Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

Mkuki Kwa Nguruwe (Kisa Cha Kweli)

SEHEMU YA 97


‘Mimi naomba aje Binti yangu wa kufikia, ..aje yeye kwanza maana anahitajika kwenda kujiandaa kesho anasafiri....’akasema mama

Na mwenyeketi akageuka kumuangalia mwenyeji wa kikao ambaye ndiye alikuwa muongeaji , na yeye ndiye alistahiki kuita mashahidi wake,…

‘Unajuaje kuwa huyo ni shahidi wake, usiharibu utaratibu, au..’akasema mwenyekiti

‘Sawa ila…’nikasema nikiwa sijui lolote kuhusu huyo bint

‘Mimi nina uhakika ni shahidi wake..’akasema mama.

‘Haya, kama muhusika umemkubali kuwa ni mmoja wa shahidi zako, aitwe, au unasemaje mwenyeji wa kikao..?’ mwenyekiti akauliza na mume wangu akawa kabakia kimia, akiwa kashika kichwa…

Tuendelee na kisa chetu

**************

Kila mmoja alikuwa na hamu ya kumuona huyo shahidi, na wengine walipumua, kwani hakuna aliyejua ni nani ataitwa kama shahidi, na hadi pale mlango unagongwa, wengi bado walikuwa kwenye kutafakari, na kuwazia ni nani huyo binti wa kufikia wa huyo mama, ambaye hajulikani, ni nani huyo binti ambaye anaweza kutoa uahshidi na alifanyiwa nini...

Mlango ukafunguliwa, na akaingia binti, akiwa kavalia kiheshima na mkononi alikuwa kashika bahasha, na , hakuwa na kitu kingine, kwanza kwa aibu alipoingia pale mlangoni, hakujua afanye nini, alishikwa na butwaa hasa alipoona watu wote wamegeuza kichwa kumuangalia yeye,...

‘Sogea huku mbele...’ilikuwa sauti ya mwenyekiti, ndiyo iliyompa nguvu huyo binti, na taratibu akawa anasogea kuja upande ule watu walipokaa, kulikuwa na kiti kipo wazi.

‘Wewe umefuata nini huku...’

Sauti iliyowafanya watu wageuka, na kuangalia muongeaji ni nani,

Kumbe mume wangu wakati watu wanahamasa ya kumuona huyo shahidi yeye bado alikuwa kainamisha kichwa, na hata sauti ya mwenyekiti, ya kumkaribisha huyo shahidi ilikuwa bado haijamshtua vyema, akawa kama katokea usingizi, akainua kichwa na kumuona huyo shahidi.

Hakuamini macho yake,, macho yakamtoka pima, mdomo ukabakia wazi, na alichosema ndio hicho…

‘Wewe umfuata nini huku……….’.

Binti yule kusikia hivyo, akawa anaonyesha hali ya kuogopa, …akawa kashikwa na butwaa, akawa sasa hajui afanye nini..

Kwa wakati huo watu wote sasa wamemtupia macho mume wangu, ambaye kwa muda huo alikuwa kasimama nusu, na mwenyekiti akawa anaangalia hili tukio kwa hamasa ya aina yeka, huku tabasamu tele mdomoni, alikuwa akisubiria hiyo hali kwa hamu kubwa sana,..

Na mimi nilipogundua kuwa ni huyo binti, moyoni nikasema, ‘huyu ni shahid wa kweli,..hata hivyo mimi sikuamini, maana sikuwa nimelifahamu hilo, kwahiyo kwangu moyoni nilitamani kusikia atakachokizungumza huyo binti…nilimuangalia yule binti wa watu kwa moyo wa huruma….

‘Haya huyo hapo shahidi wako wa kwaza, unataka uendelee naye mwenyewe, au nishike usukani mimi, maana wewe ndiye mzungumzaji..?’ akauliza mwenyekiti, lakini mimi niliishiwa nguvu, nilibakia kimia, nikiwa nimwangalia yule binti, sijui ilikuwa ni huruma, hasira, au nini sikuweza kuongea, kilichotokea ni mimi kuangusha chozi..chozi la nguvu, nikikumbuka huyo binti alikuwa kwenye dhamana yangu, nikikumbuka kuwa huyo ni sawa na watoto wangu, mtoto wa mwenzio ni sawa na mtoto wako, umtendeayo mtoto wako ukumbuke na wewe utakuja kutendewa.

Mwenyekiti akaiona ile hali, akaamua kuendelea mwenyewe, akasema;

‘Kweli inauma, hii isikie kwa mwenzako tu, lakini ukitendewa wewe utaona uchungu wake, na hasa utendewe na mtu unayemwamini, huwezi kuamini …huwezi kuamini mpaka likufike, tujiulize hivi sisi hatuwezi kuwa na watoto…’akasema mwenyekiti.

Hatukupenda aibu kam hizi ziwekwe hadharani hivi, ila naamini kuwa nyie ni wanafamilia, na hili kwa hivi sasa libakia humu humu, hadi hapo, tutakapoona sasa ni wakati muafaka wa jamii kufahamu…’akasema mwenyekiti.

‘Nawausia ndugu zanguni, mimi hapa ni mzazi, na ni mkubwa wenu wote hapa, tuweni makini sana, ..tena sana na wafanyakzi wenu wa ndani, msipende kuwaacha na waume zenu kwa muda mrefu, au kuwapa kazi ambazo sio stahiki zao, kila kitu mfanyakazi wa ndani, hata kutandika kitanda chenu..jamani, ..’akasema na watu kidogo wakacheka.

‘Binti wengine ni mtihani…yeye aje kukutandikia kitanda, afagie, ainame wewe dume upo humo..mnawatia majaribu waume zenu..’hapo watu wakacheka,

‘Lakini sahamanini,..lakini ..hahaha, msicheke jamani, sio kwamba nasema wanaume wote wana tabia hiyoo chafu, ..hapana, wapo wanaume wanajikubali, wanahulka ya utu wema, ..muulizeni mke wangu...mimi aah, maana na umri huu nao…’akasema mwenyekiti na watu wakacheka.

Ilibidi watu waachwe kwanza watulie maana baada ya kicheko, ilifuatia watu kuteta, kwa kunong’ona na mnong’ono wa wengi ni ngurumo, mwenyekiti akaacha hali hiyo ipite kidogo.

‘Huyu hapa mbele yenu ni shahidi,…kama mjumbe alivyotaka upatikane ushahid wa madhambi yake,..hajataka kukubali mpaka ushahidi, haya ushahidi ndio huo hapa, ambao, utadhihirisha urijali wa mume wa familia…’aliposema hivyo watu wakacheka.

‘Tusicheke jamani, hebu muangalieni huyu binti, afadhali sasa kakua, ..anaonekana mdada, kumbuka umri aliokuwa nao, kipindi hicho wanaishi nah ii familia, ndio ni kweli umbo lake lilikuwa kubwa la kuvutia, lakini kumbuka kiumri…na kumbuka huyu ni binti sawa na binti yako wa umri huo…napenda kurudia sana haya maneno ili nyote muwe ni mashahid kuwa nililisema hili…’akasema mwenyekiti.

‘Huyo ni sawa na binti yako mume wa familia, japokuwa binti zako hawajafikia umri wake, lakini watafikia umri huo, huyo ni sawa na dada yako, kama una madada…wewe ukaamua kula kuku na mayai yake..bado hutaki kukiri kume umekosa, una makosa, utubu mbele ya jamii…haya ngoja tuanze na huyu shahidi wetu...’akasema mwenyekiti.

‘Binti usiwe na hofu, wala usimuogope huyo mtu, kauli yake ya kukutisha haina maana mbele ya jamii…kama kakosa kakosa, ..na wewe uliyekosewa ni haki yako kusema ulichotendewa, sisi hapa tutakulinda, …’akasema mwenyekiti

‘Hebu tuambie jina lako,....?’ akaulizwa na akabakia kimia, halafu akainama, halafu akaanza kulia

‘Binti, ..ule ushujaa umekwenda wapi, kwanini unalia, sikia binti usiogope, hata tunachotafuta hapa ni haki yako,ukiogopa haki yako yote itapotea, na waliokuharibia maisha yako wataendelea kuyafanya haya kwa watu wengine, ...’akasema mwenyekitu

‘Sisi hapa tunataka ukitoka hapa, uondoke na tumaini, na haya yaliyotokea kwako, yakomeshwe, na ili hili lifanikiwe tunatakiwa tuanzie huku majumbani kwetu, kama hivi,..likitokea jambo, mkosaji aitwe, aadhibiwe, ikishindikana, apelekwe kunakostahiki,...’aksema mwenyekiti.

‘Haya jitambulishe mpendwa,...’akasema mwenyekiti.

‘Mimi naitwa Tabia...’akasema kwa sauti ya kinyonge

‘Tabia,..tabia yako ni ya upole, au sio, mchapakazi, au sio, ...sasa nasikia kuna kitu kilitokea, wakati unafanya kazi kwenye nyumba moja, kilipotokea ukakimbia jiji, ni kwanini ulikimbia jiji, wakati wenzako wanasema tutabanana hapa hapa...?’ akamuuliza mwenyekiti.

‘Sikukimbia jiji, niliambiwa niondoke, la sivyo yatanikuta makubwa, na...na...’akasita kuongea

‘Hebu sasa tuanze, maana nilikuwa nakuweka sawa, hebu niambie, wewe ulikuwa ukifanya kazi wapi , na kwa nani…?’ akaulizwa

‘Mimi nilikuwa mfanyakazi wa ndani wa nyumba, ya ya...’akageuka kuniangalia mimi

‘Ya mke na mume wa familia hao hapo au sio, hapa tunawatambua kama mke na mume wa familia, ambayo ndio tunayoiongelea hapa hii leo ..ngoja nimsaidie...’akasema mwenyekiti.

‘Ulifanya kwenye hiyo nyumba kwa muda gani?’ akaulizwa

‘Kwa zaidi ya mwaka mmoja...’akasema

‘Hebu niambie, wakati upo hapo, kulitokea nini, kilichokufanya uondoke, uliamua kuacha kazi , kwa vile umepata mume huko kwenu au ilikuwaje?’ akauliza mwenyekiti.

‘Niliondoka baada ya kugundua kuwa nina uja uzito...’akasema na watu wakaguna

‘Wakili wa mume wa familia, unalisikia hilo…sitaki uweke pingamizi najua ndio zenu kuwalinda wahalifu..’akasema mwenyekiti alipoona huyo wakili wakitaka kunyosha mkono.

‘Jamani msigune, ndio hali halisi, na tunapoongea hapa watu wanafikiria tunamuonea mlalamikiwa, yeye anafikia kusema mimi nataka kuvunja ndoa yake tu , kwa vile… ngojeni sasa myasikie na nyie kwa masikio yenu…’akasema mweneykiti.

‘Haya tuambie, unasema ulipata uja uzito, kumbe wewe badala ya kufanya kazi za ndani ulikuwa ukifanya uhuni na wavulana wa mitaani eehe...’ aksema mwenyekiti kwa sauti ya nzito, kama kumtisha huyo binti.

‘Hapana mimi sio muhuni, sijawahi kufanya uhuni na mvulana yoyote, tangia nifike hapa mjini , kazi yangu ilikuwa …...’akasema na hapo akaanza kulia

‘Unasema hujawahi kufanya uhuni na mvulana yoyote, sasa hiyo mimba uliipata kutoka mbinguni, hebu sema ukweli, ...’akasema mwenyekiti

‘Mimi nilikuwa simjui mwanaume yoyote, nilikuwa nafanya kazi zangu na sikupenda haya yanitokee, ..niliapa kwa mama yangu kuwa sitakuwa muhuni, na nilipochukuliwa na ....wazazi wangu hawo, nilijua kuwa nimefika mahali salama....sikutarajia kuwa hayo yangelitokea,....’akawa analia

‘Usilie, …ongea yaliyokukuta sasa, ilikuwaje tuanataka kusikia kuhusu maisha yako…wapi ulipotokea wazazi wako, ulifikaje hapa kwa hiyo familia ili muone ni dhambi gani huyo mtu aliibeba, na kama bado anakataa kutubu basi huyu sio mwanadamu..hebu tuambie kisa cha maisha yako;

***********

Mama yangu ni mjane, baada ya kufariki baba, kwa ghfla,sisi tulibakia na mama kwenye kibanda kibovu tu,tukiwa watoto watano, na alituacha tukiwa masikini sana, mama akawa anaangaika sana kututafutia riziki, na sisi japokuwa tulikuwa wadogo, lakini tulijijua kuwa hatuna mtu atakayetusaidia, kwani baada ya msiba, vitu vilivyokuwepo vichache viligawanywa, na wanandugu wakachukua kile walichoona kinawafaa, tukabakia mikono mitupu.

Mimi nilikuwa mkubwa ukilinganisha na wadogo zangu,kwani mimi nilikuwa mtoto wa kwanza nna kwa vile ni mwanamke , nilionekana mkubwa kidogo, basi ikawa kazi kubwa ni kumsaidia, kila tukitoka shule tunajipanga, huyu afanye hiki na yule afanye kile, ili tu tuweze kumpunmguzia mama kazi za nyumbani..

‘Kazi kubwa ya mama ilikuwa kutengeneza vyungu, kwa kutumia udongo wa mfinyazi, alikuwa akienda huko mlimani kuutafuta udongo wa mfinyanzi, na akileta anatengeneza vyungu vya kupikia, …

‘Kiukweli mama alikuwa mtaalamu sana wa kazi hiyo, lakini hata hivyo kazi hiyo ilikuwa hailipi, kwani akijitahidi sana anakuwa katengeneza vyungu, hata kumi havifiki, na bei za kijijini ni ndogo, ni kazi nzito, lakini tungefanyeje...kuna kipindi tunakuwa hatuna hata senti moja, nyumbani, inabidi mama aende kwa majirani kuomba hata kazi ya kulima, au kuosha vyombo ili angalau tupate pesa ya kula, ndio maisha niliyokulia hayo.

Wingi wetu, ulikuwa mzigo sana kwa mama, na ukumbuke baba alifariki akatuacha tukiwa tunasoma shule ya msingi, mimi nilikuwa darasa la saba, na wenzangu, la sita, la tano la nne, na la tatu, na wamiwsho alikuwa darasa la pili,tulipishana mwaka mmoja mmoja wa shule, japo kimuri tulipishana kidogo. Ilibidi tusome kwa shida, hata nguo za shule, zilichakaa, ikawa tunaweka viraka, na wengi walianza hata kututania, kuwa sisi ni viraka.....’akasema

Darasa la saba nilimaliza kwa shida sana, kwa vile mimi ndiye mkubwa, basi ilikuwa kama mimi ndiye msaidizi mkubwa wa mama, nilitakiwa kuamuka asubuhi sana, kumsaidia mama, ili aweze kukusanya, vile vyungu vilivyokuwa tayari, maana tulikuwa tukivichoma usiku,na asubuhi, tunavitoa ili vipoe, vingine vinavunjika, ndio hivyo tena...’akatulia.

Nilipomaliza darasa la saba tu, watu wengi wakaja kunitaka, niende nikafanye kazi kwao, kama mfanyakazi wa ndani, kutokana na jinsi walivyoniona, kuwa ni mchapakazi, sikupena kabisa niondoke nimuache mama yangu, lakini pia tulihitajia pesa kwa ajili ya kuwasomesha wadogo zangu, basi mtihani ukaanzia hapo, niende kwa nani..

Kabla hatujaamua ndio siku moja likaja gari, na wakaja hawa wazazi wangu , ambao mama alikubali niondoke nao,mama alisema anawafahamu vyema, na aliona kuwa watatusaidia kujikwamua kimaisha, angalau wadogo zangu waweze kusoma na kufika mbali sio kama mimi niliyeishia darasa la saba ...’akatulia.

‘Wageni hawo, waliongea na mama wakakubaliana, na kesho yake nikachukuliwa na kuja huku Dar, na kama ujuavyo, kila mmoja kule kijijini anatamani sana kuja huku, kwahiyo hata mimi nilifurahi sana, na nilishukuru kuwa nimapata kazi kwa watu wenye uwezo. Nikawaga wanafamilia, yaani mama na wadogo zangu. Mama alizidi kuniusia kuwa nifanye kazi kwa bidii nisije nikandanganyika na kuingiwa na tamaa, na kujiunga na wahuni, mimi nikamuahidi mama sitafanya lolote baya.

Mshahara wangu wa kwanza wote niliutuma kijiji kwa mama, na mama yangu mpya, yaani bosi wangu, alikuwa akinijali sana, alinisaidia mambo mengi, na kuanza kunisomesha msomo ya jioni, nikaanza kuelewa maisha na jinsi gani ya kuishi kisasa, sio kama nilivyokuwa huko kijijini, na alikuwa akinisaidia kunipa peza za kuwasomesha wadogo zangu kila nilipomweleza matatizo ya nyumbani kwetu...’akatulia kidogo.

Kwakweli mimi darasani sielewi, ninachojua ni kufanya kazi, nikamwambia mama asipoteze pesa zake bure, kunisomesha, kwania yeye alitaka kunisomesha sekondari, kiujumla kichwa changu ni kizito sana darasani, akaniuliza kitu gani rahisi ninaweza kukisomea au kukifanya, nikamwambai ufundi, na nikachagua ufundi wa kushona, na kweli huo nikauwezea sana...akaninunulia cherehani, nikawa nashona nguo hapo nyumbani, na alikuwa na mpango wa kunifungulia duka langu...lakini oh bahati haikuwa yangu....’akaanza kulia.

‘Aaah, tulishakuambia, ujikaze, mambo ya kulia hapa hatuyataki...yote ni mitihani ya maisha, unachotakiwa ni kumkabidhi mungu, ..usilie mwanangu ongea...’mama yangu akamwambia na kumpa moyo.

‘Ndoto zangu za kuwa mtu maarufu zikazimwa kama taa ya kibatili,maana nilikuwa na ndoto za kuwa mwanamitindo, nishone nguo za kila aina,lakini ndio hivyo tena yakanikuta makubwa ambayo sikuyatarajia...kwasababu ya ...ya...’akasita kusema huku akigeuka kumwangalia mume wangu ambaye kwa muda huo alikuwa kainamisha kichwa chini.

‘Hebu tuambie ndoto yako hiyo ilizimikaje, kwa maana ulikuwa unaishi na watu wenye uwezo wangeliweza kukusaidia sana tu, na nakumbuka mwanzoni nilipowatembelea ulionekana mwenye furaha,ukasema kuwa umewapata wazazi wazuri wanaokujali...?’ mwenyekiti akauliza

‘Ndio mwanzoni mambo yalikuwa mazuri sana, sikuwa na shida, na niliwaona wazazi wangu ninaoishi nao ni kama baba na mama yangu, na kwa ujumla wao walikuwa wachapakazi kweli, hawakutaka mchezo, na wakanikuta na mimi ni mchapakazi kama wao, japokuwa ni za nyumbani, kwahiyo kila mmoja alikuwa akiamuka asubuhi anakimbilia kwenye kazi yake…

‘Na mimi nikawa naendana nao,.. hakuna muda wa kuongea, na mimi nilikuwa nafanya kazi yangu vyema, bila ya kusimamiwa,...ghafla nikahisi mabadiliko, maabdiliko hayo niliyaona kwa baba, akawa analewa sana....’akasita kidogo pale mume wangua lipoinua uso kumwangalia.

‘Usimwangalie, wewe ongea ,hana lolote kwa sasa, hawezi kukufanya lolote....’akamwambia mama, ambaye alionekana kama muongozaji wake.

‘Kabla hata ya hapo, nilipokuwa nimekaa hapo kwa mwezi mmoja tu, nilikuwa nimeshabadilika sana, mwili wangu ukawa mkubwa, nikawa naonekana msichana,mkubwa kuliko umri wangu, mmmh....’akatulia na mwenyekiti akasema;

‘Msichana mrembo...eeh’akamalizia mwenyekiti, na watu wakacheka kidogo

‘Ndio ndivyo walivyokuwa wakiniambia watu, lakini mimi sikujali, maana nilikuwa nafahamu ni kitu gani kimenileta hapa Dar, nikawa nawajibika ipasavyo, sikuwa na muda na watu wa mitaani hasa wanaume…, ambao walikuwa wakinisumbua kila nilipokuwa nikitoka, kwenda dukani au sokoni, ...huko nje niliweza kabisa kuwashinda, sikuwapa muda wa kuongea nami, lakini tatizo likawa ndani,....’akatulia kidogo.

‘Ulikuwa unanyanyaswa, au hayo mabadiliko yalikuwa yapi, mpaka nyumbani kuwe ni mtihani kwako?’ akauliza mwenyekiti.

‘Baba….a-a-ah…, nilimuona baba akinitizama kwa macho yaliyonitisha..sivyo kama ilivyokuwa mwanzoni’akasema

‘Kwa vipi hebu fafanua..na ulihisje hivyo, kwani mama yeye alikuwa hakuangalii, kama anavyofanya baba ?’ akaulizwa na mwenyekiti.

‘Ni kama ..ya tamaa, maana anakutizama mpaka unaona aibu, kuna siku nilimuuliza mama mbona baba ananitizama hivyo,mama akasema hajawahi kumuona baba akifanya hivyo, akaniambia nifanye kazi zangu, nisiwe namwangalia baba, kwani utajuaje kuwa mtu anakutizama, kama wewe hujamuangalia, nikaona aibu kwanini nilimwambia mama hivyo

‘Siku moja nikashindwa kuvumilia, nilipomuona baba ananitizama nikaona ngoja nimuulize kama baba yangu, yeye, akasema siku hizi nimekuwa mrembo sana...’akasema.

‘Unaona eeh…haya endelea…’akasema mwenyekiti

‘Kauli hiyo ikanikwanza, nikaona nimwambia mama tena, kesho yake, nilimuona baba kanikasirikia, na hakutaka hata kuitikia salamu yangu, nikahisi huenda waliongea na mama kuhusu hayo niliyomwambia, na hali ikatulia kidogo, lakini baadaye, nikaona ile hali inarudi tena, baba akawa ananifuata hata sehemu ninyofanya kazi na kuanza kunitania, mimi kwa vile niliona ni baba yangu, nafurahi,naongea naye tu, ila kwa tahadhari, kwani mama alishaniambia kuwa nisipoteze muda kwa kuongea ongea...’akasema.

`Ikazidi, kwani nilishawahi kumfuma baba akinichungulia,....’akasema na watu wakaguna

‘Akikuchungulia kwa vipi?’ akaulizwa

‘Kama nimetoka kuoga, nikiingia chumbani kwangu,kama mama hayupo, baba anaweza kuingia chumbani kwangu ghafla na kujifanya kauliza kitu, na wakati huo huenda nilikuwa nipo uchi, kwani .....’akatulia

‘Tunaelewa endelea..’akasema mama.

‘Kuna kipindi alikuwa akija usiku nimelala, na kuanza kunifunua nguo...nikishituka, anasema alikuwa akinifunika vizuri,....’akasema

‘Oh, muongo mkubwa wewe, unawadanganya watu , mimi niliwahi kukufanyia hivyo, nitakukomesha kwa uwongo wako...’mume wangu akasema kwa hasira na wakili wake akamtuliza.

‘Je alikuwa akifanya hivyo, akiwa amelewa?’ akaulizwa

‘Hapana hiyo ilikuwa mwanzoni kabla hajaanza kulewa, na alipooanza kulewa, ndio akaanza visa vyake...’akasema.

‘Haya tuambie hivyo visa vyake vilikuwaje...’ akasema mwenyekiti

‘Alianza kunitongoza...’akasema na watu wakaguna

‘Hahaha, anamtongoza binti yake,…jamani…’akasema mama

‘Eehe, alikuambiaje, na ulijuaje kuwa anakutongoza, na wewe ulimjibuje vipi?’akaulizwa

‘Aliniambia kuwa ananipenda sana, na anataka...anataka tuwe wapenzi wa siri...’akatulia kidogo.

‘Akasema atanifundisha jinsi ya kupata raha ya mapenzi,...’akatulia kiogo.

‘Mungu wangu…’mimi nikasema hivyo nitaka kumwambia huyo binti asiendelee maana nilikuwa naumia ndani kwa ndani, kila hatu ilikuwa ni mateso kwangu.

‘Kwa kipindi kile mimi sikuwa namuelewa ana maana gani, ila akilini mwangu ikanituma kuwa huyu anataka nifanye naye kitendo kibaya, ..’.akasema.

Basi aliponitongoza tena, mimi nikamwambia;.

‘Wewe nakuheshimu kama baba yangu, kwanini unaniambia mambo kama hayo, yeye akasema hajanizaa, na mimi ninaweza kuwa hata mke wake, na yupo tayari kuninunulia chochote hata kunijengea nyumba ya kifahari huko kijijini,...’akasema

‘Mwongo sana huyo binti msimsikilize ni mfitinashaji huyo ndio maana nilimfukuza..’akasema mume wangu lakini hakuna aliyemsikiliza

‘Wewe endelea, cahana na huyo…’akasema mama

‘Mimi nikamwambia mimi nawaheshimu wao kama wazazi wangu siwezi kufanya jambo kama hilo, na mama yangu alinikataza kabisa kufanya huo uchafu, kwani mimi bado mdogo, na natakiwa kufanya hayo mambo nikiolewa...’akasema

‘Ulimwambia hivyo huyo baba yako, na ulijuaje kuwa anataka mfanye mambo machafu, ?’ akaulizwa

‘Ndio nilimwambia hivyo, yeye aliniambia kuwa anataka tufanye mapenzi, ...’akasema

‘Wewe mapenzi uliyajuaje..?’ akaulizwa

‘Mimi nilifahamu mapenzi ni kitu kichafu, lakini ni kizuri kwa wandoa, ..shuleni tuliwahi kufundishwa vitu kama hivyo…kwahiyo mimi hapo nilifahamu kuwa ananitaka kwa mambo machafu , mama alishaniambia hayo kuwa mwanaume akisema anataka kufanya mapenzi na wewe ujue anataka kufanya mambo mabaya ya kukuharibu usichana wako, ....’akasema.

‘Baba hakuchoka kunibembeleza na aliniambia nikumwambia mama hayo anayoniomba, atahakikisha narudi kijijini na kuwa masikini wa kutupwa,...nikaaogopa sana, kwani kule kijijini kweli baba yangu huyo wanamuogopa sana....’akasema

‘Kwanini wanamuogopa?’ akaulizwa

‘Wanasema baba huyu ni tajiri na anaweza kukufanya lolote asifungwe, kwa vile ana kampuni yake kubwa, na anajuana sana na polisi...na pia anajuana sana na yule mwanasheria aliyekufa, ...’akasema

‘Kwanini huyo mwanasheria aliogopewa…samahani kidogo japokuwa tunamteta marehemu lakini hapo kuna ushahid pia tunauhitajia,…’akasema mwenyekiti

‘Huyo mwanasheria aliyekufa naye alikuwa akiogopewa sana, kuliko hata baba, kwasababu wanasema anafahamu uchawi wa kisasa, anaweza akakuangalia hivi akakuambia yoye unayofikiria kichwani mwako,anaweza kujua kitu gani ulikuwa ukifanya nyumbani kwako, wanamsema kwa mambo mengi tu,...anaogopewa sana kule kijijini, na huyo alikuwa rafiki mkubwa wa baba yangu huyu ...’akasema

‘Kwahiyo alipokutongoza alikuambia kuwa usipomkubalia atakuloga au atakufanya nini?’ akaulizwa

‘Hakusema kuwa ataniloga,yeye alisema atahakikisha mimi na familia yangu tunasota, tutakikimbia kijiji,na kuwa omba omba...na mama yangu atakufa kwa kihoro...mimi niliogopa sana alipofikia kusema mama yangu atakufa kwa kihoro..hata hivyo sikumkubalia alivyotaka yeye...’akasema

‘Siku moja alikuja nyumbani, huwa ana kawaida ya kuja akifahamu kuwa mama hayupo, na ananiambia niache kazi zote tongee, na siku hiyo akanituma pombe, akanywa na kunilazimisha mimi ninywe, nilikataa kabisa,...kuna muda akanituma maji ya kunywa nikaenda kumletea, akanywa, na mimi nikaondoka kufanya kazi zangu , baadaye akaniita, nikashangaa ananimiminia maji ya kunywa na kuniambia ninywe, kweli nilikuwa na kiu, lakini niliingiwa na wasiwasi nikijua huenda kaweka kitu.

Akanishika kwa nguvu mpaka nikayanywa yale maji..yalikuwa hayana ladha nzuri, sijui ilikuwaje, maana niliona macho yote mazito, ...nikawa sina nguvu tena, akanibeba, hadi chumba cha akiba, akanilaza kitandani...hapo akaanza kulia ...’ hapo hakuweza kuendelea akaangua kilio..

Kulitulia kwa muda..mimi niligeuka kumuangalia mume wangu…unajua chuki, uso uliomwangalia ulikuwa sio wangu…lakini niliwastahi wazazi wangu nikabakia kutikisa kichwa tu

‘Niliumia sana siku hiyo, aliniumiza..alinishika kwa nguvu, na sikuwa an nguvu za kujitetea mwili wangu wote ulikuwa umelegea, lakini niliweka kuhangaika, na.....akaniumiza....sikuamini yaani baba yangu niliyemuamini kama baba yangu mzazi, alifikia hatua ya kunifanyia hivyo,mungu ndiye anayejua, ...’akatulia akilia

‘Hapo nikamkumbuka mama alivyoniusia, nikajitahidi kutimiza wajibu, nikawa namuogopa mungu, lakini baba akayaharibu yote hayo,..ningefanya nini hapo jamani, ..ina maana sisi kwa vile ni masikini wetu ndio watufanyie wanavyotaka, niliumia sana siku hiyo...nililia sana mpaka macho yakavimba…’akawa anaongea huku akiwa analia.

‘Endelea, usilie, ongea ili watu wasikie, unyama wa mtu anayejiona mwema usoni kwa watu kumbe kavaa ngozi ya kondoo..’akasema mama.

‘Alipomaliza shughuli zake, akaondoka, huku akisema nikimwambia mtu ataniua, atamuua na mama yangu...sikuweza kumwambia mama, wiki nzima nikawa kama mgonjwa, nikawa nalia,hadi mama akaja kunifuma nikilia, sikuweza kumwambia, kwa vile niliogopa kuvunja ndoa ya watu, na pia kwa vile baba alinitishia kuwa nikimwambia mama atamuua mama yangu. Nilimwambia kuwa nimemkumbuka marehemu baba yangu alivyokuwa akinipenda.

‘Tatizo mama kipindi hicho alikuwa na kazi nyingi, na kila unachomuambia anakuamini, hakupenda kunidadisi sana, akanipa pole, na kunishauri kuwa nisikumbuke sana kwani hayo ni mapenzi ya mungu, halafu akaniuliza kuwa baba ananisumbau tena,...kwa kuogopa nikamwambia hanisumbui...

‘Ikapita hiyo siku, na wiki nikijua hilo limekwisha, siku moja akiwa amelewa akanijia chumbani, ilikuwa usiku akanishika kwa nguvu,....na karibu aniue, alinikaba nikafikiria kuwa huenda alikuwa anataka kuniua, nilipigana naye sana, lakini akanizidi nguvu, baadaye akaanza kunizalilisha tena, ...’akasema

‘Kwahiyo kumbe ilikuja kwua ni tabia yake…?’ akauliza mama

‘Ndio…yaani karibu nimtapikie akwa jinsi nilivyo kuwa najisikia, harufu ya pombe na matendo yake, ...nilijua nafanyia yote hayo kwa vile mimi ni masikini, nitasema nini nieleweke kwa jamii, akafanya alichotaka akaondoka...kesho yake nikataka kumwambia mama, lakini ikashindikana, kila nilipotaka kumwambia mama, baba anakuwa karibu, na siku ikapita., Siku ikipita unajikuta umesahahu, ukikumbuka inaishia kulia.

Basi nikaona niache tu iwe kama iwavyo, akawa akifika, usiku anajifanya halali na mama, anakuja kulala chumba cha akiba, akiona kupo kimiya anakuja kwangu..nikawa najitahidi hivyo hivyo, ila sikuwa na raha, nikawa nalia sana, na kuanza kukonda, na baadaye ndio nikagundua kuwa nina miimba..sikujua kuwa ni mimba, siku hiyo nilikwenda kupima malaria, nilikuwa najisikia vibaya sana, mama akaniambia nikapime malaria, ndio docta akaniambia nina mimba...

Nilipotoka pale nikapitia duka la dawa za mifugo nikanunua sumu ya kuulia wadudu, baada ya kuuliza na kuambiwa hiyo dawa binadamu akinywa anakufa mara moja,..akilini , nilishazamiria kujiua tu, sikujiona binadamu mwenye thamani kwenye hii dunia, kwani sikuweza kuvumilia tena,nilishaona kuwa nimefanya makosa makubwa, kwanini sikumwambia mama yangu huyo wa kufikia mapema...nilijiona mzembe, ...mkosaji asiye na maana .

Akilini mwangu, nilijua hata nikimwambia mama kwa sasa hataweza kuniamini tena, ataona mimi nilikubali kirahisi , na atanichukulia mimi ni mzinzi, Malaya. Na pia sitaweza kumwambia mama, yangu mzazi, nitamuumiza sana, mama ambaye siku zote alikuwa akinionya,nisije kujiingiza kwenye uchafu wa zinaa, je nitmwambieje mama yangu, nikaona bora nikajiue tu....niondoke kwenye hii dunia, wabakie wenye pesa zao.

Nilipofika nyumbani nikaikoroga ile sumu kwenye kikombe cha plastiki, ilikuwa haiwezi kuonekana maji hayakubadilika rangi, nikaweka kwenye meza karibu na kitanda changu, nikachukua karatasi na kuandika ujumbe nikielezea kila kitu ilivyotokea...

Nilipomaliza hiyo kazi ya kuandika,... sikutaka nife kabla sijatimiza wajibu wangu, kwahiyo nikahakikisha nimefanya kazi zangu zote za nyumbani,...nilipomaliza nikaoga, nikamuomba mungu, nikaingia chumbani kwangu,nikaichukua kile kikombe, ambacho kilikuwa na maji niliyochanganya na ile sumu ....

Wazo likanijia, kuwa nisifie chumbani kwangu, nikaona sehemu nzuri ya kufia ni kule kule nilipozalilishwa , nikavua nguo zangu za kawaida, nikachukua gauni kubwa jeupe, refu, lenye mikono mirefu, nikalivaa, halafu moja kwa moja nikaenda chumba ambacho baba alianzia kunizalilisha

‘Pale nikamuomba mungu tena, na kulia, nikisononeka, na kila uchungu ulivyonizidi, ndivyo tamaa ya kujimaliza ilivyozidi kunijia, kuna muda nilikuwa nasita kufanya hivyo, nikimkumbuka mama yangu, lakini baadaye nikaona jambo jema, ni kuondoka hapa duniani, bila kupoteza muda nikanywa yale maji niliyokuwa nimechanganya na sumu...

NB: Tuendelee na huyo binti, au ..tukutane sehemu ijayo.


WAZO LA SIKU: Tuweni na ubinadamu kwa wafanyakazi wetu wa ndani, visa vingi vinaelezewa jinsi gani wafanyakazi hawa majumbani wanavyonyanyaswa au kuzalilishwa, lakini wengi wanaofanyiwa hivyo wanashindwa kuongea ukweli kwa wazazi wao kwa kuogopa , na wengi wanaofanyiwa hivyo ni watoto wa kike,wasichana….je wewe uliwahi kumuuliza mfanyakazi wako wa ndani kuhusu shida zake, je yupo salama na baba….tuwaulize kama mabinti zetu wa kuzaa.
 
Kwa kuwa wewe ni msomaji mkuu, sitaki kukupoteza mapema.
But nakuahidi utazisoma sehemu 5 za mwisho pm kabla ya watu wote.

nb. Zimebaki episode 28
Kwa siku ni episodes 15, by jumapili, kisa kitakuwa kimefikia tamati.
wow nazisubiria kwa ham aisee
 
mimini shabiki yakomuda tu nipokote kotelakinihii imenibamba zaidi, asante mkuu kwa kuongeza nimefrah haya fanya kunitumia hizo pm ngoja nikawasome kina angel nipitie kwa may lee mwisho nimalizie kwa irene
 
SEHEMU YA 98


‘Bila kupoteza muda nikanywa yale maji yaliyochanganywa na sumu , sumu ambayo ukiinywa kutokana na maelezo ya muuza dawa za mifugo:

‘Hii sumu ni hatari sana kwa watu, usije kuiweka sehemu ya ovyo, ..tafadhali, kama unataka kuua, panya,..na wanyama wakubwa wakubwa, weka kidogo kwenye maji, watakufa hapo hapo..unasikia…’alisema muuza madawa.

Tuendelee na kisa chetu

*********

Wakati binti wa kijijini, anaendelea kutoa ushahidi wake huo mimi nilikuwa napigana na dhamira yangu, maana, nilihisi chuki, hasira, na kutaka kufanya jambo, sijui hali hiyo ilikuwa ikielekezwa kwanani, kwani mimi nilishaapa kuwa yoyote atayeingilia ndoa yangu, nikimgundua, sitajali ni nani, sitasubiria polisi au kwenda kumshitaki, nitachukua hatua mimi mwenyewe, na nilishabuni njia ya kuwaadhibu watu wa namna hiyo.

Sasa huyu binti wa watu wa watu, ndio kaingilia ndoa yangu lakini sio kwa kupenda, je na yeye anastahiki adhabu hiyo…hapana

Hapa mkosaji ni mume wangu, yeye ndiye atabeba madmabi yote hayo, na sijui nitampatia adhabu gani ili nafsi yangu iridhike..Kilichoniuma zaidi ni kuwa mambo hayo yalifanyika ndani ya nyumba yangu, mimi nikiwepo, mimi ambaye nilibeba dhamana ya huyo binti, … japokuwa sikufahamu hilo..ila kwa namna nyingine nalaumiwa mimi

‘Nilimualezea mama lakini alionekana hakujali, yeye alijali kazi zake, ..’ nikauli ya kunishitakia.

Yule binti mtoa ushahidi akawa anaendelea kutoa maelezo yake;

‘Nilikunywa yale maji ambayo nilikuwa nafahamu kuwa yana sumu, kwanza nikapiga fundo moja, nikaona yananyweka, nikaweka la pili, na baadaye nikayanywa yote hadi tone la mwisho halafu nikaweka kile kikombe, juu ya karatasi niliyokwisha iandika, na mimi taratibu nikapanda juu ya kile kitanda, kilichonitesa, nikalala nikiangalia juu, nikisubiri kufa, dakika tano zikapita, kumi zikapita, robo saa,sikuoni hata dalili zozote za kufa, sikusikia maumivu ya tumbo, tofauti na maelezo ya muuza duka..

‘Ina maana hii dawa ime-ekisipaya nini, ‘nikajiuliza,akilini nikapanga nichukue ile dawa iliyobakia, ambayo niliicha chumbani kwangu,nikataka niinuke nienda kule lipo, niikoroge ninywe hata nikizidi kipimo, haijalishi..ninachotaka mimi ni kufa tu..

Nikawa sasa nataka kuinuka, mara mlango ukagongwa,...nikashituka,

‘Labda ni malaika wa mauti anakuja kihivyo…’nikajisema moyoni, huku bado nimelala pale pale..kukawa kimia, nikainua kichwa, na wakati huo mlango ukawa umegongwa tena.

Hapo sasa nikajua ile dawa ni ya uwongo, huenda muuza duka, aliafahamu dhamira yangu akanipa dawa ambayo sio…nikajiinua kidogo, mwili ulikuwa hauna nguvu, mawazo,…nikawaza huenda ndio hiyo dawa inafanya kazi,mimi nikatulia..

‘Mlango ulivyoendelea kugongwa tena, nikahisi ni baba wa nyumbani kaja,...lakini yeye hana tabia ya kugonga mlango, huwa akija anaingia moja kwa moja hajali kuwa mimi nipo katika hali gani,...

‘Huyo atakuwa ni mtu mwingine , …atakuwa nani muda kama huu..’nikajiuliza
Hata hivyo sikutaka kusimama kusimama, nilikuwa bado nina imani kuwa hiyo dawa itafanya kazi, labda inachukua muda, na nilitaka mimi nifie hapo hapo kitandani

‘Hodi hapa…’ilikuwa sauti ngeni…lakini dio ngeni sana,…hata hivyo akili yangu ilishakwenda kwa wafu, sikutaka kuifikiria dunia, kwahiyo nikawa kama nimedharau, ili huyomgongaji, akate tamaa aondoke zake, na mimi niendelee na zoezi langu.

Nikawa nimefumba macho nikiwaza kuwa huenda dawa ndivyo inafanya kazi taratibu kwahiyo sasa naelekea kukata roho, lakini kwanini tumbo haliumu, mara nikahsi mlango umefunguliwa..sikfumbua macho kwa haraka

Na mara nikahisi mtu akikaribia pale kitandani nilipolala, nikaanza kufungua macho taratibu,, na sura niliyoiona mbele yangu, ikanifanya nifungue macho kwa haraka, na kujikunyata , nikiogopa, na kuuliza kwa haraka;

‘Wewe umefuata nini huku chumbani?’ nikauliza na yule mtu akasema kwa sauti ya pole pole, kama mwalimu anayefundisha watoto wadogo;

‘Unafahamu nilikuwa nakuamini sana,kuwa wewe ni binti jasiri...’yule mtu akaniambia

‘Toka humu ndani..’nikasema

‘Umenisikitisha sana,, ....’akasema

Hapo, nilikuwa nimejikunyata kama mtu anayejikinga asipatwe na baya, nikainuka kwa haraka pale kitandani na kukaa, nikanyosha lile gauni vizuri, na kumwangalia huyo mtu aliyeingia, alikuwa mkononi kashikilia kikombe, kinachofanana na kile kile nilichokuwa nimeweka sumu. Vikombe kama hivyo vipo vingi hapo nyumbani. Nikamuuliza

‘Unataka kunifanya nini, kwanini unanifuata huku chumbani?’ nikamuuliza nikiwa nimeshamuweka kwenye kundi hilo hilo la watu wabaya, ....

‘Hahaha, unafikiri nitakufanya nini, mimi sina tabia hiyo, tabia yangu ni nyingine kabisa, pesa…hiyo ndiotabia yangu…’akasema

‘Sasa umefuata nini huku ndani…?’ nikauliza

‘Nilikuona ukitaka kujiua..’akasema

‘Uliniona…!!?’ nikauliza kwa mshangao
‘Ndio nilikuona..nikiwa ofisini kwangu ikanibidi nichukue pikipiki kwa haraka kuja hapa kukuokoa,...’akasema

‘Kwanini umefanya hivyo…?’ nikamuuliza

‘Kwasababu sitaki wewe ufe, unahitajika sana ..kwenye mipango yangu, na nikuambie kitu, wewe hutakiwi kujiua, nafahamu yote yaliyotokea dhidi yako, na nilikuwa natafuta njia za kukusaidia, lakini imekuwa vigumu kukupata, na kila nikija hapa unanikwepa, unaniogopa...kama vile mimi ni mtu mbaya, mimi sio mtu mbaya, nakujali sana’akasema huyo mtu

‘Umejuaje hayo wakati sijamwambia mtu dhamira yangu?’ nikamuuliza

‘Mimi macho yangu yanaona mbali, kila wanachokifanya watu kwenye hii nyumba mimi nawaona, mimi nakupenda sana, na nilishakuambia awali kuwa mimi nakupenda sana, unakumbuka…’akasema

‘Sikumbuki mimi, wanaosema hivyo wote nawaogopa, hawana ukweli..’nikasema

‘Mimi sikupendi kwa nia hiyo unayoifikiria wewe, …mimi nakupenda kwa moyo, na kukujali, .. na unakumbuka nilikuambia mimi ningeliweza kukusaidia kwa kila hali, nilikuomba uwe rafiki yangu wa karibu, ukawa unamjali sana huyo unayemuita baba yako, sasa kipo wapi...’akasema

‘Uliingije humu ndani na hicho kikombe kina nini,?’ nikamuuliza

‘Hilo sio muhimu sana, ila usijaribu tena kutumia hii sumu, usijaribu tena kujiua,kwanini ujiue wakati aliyekufanya hivyo, yupo hai, anastarehe, na hata ukifa yeye, hatapata shida, utazika na wote watakusahau…’akasema

‘Mimi sijali,..i bora nife tu….’nikasema

‘Sikiliza nikufumbue macho na masikio, kwanini unajipa shida wakati keshakutengenezea njia ya kuondokana na huo umasikini ulio nao.’akasema na mimi hapo nikashituka, japokuwa bado sijamuelewa.

‘Nielewe vyema…mimi nataka kukusaidia jambo, … mimi nitakufundisha kila kitu, cha kuweza kukusaidia na kusahau umasikini wako…na kuanzia leo jihesabu kuwa wewe sasa ni tajiri..kama utakubaliana na mimi.’akaniambia huku akinusa ile dawa kwenye kile kikombe.

‘Hii ni sumu mbaya sana, kama ungekunywa, ungeharibika matumbo yote, na ungekufa kwa machungu makali, sana, kwanini unataka kujitesa kiasi hicho?’ akaniuliza

‘Kuna haja gani ya kuishi baada ya haya yote..’nikasema

‘Hayo yote uliyoyaandika kwenye hiyo karatasi, niliyasoma, ni ujumbe tu usio na maana na ambao wangeusoma, wangelikuona wewe ni mjinga tu, wangekuzika, wakakusahau, usiwe mjinga kiasi hicho…’akasema

Hapo ndio nikagundua kuwa kumbe ni yeye alibadili kikombe nilichokuwa nimeweka sumu na kuweka kingine kisichokuwa na sumu, moyoni nikajiuliza huyu mtu anadhamira gani kwangu.

‘Ujue,...mimi nilishaanza kuwafuatilia wote kwenye hii nyumba, nayafahamu yote yaliyotokea, ...hebu angalai hii hapa...’akatoa kitu kama simu, lakini kubwa, kama komputa ndogo, akaiwasha, halafu akawa anafanya kitu kwenye hicho kidude, akainama kunionyesha

‘Unaona yote yaliyotendeka hapa ndani nayafahamu, ...’akasema huku akinionyesha, tukio mojawapo wakati baba huyo hapo akinibaka kwa nguvu, na akaonyesha na jingine …sikutaka hata kuangalia.

‘Wewe ni mchawi, umeyapataje hayo..’nikasema.

‘Hahaha, lakini mimi sio mchawi wa kiafrika ni kisasa, wa kidhungu,…hahaha..’akacheka huku akizima kile kidude chake kama simu.

‘Sasa sikiliza fuata yote nitakayokuambia, ili upate haki zako, ...sasa ninakupa mbinu za kuwa tajiri, kama kweli utayafuata hayo nitakayokuambia,... kwa hivi sasa, akija baba yako mwambie una mimba yake, usimfiche kabisa, kama ulivyoeleza kwenye huo ujumbe kuwa una mimba yake, umweleze hivyo hivyo, na baada ya hapo ..’akatulia

‘Sitaki kumuambia…ataniua…’nikasema

‘Hwezi kukuua, sikiliza kwa makini maagizo yangu, sasa hivi usiogope kabisa, jenga ujasiri,..sasa ni muda wa kutengeneza pesa, …ni lazima unamdai pesa, tena pesa nyingi...’akasema na mimi nikamtolea macho ya kushangaa.

‘Usishangae, hawa watu wana pesa nyingi sana, ndio zinawapa kiburi cha kufanya hayo waliyokuanyia…’akasema

‘Kwa vipi…?’ nikauliza

‘Kwa vipi ni hivyo nitakavyokuelekeza…’.akasema na ndio akaanza kunielezea kwa kirefu jinsi gani niongee na baba wa hiyo nyumba akija...aliyoniambai niliona kama ni mambo yasiyowezekana, lakini yeye akanipa moyo kuwa hayo yanawezekana, maana baba wa hiyo nyumba, anamfahamu vyema na udhaifu wake, akiambiwa hivyo ni lazima ataogopa...’akaniambia

‘Mhh,..’nikaguna tu hivyo, sikumuamini

‘Baba yako huyo udhaifu wake upo kwa mkewe, fanya kama nilivyokuagiza…’akasema

Mimi sikuwa na chohote cha kusema au kukataa, maana yale niliyoyaona kwenye hiyo simu yake,yalinifanya nimuogope zaidi huyo mtu, na nilifahamu nisipofanya hayo anayoyataka, huenda ataweza kunifanyia lolote, na kuzionyesha kwa watu, hizo picha chafu na mimi nitazalilika zaidi, na watu huenda hawataniamini, kwangu mimi hayo yalikuwa ni aibu tupu, nikawa sina jinsi nikamkubalia hayo aliyonielekeza, na mwishoni akaniambia.

‘Kwanza kabisa unamdai shilingi Milioni kumi..’akasem

‘Mungu wangu…’nikasema hivyo

‘Hahaha, milioni kuwa kwa hawa watu ni kitu kidogo tu, hasa akiona hatari kaam hiyo, …unaona eeh, hebu fikiria ukiwa na pesa kama hizo utafanyia nini, utakuwa tajiri, kwa dhambi zake…’akasema

‘Na huo utakuwa ni mwanzo tu,...maana kwa sasa una ushahidi wa kumfanya lolote unalolitaka, ukizipata hizo pesa, nusu yangu na nusu yako..unanielewa...baada ya hapo nitakuelekeza namna nyingine ya kuzipata hizo pesa nyingine kila mwezi,..na atazitoa tu hana ujanja, vinginevyo….’akaniambia na mimi nikamuitikia kwa kicha kukubali,na hakukaa sana akaondoka zake...

********a
‘Milioni kumi…’nikajikuta nikisema hivyo, maana ni kitu ambacho sijawahi kukifikiria kichwani, kupata pesa nyingi kiasi hicho, hapo hapo ibilisi la pesa likaanza kuningiia,
‘Milioni kumi…kweli..’nikawa nasema hivyo tu

Mimi nikatoka pale chumbani na kwenda kuendelea na shughuli nyingine nikimsubiria baba mwenye nyumba aje.., nilifahamu kuwa muda kama huo atakuwa anarudi, na kweli kabla sijatulia, mlango ukafungulia na mwenye nyumba akaingia, akiimba nyimbo zake za kilevi...

***********

Kama kawaida yake, alikuwa kalewa, na siku hizi alikuwa kazidisha kweli kweli, utafikiri sio yeye, niliyemfahamu kipindi cha mwanzoni, alikuwa kalewa, anapepesuka, na moja kwa moja akaingia kwenye chumba hicho anachopumzikia, na nilijua baada ya muda ataniita, mimi nilikuwa nimeshatoka nipo nje, na nikasikia akiniita,

Nikajivunga kidogo, akaniita sasa kwa ukali, na hapo ndio taratibu nikaenda huko chumbani, nikijua ni nini kitafuata, …nikaingia ndani na kumkuta kavua nguo kabakia na chupi tu, yaani hana hata aibu mbele yangu, akaniambia niende tulale naye, nikakataa..

‘Unaleta kiburi eeeh, kwanza leo sikutaki, nilikuwa nakujaribu tu, nimechoka, nimeshastarehe huko nilipotoka, na watu wanaofahamu mapenzi, sio wewe mpaka tushikane miereka, mmh, ni shida tu, japokuwa kuna raha yake…’akasema

‘Lakini..eeh, ,..lakini-kumbuka kuwa nikikuambia kitu, ukanikatalia ujue kuwa mama yako nitam-maliza,.yule mama yako masikini masikini, eeh, nita-mu-maliza,…kwanza nilishampigia simu kuwa wewe siku hizi una kiburi, ..akalia sana..anasema hajakufundisha hivyo….’akasema kilevi

Sikutaka aendele kuninyanyasa kwa kupitia kwa mama yangu, nikasema kwa kiburi;

‘Fanya unalota, sasa hivi siogopi, maana mimi sina maana tena kwenye hii dunia..ulichonifanyia, kinatosha, umenizalilisha vya kutosha..kunizalilisha huku ni sawa na kuizalilisha familia yangu…’nikasema

Kwanza akashangaa…hakutegemea mimi kuongea vile, akanikodolea macho, na mimi sikumjalia nikaendelea kusema

‘Na nafahamu unatufanyia hivyo kwa vile sisi hatuna maana kwenu…ni masikini, lakini kumbuka na wewe ulipotoka…na sisi hatukuomba tuwe hivyo, mungu anayaona haya yote…’nikasema na yeye akasimama, na kutaka kuja kunishika kwa nguvu kama kawaida yake, mimi nikamsukumiza kwa nguvu zote, akadondoka chini, alikuwa kalewa, hakuwa na balansi, ila akikukamata ana nguvu za ajabu, sikupenda aniwahi kunikamata, nikamwambia;

‘Mimi nina mimba yako..’nikasema hivyo

Hiyo kauli ilimfanya ashtuke,..na haraka akasimama juu, na ikawa kama pombe zote zimemuishia, akatikisa kichwa na kupangusa macho akaniuliza

‘Unasema nini wewe...?’ akaniuliza

‘Nina mimba yako,..umenibaka na sasa umenipa mimba…je ulivyokuwa ukinibaka , ulitegemea nini, sasa nina mimba yako, nilikwenda kupima leo mchana, nikaambiwa nina mimba, na mimi simjui mwanaume mwingine zaidi yako wewe, ..wewe ndiye uliyenianza, na sasa nina mimba yako, nitamwambia mama akija..’nikamwambia.

‘Nitakuua,..unasema nini wewe Malaya, , kwanza toka kwenye hiinyumba haraka, sitaki hata kukuona, toka kimbia na potelea mbali Malaya mkubwa wewe....’akasema

‘Mimi nitaondoka tu, sina haja ya kukaa hapa, ...’nikasema

‘Sawa, sasa hivi fungasha, ..ondoka, ..vinginevyo nitakuua…’akasema

‘Nitaondoka …lakini kwa masharti, nataka pesa za kujenga nyumba kama ulivyoniahidi, pesa za kutosha, nyumba nzuri kule kijijini, kwa sasa utanipa kiasi cha kuanzia, nataka pesa za kunitosha kuilea hii mimba yako, unawajibika nayo, , ...’nikasema

‘Nini…! ‘akasema hivyo kwanza

‘Ndio hivyo, ukifanya hivyo ndio nitaondoka humu ndani, mbali kabisa na nyie, la sivyo…’nikasema

‘Wewe Malaya mkubwa, ina maana unanisingizia kuwa nimekupa mimba ili nikupe pesa, pesa hupati, na humu ndani utaondoka...’akaniambia huku akinitolea jicho.

Nikachukua ile karatasi niliyopima hospitalini, na kuna picha aliniachia huyo jamaa ambaye alikuwa na kumbukumbu zote za hapo nyumbani, na matendo aliyonifanyia, nikampa
‘Ni nini hiki…?’ akauliza

‘Angalia mwenyewe ushahidi wa madhambi yako…’nikasema

Akawa anaisoma ile karatasi ya docta, na alipofikia kuziangalia zile picha akatupa chini, kwa hasira, akisema;

‘Nitakuua, unasikia, ninaapa nitakuua,...ni nani kakusaidia kuyafanya haya, ..’akasema akiangalia ile picha pale chini, ilikuwa imekaa vyema inaonyesha lichokuwa akinifanyia.

Akaipiga teke lakini hakigeuka, akasema

‘Kwa hili mimi,, ...nitakuua, usipoondoka kwenye hii nyumba, usiku wa leo nitahakikisha unakuwa maiti..’akaniambia huku akitaka kuinama kuchukua ile picha na ile karatasi ya vipimo nilivyompa, sasa akawa anaviangalia huku katoa macho, kama kaona kitu cha kutisha, mimi nikamwambia;

‘Mimi siogopi kufa, nilishajiandaa kufa, lakini bahati nzuri kuna mtu kaja kaniokoa, na yupo tayari kunisaidia hili jambo, ikibidi tutalipeleka mahakamani, lakini kwanza ni lazima nimfahamishe mama..’nikamwambia

‘Ni nani huyo aliyekusaidia?’ akaniuliza kwa hasira, sasa akionyesha wasiwasi.

‘Haina haja ya kumfahamu kwa sasa…, ninachotaka ni hizo pesa kwa haraka, ili niondoke hapa kabla mama hajarudi,na ikitokea akaja na kunikuta hapa nyumbani nitamwambia yote na ushahidi wote nitamuonyesha...’nikamwambia

‘Ohoooo, kumbee, …sikujua, wewe ndio janja yako, ndio tabia yako, eeh,..kwanza ni nani huyu..aliyekusaidia kufanya huu uchafu.’akasema kwa hasira, akijua labda nitatishika, hakujua kuwa sasa nimepata ujasiri niliokuwa sina kabisa.

‘Unapoteza muda, nataka kuondoka...sikuwa na tabia chafu, kama unavyosema wewe, uchafu huu, ulinianzishia mimi, na sikuwa na wazo kama hilo kabisa, ila kutakana na haya sina jinsi, na sitarudi nyuma, ….’nikamwambia

‘Wewe ondoka, nitakutumia hizo pesa,kwasasa sina pesa za kukupa ...’akasema sasa akiwa anaongea sauti ya kawaida sio kama ile ya ulevi, naona alishahisi hatari.

‘Mimi sitoi mguu wangu humu ndani, nizipate hizo pesa bila kupungu ahata senti moja,…kama nilivyokuambia sipo peke yangu kwa hili, huyo aliyenisaidia ana kila kitu zaidi ya hiki, ana picha ya video ukinibaka,..kila kitu kipo wazi, ukinua mimi yeye atakuja kwakokama mbogo aliyejeruhiwa..’nikasema

‘Shilingi ngapi, unataka wewe Malaya tu, nia yako si pesa nitakupa uondoke humu ndani kwangu...?’ akauniuliza huku akinitolea macho ya kunitisha, lakini niliona ajabu, sikuwa naogopa tena, utafikiri kuna nguvu za ajabu ziliniingia.

‘Milioni kumi...’nikasema, na aliposikia hicho kiasi akashituka, karibu adondoke, na kuniangalia kwa macho ya chuki, akasema;

‘Ni nani huyo kakufundisha uchafu huo, milioni kumi, wewe unaota, pesa zote zote hizo unazitaka wewe za nini wewe masikini?’ akaniuliza

‘Ni mtu wa usalama wa taifa, nilimwambia akanifundisha jinsi gani ya kuwakomoa watu kama nyie..hata kama ni masikini , lakini ni bora ya uamsikini wangu kuliko utajiri wenu wa kinyama, wenye tabia chafu ya unyanyasaji, ubakaji,....wizi na dhuluma..’nikamwambia

‘Unasema usalama wa taifa...ni nani huyo?’ akauliza sasa akinywea.

‘Utanipa hizo pesa au niendelee na shughuli zangu nimsubiri mama, aje, nimwambia hivyo, na sasa nikamuona hana jinsi, akabadilika akawa mnyonge, akawa yule baba niliyemfahamu awali

‘Hebu subiri nifikirie...’akasema na pombe zote zikaisha, na mara akachukua simu na kuanza kuongea na watu wake kama watatu, kila mmoja alikuwa akimuomba pesa, milioni tatu tatu, na wa mwisho milioni moja, akawaambia wampe mdogo wake, atazileta hapo nyumba

**********


Mdogo wake namfahamu sana, huwa yeye hakai sana hapo nyumbani, na akija huwa na chumba chake nje ya nyumba kubwa, kwahiyo mara nyingi hafahamu kinachoendelea humo ndani, lakini mara nyingi ndiye anayemtuma mambo yake..na wakati mwingine wanakwenda kulewa pamoja, akizidiwa ni kazi ya mdogo wake kumrudisha nyumbani.

Nikaenda chumbani kwangu nikajiandaa, na huku nikiwa na tahadhari, kama nilivyoambiwa na huyo mtu aliyenifundisha hayo yote, maana niliambiwa kuwa nikimwambia hivyo huyo baba anaweza akaniua, kwahiyo nikawa nina kisu kikali tayari kwa kujihami, hakupita muda nikasikia pikipiki nje,...

Nikachungulia nje, nikamuona mdogo wa huyo baba akiwa na pikipiki, akaingia ndani nikasikia wakiongea na kaka yake kwa muda, baadaye nikasikia mlango wa chumbani kwangu ukigongwa, alikuwa huyo mdogo wa baba mbakaji, akaniita nitoke pale chumbani, nikatoka , akaniambia kuwa kaka yake kasema nichukue kila kitu changu , yeye atanichukue na pikipiki, na kunipeleka sehemu nitakapolala hadi kesho,..

‘Yeye yupo wapi?’ nikamuuliza

‘Yupo ndani kalala, kasema kila kitu kipo kwenye huu mfuko, akanipa mfuko, nikaangalia ndani na kukuta mabulungutu ya pesa, nikayahesabu moja moja, hadi yakatimia idadi , kwa yalivyofungwa, sikuweza kuhesabu moja moja, lakini kwa bunda moja moja, ambalo liliandikwa juu, milioni moja, nilifahamu kuwa zimefika milioni kumi, nikazichukua na kuziweka kwenye mkoba wangu wa safari, nilizifunga vizuru sana.

‘Twende, kaka kasema hana haja ya kuonana na wewe...’akaniambia,na mimi nikafanya kama alivyosema huyo mdogo wake, tukaondoka naye kwa pikipiki , hadi sehemu aliyoniambia kuwa nitalala hapo hadi kesho.

‘Mimi nakwenda kukata tiketi, kaka kaniambia unaondoka kesho asubuhi na mapema, sijui kuna nini kinachoendelea kati yenu, sitaki kufahamu, ila nakuonya ,kama kuna mtu anayekudanganya ujue umajipalia mkaa, hizo pesa unaweza usionje hata utamu wake, ni pesa haramu hizo,..na kaka kakasirika kweli, kwa jinsi ninavyomuona anaweza hata kukua,...’akaniambia

‘Mimi sijali kukasirika kwake, alichonifanyia mimi ni dhaidi ya hizo pesa,..., nimeshamuambia kwa hivi sasa sijali kufa, ameshaniua moyoni, kilichobakia hapa ni kiwiliwili tu,...’nikamwambia, na huyo ndugu yake akaonyesha kushituka kidogo, baadae akaondoka zake baada ya kuhakikisha nimekula, na pesa za matumizi.

‘Mimi sitakuja leo, tutaonana asubuhi sana usitoke nje,...’akaniambia

‘Mimi sitoki nje niende wapi sasa nsubiria aje kunai…na kama nikitaka kutoka nje, sitakaa sana, nitarudi humu humu,..na zaidi kama nikiona vipi nitarudi kule kule nionane na mama, mwenye nyumba’nikamwambia.

‘Wewe..usirudi tena kule kuonana na shemji yangu, kaka kasema usirudi huko kabisa, wala usije kuonana na huyo mama mwenye nyumba, mimi nakuamini, ndio maana nakuacha peke yako, la sivyo, niliambiwa nikuchunge hadi hapo utakapoondoka kesho, niahidi kuwa hutatoka nje, mpaka kesho’akaniambia.

‘Niende wapi, siendi mahali, ..nakusubiri wewe na mkileta ujanja nimeshampigia huyo mtu wa usalama wa taifa, ananifuatilia kila ninapokwenda...’nikamwambia

‘Usalama wa taifa..ni nani huyo !! ..ooh kumbe ndio maana eeh, kuna mtu nimemuona akitufuatilia nyuma, toka tunatoka kule nyumbani, na nahisi yupo hapo nje,..’akasema

‘Habari ndio hiyo...’nikamwambia na hapo hapo akachukua simu na kumpigia simu kaka yake,akimwambia kweli kuna mtu ametufuatilia kwa pikipiki, na huenda ni usalama wa taifa. Mimi sikujua kuwa kuna mtu alikuwa akitufuatilia, na siwezi kujua ni nani, labda ni yule jamaa aliyenipa hizo mbinu, ambaye kwenye zile pesa, alitaka nimpe nusu.

Moyoni nikasema huyu mtu simpi hata senti moja, kwa kazi gani aliyonifanyia...na mimi tamaa za pesa zikawa zimeniingia.

Alipoondoka huyo mdogo mtu, nikatoka pale ndani na kuangalia huku na kule, sikuona mtu, haraka nikachukua begi langu, kwa kupitia mlango wa nyuma, nikatoka,...na kuingia mitaani, nikachukua boda boda hadi sehemu nyingine, nikatafuta nyumba ya wageni nikalipia kwa siku moja, nikalala huko, na hiyo ilikuwa salama yangu. Nilikuja kupata taarifa kwa mtu anayenifahamu, ambaye aliniona nikifika pale, mtu huyo aliniambia kuwa kwenye ile nyumba, usiku kulitokea ujambazi,

Aliniambia kuwa kuna kundi la watu walifika wakinitafuta mimi,lakini waliponikosa, ikabidi wawapore watu pesa zao, ...aliniambia huyo jamaa ambaye nilikuja kukutana naye huko kijijini, baada ya siku nyingi.

Asubuni ya siku ile, niliwahi kituo cha Ubungo, nikampigia simu huyo mdogo wa baba..alishangaa kunisikia nikiongea

‘Ulijua nimekufa sio…’nikasema

‘Ha-hapana, ni kwa vile umenipigia simu, nitakuja kukukatia tiketi…’akasema

‘Kwahiyo kumbe ulikuwa hujakata tiketi…’akasema

‘Niliwauliza hapo ubungo wakasema tiketi inakatwa siku hiyo hiyo…’akasema

‘Sawa, sasa mim nitakata tiketi mwenyewe haina haja yaw ewe kufika huku tena, nitaondoka usiwe na wasiwasi na mimi, mwambie kaka yako, kuwa nikifika nitawasiliana naye…’nikasema

‘Usikate wewe mwenyewe nitakuja kukukatia tiketi mimi, kaka alisema nihakikishe kuwa umeondoka…’akasema

‘Uhakikishe nimeondoka wakati alitaka kuniua..au una njama nyingine tena za kuja kunimalizia, ukija safari nitakuitia mwizi, unasikia usije kabisa hapa kituoni..’nikamwambia, na kukata simu

************



Ni kweli, nilinuna tiketi, ya usafiri wa kwenda huko kwetu, na mara kwa mara huyo mdogo wa baba, akawa ananipigia simu, lakini nikawa sipokei, hadi tunaondoka, sikuonana naye...’

Alipofika hapo akatulia na kusubiri, kama ataulizwa swali na mwenyekiti akamuuliza.

‘Huyo mtu aliyeweza kuchukua picha za tukio la hapo ndani, ulikuwa na mazoea naye kabla?’ akauliza mwenyekiti

‘Alikuwa mara kwa mara akija hapo nyumbani kabla, lakini hakuwa akionana na mama wala baba, na kila mara akija alikuwa akiniuliza mambo ya hapo nyumbani, nilifahamu kuwa ni rafiki wa baba wa hiyo nyumba, kwani kuna siku nyingine walikuwa wakija wote,

Alijaribu kunizoea sana, akisema yeye ni ndugu yake baba, kwa baba mwingine, na anamsaidia baba kwenye shughuli zake za biashara, nilishangaa ni kwanini baadae alikuja kumfanyia hivyo..mimi sikutaka hata kufahamu zaidi

‘Ila nakumbuka kuna siku moja alikuja, akanituma kumchukulia maji, na niliporudi akawa hayupo pale nilipomuacha, baadaye akatokea, nilimuona kabisa akitokea chumba anacholala, huyo baba aliyenitenda hayo machafu. Chumba cha wageni, nilitaka nimsemee kwa mama, lakini nikasahau

‘Unafikiri alikwenda kufanya nini?’ akaulizwa

‘Kwa kipindi kile sikujua alichokwenda kufanya, lakini alikuja kuniambia kuwa kwenye ile nyumba,a likuwa kaweka vyombo vya kunasa matukio yote ya humo ndani, kwahiyo alikuwa akifahamu kila kitu kinachoendelea humo ndani..na aliniambia hayo alipokuja huko kijijini, kumbe ni mtu wa huko huko kijijini,..na anafahamika sana, mimi sikuwa namfahamu kabla...’akasema.

‘Kwahiyo mkajenga urafiki wa karibu kutokana na hilo tukio…?’ akaulizwa

‘Sikujenga urafiki naye kihivyo, ni urafiki tu wa hilo tukio, na ilibidi anielekeze jinsi gani ya kuzipata hizo pesa za kila mwezi,…na akija hapo kijijini anakuja kudai pesa zake, nikawa simpi kama anavyotaka yeye, na ilifikia kipindi alitishia kuwa atanifanyia kitu kibaya, kweli namuogopa, lakini moyo wangu ukajaa usugu fulani, sikujali kufa tena.

Baada ya kuondoka na zile milioni kumi, alinifundisha kuwa kila mara nitakuwa nadai milioni mbili mbili, moja yake, kuna muda alikuwa anapandisha kiwango kuwa nimwambie huyo baba aitumie milioni tatu, hata tano,.akijua huyo baba ana pesa, kama hana anasema tudi milioni mbili zisishuke hapo

‘Nikawa namuuliza yeye anataka pesa za nini, wakati hana baya lolote alilofanyiwa, akasema ni gharama ya vyombo vya kunasa matukio yote kwenye hiyo nyumba.

‘Vyombo hivyo vinauzwa pesa nyingi, nataka nipate hizo pesa kuwalipa watu walioniazima hivyo vyombo, kwasababu asingeliweza kuvinunua, kwani vinauzwa pesa nyingi, kwahiyo alikuwa akiazima kwa muda fulani...’akasema

‘Je ulipofika huko kijijini ilikuwaje?’ akaulizwa

‘Sikuenda moja kwa moja kwa mama, nilikwenda kijiji cha jirani, huko nikanunu shamba na kujenga nyumba yangu nzuri, na ilipokamilika ndio nikaenda kumchukua mama...’akasema

‘Ehe, endelea…’akaambiwa

‘Kiukweli mama hakuamini, na sikutaka kabisa kumwambia mimi kilichotokea, alisikitika tu kuwa nimezaa bila kuwa na mume..nilikaa na mama yangu mpaka nikajifungua, nikamlea mtoto wangu huku nikiendelea kudai pesa mwanzoni alikuwa akinitumia,..’hapo akatulia kidogo

‘Lakini baadaye akawa hafanyi hivyo, na siku zikawa zinakwenda, nikaona maisha yanakuwa magumu, kuhangaika na mtoto mgongoni, maji, kulima, na biashara, nikaona ni bora nije nimuone...aliyenifanya hivi, nijue ni nini hatima ya mtoto wangu, kwani yule mtu aliyekuwa akinisaidia alikuja kufariki.....’akasema huyo binti huku akimwangalia mume wangu kwa jicho baya, na mume wangu alikuwa kainama tu hainui kichwa.

‘Naona umeongea vya kutosha, ushahidi tulioutaka tumeupata je wakili mtetezi una swali dhidi ya huyo shahidi, ?’ akaulizwa.

********

‘Mteja wangu anakana yote aliyoyaongea huyo binti, je kama alifanyiwa hivyo, kwanini hakushitaki, hii inaonyesha kuwa huyo binti ana michezo yake ya namna hiyo, kuwarubuni wanaume ili aje kuwadai pesa, kwasababu mtu hivi hivi, asingeliweza kufanya jambo kubwa kama hilo, adai shilingi milioni kumi, mtoto wa kijijini...!’akasema wakili kwa mshangao.

‘Ushahidi ninao, kuna kanda alinipa huyo jamaa aliyenisaidia kama mnataka ninaweza kuwaonyesha..’akasema huyo binti, na wakili akanong’onezana na mteja wake, na wakili akasema;

‘Unasema ulipewa mimba, huyo mtoto yupo wapi?’ akaulizwa

‘Hilo lingelifuata baadaye, kwanza tulitaka kauli ya mlalamikiwa je, ni kweli hayo anayoyaongea huyo binti, kama si kweli, tutaonyesha hiyo kanda, inavyoosha anavyombaka huyu binti, ....ionyeshe tukio zima, ni ya aibu, lakini kwa ushaidi tutaionyesha,...kama anataka,..’akasema mwenyekiti.

‘Tunataka kumuona mtoto kwanza...’akasema wakili.

‘Haaah, ina maana bado tu mume wa familia hujaona umefanya kosa ukatubu, sawa, sisi tutafanya utakavyo, lakini hatutasita kuonyesha hiyo video, baada ya hapo…’akasema mama.

‘Sawa…’akasema wakili, mume wangu hakutaka hata kuinua uso wake, alikuwa kainama tu.

‘Sasa kabla ya kuonyeshwa huyo mtoto, kama anavyotaka …’samahani kidogo mzungumzaji, mimi nataka hili jambo tuliendeshe kisheria zaidi, kama mahakamani,..kuonyesha mtoto tutafanya, lakini mimi ningelipenda shahidi mmojawapo aje hapo..’akasema mwenyekiti

‘Sawa mwenyekiti,uonavyo maana mimi hapa akili haipo sawa..’nikasema

‘Mimi ningependa kumuita shahidi mtaalamu anayekubalika kisheria, yeye aje kutoa ushahidi wa kitaalamu zaidi, ili kumuonyesha mume wako kuwa sisi tunamfahamu zaidi anavyojifahamu yaye, na sisi sio lengo letu kuvunja ndoa yenu,lakini tunamfahamu kuwa hataweza kuishi na watu wastaarabu, kazoe vya kunyonga,,lakini siwezi kuhukumu hapa, hilo ni juu ya kikao baadae...’akasema mwenyekiti.

‘Shahidi huyo ni docta…’akasema mwenyekiti

Rafiki wa mume wangu alikuwa kama kashitukiziwa, na alionekana kubabaika, pale alipotajwa yeye kuwa anahitajika kutoa ushahidi.

**********

‘Ndugu docta samahani kidogo, nafahamu hukutarajia hili, lakini inabidi uwajibike, wewe ni docta, na huyo binti unamfahamu kwasababu alikuwa jirani yako, tunataka ukweli wako, utuambie je wakati unafika hapo nyumbani kwao kwa jirani yako, uliyaonaje maisha ya hapo ?’ akaulizwa

‘Mh,h, yalikuwa ya kawaida, tu, sikuona tofauti yoyote...’akasema

‘Huyo mlalamikiwa hakuwahi kukuambia lolote kuhusu huyo binti?’ akaulizwa

‘Mhh, kama lipi, ..ndio kuna ya hapa na pale, kuwa huyo binti ana adabu mchapakazi, na mambo kama hayo, baadaye akasema ametoroka, lakini sio mambo kama alivyoyaongea huyo binti..’akasema

‘Hukuweza kuhisi lolote katika tabia za rafiki yako dhidi ya huyo binti?’ akaulizwa

‘Kwakweli hapana, kama yalikuwepo basi hayo aliyoyaelezea huyo binti yalifanyika kwa siri sana, mimi sikuwahi kuyashuhudia...’akasema

‘Huyu binti alikuwa anatibiwa kwenye hospitali yako mara kwa mara, kama sikosei, je aliwahi kuja kwako ukampima na kumwambia ana mimba?’ akaulizwa

Wakili wa mtetezi akalipinga hilo swali, na kusema doctari analazimishwa kusema jambo, hakupewa nafasi ya kuelezea yeye mwenyewe...’akasema

‘Niambie docta huyo binti aliwahi kuja kwako kutibiwa kabla hajatoweka hapa Dar?’ akaulizwa

‘Ni kweli kwa mara ya mwisho kuja kwangu, alifika akisema anajisikia vibaya, na alitaka kupima malaria, na alivyojielezea, kama docta nikahisi mbali zaidi, nikamwambia inabidi tumpime mkojo, damu na choo, na hakupinga, tukachukua vipimo vyake, na majibu yake, yakaonyesha kuwa ni mja mzito...’akasema.

Hapo kila mtu akamgeukia mume wangu kuona atasema lolote, lakini alikuwa kainama chini tu

‘Ulimwambia moja kwa moja, kuwa ana mimba...?’ akaulizwa

‘Mimi naifahamu hiyo familia, na sikutaka kuingilia ndani sana, nilipogundua kuwa ana mimba, nilitaka kuongea na mama, yaani mke wa hiyo familia, lakini nikaona nitakuwa nimeliingilia hili jambo kwa ndani sana, nikaamua kumhoji huyo binti kwa kadri ya kujua kama anafahamu ni nani aliyempa hiyo mimba..’akasema docta

‘Alikuwa kachanganyikiwa kwa siku ile hakuweza kusema kitu, na aliniomba sana, nisimwambia yoyote, mpaka atakapoweza kuliweka sawa,...nilimuelewa, hata hivyo, nilitaka niongee na rafiki yangu kuhusu hilo, na shughuli zikawa nyingi, kiukweli sikuweza kuongea naye kwa muda wa karibu

‘Nilikuja kulikumbuka hilo baada ya siku kandaa mbele, nikamuuliza rafikii yangu kuhusu binti wao wa kazi, na rafiki yangu akaniambia kuwa huyo binti ni muhuni, katoroka, nikamuuliza kwanini katoroka yeye akasema, ni uhuni tu, hana lolote.
‘Hakuna lolote lilitokea ambalo limemfanya kutoroka, baada ya kupimwa, kuhusu afya yake, ?’ nikamuuliza

‘Achana naye, sitaki hata kumsikia, hata mke wangu hataki kusikia habari zake, usiongee lolote kumuhusu yeye kwa mke wangu,maana kakasirika sana, mtu anaondoka bila kuaga, kaniibia pesa zangu, tapeli mkubwa yule...’akaniambia

Mimi sikutaka kuliongea hilo la ujauzito, maana kama docta, unastahiki kuficha siri za mgonjwa,nikawa kimiya kuhusu hilo, lakini nilihisi kuna kitu zaidi ya hicho,lakini sikupenda kuyachimba sana mambo yao, kwani, nilikuwa na mambo yangu yanayonisumbua, na aliposema kuwa ni muhini, na kaondoka na hata mama wa familia hajataka kuliongelea hilo nikayaacha kama yalivyo..’akasema

‘Ina maana hukuongea na mke wa familia kabisa…?’ akaulizwa

‘Kuna kipindi nilitaka kuongea na mke wa hiyo familia, nikaona na yeye hanipokei kama tulivyokuwa awali, baadaye nikaona hilo jambo halina nguvu sana, kwasababu huyo binti keshaondoka, na wenyewe waliokuwa nao hawalalamiki au kuulizia ulizia, nikaona yamekwisha, huenda wenyewe wameyamaliza hayo mambo kifamilia, sikuwahi kuliulizia tena...’akasema

‘Mnaona, ...huyo ni docta, ndiye aliyethibitisha kuwa huyo binti ana mimba..sasa niambie bado mteja wako anapinga,kuwa huyo binti hakuwa na mimba yake, au anataka ushahidi gani mwingine?’ akaulizwa

‘Inawezekana alipewa mimba na mtu mwingine akaona sehemu ya kupatia pesa ni kwa mume wa familia, .ndio maana tunataka tumuone huyo mtoto wake.’akasema wakili.

‘Halafu mkisha muona mtathibitishaje kuwa ni kweli..?’ akaulizwa wakili

‘Kwanza tumuone, mteja wangu anasema akimuona atathibitisha na atakuwa tayari kusema lolote…’akaswa wakili

‘Sisi tutafanya kila kitu akitakacho,lakini na sisi hatutarudi nyuma, maana hatua iliyofikia, sio ya kuaminiana tena, unasikia..’akasema mwenyekiti

‘Mteja wangu anazidi kusisitiza kuwa anataka kumuona huyo mtoto, maana hakumbuki hayo aliyoongea huyo binti, hana uhakika na maneno yake..’akasema wakili na watu wakacheka kidogo

‘Hebu mleteni huyo mtoto...’akasema mwenyekiti, na mama yangu akatoka nje, na aliporudi akawa kambeba mtoto, kila mmoja akawa na shauku ya kumwangalia huyo mtoto.

NB: Njia za muongo ni nini..kila ushahidi utatoka lakini imani ya mtu, ni ngumu sana, hasa ikiwa na malengo fulani...


WAZO LA LEO: Usimtendee mtoto wa mwenzako ubaya, eti kwa vile sio mtoto wako, hiyo ni dhambi ambayo malipo yake ni hapa hapa duniani, ulivyomtenda mtoto wa mwenzako ujue na wewe watoto wako atakuja kutendewa hivyo hivyo. Ukitaka kufanya lolote baya kwa mtoto wa mwenzako kwanza jiulize na mimi nikitendewa hivyo, au mtoto wangu akitendewa hivyo nitajisikiaje. Isije kuwa mkuki ni kwa nguruwe tu.
 
SEHEMU YA 99



‘Hebu mleteni huyo mtoto...’akasema mwenyekiti, na mama yangu akatoka nje, na aliporudi akawa kambeba mtoto, kila mmoja akawa na shauku ya kumwangalia huyo mtoto.

Kila mtu alitaka kumuona huyo mtoto kwa sura, na huku wakijiuliza ni kwanini mume wa familia akang’ang’ania mtoto aletwe…

Tuendelee na kisa chetu

********

Mtoto akaletwa na mama hadi kwenye kiti kilichowekwa maalumu kwa mtoa ushahidi, na mama akakaa naye hapo, huku akiwa kambeba yule mtoto, hakutaka kumpa yule binti, mama wa huyo mtoto, sasa akawa anamfunua ili kila mtu amuone kwa uwazi mkubwa, na wa kwanza kusema alikuwa rafiki yake mume wangu, yani docta akasema;

‘Bro, wewe kweli damu yako ni kali, huwezi kukataa hapo, utafikiri ni pacha mwenzako...’akasema docta.

Mume wa familia, alikuwa katulia kimiya, hakuinuka, wala kusema neno, aliyeinuka alikuwa ni wakili wake, ambaye alikwenda hadi pale alipokaa mama, na kumwangalia yule mtu, akatabasamu, na kugeuka, akarudi pale alipokaa, mteja wake, akamnong’oneza kitu.

Mume wangu akamwangalia kwa macho ya kuonyesha mshangao, lakini hakusema kitu, akabakia kimiya, na mwenyekiti alipohakikisha kila mtu kafika kumuona yule mtoto, na ambaye hakuweza kufika alikuwa mume wangu, mume wangu hakuinuka, alibakia pale pale akiwa kainamisha kichwa chini, na mwenyekiti akasema;

‘Mume wa familia ni zamu yako kumuona mtoto, usikatae, maana hilo tumelifanya kutokana na ombi lako, ulifahamu kuwa una mtoto, lakini ukajifanya hujui, ukifikiria kuwa huyo binti kaja peke yake, hana ushahidi, sasa mtoto ndiye huyo hapo, nenda kamuona, je ni mtoto wako, je ni damu yako, sasa uikane damu yako mwenyewe,...’akasema mwenyekiti.

Hata hivyo mume wa familia hakuinuka, mimi nikainuka na kwenda kumchukua yule mtoto kutoka kwa mama, nikaenda naye hadi alipokaa mume wangu nikamuonyesha mume wangu.

‘Huyu hapa, muone anavyofanana na watoto wangu, utafikiri mapacha, muone anavyokuangalia, katambua kabisa kuwa wewe ni baba yake..humdanganyi mtu hapa, sura yake haijifichi, anafanana kabisa na wewe...kwa kila kitu, haya niambie, ..’nikamwambia

Mume wangu badala ya kumwangalia mtoto akawa ananiangalia mimi usoni, na macho ya kutahayari, nilipoona hamuangalii mtoto, ananiangalai mimi tu, nikamuweka yule mtoto mapajani kwake, hakusogeza mikono yake, wala kusem a neno, moyoni nikasema ;ujumbe umefika. Nikamchukua na kumrudisha kwa mama, ambaye alimwangalia mwenyekiti kujua ni nini kinachofuata

‘Haya naona zoezi hilo limekamilika,...’akasema mwenyekiti na mama akamchukua yule mtoto na kwenda kukaa sehemu yake, pale alipokuwa amekaa awali.

‘Bado mwenyekiti, mimi nataka mume wa familia akubali kuwa huyu ni mtoto wake au sio mtoto wake, na kauli yake, ichukuliwe hapa rasmi ndani ya kikao hiki, kama akimkana, basi kwa vile wapo wanasheria hapa, wataandika, mkataba rasmi wa huyo mtoto kuchukuliwa na mtu mwingine, maana hatakuwa hana baba...’mimi nikasema.

‘Sawa, ni wazo zuri, na sisi tupo tayari kumchukua huyo mtoto kama baba yake atamkana kuwa sio mtoto wake,..’akasema mwenyekiti.

Wakili wa mume wangu akawa anaongea na mume wangu, na niliona mume wangu akisita kusema neno, na baadaye akasema neno kwa wakili, na wakili akasema;

‘Mteja wangu kasema hilo ni jambo lake binafsi, asingelipenda mtu kumuingilia, kwasababu kila kitu kipo wazi, anaona hilo la mtoto liachwe kama lilivyo, ataongea na mimi na ni jinsi gani ya kufanya..’akasema wakili wake.

‘Swali lwetu lipo pale pale, je huyo ni mtoto wake, au sio mtoto wake, kikao kinataka majibu?’ akaulizwa

‘Ni mtoto wake kwa mtizamo wa haraka, lakini kuna maswala ya kuthibisha kitaalamu, maana kufanana sio tija….yeye anafanana na wadogo zake, je haiwezekani akawa mtoto wa wadogo zake, kwahiyo mteja wangu kaomba apewe muda,…tuhakiki hakiki hilo kitaalamu zaidi...’akasema wakili na watu wakaguna, maana hapo hakuna cha kuhakiki, kila kitu kipo wazi.

‘Pamoja na hayo kuna swali la ziada, namuuliza mume wa familia, je anakubali sasa kuwa alimbaka mfanyakazi wa ndani…?’ akauliza mwenyekiti

‘Ndugu mwenyekiti, kama mteja wangu alivyosema awali, hawezi kuwa na uhakika na matukio hayo ya nyuma, kuna mengine mpaka sasa hayakumbuki, kwahiyo kwa hivi sasa hana jibu la swali hilo mpaka kupatikane vipimo vya kitaalamu.

‘Je vipimo vya kitaalamu vikisema huyo sio mtoto wake atafanya nini..?’ akaulizwa

‘Basi yawezekana akawa mtoto wa ndugu zake wengine..’akasema wakili

‘Na je ikithibitishwa kuwa ni mtoto wake, yeye ana kauli gani , rejea mkataba wao ulivyokuwa unasema..?’ akaulizwa

‘Mpaka sasa hatuwezi kusema lolote kwa hilo ..kwanza tupate uhakika, mfahamu alivyo mteja wangu yeye anathamini sana ushahidi, maana mambo mengine ya nyuma ameyasahau, na ikitokea ni kweli, basi hapo atakuja kutoa tamko lake..’akasema wakili wake.

************

'Huo ushahidi umakamilika, iliyobakia ni je katiba inasema nini,. Asileta ujanja ujanja wa kusahau hapa…tumekuwa tukienda na yeye kiuungwana ili tuone na yeye ni muungwa na kiasi gani..hana hiyo hulka…’akasema mweneykiti

‘Sasa tuspoteze muda, tuone kosa kaam hilo mkataba wao unasema nini, na je ni nini mkataba wao, unasema kwa watoto wa nje au hilo halipo, maana hata kama baba yake kakubali kwa shingo upande,lakini sisi kama familia ni lazima tujue hatima ya huyu mtoto kifamilia, kwani kazaliwa ndani ya familia,na hatuwezi kuliachia hivi hivi, zaidi alifanyiwa kitendo hicho kwa nguvu...’akasema mwenyekiti.

Mwenyekiti akakaa kimia akisubiria mawazo ya watu, na docta akasema;

‘Hatuwezi kukimbilia kwenye hukumu kwanza maana bado sheria, haijabaini kuwa mlengwa ni mkosaji, sisi bado tupo kwenye ushahidi au sio, mimi naona ukianza kuangalia katiba inasema nini utakuwa umeshahitimisha kila kitu..’akasema docta

‘Nafahamu hilo, kama nilivyosema awali, binti anastahiki kuondoka kwenye kikao hiki mapema ili akaweze kujiandaa, kwani yeye ana safari, kwahiyo tunahitajia aondoke hapa akiwa na ufahamu kamili ni nini hatima ya mtoto wake…’akasema mwenyekiti

‘Kwa hali kama hii, mimi ningelishauri huyo binti asisafiri, aahirishe hiyo safari yake, ili muafaka ufikiwe kwanza, ni muhimu sana aondoke akiwa na uhakika, kuliko kusubiria au kutumia njia zisizo faa…tunafahamu baba wa mtoto wake anastahiki kuwajibika kwa hilo, lakini je ni kweli, huyo baba wa mtoto ni nani..ni huyu au yupo mwingine..’akasema docta

‘Mimi sijawahi kutembea na mwanaume yoyote mwingine zaidi ya yeye, yeye ndiye alinibaka, na sikuwa hiyari kwa hilo tendo, aliniumiza, alishika kwa nguvu kama nilivyokwisha kusema awali…’akasema binti.

‘Bado nahitajia mawazo, …maana ni lazima huyo mtoto ahakikishiwe anapewa haki zake zote ikiwemo mama yake,..na kwa ushahidi wake imedhihirisha hali halisi, ni ipi tabia ya mume wa familia, na inavyoonekana ni kama vile bado ana watoto wengine nje, hilo nalo litakuja kutolewa ushahidi, sina shaka, …’akasema mwenyekiti na mume wa familia akainua uso kumuangalia mwenyekiti.

‘Kama nasema uwongo, nataka mume wa familia anikane…nina ushahidi wa hilo..’akasema mwenyekiti. na mume wa familia akawa anateta na wakili wake.

‘Haya mimi namuachia mke wa familia atoe kauli yake kwanza, maana tumempa muda wa kutosha wa kutuliza akili yake , haya mambo yasikieni kwa wengine, yanagusa mioyo ya watu…’akasema mwenyekiti

‘Lakini kabla sijalirejesha hilo jukumu kwa mke wa familia hii, nataka nisisitize wazo langu, kuwa kwa huyu mtoto, kwa vile imeshathibitika hivyo, tunataka kikao hiki, leo hii , kitoe tamko rasmi, tena kisheria, ili mtoto huyu atambulike rasmi kuwa ni mtoto wa nani, je ni mume wa familia, au ni wa nani,...'akasema mwenyekiti akimuangalia mume wa familia

'Ushahidi upo kuwa huyo mtoto ni wa mume wa familia,..huo utaalamu anaouhitajia yeye, upo, hautahitajia, kusubiria yeye, kuwa eti anahitajia utaalamu wa zaidi , hiyo ni namna ya kupoteza muda,..au sio jamani, lakini huko tutafika kama bado atazidi kuwa mkaidi, au sio jamani...?' akauliza mwenyekiti, na kabla watu hawajajibu mimi nikasema;

'Kama wao wanahitaji kuthibitisha kitaalamu, kivyao.. sisi hatulipingi hilo, lakini akumbuke kuwa kuna matendo kayafanya na huyo binti, na iwe isiwe kuwa huyo mtoto ni wake, au si wake, bado yeye ana madhambi, ya kavunja sheria za ndoa yake yeye mwenyewe, na pili kavunja sheria na haki za huyo binti,..huo ushahidi upo dhahiri...labda aulizwe hata ushahidi huo wa kumzalilisha huyo binti, anahitajia vipimovya kitaalamu…?’ akauliza mama

‘Wakili unasemaje..?’ mwenyekiti akauliza, na wakili akawa anateta na mteja wake

‘Mteja wangu anasema hayo ya ushahid ni kuzalilishana, hayana umuhimu kuonyeshwa, lakini hilo la mtoto lina umuhimu wake, maana baada ya hapo, ndio ataweza kutoakauli yake..mengine kama alivyosema hakumbuki..’akasema wakili.

‘Akionyeshwa huo ushahidi alivyokuwa akizalilisha mtoto wa wezake atakumbuka tu…’akasema mama

‘Mimi naona ushahidi dhahiri upo hapa hapa,..kama alivyosema mke wangu, na ushahidi huo unaonyesha dhamira ya kweli ya mtendaji, ..aisje kusingizia ulevi, maana humo humo kuna sehemu kabisa hajalewa…’akasema mwenyekiti

‘Kiukweli nimeuangali huo ushahidi wote, ilibidi nifanye hivyo ili kujirizisha, sio kwamba nilifurahia kuuona uchafu huo, kiukweli inakera, na ukiangalia hiyo video, unaweza ukafanya jambo baya sana,..mliona kipindi fulani nilikuwa na hasira sana na huyu mtu..ni sababu hiyo..’akasema mwenyekiti.

‘Sasa kwangu mimi, nataka sheria ichukue mkondo wake, sio haki kulifumbia macho hilo, sisemi hivi kwa vile namchukia huyo mkwe wangu, hapana, ila namuangalia huyu binti, …alichotendewa sio halali, na kama mtasema liachwa hivyo hivyo, jiulize ni ni haki ya huyu binti..hilo mimi nitawaachia wana kikao hili muamue wenyewe..’akasema mwenyekiti,na kuniangalia mimi, na mimi nikasema;

‘Huo ulikuwa ushahidi mmoja katika madhambi yake mengi, kuna mtoto mwingine ambaye hajajulikana, naona sasa ni zamu ya mume wangu kuongea mwenyewe, kwasababu anafahamu hilo, na anafahamu huyo mwingine kazaa na nani, mimi naona ni muda wa yeye kujirudi, ili tusipoteze muda....’nikasema

‘Haya mume wa familia, unasikia sasa wewe mwenyewe unaitwa kama shahidi, usema ukweli wako, na ninafasi nyingine ya kutoa lako la moyoni, hatuwezi kukulazimisha kutubu, lakini unatakiwa sasa useme neno, ..maana kumbe wewe ni dume la mbegu..’akasema mwenyekiti na watu wakacheka

Na hapo wakili tena akawa akiteta na mteja wake, na wakawa kama wanasigishana, na baadaye wakili akasema;

‘Mteja wangu anasema hayo ni mambo yake binafsi hataki kuyaongea hapa,..na hata hivyo, yeye hana mtoto yoyote mwingine kama mnavyo dai nyie, hayo yote yanayoletwa kwa hivi sasa ni shinikizo, na inabidi akubali tu,...lakini huo sio utaratibu mzuri, ....kwahiyo kwa swala la watoto, analiomba lisitishwe, tuongee mengine, yeye anahitaji muda wa kulifanyia kazi...’akasema wakili.

‘Kikao hiki kinatoa madhambi ya mume wa familia, ambayo yeye aliyakana tokea awali, kama yeye angekubali kuwa kuna madhambi kayafanya, akayasema japo kwa uchache, sisi kama waungwana tungemuelewa, tukatafuta jinsi ya kumsafisha, lakini kwa ujeuri wake, akaona sisi hatujui lolote..yeye ni mjanja, aliju yeye anaweza kutuvunga akafanya apendavyo, sasa hatutayaacha madhambi yake yapite hivi hivi, yatatajwa yote, ...’mimi nikasema.

Na hapo mume wa familia akafunua mdomo na kusema;

‘Hivi wewe unaposema nina madhambi, wewe ni mungu, unafahamuje kuwa nina madhambi, huwezi kunihukumu kihivyo, hayo ni makosa tu, yoyote anaweza kuyafanya, na kwanini unasema kuwa na mtoto ni dhambi..huyo mtoto alipangwa patkane hivyo, sio kusudio langu..?.’akasema mume wangu kama ananiuliza huku kakunja uso kwa hasira.

‘Swala hapo ni je huyo mtoto umempataje,mtoto hana kosa..ndio.., ila taratibu za kumpata huyo mtoto ni zipi,....hebu tuambie, huyo aliyeletwa hapo umempata kwa njia gani, sio kwa njia ya kumbaka, hiyo sio dhambi, .?’ akauliza mama sasa kwa ukali.

‘Nimesema hilo sikumbuki mimi…’akasema mume wa familia

‘Aaah, unaulizwa kubaka sio dhambi, au wewe dhambi unaielewaje, kutembea nje ya ndoa sio dhambi au ulikuwa umefunga ndoa ya muda na huyo binti..?’ aakulizwa

‘Mnielewe jamani…sikumbuki hayo madhambi kama kweli mimi nilifanya, sikumbuki…’akasema

‘Je na huyo mtoto mwingine, hatujui umempataje huenda ni kwa kubaka hivyo hivyo, huenda hiyo ndio tabia yako ya kubaka, na ujue, uliyafanya hayo ukiwa wewe ni mume wa mtu, ukaikana ndoa yako kivitendo, ukaisaliti ndoa yako, je hiyo sio zambi?’ akaulizwa na mama.

‘Kwahiyo nyie mnataka mimi nisema nini, kama mumeamua kama familia, baba, mama mke mniandamu mimi sawa, semeni mnavyopenda, ..mimi kwa sasa nasubiria maamuzi yenu, ila nasema hivi, ndoa yangu haitavunjiki, na haki zangu zipo pale pale...kama mumelipanga hili liwe hivyo, na nyie ni waungu wa kuhuku kuwa mimi nina dhambi…sawa, lakini mkumbuke kuna mimi nina nafsi, hamjui nilivyomlilia mola wangu...’akasema kwa sauti ya kukerwa.

‘Hayo yatafuata baadaye kama unavyodai kuwa ndoa haivunjiki, na haki zako zipo pale pale. Ni sawa tutaliona hilo, hapa tumekamilika, sheria itasema, na hatutako hapa mpaka kieleweke, ...sawa si sawa…?’ akauliza mwenyekiti akimuangalia docta

‘Tupo pamoja…hata mimi ningelipenda haya matatizo yafikie muafaka, lakini pia, nisingelipenda kuwe na maamuzi ya haraka kihivyo, kama ni hukumu au maamuzi inafaa tupate muda, muhimu leo tujadilianeni tu..’akasema docta.

‘Leo kila kitu kitabainika, na maamuzi hayatasubiria,… sisi tulitaka tushirikiane na yeye kama ndugu, tukamuomba na kum-bembeleza, ili hili tatizo tulimalize kindugu, lakini yeye amasaidia vipi kulitatua hili, na umesikia kauli zake za sasa hivi, kwahiyo wakili wake ana kazi kubwa ya kufanya, kama ana ubavu huo wa kugeuza hayo makubaliano yao kimkataba, lakini pia makubaliano yetu kama ndugu,.....’akasema mwenyekiti.

‘Makubaliano gani mnayoyasema, ya huo mkataba wenu, hapana mimi hayo makubaliano siyatambui, nilishasema toka awali kuwa ninachokitambua mimi ni huo mkataba niliokuwa nao mimi, huo mwingine sijui umetoka wapi...mnanichangany tu, mara huu mara ule, kwanini iwe mikataba miwili mimi sijui…’akasema kwa hasira

‘Naona wewe hujui sheria, kwa kukusaidia tu, wewe kaa uongee na wakili wako vizuri, atakushauri vyema kuhusu sheria, maana hapo unavyoongea, unaongea kama mtu asiyesoma, mkwe, usiniangushe...’akasema mwenyekiti, na kumfanya mume wangu amuangalie mkwe wake kwa macho yaliyojaa hasira.

**********

‘Tunaendelea na jingine, mke wa familia ulisema dhambi alizokufanyia mume wako ni nyingi, na tunaona kuwa yeye sio mtu wa kukubali na kukiri kosa, sasa ili tusipoteze muda, labda tukuulize, kuna dhambi gani nyingine, ambazo, amekiuka, na anahitajika kuwajiba nazo, au tumuulize tena mwenyewe muhusika, kuwa yupo tayari kukiri makosa yaliyobakia, ili tusipoteze muda?’ akauliza mwenyekiti.

‘Mimi sipendi kuyaongelea machafu yake,lakini yeye ananilazimisha nifanye hivyo, kama nilivyosema awali mume wangu ni mzinzi, ana tabia chafu, ambayo haivumiliki, inasadikiwa kuwa ana mtoto mwingine nje ya ndoa zaidi ya huyo aliyempata kwa kubaka…’nikasema

‘Ndio maana ningelipenda akiri yeye mwenyewe hilo, ili nimuone kuwa kweli sasa kawa ni muungwana, na yupo tayari kuwa raia mwema, kwa jamii, kwani yote tuliyomshukutumu nayo yamethibitika kuwa ni kweli, je na hili la kuwa na mtoto mwingine nje, atalikataa...nataka nisikie kauli yake yeye mwenyewe?’ nikauliza, na mwenyekiti akamwangalia mume wangu.

Mume wangu alipoona watu wapo kimya wanamuangalia yeye, kwanza akamuangalia wakili wake, na wakali wake akamuonyesha ishara kuwa aongee, na hapo mume wangu kwa hasira akasema;

‘Sina mtoto mwingine, kama unavyodai wewe, mimi nimeona lengo lenu ni kunizalilisha, sasa mimi nasema sina mtoto mwingine, kam yupo huyo mtoto mwingine mleteni nimuone, ili nijaribu kuvuta kumbukumbu zangu kama ni kweli….’akasema mume wangu kwa hasira

‘Una uhakika na hilo, maana sasa tukianza kutoa ushahidi mwingine, hakuna kurudi nyuma sisi tutachukulia kuwa wewe ni jeuri, hututhamini, na kwahiyo kama wanafamilia, tutahukumu, bila msamaha...’akasema mwenyekiti.

‘Nimeshawaaambia kuwa sina mtoto mwingine, kama yupo Malaya anayedai hivyo aje kama livyofanya huyo,wote kwangu hao ni wahuni tu walaghai, walifanya hivyo ili labda kunitega, ili wapate pesa, hakuna kingine ...’akasema na kila mtu akawa kimiya kwa kauli yake hiyo chafu.

‘Kwanini unazungumza hivyo, huoni kuwa hiyo ni lugha chafu kwa walengwa, na wakati wewe uliwabaka…?’ mwenyekiti akamuuliza

‘Nimechukia sana, kwani kinachoendelea hapa ni kunizalilisha na mimi, hilo hamlioni au mimi sio binadamu,..nia yenu ni kunichafua , ili nionekane mbaya, na mwisho wa siku mfanye mnavyotaka, mimi nimechoka, na labda niseme hivyo, maana hamtaki ombi langu, nyie fanyeni maamuzi yenu muonavyo ni sahihi…’akasema

Na watu wakabakia kimia, hawaamini anachokiongea huyo mume wa familia.

‘Na narudia hivi, kauli yangu ni ile ile, mimi sikubali kuvunja ndoa yangu,na wala sikubali kuachia chochote kilicho changu, kwa ajili ya hawo wajanja wajanja, hao ni wahuni tu ,…na sitasita kuwaita Malaya,..’akasema na wakili wake akamzuia kuongea hivyo.

‘Ni Malaya tu,..kama wameamua kutumia ujanja wa mwili wao kupata pesa kutoka kwangu, na kudai eti watoto wangu, kama yupo malaya mwingine kama huyu aje athibitishe hayo, kuwa ana mtoto wangu, mimi sina mtoto na Malaya yoyote zaidi ya mke wangu huyu hapa...’akasema na kauli yake ilikatishwa, kwani kuna mtu aligonga mlangoni, na sote tukageuka kuangalia mlangoni.

Haikupita muda, huyo mtu akagonga tena , na kufungua mlango, ….

Kiukweli pale nilipokuwa nimekaa nilijikuta nikishikwa na mshangao, .na niliona hali hiyo pia ilitokea kwa wengine…!

Hakuna aliyetegemea…..

Rafiki yangu alikuwa kasimama kati kati ya mlango, akiwa na mtoto wake mkononi..

‘Hiyo kauli chafu imenikera, ...unafikiaje kutuita sisi Malaya, wewe ambaye uliyetembea na wanawake wengi tutakuitaje, au unataka tuseme kila kitu, sasa mimi nimefika, nasema hivi huyu hapa ni mtoto wako niliyezaa nawewewe,....’akasema rafiki yangu, ...’

Watu wote walijikuta wakishikwa na mshangao, hakuna aliyesema neno kwa muda huo hata mwenyekiti alikuwa kimia, akimuangalia huyo aliyeingia, na mimi hapo nikapata nafasi ya kugeuka na kumuangalia mume wangu, alikuwa kwenye mshangao wa aina yake..ni kama haamini.

Mwenyekiti alipoona hiyo hali, akasema;

‘Hebu kidogo,..naona haya mambo yanajirudia , nilichokikataa kinajirudia tena, hii maana yake ni nini…huyu mtu alistahiki kuwepo kwenye hiki kikao.., na ni ustaraabu gani huu…’akasema mwenyekiti.

‘Samahani mwenyekiti, nilipewa taarifa ya kuwepo kwenye hiki kikao, lakini kutokana na yaliyotokea, sikupenda kufika kabisa…hata hivyo, ikafika muda, nikaona ni kwanini nisiwepo, ni kwanini isiwe nafasi ya kuja kuusema ukweli..’akasema.

‘Na kwa bahati, …ila sikutarajia hili, ..nilikuwepo hapo nje muda mrefu tu, nikisita kuingia ndani, na kauli hizo chafu za kutuzalilisha sisi wanawake ndizo zimenifanya niingie, nije ..nipambane na huyu mtu anayetuzalilisha wanawake..’akasema

‘Lakini sio ustaarabu ulioufanya..’akasema mwenyekiti

‘Samahani sana,…ila mwenyekiti, mimi naona mnapoteza muda wenu na huyu mtu , hatutaweza kukaa kimiya tukisubiri huyu mtu aseme ukweli, ambao hataweza kuusema, huyu mtu ni mwongo,mzalilishaji mbakali na pia anahusika na uuwaji,..’akasema

Mume wangu akataka kusema ..lakini wakili wake akamzuia..

‘Kama mtu huyo ana tabia hizo, unategemea nini, nawaambia ukweli, mnapoteza muda wenu bure, je hamna mambo yenu mengien ya kufanya, mpaka mumbembeleze mtu kama huyu,, imeniuma sana, …anafikia kutuita sisi malaya...’akasema rafiki yangu kwa sauti .

‘Mimi nataka anijibu swali langu kuwa ni nani Malaya, yeye aliyetembea na wanawake wengi huku ana ndoa yake halali au sisi ambao kwa hadaa zake alituzalilisha, ..ni nani Malaya?’ akauliza rafiki ynagu kwa hasira.

‘Kwani nilikuja nikakushika kwa nguvu,....wewe ulijileta mwenyewe kwangu, ukidai unataka mtoto, au umesahau, usitake nikakuumbua bure hapa...’akasema mume wangu kwa hasira.

‘Wewe mwanaume, mimi nilikuja kwako nikakuambia nataka mtoto,..?’ akauliza kwa mshangao.

‘Umesahau eeh…’akasema na kutulia, baada ya kuhis wakili wake akimzuia.

‘Sio kwamba mipombe yako ilikutuma na kunitilia dawa ya kulevya kwenye kinywaji kwa siri, nikazidiwa, ukanifanya ulichonifanya huko sio kubaka, wewe ni mbakaji, na sio mara moja, kama wewe ni mwanaume kweli kwanini utumie mbinu hiyo,…’akasema

‘Sema sasa kama wewe ni mwanaume kweli kwanini ulishindwa kuongea.....na ole wako, chunga sana kauli yako, na ninakuambia hivi yale yote uliyoyaandikisha kwa ajili ya huyo mtoto ninayataka yote, nimeshayawakilisha hayo maombi kwa wakili wangu, sikutaka kufanya hivyo lakini sasa utawajibika,…unasikia utawajibika...’akasema rafiki yangu kwa hasira.

‘Kama una wakili wako na mimi nina wakili wangu, usinibabaishe, ...hukutaka kukubali matakwa yangu toka awali, sasa unakuja kwa nyodo, hupati kitu hapa, nimeshakuambia,..wewe si umekataa na mtoto wako, haya kaa naye sasa, umtafute baba yake, sio mimi...’akasema na wakili wake akamkatisha na kumtuliza.

‘Jamani hebu kwanza…’akasema mwenyekiti, lakini mama akamzuia, amueche huyo mdada aendelee kuongea;

‘Ndugu mwenyekiti samahani sana, sikutaka kuyasema haya yote kama hivi, ilitakiwa niyasema ili kuondoa hii sintofahamu lakini sio kwa utaratibu huu, ila hatua iliyofikia inabidi niseme kila kitu, ili mumuone huyu mtu jinsi alivyo, nakiri kuwa kweli nilimkosea rafiki yangu, lakini ni lazima mwisho wa siku tumtambue mbaya wetu ni nani...’akasema rafiki yangu.

‘Mimi nimekuwa hapo nje nikisiliza yote , awali nilikuja na ajenda nyingine kabisa ya kutaka kumsaidia huyu mtu, kumbe ni mtu mbaya sana , sikumuelewa kabisa,..sasa wakati umefika wa kusema ukweli wote, na nasema ukweli wote sitaficha kitu ili haki itendeke, hata kama mimi ni mkosaji, basi niwajibike kwa madhambi yangu…’akasema rafiki yangu

‘Najua rafiki yangu hatanielewa kwa hivi sasa…, lakini univumilie kwa hili..na yale uliyokuwa ukiniuliza leo utayapata majibu yake hapa hapa, kuwa huyo mume wako sio mtu mnzuri, ni Malaya, mbakaji, muongo, mwizi, ..na sifa zote mbaya, anazo, hakustahili kabisa kuwa mume wako…’akasema akimnyoshea kidogole mume wa familia

‘Usininyoshee kidole wewe mwanamke, ..usitake kikao hiki kikaharibika,.kama umekuja na yako, fanya yaliyokuleta, si unataka upate mali, haya,…endelea na tabia hiyo kama utazipata…ndio zenu.’akasema mume wa familia na wakili waka akawa anamsihi.

‘Nitakunyoshea sana maana, muda wa kukueshimu umepita, nilikuheshimu sana kipindi cha nyuma, lakini sio sasa, umejivunjia heshima yako wewe mwenyewe, umajitoa kwenye ubaba, ulezi, ..ushemeji na kujitwika yasiyostahiki…na ..’akajizuia kulia

‘Ongea tu, hiyo ndio shukurani yako…na toka humu ndani maana hujaalikuwa, umekuja na mihasira zako, ulitaka nikumbembeleze, sasa sikiliza hupati kitu , Malaya mkubwa wewe..’akasema mume wangu na wakili wake akamzuia.

‘Shukurani gani wewe upewe, ..utufanyie unyanyasaji, utuzalilishe, ututukane , halafu utegemee shukurani, ..nakuambia hivi mimi sikuogopi, usinione hivi, mimi ninaweza zaidi ya hili, mimi sio mwanamke kama wanawake wengine, kama ni kupigana nipo tayari, na wewe wala hunishindi, nitakuzalilisha mbele ya watu hawa, umeniuzi sana mimi…’akasema.

‘Kwahiyo unataka nikuonyeshe mimi ni nani, sio…ukweli umekuuma eeh..’akasema mume wangu.

‘Ukweli gani, ..sasa, ulikuwa hujaniafahamu mimi upande wa pili wangu,s asa utanifahamu…umemtoa nyoka pangoni, sasa atakuuma, mimi nitawaambia watu wote hawa kila kitu ...bila kuficha, nilishaahidi kuwa nitasema kila kitu siku ikifika, naona sasa muda umefika...’akasema rafiki yangu sasa akimsogelea mume wangu.

‘Aah, usimsogelee, kaa pale kwenye kiti kile cha ushahidi…’akasema mwenyekiti wake..

‘Ndugu mwenyekiti, huyu mtu hajaalikwa hapa, mnamkaribisha, huyu kaja na yake kwa vile kakosa alichokitaka, huyu mtu ni muongo mkubwa, hana jipya hiyo ndio tabia yake,…amekuwa akimtimua mke wangu, kujinufaisha, na baadae kaja kumsaliti rafiki yake mwenyewe, ..hapa, sasa a jifanya kujikosha..nakuambia hivi, wewe mwanamke kwa sasa hupati kitu kwangu na kwa rafiki yako umeharibu,umalaya wako umekuponza ....’akasema mume wa familia, bila kujali

Na hapo mwenyekiti akaingilia kati na kusema;

‘Hebu tutulizane kwanza, na nawaombe nyie wajumbe wawili mrekebishe hizo kauli zenu, tusija kukifanya hiki kikao cha watu wasio wastaarabu, .na kwa hizo kauli tutahitaji uhalali wake, huwezi kutamka tusi,au nen la kashifa kwenye kikao kama hiki lipite bure, utastahiki kulitolea ushahidi, vinginevyo, wewe mtamkaji utashitakwia kwa kutoa maneno machafu mbele ya kikao halali..’akasema mwenyekiti

‘Mimi nitathibitisha kauli yangu mwenyekiti, hayo maneno niliyotamka dhidi ya huyu mtu ni kweli na nina ushahid nayo…’akasema rafiki yangu

‘Hata mimi nitathibitisha hayo ya kwango dhidi yako, ya kuwa wewe umekuja hapa kwa nia ya kujikosha tu, na ni kutokana umekosa ulichokitaka kutoka kwangu, mimi sio mtu wa kuchezewa...’akasema mume wangu.

‘Subirini tutakwenda hatua kwa hatua,.., tutakuhitaji nyote kuyathibitisha hayo maneno yenu la sivyo kikao kitawajibika kuwachukulia hatua…. kwanza nataka tutulie, maana naona mambo yanajileta yenyewe, tunakuomba ndugu uliyeingia, utulie kwanza, ili tufuate utaratibu wetum huwezi kutuingilia na kuharibu ajenda zetu...’akasema mwenyekiti.

‘Ndugu mwenyekiti, naomba mnipe hii nafasi , niongee, nafahamu mna utaratibu wenu, lakini naona kuna mengi yalitokea, na imefikia mimi kuonekana mbaya, hata kwa rafiki yangu, na ubaya zaidi ukaka kupandikizwa juu yangu,…’akasema

‘Ubaya huo ni wa mauaji ya Makabrasha, nakuja kushangaa, naambiwa mimi nilihusika, wakati huyo mnayemuita mume wa familai siku hiyo alikuwepo, wakati marehemu anauliwa, yeye anafahamu kila kitu,.. hebu muulizeni vizuri siku hiyo kule kwa Makabrasha alifuata nini, na wakati alistahiki kuwa hospitalini,…je aliwezaje kufika huko..huyu ndiye muuaji, anafahamu kila kitu...’akasema na watu wakawa wametulia kimiya.

‘Hayo ni yako…mimi sijui kutumia silaha, wewe ni mtaalamu wa silaha, je sio wewe uliyefanya hayo mauaji, ili kunibambikia mimi, unejileta mwenyewe…’akasema mume wangu

Mwenyekiti hapo akatulia kwa makusudi…

‘Unataka nielezee siku ile ilivyotokea au sio, maana wewe huamini kitu mpaka uambiwe ukweli, wakati ni kweli ulikifanya, ndio tabia yako, sio…sasa ‘akatulia akimgeukia mwenyekiti.

‘Naomba kibali chako, ndugu mwenyekiti ili nisema kila kitu kwa ukweli wake na ushahidi, sitako niongee kama yeye, umeniuma sana, maana nimefika kutoka masomoni na kukamatishwa watoto wa kihuni wanifanyie unyama,…mimi, wakati mbaya mwenyewe yupo, kwanini yeye asifanyiwe hivyo, leo ni lazima niseme…’akasema

‘Sawa utasema lakini ngoja tufuate utaratibu..’akasema mwenyekiti

‘Samahani mwenyekiti ninaona kabla huu mukari haujashuka, uniache mimi niendelee kwanza, sitaweza kuvumilia, mkizunguka zunguka, wakati muhalfu yupo nanyi, na ninavyomfahamu hatakubali ukweli, mtazungushana naye tu, tafadhali mwenyekiti, mimi nafahamu kila kitu mnachokihitajia…’akasema

Mwenyekiti akageuka kuniangalia mimi, halafu wakili wa mume wangu, kabla hajasema neno, rafiki yangu huyo akasema;

‘Mimi sijawahi kutukanwa hivyo, eti mimi ni malaya… eti kwa vile nimetembea na mume wa mtu, yeye huyo mume wa mtu ataitwa nani, mbakaji mkubwa huyo, yeye ndio Malaya, tena wa hali ya juu, mbakaji ana sifa gani..ni nani mwenye dhambi kubwa, kati ya mtu mwenye ndoa na asiye na ndoa, kwenye maswala ya uzinzi, aniambie yeye,..’akasema na alipoona mwenyekiti anamuangalia yeye, akasema

‘Samahani sana mwenyekiti,..naomba nikae hapo kwenye hiki kiti maalumu, ili niweze kuwaelezea kila kitu kiushahidi na mwisho wake, tutaona ukweli upo wapi, kuwa mimi ni Malaya au ni yeye...’akasema na kwenda kukaa kwenye kiti cha mashahidi.

**********

‘Mke wa familia unasemaje, tuendee naye au una shahidi mwingine?’ akaniuliza mimi na wakati huo nilikuwa nimeshikwa na hasira, sijui kwanini nikimuona huyo rafiki yangu, ninakuwa hivyo, nilitamani wale wahuni waje, wamfanyie ubaya mbele ya watu wote hawo, nikamwangalia huyo rafiki yangu kwa macho ya hasira, maana nilishampatia dhabu yake na haikuwahi kufanyika,…hapo nikamwambia mwenyekiti.

‘Nataka huyu mtu asema ukweli wote, na haki itendeke, kwani wote lao ni moja, mume wangu, na huyo rafiki yangu, alikuwa rafiki yangu, kwasasa hivi sio rafiki yangu tena, nawaona wote lao ni moja, kwangu mimi ni wasaliti, sina msamaha na hawa watu wawili, ....’nikasema

‘Mke wangu…’akataka kuingilia mume wangu na mwenyekiti akamzuia kwa ishara ya mkono, na rafiki yangu akachukua nafsi hiyo kwa kusema;

‘Hata wewe usijitetee, na kujiona msafi sana nakuheshimu sana, na nitaendelea kufanya hivyo…ila na wewe una mapungufu yako.., kwani isingelikuwa wewe kunishauri haya, unafikiri mimi ningeliyafanya …nisingeliingia kwanye ubaya na mume wako,..’akasema

‘Lakini hayo kwangu nimeyasahau, ..najua hata nifanye nini, ubaya wangu hauwezi kuzidi haya niliyokufanyia, lakini…kuna mbaya wetu zaidi, ambaye anastahiki kuzibeba lawama zote hizo,..huyo mume wako,…, uneyemuita mume wako, nataka leo akitoka hapa, anaelekea jela, kwani hastahili kuishi kwenye maeneo ya raia wema, nina ushahidi wa kutosha, kwa hilo wa kumweka, ndani...’akasema rafiki yangu.

Mume wangu akajifanya kucheka na kutikisa kichwa, huku akimuangalia wakili wake, na wakili wake akamuashiria atulie kwanza..lakini mume wangu hakuweza kutulia akasema;

‘Usinitishe wewe, ....toa huo ushaidi wako, na mimi nitakuja kutoa ushahidi wangu kuwa wewe ni Malaya, pili mlaghai, na tatu, msaliti, na pia wewe unahusika na mauaji ya Makabrsha,..utasema ukweli ulikuwa wapi siku ile…nilikuja kuyafahamu hayo, wewe siku ile tokea muda mrefu ulikuwa na marehemu, ukajifanya kujificha uwanja wa ndege…’akasema mume wangu

‘Haya sawa, ngoja tuone mimi na wewe ni nani zaidi, si ndio hivyo, kikao kitatusikiliza, kila mtu atoe ushahidi wake, na uwe wa ukweli, na hapo ndio tutaona ni nani malaya, ni mimi au wewe, ninani ana sifa hizo mbaya, usaliti, wizi, ubakaji, umalaya na uuaji, tuanza kazi mwenyeki....’akauliza akimgeukia mwenyekiti, na mwenyekiti akageuka kuniangalia mimi.

Na mimi nikaguka kumuangalia wakili wangu…

NB: Haya mambo yamekwenda haraka kihivyo, tumerahisishiwa kazi…, lakini ndivyo ilivyotokea, tuwepo kwenye sehemu ijayo,


WAZO LA LEO: Tuchunge sana kauli zetu tunapoongea, kuna maneno yakitamkwa mbele za watu, yanakuwa na picha mbaya, lakini kuna watu ni wepesi kuyamtamka hayo maneno kama vile ni maneno ya kawaida, kwa lugha sahihi, yanaitwa ‘lugha za matusi’ .


Kuna baadhi ya watu wanayatuma haya maneno bila kujali anayamtaka wapi, na kwa nani, na anamlenga nani, baya zaidi, wengi wanaozalilishwa kwa maneno hayo ni akina mama, ...iweje ugombane na mtu mwingine baki, wewe unakimbilia tusi linalomlenga mama, mzazi wa mwenzako, unamtusi yule mtu mwenyezi aliyekuzaa, je huyo mama kakukosea nini, ...tuchunge sana ndimi zetu, kwani tunajilaani sisi wenyewe kwa kauli zetu chafu.
 
SEHEMU YA 100



Mwenyekiti alituliza kikao baada ya kuona kuna majibishano makali kati ya rafiki yangu na mume wangu, kiasi kwamba kama asingeliingilia kati yangelizungumzwa mengi ambayo hata hayakustili kuzungumzwa kwenye hicho kikao bila mpangilio maalumu..

Tuendelee na kisa chetu…

************.


Rafiki yangu alipewa kibali cha kuongea na mwenyekiti, akawa anatoa maelezo yake, japokuwa mimi akili yangu ilikuwa mbali sana, lakini niliweza kumsikiliza, rafiki yangu alisema;

‘Nitatoa maelezo yangu katika sehemu kuu mbili, ya kwanza ni ukweli kabla sijapata mtoto na sehemu ya pili yenye ushahidi mnzito, ni ukweli baada ya mimi kujifungua, naomba muwe watulivu, ili niweze kuyasema yote niliyoyakusudia kuyaongea leo hii...niliahidi na sasa natimiza’akasema na kuniangalia mimi.

‘Mimi ninaamini kwamba kila jambo huja kwa minajili fulani, na hili la kupata mtoto huenda na kweli limetokea ili iwe fundisho sio kwangu tu, na hata kwa wale wote lililowagusa kwa namna moja au nyingine. Ni changamoto, ambayo sitaweza kuisahau katika maisha yangu, ....’akasema

‘Hii ni changamoto iliyonipa fundisho moja kubwa, kuwa kutaka kupata kitu kwa njia zisizo halali, zina mateso baadae, usijione umepata ukadhani umefanikiwa, mitihani yake ya hicho ulichokipata kwa njia isiyo halali huja baadae, na huko ndipo kwenye majuto…’akatulia

‘Kiukweli mimi nimechelewa kuzaa, na sababu kubwa, naweza kukiri kuwa ni madhaifu yangu ya kupenda kuchagua…nisipoteze muda huko, ni kwanini ilikuwa hivyo, lakini kitu kilichokuja kunigusa baadae ni kuwa, nilikuwa nataka kupata mtoto, sasa swali likaja nimpateje..’akatulia

‘Madhaifi yangu yapo pale pale, nikitaka kitu nakichanganua sana, haya nataka mtoto aweje, na ..afananeje..hilo likawa ni changamoto pia kwangu, kiukweli sio siri, kuna watu niliowapenda, bahati mbaya wengi niliowapenda walikuwa waume za watu, siwezi kulificha hili..hata hivyo sikupenda kuvunja ndoa za watu, nikiwa na maana sikutaka kabisa mahusiano na mume wa mtu.

‘Mimi nilifikia kuhini ahadi yangu ya kuzaa ndani ya ndoa, na pili kwa mume asiye kuwa mume wa mtu, na ilipotokea nilitaka iwe siri kubwa..na pia nikata mtoto huyo asiwe na baba, japokuwa huwezi kuzaa mtoto bila baba, haya nitayaeleze kinamna, kwa jainsi tunavyokwenda..’akasema

Japokuwa nilipanga iwe hivyo, kuwa mtoto ni wangu, na hana baba, lakini mume wa familia alipogundua kuwa nimejifungua, akawa wa kwanza kufika hospitalini, na alipomuona tu huyo mtoto, aligundua kuwa ni wake...haijifichi.

'Kiukweli mume huyu alipagawa hasa pale alipojua kuwa mtoto huyu ni wa kiume maana ndoto yake kubwa ilikuwa kupata mtoto wa kiume,na hapo hapo akasema huyo ni mtoto wake, hakuna ubishi,...

‘Siku ile nilipojifungua nilijaribu kila njia ili huyo mume asijue lolote, lakini ilishindikana, na kama nilivyosema kila kitu huja kwa sababu fulani, nahisi hata kufanana kwa mtoto huyu na huyu mwanaume ni sababu maalumu ya kuliweka hili jambo liwe bayana.

‘Siku ile ile nikajua sasa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yangu, kinyume na makubaliano yangu na mshauri wangu mkuu, kuwa nikizaa, hata kama nimezaa na mume wa mtu , hiyo iwe iri yangu mimi mwenyewe asije kufahamu mtu yoyote.

‘Mimi ninahisi kilichomfanya mume wa familia ang’ang’anie sana ni kwa vile nimepata mtoto wa kiume, na yeye kwa kauli yake mwenyewe, alikuwa akitaka mtoto wa kiume, maana watoto alio nao hadi sasa na mke wake , ni watoto ni wa kike...'akarudia sehemu hiyo.

'Kiukweli mimi sikuyajali hayo kwani mipangilio wangu ulikuwa nizae mtoto, na huyo mtoto awe ni wangu wote hata nikiandikisha jina lake kwenye cheti chake, lisomeke jina lake,na ubini wa baba yake, liwe ni jina langu kwa herufi yangu ya mwanzo, halafu jina la tatu liwe la baba yangu mzazi ndio nilivyotaka iwe hivyo...'akatulia

Lakini baadaye tulipokutana mimi na mwanasheria wao na mume wa familia, mume wa familia akasema hilo halikubali, mtoto huyo ni wake, kwani yeye ndiye mume aliyeweka mbegu, naye pia ana haki zake na anawajibika kwa mtoto,na hata kisheria za nchi, inabdii iwe hivyo.

Kwahiyo akanisihi kuwa mtoto huyo aandikwe kwa ubini wa baba yake, nilikataa, na huyo wakili akarudi kwa mume na wakaongea walichoongea, na aliporudi kwangu, akasema mume huyo kasema huyo mtoto ni lazima atambulikane kuwa yeye ni baba yake, na hili atalifaya nipende au nisipende.

