Mkude Simba Special Thread

Mkude Simba Special Thread

Tatzo la Jf mwisho wa kuweka audio ni 20 na kutupia audio humu inagoma kwa new version had nipate apk ile ya old version ndio nitaziupload

Tunasubiri mkuu uendelee kuziweka humu tufurahie. Wengine muda wa kusikiliza radio hatuna.
 
MZEE: Dokta nina tatizo...
DOKTA: una tatizo gani?
MZEE: uume wangu hausimami...
DOKTA: una mke?
MZEE: hapana...
DOKTA: una mchumba?
MZEE: hapana...
DOKTA: unatarajia kuwa na msichana yoyote kimapenzi?
MZEE: hapana..
DOKTA: sasa mzee unataka Uume wako usimame ili uwe unatundikia koti ama?
 
MASSAWE....YELE WIIIIIIII
Massawe alikuwa kanisani, kapu la sadaka likaanza kupitishwa, lilipofika kwake akatoa noti ya shilingi mia tano akaikunja kisirisiri akaitumbukiza kwenye kapu.
Mara ile ile akaguswa begani na mtu aliyekuwa nyuma yake, kugeuka akakuta jamaa anampa noti tano za elfu kumi, akajua jamaa anataka kutoa sadaka, akazipokea na na kuzitia katika kapu.
Walipomaliza ibada tu Massawe akamfuata nje yule mheshimiwa aliyetoa shilingi alfu hamsini, na kuanza kumpa hongera kwa kujitolea fungu kubwa vile katika sadaka.
Mheshimiwa akajibu,’Hapana haikuwa sadaka yangu, ulipokuwa unatoa sadaka yako mfukoni, zile hela zilidondoka kutoka kwenye mfuko wako, nikaziokota na kukurudishia.
Massawe akapiga ukunga "yele uwiiiiiii, yesu na maria".
Akamfuata mchungaji ili amrudishie elfu 50 yake,.
Akajibiwa imeshakabidhiwa kwa mungu...
Jamaa akaanguka akazimia.
Watu wakampeleka hospital, alivyozinduka akakuta yupo na dada mwenye nguo nyeupe akamwambia "afadhali nimekuona malaika naomba mwambie Mungu anirudishie hela yangu niliitoa kimakosa kanisani ".
Dada akamjibu mimi ni Ness na hapa sio kwa Mungu ni hosipital.
Massawe akazimia tena...
SHARE NA WENGINE WAFURAHI MAANA HAMNA NAMNA NYINGINE
 
Hapa utapata vichekesho vya mkude simba kwa kadiri nitakavyokuwa navipata sio mbaya kama nawe unavyo tukashare pamoja

*********UPDATE******
VICHEKESHO VILIVYOONGEZWA NI VITATU VYA CHINI
hii imetokana na jamii forum kutoruhusu zaidi ya file 20 hvyo tutakuwa tunafuta na kuweka vipya
 
Mtalii ; "Nasikia mbongo ukimuuliza swali nae anakuuliza swali?"

Mbongo; "Wewe umejuaje?"


Hapo mtalii akawa kisha pata jibu.[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Hapa mtaani kuna mwizi sugu ameshinda milioni 10 za bahati nasibu, alipoulizwa atazifanyia nini hizo pesa zake?

akasema he wants to expand his business "Atazitumia kukuza biashara yake"

watu wameanza kuhama mtaa..!!

[emoji23][emoji23]
 
Nimetumiwa sms na bodi ya mikopo kuwa nadaiwa .wamenipa siku 30 nijisalimishe.

Nimewambia mbona sijasoma chuo kikuu wananambia mbona kila siku najiunga vifurushi vya chuo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom