Mkude akaribia kutua Yanga

Mkude akaribia kutua Yanga

Soma tahariri ya Habarileo kuhusu TFF na timu fulani na mwenendo wa ligi ndio utaelewa kwanini timu zinalalamika.
kwani tahariri hiyo kaandika nani?Si mtu kama we,tena inawezekana akawa mbumbumbu fc kisirisiri
 
Anaweza akawa mpiga magoti kwa baniani lakini mpenda haki.
 
Maneno ya Hans ni upuuzi,kusema mkude hana mchango mkubwa ni undezi sana. Singano aliondoka kwa upuuzi wa huyu huyu, kumlea na kumkuza mchezaji siyo justification ya kutompa dau zuri. Ina maana players wasihitaji maslahi mazuri kisa tu timu imewalea na kuwakuza!!! I bet round ya pili timu itapotea kwa upuuzi wa hawa akina Hansi & Co.

KADA

80M, kwa mpira gani haswa ??
Hakuna viongozi siku hizi na hizi tabia wameziendekeza wenyewe....

Huyo Singano aliondoka na kaishia wapi zaidi ya kuchoma mahindi !!
 
Mkubwa anadaiwa bilioni 13 au mali zinapigwa mnada wewe umekalia kushahadia ya wenzako. Tembeza bakuli kama enzi za Matunda. Wakati huu sio wa mchezo. OCH shauri yako.
Kwani wewe ushamalizana na bodi ya mikopo maana jina lako lipo kwenye list ya wadaiwa sugu?
 
19:27LIGI KUU BARA
Shaffihdauda

Kudai haki yake ya msingi kumesababisha mchango wake ndani ya timu kutothaminika na kutishiwa kutemwa mwishoni mwa msimu huu
Klabu ya Simba ipo kwenye mpango wa kusajili mbadala wa nahodha wao Jonas Mkude, baada ya mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya huku akiutolea maneno ya hovyo viongozi wake.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili Zacharia Hans Poppe ameiambia Goal, wamechoshwa na maneno ya mchezaji huyo na sasa wanaona nivyema wakamtafuta mchezaji mwingine ambaye atamudu kwenye nafasi hiyo.

“Tumeanza mipango ya kutafuta mchezaji mwenye uwezo zaidi ya Mkude, wa nafasi ya kiungo mkabaji kwasababu mchezaji huyo amekuwa na maneno mengi kuliko mchango wake kwenye timu,”amesema Hans Poppe.

Kiongozi huyo amesema mchezaji Mkude anataka kupewa dau kubwa kama ilivyo kwa wachezaji wa kimataifa, lakini kiwango chake ni chakawaida hivyo wanaona nivyema wafanye maamuzi mapema katika kipindi hiki cha dirisha dogo.

Amesema hadi sasa hakuna mchezaji waliyemlenga lakini wamepanga kumtafuta mchezaji huyo kwenye mataifa ya nje kwakua wanataka mtu mwenye uwezo tofauti kwa ajili ya kuifikisha mbali timu yao hasa ukizingatia wanamatarajio ya kupata nafasi ya kucheza michuano ya kimataifa siku zijazo.

“Mkude ni mchezaji ambaye tumemkuza wenyewe na tumekabidhi majuku, lakini anajifanya amekuwa na wakati hata asipokuwepo kwenye timu hatupati madhara yoyote,”amesema Hans Poppe.

Yanga yamtema rasmi Mbuyu Twite

Katika siku za karibuni Mkude, aligoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuichezea Simb, baada ya viongozi wa timu hiyo kumpa kiasi kidogo cha pesa na yeye kutaka kupewa dau la milioni 80 badala ya 50 wanazotaka wao.

Baada ya uongozi kugoma kutoa kiasi hicho cha pesa Mkude amesema ataondoka na kujiunga na mahasimu wao Yanga baada ya mkataba wake kuisha mwishoni mwa msimu huu.

Mkude amekuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi cha Simba, na amecheza mechi zote za mzunguko wa kwanza wa ligi ya Vodacom Tanzania na kuifaya timu hiyo kumaliza nafasi ya kwanza wakiwa na pointi 35.





View attachment 442508
ayabaaanaa
 
Uongozi wa Simba ni tatizo sana mtu mmoja ndo anafanya maamuzi ya mchezaji gani anafaa na yupi hafai
 
Mbona kajipeleka mwenyewe kambini? Wachezaji wakibongo uelewa wao mdogo sana.Anazima simu kisha anajianika magazetini.Simba si mkude wapo wengi wenye mapenzi na timu kama anaipenda vyura aende tu.
 
Mbona kajipeleka mwenyewe kambini? Wachezaji wakibongo uelewa wao mdogo sana.Anazima simu kisha anajianika magazetini.Simba si mkude wapo wengi wenye mapenzi na timu kama anaipenda vyura aende tu.
Safi sana mkuu..
Anaye penda vyura FC aende, timu yako kusaini mkataba tu eti unataka hela kama unanunuliwa kutoka timu nyingine ...!?
 
Misaada itapungua akianza kulipa deni la bilioni 13 au mali ziuzwe. Isije ikawa deni analowadai la bilioni 11 likafufuka. Mtaanza kupitisha bakuli kama enzi za Mzee Matunda. Mlichanga mpaka maharage leo mmesahau. Pesa za sponsor zitakatika soon.
Jamaa ana worth $ 400 m zinazojulikana Forbes
 
Uongozi wa Simba ni tatizo sana mtu mmoja ndo anafanya maamuzi ya mchezaji gani anafaa na yupi hafai
Afadhali ya Simba. Yanga mtu mmoja ndio analia maamuzi ya kila kitu.Akipiga chafya wanayanga wote wanashikwa na mafua. Akitishia kujiuzulu majitu mazima yanampigia magoti.Toeni boriti kwenye macho yenu kabla ya kuzungumzia vibanzi kwenye macho ya wengine.
 
Ila saa zingine wachezaji licha ya kutaka pesa nyingi ambayo ni haki yao ludai ila waangaliage na wanakoenda je wana nafasi?? Kwa hiyo anaenda kumuweka benchi Kamusoko?? NEVER!!
 
Jamaa ana worth $ 400 m zinazojulikana Forbes
Ajabu kwani ndio anakuwa tajiri wa kwanza aliyepo kwenye Forbes list kutupiwa nje vifaa vya ofisi zake kwa kudaiwa kodi ya pango.
 
Afadhali ya Simba. Yanga mtu mmoja ndio analia maamuzi ya kila kitu.Akipiga chafya wanayanga wote wanashikwa na mafua. Akitishia kujiuzulu majitu mazima yanampigia magoti.Toeni boriti kwenye macho yenu kabla ya kuzungumzia vibanzi kwenye macho ya wengine.
Mkuu ila sasa Yanga wanakusanya makombe tu kila msimu hao simba wanabaki kufukuza wachezaji na makombe wanasikia kwa wenzao tu
 
Aliyewaita mbumbumbu f.c wala hakukosea team kila siku inamigogoro na wachezaji wake
 
Mkude angetulia angekuja kuwa mchezaji mkubwa sana ila kwa tamaa zake mpira ndio umeishia hapo kama Kessy! Kama ni kwenda aende hana dhamani ya milioni 80
Siyo DHAMANI ni THAMANI.... Rage hakukosea kuwaiteni MBUMBUMBU
 
Endeleeni kuamini kuwa mtakuwa Mabingwa wa LigiKuu msimu huu ikiwa wachezaji wameshasoma alama za nyakati.....
Mbona inaelekea una uchungu sana Simba kutokuwa bingwa!? Si ndio vizuri Simba idhoofike ili timu yako ya Yanga isipate shida kuwa bingwa!? Mchukueni ninyi Yanga. Tena buuure.
 
Mbona inaelekea una uchungu sana Simba kutokuwa bingwa!? Si ndio vizuri Simba idhoofike ili timu yako ya Yanga isipate shida kuwa bingwa!? Mchukueni ninyi Yanga. Tena buuure.
Tena uchungu wa aina ya wanawake wanapojifungua. Unashangaa mtu povu na jasho linamtoka na huku anakwambia hiyo timu haipendi. Ikiacha mchezaji analalama na kuanzisha post chungu nzima. Inashangaza sana. Watu wapo chumbani kwao wewe upo nje unataka kiuno.
 
Back
Top Bottom