'Sasa hiyo upende au usipende ina maana gani, ndio hapo utaona mbinu walizokuja kutumia baada ya kuona mimi nimekaidi maagizo yao, nitayaeleza hayo kwenye ushahidi wangu wa pili,..ambao una mambo magumu zaidi…

Kabla ya hiki kikao tulikutana mimi na yeye, moja ya ajenda yake ni hiyo ya mtoto kutambulikana kuwa huyo ni mtoto wake kisheria, ...maana mimi nilishakataa...pamoja na mengine mengi aliyoyataka, mimi nikawa kinyume chake...'akatulia

Kwahiyo yeye akaja huku kwenye kikao, akisema akifika huku kwenye kikao atahakikisha kuwa huyo mtoto anatambulikana, kwa vile anao uwezo wote kikatiba yao ya kifamilia,

'Kwa vipi ...?' akaulizwa

'Alisema mkataba alionao yeye unampa hiyo nafasi, alinionyesha huo mkataba, lakini niliuona una utofauti mkubwa na ule mkataba ambao niliwahi kuusikia kutoka kwa rafiki yangu , sikuwahi kuusoma huo mkataba wao wote kiundani maana ni mambo yao ya kifamilia, lakini kwa kauli ya rafiki yangu, mkataba wao, ulikuwa hauruhusu mume au mke, kujitwalia madaraka bila kumshirikisha mwenzake. Ndivyo nilivyokuwa nafahamu hivyo.

Na nakumbuka rafiki angu huyo aliniambia kuwa kama mmoja akimsaliti mwenzake, na ukapatikana ushahidi bayana, na ushahidi bayana unaweza ukawa wa kuona tendo likitendeka, au ushahidi wa vielelezi kama hivyo mtoto wa nje..basi mtenda kosa kavunja mkataba, na hapo atawajibika, ..kama mkataba wao unavyosema

'Kwahiyo mpaka hapo nilijua kabisa hili jambo likija kugundulikana ndoa hiyo haipo tena,..na ukumbuke kufahamu kuhusu mkataba wa kifamilia nimekuja kulifahamu hilo baada ya mimi kupata mtoto, mkataba wao huo ulikuwa siri yao, wanafamilia haou….mnielewe hapo,….'akatulia

'Na nilikuja kumwambia wazi huyo mume wa ndoa siku kadhaa alipokuwa akizidi kung’ang’ania kuwa huyo mtoto ni wake, ilibidi nimkumbushe hilo, baada ya kugundua kuwa kumbe wana mkataba mkali kama huo...'

‘Wewe unataka huyu mtoto hujui kutambulikana kwake ndio utakuwa ushahid wa kuvunja ndoa yenu? Nilimuuliza hivyo, sasa uone alivyonijibu…’akasema


‘Hilo nimeshalifanyia kazi, kila kitu kitakwenda sawa, mimi ndiye mumiliki wa kila kitu,na nina madaraka yote, kuna mambo macheche tu hayajakamilika, lakini yapo mbioni kukamilika,..'akasema

'Kwa vipi..?' nikamuuliza

'Wewe utayaona tu, haya yalishapangwa, na yatafanyika tu, usicheze na watu na fani zao, kuna mtu mkali analifanyia kazi, hutaamini..'akasema

'Kwahiyo unataka mimi nifanye nini..?nikamuuliza baada ya kuona ananitishia maisha’

'Wewe ninavyotaka mimi, hii hatua ya kwanza ikipita, utaona, kuna ujanja ujanja mwingine unatakiwa utumiwe, mke wangu akikubali baadhi ya mambo, na ukapatikana ushahid basi mkataba huo utakuwa umeshafanyiwa kazi,...kila kitu kitakuwa mali yangu, na hapo nitajua jinsi gani ya kukuingiza wewe.

‘Kuniingiza mimi kwa vipi..?’ nikamuuliza

‘Kama mshirika mwenza, wa kila hali, na huenda tukajaliwa kupata watoto wengine zaidi...'akasema

‘Kwanini unataka upate watoto na mimi, kwani mke wako hatoshi..?’ nikamuuliza

‘Hataki, mke wangu hataki, yeye anasema kazi kwanza, tuej kuzaa kwa malengo, mimi sioni ubaya wa kuzaa, maana mali tunayo, na watoto ndio wa kuzitumia, na sasa hivi tuna mabinti, wataolewa ni nani wa kuendeleza mali zetu…’akaniambia hivyo

Hapo mume wa familia hakuweza kuvumilia akasimama na kusema;

'Mwongo wewe, hivi kwanini unataka kusema huo uwongo, usiseme lolote kuhusu watoto wangu, mimi nawapenda sana watoto wangu, sikiliza tunga uwongo wako wote lakini usiguse watoto wangu, …mke wangu usimsikilize huyu lengo lake ni kuniharibia ndoa yangu…na wewe,..' mume wa familia akaingilia kati kumkatisha mzungumzaji huyu.

'Hahaha, unataka nitoe ushahidi,…?’ akauliza

‘Ndio toa, una ushahidi gani wewe acha uwongo wako..?’ akasema

‘Una uhakika na unachokitaka, unauhakika unataka nitoe ushahidi au unasema tu kujihami?’ akuliza mzungumzaji na mume wafamilia alitaka kuongea kitu, lakini wakili wake akamzuia. Wakawa wanateta kwa chini chini…

‘Kama unataka niyathibitishe haya kwa ushahidi mimi nipo tayari, ushahidi upo, nikipata kibali kutoka kwa mwenyekiti nitafanya hivyo…’akasema mzungumzaji

‘Ushahidi gani ulio nao wewe…?’ akauliza wakili wa mume wangu

‘Muhimu ni ushahidi, ..siwezi kukuambia kwa hivi nina ushahidi gani, lakini ushahidi upo, nikipata kibali nitauotoa hadharani, ..’akasema akimgeukia mwenyekiti

‘Je naweza kuutoa huo ushahidi…?’ akauliza, na mwenyekiti akageuka kuniangalia mimi, halafu akageuka kumuangalia wakili wake, halafu akasema;

‘Kama kikao, kwa hivi sasa tunahitajia maelezo tu, nia yetu ni kuwaptia nafasi waliokosea wajirudi, wawe wakweli kwetu, tulimalize hili kwa amani, na kama kuna makosa mengine ya kisheria, hayo sio juu yetu,…sasa mpaka tunafikia hatua hii ni kwamba watu hawataki kujisalimisha na kuomba msamaha, lakini sasa wataendelea hivyo haitakuwa na budi, kila kitu kitawekwa hadharani..’akasema mwenyekiti

‘Kwahiyo mwenyekiti unasemaje..?’ akauliza mzungumzaji.

‘Labda utupe maelezo yako tu, kuwa una ushahid wa namna gani, mengine yatafuata baadae…’akasema mwenyekiti.

‘Tulipokuwa na kikao hicho mimi na yeye tulikuwa wawili tu, lakini mimi nilikuwa na kitu cha kurekodi mazungumzo yetu, na kipo tayari hapa kama ushahidi je nitoe hayo mazungumzo yetu yasikike na kila mtu, na tusije kulaumiana baadae..?’ akauliza mzungumzaji

‘Ndio toa…’akasema mume wa familia, baadae wakili wake akawa anamzuia, wakawa wanateta, jambo, mzungumzaji akawa anasubiria wamalize, na alipoona wanaendelea kuongea kupoteza muda, yeye akasema;

‘Nilishajiandaa kwa haya yote na usahidi kila hatua ni muhimu sana, kama itabidi, nitautoa huo ushahidi na watasikia yote na yale ambayo mume wa familia hatapenda yasikike hapa kikaoni, …’akasema

‘Sawa tumekuelewa…’aliyesema hivyo sasa ni wakili wa mume.

‘Ni kweli maana mume wa mtu alikuwa akinibembeleza, akasahau kuwa ana mke, sasa hayo yakisikika, sio vizuri, au sio, au niyasema hapa ulivyokuwa unanitongoza,..’akasema na watu wakaguna

‘Ni kweli haya ninayoyaongea, ameongea mengi sana na ya aiabu,…wakati mwingine nahisi huyu jamaa yetu hayupo sawa, namuheshimu sana, lakini kavuka mpaka,..na jamani kwa hali kama hii aliyo nayo bado huogopi,.. lakini ndio hivyo, mimi nahisi marehemu alimteka sana akili yake maana yule shemeji ninayemfahamu sio huyu wa sasa,…na pengine, ila mimi sina uhakika na hilo, nasema pengine, hiyo ajali yaweza kuchangia..’akasema.

‘Wakati mnaongea naye, kwa kugusia tu mliongea maswala yapi na yapi, ambayo ni muhimu kama kikao wakayafahamu…?’ akaulizwa

‘Kuna mengi, aliyaongea, mimi kama binadamu siwezi kuyasema au hayafai kusikilizwa hapa mbele za watu, ..maana huenda hakunifahamu kuwa mimi ni nani, wakati namchota akili, na akaingia kwenye anga zangu, akajikuta anaongea kila kitu, hahaha, wewe mtu, uwe makini, hajui kwa hivi sasa kila kauli yake inachukuliwa kwa uzito mkubwa sana, chunga ulimi wako wewe mtu..kwa kuhusu seehmu hii kwa tuliyoyaongea ni hayo, labda kwenye shemu ya pili...'akasema na hapo mume wangu akanywea.

‘Endelea,…kama ushahidi tutauhitajia tutakuambia baadae … ila nina swali..’akasema wakili mtetezi

‘Kuhusu nini…?’ akuliza mzungumzaji
‘Wewe, unaposema kuwa hayo uliyoyafanya uliyafanya kwa kushinikizwa, sio kwamba ulifanya baada ya kuona kuwa mkataba wa familia utakuja kukunufaisha, na sasa unajifanya kujikosha ili uonekane wewe ni mwema..?’ akulizwa na wakili.

‘Kuhusu huo mkataba wao, sikuwa naufahamu kabla, kwani pia unaweza kusema kuwa nilifanya makusudi ili nipate mtoto na huyo mume, ili ndoa yao ivunjike, ili mimi nije kuchukua nafasi ya mke wa mume wa familia, na mali iwe imeshaandikiswha kwa mtoto wangu,..ndio mawazo yak ohayo sio…, au sio..?’ akawa kama anauliza. Na wakili akabakia kimia tu!

‘Hiyo sio kweli, mimi tokea awali nilishawaambia sitaki lolote kuhus mtoto wangu, na pia sina tamaa ya mali, hasa mali hizo za kitapeli, niliwaambia hilo mapema sana wakanishangaa…, na hata kwenye kikao chetu cha hivi karibuni, kama mtataka kuyasikiliza haya mazungumzo utasikia nikilisisitizia hilo, naombeni sana mniamini kwa hilo. Hapa nazungumzo ukweli kutoka moyoni mwangu...'akasema.

‘Kwani kuwepo kwa huo mkataba wao, ulifahamu lini…?’ akaulizwa

Mimi huo mkataba wao wa familia, niliufahamu kutoka kwa maelezo y abosi wangu maana alikuw ani rafiki yangu, hakunificha hilo, lakini sio kwa undani wake, na wala hakuwahi kunionyesha …lakini huo mwingine uliokuja kutengenezwa baadae, nilikuja kuelezewa tu , juu, kwa juu, hawakutaka uonekane.

Nilioweza kuuona, ni huo wa kuhamisha hisa..ili nione kuwa hata mimi nipo, na huo niliuona baada ya kuchukuliwa na wao hado ifisini kwao, niliporudi kwa dharura..’akasema

‘Ulirudi kwa dharura, au ulirudi kwa vile umehakikishiwa mafao…usitake kudaganga watu hapa, hilo jambo la kibali ungeliweza kulimalizia huko huko…’akaambiwa

‘Ushahid upo, huko chuoni, na sehemu za vibali za kwenda kusoma nje, nenda kafuatilie, hapa nina ushahidi wa barua niliyoandikiwa, kuwa kuna tatizo la kibali changu natakiwa kurudi nchini kukamilisha baadhi ya taratibu, ‘kurudi nchini’ ipo wazi inasomeka, mimi nisingelipoteza muda wangu wa masomo kwa hayo mambo yao ya kitapeli..’akasema

‘Je wewe unahisi, hiyo kurejeshwa nchini ni mbinu au ni taratibu za kawaida za vibali…?’ akaulizwa sasa na mwenyekiti.

‘Mpaka sasa kwa uhakika sijalithibitisha hilo, kuwa labda kuna watu wapo nyuma ya hilo tukio, ila kikao kikitaka mimi naweza kuifanya hiyo kazi na nitaweza kuwatolea maelezo yenye uhakika..’akasema

‘Haya endelea na maelezo yako..’akaambiwa na mwenyekiti, japokuwa wakili mtetezi bado alikuwa na maswali anataka kuuliza.

*************.

‘Siku nilipofika uwanja wa ndege nikiwa najiuliza kuna nini kimetokea kuhus kibali changu, kiukweli, moyoni nilikuwa nimemuhisi mdhamini wangu, yaani rafiki yangu kuwa huenda kayafanya hayo kwa makusudi, lakini nimjuavyo yeye, asingelifanya hivyo, angeliniambia moja kwa moja..’akasema

‘Na mpaka nafika uwanja wa ndege bado nilikuwa najiuliza. Na ujuavyo kazi zangu huwa zinanifanya niwe na akili ya ziada, nikawa najiuliza je kama ni kuhusu tatizo la mtoto labda,…ili kumpata baba wa mtoto,basi mtoto wangu anaweza kuwa hatarini.

Nilipojiwa na wazo hilo, kuna mtu nilikuja naye namfahamu na anaifahamu familia yangu, nikaongea naye, ni wazo la haraka lilinijia na bila kusubiria, nikalifanyia kazi..kwahiyo nikamelekeza huyo jamaa yangu , ni nini cha kufanya, tukifika hapo Dar, hakuwa na kipingamizi, akasema atafanya hivyo huyo jamaa yangu.

‘Kama nilivyohisi nilipofika tu, nikavamiwa uwanja wa ndege, walisubiria wakati nimeshaingia kwenye taksii, kumbe hata huyo mtu wa taksi, alikuwa mtu wao, wakasema mimi nipo chini ya ulinzi, nikawauliza kwa kosa gani, wakasema nitaambiwa nikifika kituo cha polis, nikawaomba vitambulisho, wakanionyesha, sikutia shaka

‘Walikuwa ni polisi kweli…?’ akulizwa

‘Mhh…vitambulisho vilikuwa vinaelezea hivyo, sikuwa na muda wa kuhakiki zaidi, na kiukweli sikuwa na muda sana wa kupoteza,…’akasema

‘Sasa wakati tupo njiani, nikasikia wakipigiana simu,, wakaulizwa kuwa mtoto ninaye, wakasema sina mtoto, wakaambiwa waniulize mimi nikawadanganya kuwa sijarudi na mtoto, nimemuacha huko nilipotoka, huyo aliyewapigia akawaambia mimi ni muongo, lakini baadae wakasema;

‘Mkuu kasema, atakuhitajia kuongea na wewe baadae sasa hivi uende nyumbani kwako, na usiwe na wasiwasi, nia ni kukuonyesha kuwa ujio wako una manufaa makubwa, ila usipoleta ushirikiano, kusoma kwako ndio basi tena, hutasoma tena, na mtoto hutampata…’wakasema na hapo nikawa na mashaka, mtoto sitampata tena, ina maana labda walishamteka mtoto wangu..nikasubiria mpaka waliponiachia, ndio nikampigia simu jamaa yangu

‘Mtoto keshafika hapo kwako…?’ nikamuuliza

‘Ndio, mbona…?’ akataka kuniuliza maswali mengi, nikamkatiza kwa kusema

‘Usijali, gharama zote nitakutumia, hakikisha huyo mtoto anabakia hivyo hivyo, ukimaliza kumuogesha, unamvalisha hivyo hivyo…na usimtoe nje, kuna wabaya wanataka kumchukua mtoto wangu…’nikawaambia na kwa vile huyo ndugu yangu ni jamaa yangu anafahamu mambo yangu kidogo, akanielewa.

‘Kwahiyo hadi hapo nikafahamu kuwa mtoto wangu yupo salama, na maelezo mengine kama nilivyotoa kwa rafiki yangu, aliponiuliza kuhusu mtoto wangu, mengi yalikuwa ni namna tu ya kuhakikisha mtoto wangu yupo salama, na kipindi hicho sikuwa nafahamu ni nani wa kumuamini,…nilijitahidi hakuna anayefahamu wapi mtoto wangu yupo, hadi pale niliporudi chuoni…’akasema

‘Hata hivyo, wao hawakujali hilo la mimi kutokuwa na mtoto, hawakulijali sana, walifuatilia wakajua kuwa moto nilikuja naye, sasa kaenda wapi, hapo hawakuweza kupata jibu, wakaona wasipoteze muda na hilo, walichotaka ni mimi kukubali huo mpango wao,

‘Kwanza alitumwa mtu, akiwa na hiyo mikataba nikatakiwa nisome na nielewe, baadae nikapigiwa simu isiyo na namba ya mpigaji, akaniulize kama nimesoma na kama nimesema nasemaje, nikawaambia, mimi siwezi kuongea mambo hayo kwenye simu, na ndio maana baadae nilikuja kuchukuliwa na hao watu hadi ofisi moja, huko uwanja wa ndege, kwa wakili marehemu’akasema

‘Hapo ...nikaonyeshwa tena huo mkataba maalumu, nikaambiwa kuwa, kila kitu kipo kisheria, kilichobakia ni sahihi yangu tu, na nikikubaliana nao, basi nitapata mafanikio mengi, na haki za mtoto wangu, ila nikikataa, mtoto atachukuliwa na mimi nitakipata cha moto, kiukweli sikujali hayo, lakini mtu akinigusia mtoto wangu nahisi kuchanganyikiwa.

‘Hapo nikapima vipi nifanye hilo, kwanza kwa ajili ya usalama wa mtoto wangu, nikaona bora nikubaliane nao tu, halafu mengine yatakuja kufauta baadae,..naona hayo na mengine yaliyofuata baadae nitayaelezea kwenye sehemu ya pili, maana ndani yake kuna mambo ya kisheria, na usalama , kama ni lazima itabidi nitete na mwenyekiti kwanza..’akasema na kutulia kidogo

‘Swali…’ilikuwa sauti ya wakili mtetezi, na hakusubiria kupewa kibali akauliza

‘Wewe umesema uliwahi kusikia mambo kuhusu mkataba wa familia kupitia kwa rafiki yako, na ina maana kuwa wewe ulikuwa unafahamu vipengele vyake, na ulifahamu kuwa ukifanya lolot baya, inakuwa ni tatizo kwa mume wa familia, huoni hapo unatudanganya,..kuwa wewe ulijua hatari yake na bado ukatumia mbinu ili umpate mume wa familia, ukijua masilahi yake…?’ akauliza wakili

‘Kwanza futa maneno yako,..vipengele vipi nilikuwa navifahamu, maana unavyouliza ni kama unafahamu ufahamu wangu wa vipengele ninavyovifahamu kwenye huo mkataba,…lakini pili futa kauli yako kuwa, mimi ndiye nilitumia mbinu kumpata mume wa familia, sio kweli, ngoja nije kuelezea ukweli hasa kwa jinsi gani ilitokea…..’akasema

‘Elezea sasa..mimi siwezi kufuta kauli yangu, wewe ndiye wa kuifuta hiyo kauli kama unaona sio sahihi,..kwa maelezo yako, yenye ushahidi sio unatutungia hadithi hapa…’akasema wakili kukawa na malumbano kidogo na mwenyekiti akaingilia kati na kusema

‘Endelea na maelezo yako, mzungumzaji…’akasema mwenyekiti

NB: Bado kuna muendelezo wa maelezo haya kabla ya sehemu hii ya kwanza, najaribu kupitia pitia, maelezo yake n marefu sana, huenda mengine ni kupoteza muda, kwahiyo ili siku isiende bure, tusome hayo maelezo ..ni muhimu sana, kwani ndio hitimisho ya mambo mengi yaliyotokea kwenye hiki kisa..

WAZO LA LEO: Tusiongee uwongo ili kuhalalisha ubaya wetu, tusisingizie uwongo ili tuonekana sisi ni wema, tusitafute kashfa mbaya kwa wengine ili sisi tuonekane wema, kwa ajili ya masilahi tu ya kidunia. Uwongo, kashfa na fitina kwa wengine kwa ajili ya masilahi kidogo ya hapa duniani, kama kupata cheo, mali, nk.., ni mzigo mkubwa wa madhambi tunayoyabeba mbele ya mola wetu.


Tukumbuke kuwa hayo yote tutakuja kuulizwa siku hiyo ya hukumu. Jiulize swali, je unataka kuyafanya hayo kwa manufaa ya nani, na je una uhakika gani kuwa utapata muda wa kutubia hayo madhambi, na je huyo uliyemtendea kaumia kiasi gani, na je maumivu yake utaweza kuyafidia vipi kwa huyo uliyemtendea...
 
