Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Vifo vya polisi vimefuatana jamani! huyu ni watatu kifo chake ni cha ajali ya kugongwa na pikipiki
Pia namuonea huruma sana huyo dereva boda maana anakesi kubwa ya kujibu Mungu amsaidie tu
================
Mkufunzi wa Shule ya Polisi Moshi (TPS), SP Emmanuel Eliuta, maarufu Mtatifikolo, amefariki dunia baada ya kugongwa na pikipiki wakati akifanya mazoezi ya mchakamchaka na askari wenzake.
Akithibitisha tukio hilo leo Alhamisi, Septemba 10, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Simon Maigwa amesema ajali hiyo ilitokea Septemba 5, 2026 saa 10:40 alfajiri katika Barabara ya KCMC, eneo la Kwa Mwakyoma, Kata ya Longuo, Moshi Mjini.
“Pikipiki yenye namba MC 873 DVX aina ya Sinoray, iliyokuwa ikiendeshwa na Jordan Kisima, Mchaga (25), mkazi wa Njiapanda KCMC Maduka ya Chini, ilimgonga SP Emmanuel Eliuta aliyekuwa akifanya mazoezi ya mchakamchaka na askari wenzake,” amesema Maigwa.
Amesema Emmanuel alipata majeraha na alifariki dunia wakati akipatiwa matıbabu katika Hospitali ya Rutaa ya KCMC, huku mwili wake ukihifadhiwa hospitalini hapo.
“Chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva wa pikipiki kwa kuendesha bila kuchukua tahadhari katika eneo la makazi ya watu, hali iliyomfanya ashindwe kuidhibiti pikipiki na kumgonga marehemu,” amesema Maigwa.
Soma Pia: Pwani: Polisi wawili wagongwa kwa mkupuo na kufariki
Amesema dereva huyo amekamatwa na pikipiki imehifadhiwa
kituoni kwa ajili ya ukaguzi.