bariadi.

Kutokana na umahiri huo wa mwenyekiti wa mkoa wa simiyu kuna tetesi huenda akateuliwa kuwa mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya kama walivyoteuliwa wenyeviti wa ccm wa mikoa ya mwanza na mbeya ambao waliteuliwa nafasi za ukuu wa wilaya.


View: https://youtu.be/iCVavE_tW-I?si=MSrtLXPUYPztgQJQ
 
Fitina hizo za siasa.....siasa Fitna !!!
 
Mwenyekiti wa CCM Mkoa hafai hata kuwa kiongozi wa familia.
 
Huyu Mwenyekiti CCM Simiyu, HAFAI hata kua Mjumbe wa Nyumba 10 .
Kwanini mkuu. Sikuhizi hudanganyi wale wapuuzi kwenye uzi wa kula zumda baada ya jamaa kukushtukia kuwa unajiandikia na kujijibu zile sms unazidi screen short. πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Kipindi cha uchaguzi kila mtu anatafuta credit zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…