SEHEMU YA 101



‘Wewe umesema uliwahi kusikia mambo kuhusu mkataba wa familia kupitia kwa rafiki yako, na ina maana kuwa wewe ulikuwa unafahamu vipengele vyake, na ulifahamu kuwa ukifanya lolot baya, inakuwa ni tatizo kwa mume wa familia, huoni hapo unatudanganya,..kuwa wewe ulijua hatari yake na bado ukatumia mbinu ili umpate mume wa familia, ukijua kuwa utapata masilahi fulani baadae…?’ akauliza wakili

'Masilahi gani...' akauliza mdada

'Mali, na hata kama ndoa hiyo ikivunjika wewe utaolewa na mume wa familia

'Kwanza umesema mali, kama ndoa itavunjika, huyo mume atapataia wapi mali, wakati hana kitu, atarudia kwenye umasikini wake, maana atanyang'anywa kila kitu si ndivyo mkataba unasema wao halali unasemaje...?' akauliza mdada.

'Kwahiyo kumbe wewe ulikuwa unafahamu kila kitu, kwanini sasa hukufanya juhudi za kuhakikisha hilo tendo halifanyiki...?' akaulizwa

'Tendo gani...?' akaulizwa

'Lililokufanya upate huo ujauzito..kama kweli hukudhamiria hilo litendeke kwa kuangalia masilahi fulani kwako...'akaambiwa.

Tuendelee na kisa chetu

*************.

'Kuhusu undani wa huo mkataba nilishasema nilikuwa nasikia rafiki yangu akiongea baadhi ya vipengele vyake, na moja ya vitu alivyoviongea kuhuus vipengele hivyo, ni kuhusu miiko ya ndoa, alinielezea kuwa mume wake asingeliweza kusaliti ndoa yake, kwani anafahamu ugumu wa mkataba wao ulivyo…’akasema

‘Kwahiyo kwa vile ulilifahamu hilo ukataka umshawishi mume wa familia ili umpate wewe, kwa yeye kuvunja hiyo miiko, ili ndoa yao, ivunjike, na wewe uchukue nafasi ya mke wa familia au sio…’akaulizwa

Mdada huyo kwanza akamuangalia huyo wakili kwa makini, halafu akatabasamu na kusema

‘Kama ni kufanya hivyo ningelifanya hivyo zamani sana, lakini hiyo sio tabia yangu, ulizia, utaambiwa, usitake maneno ndio yawe ushahidi, wakati matendo yalikuwepo, mume wa familia alikuwa akijifanya mpole kwa watu lakini mkibakia naye wawili huwezi amini kuwa ndio yeye, …’akasema

Mume wa familia akatikisa kichwa kama kulipinga hilo.

‘Kiukweli hata walivyoniambia kuwa mkataba wao unawapa mamlaka ya kufanya kila kitu sikuamini, maana mkataba ulikuwa umesajiliwa iweje leo mkataba uwe tofauti,…nikajua kuna jambo limefanyika, nyie mawakili tunaowaamini mnageuza batili kuwa haki, au sio...baadhi yenu nyie, mnathamini sana pesa, na kuacha taaluma zenu pembeni…’akasema na hapo wakili akanywea, na kuangalia pembeni

‘Niambie muheshimiwa wakili, kwanini mligushi huo mkataba, maana hilo sasa lipo wazi,..wewe ndiye wakili wa kutetea mkataba wa kugushiwa, kwanini ulikubali kuusimamia mkataba uliogishiwa,...?’ akauliza mdada

‘Wewe hutakiwi kuniuliza maswali mimi, wewe kama shahidi, unatakiwa ujibu maswali yangu, na sio wewe kuniuliza maswali…’akasema wakili

‘Haya uliza hayo maswali yako, lakin ukae ukitambua kuwa wewe unatetea mktaba batili,.. na ukizungumzia mkataba ujue unazungumzia mkataba upi, mliogushi nyie , au huo wa kitapeli, au..wa halali, ubainishe maswali yako, maana wewe ndiyewakili wao, na unawatetea matepeli…’akasema mdada na mume wa familia akataka kuongea lakini wakili wake akamzuia

‘Endelea na maelezo yako…’akasema mwenyekiti.

‘Kwahiyo kiukweli ndugu mwenyekiti, mimi nilikuja kuutambua ukweli kuwa mkatba umegushiwa, baada ya kurudi masomoni. Na nikagundua ubabaishaji wao wote…na ushahidi ninao, mkitaka kila kitu naweza kukiweka hadharani..’akasema

‘Endelea na maelezo, ushahidi baadae…’akasema mwenyekiti

‘ Huyu mume wa familia kwa kujiamini aliniambia kuwa akitoka huku kwenye kikao atakuwa kamaliza kazi, kila kitu kitakuwa kwenye miliki yake, kwahiyo kinachofuatia ni kuhakikisha kila kitu sasa kinakuwa wazi, mambo ya urithi, na umiliki za mali, nay eye kuchukua hatamu kama mume wa familia…’akasema.
‘Kiukweli kimoyo moyo nilicheka sana, maana ukweli nimeshauafahamu, nikajua huyu mtu keshaharibiwa akili, nilitumia lugha ya kumuonya kuwa hilo haliwezekani, yeye aliniona mimi ndiye mjinga nisiyeelewa, na akaniambia, kama ikishindikina yeye ana plan B, sasa muulizeni plan B, ni ipi hiyo, ndugu wakili mtetezi…’akasema mdada, akimuangalia wakili.

Wakali akawa kimia, akimuangalia tu

' Mimi nilimwambia cha muhimu kitakachomsaidia, ni yeye kupigania ndoa yake tu, vinginevyo, atakosa kila kitu, ndoa, na mali, nilimuambia kuwa kilichomuharibia ni tabia yake hiyo mbaya, tamaa, na umalaya, ..na nilipotamka neno hilo akanijia juu, kuwa nimemtukana, nahisi ndio maana alipokuja hapa, akawa na jaziba hizo hizo za kauli hiyo, lakini matendo…yanajionyesha….’akasema

'Je sio haki kwa baba kudai haki za mtoto, je sio haki kwa mume mliyezaa naye kudai haki za mtoto wake,…?’ akauliza wakili

‘Anaweza kufanya hivyo, lakini sio kwa kugushi, sio kwa utapeli, na mimi nilishamuambia ukweli, kuwa huyu mtoto ni wangu, haina haja ya yeye kuhangaiia, nitaweza kumuhudumia mwenyewe, ….’akasema.

‘Lakini ni lazima mtoto awe na baba yake, na mtoto kama mtoto ana haki ya kuja kumfahamu baba yake, kwanini utake kuuficha huo ukweli, huoni hapo unatuficha mambo kwa kujikosha, ili uonekane wewe ni bora…?’ akaulizwa

‘Ni kweli kuwa mtoto ni lazima awe na baba yake, lakini kwa mazingira niliyompatia huyu mtoto sikutaka kuwe na mtu anayeitwa baba, ukumbuke kuwa hii mimba nimeipata kutoka kwa mume wa mtu, na katika maisha yangu niliipa kuwa sitatembea na mume wa mtu..

'Kuna uwongo ulipangwa kuwa mimi nilikuwa na mahusiano na huyu mwanaume kabla sio kweli...yaliyoyokuwa yakiendelea kati yangu na huyu mwanaume yalikuwa maswala mengine kabisa ya kazi nyingine...sio lazima kuyataja, hayahusiani na hii familia, mimi nina mambo yangu mengi ya kimaisha...lakini pia nilitumia muda huo kumlinda huyu mwanaume, hamjui tu alivyo...kuna mengi nimemuokoa nayo..

'Na pia hili lazima niliseme tu,...hadi mimi kufikia kutembea na mume wa mtu, sio kazi rahis kama inavyoonekana kwa wengi, mimi sipo hivyo jamani.., ilitokea baada ya hawa watu kunifanyia huo ubaya,...na baada ya tendo hilo, sikuwa nimejihakikishia kuwa kweli nina mimba, au mimba ni ya nani hasa,..mtasema kwanini sikuchukua hatua...nisingeliweza maana hata mimi nitaonekana tu nilipenda iwe hivyo,..

'Baada ya kugundua kuwa nina mimba,nikawa nimechanganyikiwa,nilianza kujiuliza ni ya nani, ni ya …unajua usiku ule sikuwa na ufahamu kabisa,..hata hivyo, niliomba mungu na kuvuta subira…

‘Unaona unaanza kujionyesha mwenyewe, unasema, hukujua ni nani aliyekupachka hiyo mimba, kwasababu gani, ulikuwa na wanaume wengi au sio…?’ akaulizwa

‘Hapana sio kuwa na maana hiyo, mimi sikuwahi kukutana na mwanaume mwingine kabla, na mimi sina tabia hiyo ya kihuni, ukiniona na wanaume ujue naongea tu nao tu, au nipo kazini..

‘Tutaaminije hilo, una ushahidi gani wa kulithibitisha hilo..?’ akaulizwa

‘Ushahidi upo…mimi huyu mtoto sikumpata tu kama unavyofikiria wewe,…’akasema

‘Utoe sasa huo ushahid wako, ulimpataje huyo mtoto, kama sio umalaya wako…’aliyesema sasa ni mume wa familia

‘Endelea na maelezo…’akasema mwenyekiti

**********

' Ndugu mwenyekiti, kuna jingine ambalo nataka kulisema hii leo, japokuwa wengi watanishangaa,...inabidi na lenyewe nilisema tu, kuwa ushauri wakati mwingine unaweza kukutumbukiza kubaya, sio kweli kuwa mimi nachukua ushauri tu bila kufikiria, hapana, lakini ushauri mwingine unategemea kama una manufaa,...'akasema

Alipoanza kusema hivyo nikajua sasa anataka kunilaumu mimi, lakin sikujali hilo, nikasubiria tu aongee apendavyo...

'Mimi nilikuja kupata ushauri kwa watu, ni kipindi ambacho, hata mimi nilikuwa kwenye wakati mgumu, unatamani na wewe uwe na mume, uwe na watoto, lakini hajapatikana, ufanyeje…unatamani upate mtu wa kukushauri ufanye nini ili ufanikiwe hilo…kiukweli umri umri wangu ulishakwenda…’akatulia

‘Naombeni mnielewe hapo, simlaumu mtu kwa hilo,..ila naongea ukweli, wa nafsi yangu, nilivyovutika hadi kuhamasika, na hata ilipotokea , sikupenda kujilaumu sana, na siwezi kusema nilivutika kufanya hivyo, kwa vile mimi sikufanya kiutashi wangu pia,…sasa ukiwa kwenye hiyo hali, na ghafla unakutana na ushauri, tena sio wa hivi hivi, wakitaalamu, kutoka kwa mtaalamu mwenyewe, utafanyaje, ..na zaidi unakuja kuupata ushaudri huo huo, kwa watu wako wa karibu unaowathamini, kuwa ukichelewa hutaweza kuzaa tena, au ukizaa unaweza kuwa matatani..hivi kweli tuangalai kote kote, hali niliyokuwa nayo, ilinishinikiza kujiingiza kwenye …’hapo akatulia

‘Mimi ni binadamu, na siwezi kukwepa ukweli kuwa mimi ni mwanamke pia, sisi tulivyo tuna hulka zetu aaah, ndio, naweza kusema hivyo,… ‘akashika kichwa kama anawaza jambo

‘Ni hivi.., nataka muone jinsi hali hiyo ilivyojijenga akilini mwangu hadi kufikia huko, hata kujichanganya na wale ambao nilikuwa nakutana nao, lakini sikuweza kuwapatia ukaribu ule,…ni kweli, nilijikurubish kihivyo, hata hivyo dhamira yangu ilikuwa bado haijakubaliana na kutenda tendo hilo…sikupenda hivyo, sikutaka hivyo, nahasa kwa ..mmh nataka niliongee hili ili munielewe...'akasema huku anakatisha kumalizia..

‘Ndio sikudhamairia hilo…huyo mume wa familia, moyoni analifahamu hilo, hata mbele ya mungu atakuwa ni shahidi..hapa duniani anajidanganya tu..huyo ni kigoo jamani msimuone anatembea kichwa chini…’akasema

Wakili akacheka, na mume mtu akatikisa kichwa kusikitika…n watu wakacheka kidogo.

Kabla ya kuja kulielezea hilo, kuna jambo jingine nataka liwe wazi kwenu, kama mna vichwa vya kuomba mbali, mnaweza kuafikiana name, maana naona muda umekwenda, kuna mambo ambayo hatuyaoni kwa jinsi yalivyo,..kwa ukaribu wa akili zetu, lakini yapo, kwa wenye kuona mbali, sikuwa makini na hili, ila baadae nimakuja kuliona hilo..

‘Yawezekana ikawa ni bahati mbaya, au wanzetu wanasema ‘coincidence’ haya kutokea, au kuna mipango ya kitaalamu ilitengenezwa, hapa sisemi kuhusu kupata mtoto, nasema yawezekana kashfa zilipangwa iwe hivyo, siwezi kuwalazimsiha kuliamini hivyo, maana ushahidi wake ni mgumu kupatikana, ila kwangu mimi nimeamini kuwa kuna namna hiyo ilipangwa, chochote chawezekana kwenye uwanja wa kisiada..’akatulia

‘Unajitetea, au unatoa ushahidi..?’ akauliza wakili

‘Nimeshakuambia, mwenyekiti akiruhusu ‘ushahidi’ hilo litafanyika, usitake kunipotezea muda, hapa…’akasema mdada

‘Endelea na maelezo yako..’akasema mwenyekiti

' Nasema hili hata baba, mwenyekiti wetu hapa ni shahidi, hili tukio zima limekuja kutumiwa kisiasa baadae, je lilijulikana kuwa litatokea, au ni hiyo ‘bahati’ kuwa limetokea sasa tutumie hiyo, kashfa kisiasa, hapo ndio pale tunamuhitajia, mume wa familia afunguke, auseme ukweli, atatusaidia sana kwa hilo…’akasema

Mume wa familia kusikia hivyo, kwanza alionyesha ishara ya ‘huyu anasema nini’ halafu akacheka

‘Kama nilivyosema wengine hatutaweza kuliona hili kwa uoni wetu wa kawaida,..haya kama yalipangwa au la, ila baadae haya sasa yamegeuzwa kisiasa kama kashfa, kwa jaili ya kuibomoa familia ya mzee, na sisis wahanga tunakuwa kwenye wakati mgumu hasa mimi ambaye nilikuwa mmoja wa watekelezaji na walinzi wa hizi familia, inaniuma sana,..’akasema

‘Hayo unayoyaelezea kuwa ni mbinu za kisiasa, ni kujitetea au umeyatoa wapi…?’ akaulizwa

‘Haya nimekuja kuyagundua, baada ya mimi kuingizwa huko, ili nitoe ushahidi kuwa haya yapo, nitaje kuwa nimezaa na nani, na kuahidiwa pesa nyingi, ikiwemo vitega uchumi, na hata kupewa hisa kwenye makampuni mbali mbali, …’akasema

‘Na akina nani…?’ akaulizwa

‘Na akina nani siwezi kuwataja,…lakini mimi sio kama walivyonifikiria wao, kuwa nipo hivyo..hawakupata kitu kutoka kwangu, na hawatapata kitu kutoka kwangu,..nimekana na kukataa mipango yao yote, hilo mniamini, na vitisho vyao kwangui haviwezi kufua dafu,..nimezoea vitisho…’akasema

'Sasa muone ajabu kwa huyo mnayemuita mume wa familia,…hata yeye aliitwa huko, je anaweza kulikiri hili, kuwa hata yeye aliitwa huko, na je aliweza kuitetea familia,je hakuweza kuukubali ukweli, maana haya yote yamejulikanaje huko, ..kiukweli mimi nililificha sana hili,lakini hutaamini huko wanafahamu mengi ya haya,..’akasema

‘Ni nani aliyetoa siri za upande huu na kuzipeleka huko,..yeye asema ukweli, kama hakutumiwa, na huenda alipoahidiwa manono akakubali kushirikiana nayo,…’akasema.

‘Uwongo, acha fitina, toa ushahidi wa jinsi ulivyobeba hiyo mimba, kumbe ulikuwa na mabwana wengi, eeh…ndio maana ulikuwa unaficha ukweli, sasa nimeshagundua.’akasema mume wa familia.

‘Kiukweli huyu mume wa familia alishatekwa huko…na asiposema ukweli, tunaweza kumuona ni msaliti wa hii familia, ndio maana nikasema hapa hapa tutaweza kulibaini hilo, ni nani msaliti wa hii familia,..na huenda hajijui hivyo, na huenda hajataka ila wanamtumia bila ya yeye kufahamu, atuambie basi, akiri ukweli, kama mimi hapa…’akasema

‘Mwongo wewe, kwanini unajenga fitina zisizo za ukweli, unataka nini , ili ndoa yangu ivunjike, ili wewe upate nini…’akasema mume wa familia

‘Kama hujakubaliana nao, na unafahamu fika ni maadui wa mkwe wako, uliwahi kuwaelezea lolote wakwe zako, au mkeo kuwa kuna maadui wa mzee wanataka kukutumia wewe kwa masilahi yao..sema ukweli wako..je uliwahi hata mara moja kuwaonya wanafamilia wenzako, maana hili sio jambo dogoa..?’ akamuuliza mume wangu.

‘Nisingeliweza kukimbilia kuwaelezea hayo, mimi mwenyewe nilijua namna ya kupamabana nao, mimi ni mume wa familia nilijua ni namna gani ya kuilinda familia yangu, maana kama ningelichukulia pupa, je wangekuja kuifanyia ubaya familia yangu, ingelikuwaje,…wewe kwa vile ..huna familia, ok, ndo sasa umepaata mtoto jiulize mtu akitishia familia yako utafanya nini,…’akasema

‘Kwahiyo kumbe ulitishiwa ndio maana ukajiunga na hao watu, kisiri au sio..?’ akauliza mdada

‘Mimi sijasema nimejiunga na hao watu, kwanza hao watu akina nani, sikuelewei kabisa, mimi sio mwanasiasa,..na kuna watu ndio waliniuliza hayo kuwa eti nimzaa na wewe, na vitu kama hivyo, lakini sikuwa na majibu ya kuwaambia, na nilichofanya ni kwa masilahi ya familia yangu, siwezi kuyaonga hapa maana nafahamu athari zak kwenye familia yangu…’akasema mume wa familia, na wakili akawa anamzuia asiendelee kuongea.

‘Mimi nina ushahid mkubwa zaidi ya unavyofikiria wewe, natumai unanifahamu ninafanya kazi gani, kwahiyo siongei haya kwa nia ya kukufitinisha wewe na wakwe zako, hapa na ongea ukweli ulivyo, ukitaka ushahidi upo….’akasema halafu akawageukia wajumbe na kusema
‘Huyu mtu, nilishamuambia akitaka kupambana na mimi ajipange vyema, yeye kwangu kwa mambo hayo sio saizi yangu kabisa, hapa nina kila kitu, ushahidi na sheria bado inanilinda, maana mimi sivunji sheria, mimi sigushi, natafuta hakika na kweli, kama vielelezo viambata, huyu mtu atakuwa alitekwa na kuanza kutoa siri za familia hii, apinga kama nasema uwongo…’akasema

Mume wa familia akasimama na kusema;

'Wewe ni mwongo, mfitini mkubwa wewe..na kuambia, shauri lako, unafikiri kwa kusema hivyo, ndio watakuona ni mnzuri kwao, kuwa uniharibie mimi ili wewe wakuone ni mnzuri,.., kama umeharibu umeshaharibu tu..na ole wako, hao watu wakija kusikia unavyoongea hapa, unafikiri marehemu kafariki vipi, hao watu hawana simile wakiona kuwa wewe umewasaliti, hawasiti kukumaliza, au mtoto..'akasema

'Hahaha, unaogopa eeh, mimi ndio uwanja wangu huo, kifo kwangu kimeshaandikwa, mimi nipo vitani, ndio maisha yangu yalivyo, vitisho, ndio sehemu ya maisha yangu..lakini pamoja na hayo, niliapa kuwa sitakwenda kinyume na mkuu wangu wa kazi, hiyo ni ahadi hata kama hataniamini, yeye ndiye alinijenga hivyo, na yeye ndiye alinionyesha njia, haya yaliyotokea ni bahati mbaya tu...'akasema

‘Hahaha ‘bahati mbaya tu’…, wadanganye hao hao, lakini sio mimi, namimi nina ushahid kuwa wewe una wapenzi wengi na mimi hatukuanza mapenzi..nini, acha niseme…’hapo akatulia, wakili akimzuia kuendelea kuongea

‘Ongea mbona unasita, sema, mimi na wewe tulianza lini, nilipokuwa naishi kwenu au sio……hahaha, ulikuwa unanitongoza, nikawa sikutaki, sema ukweli ili wakusikie huo ni ushahidi mwingine wa kauli yako hiyo, hiyo kauli yako japokuwa wakili wako kakuwahi ni ushahidi mwingine…’akasema

‘Wewe ni mnafiki tu wewe… mbona hutoi maelezo ya ushahidi kuwa huyo mtoto hukumpata kwasababu ya umalaya wako, eeh, jitetee sasa, unanitumia mimi kama ngazi ya kuficha maovu yako au sio…’akasema mume wa familia

'Tutakuja kuliona hilo kuwa mimi na wewe ni nani Malaya au mnafiki, eeh,…’akasema rafiki yangu.

‘Endelea na maelezo yako, tusipoteze muda, mnajichelewesha wenyewe..’akasema mwenyekiti naona hata sauti yake, iliashiria hayupo sawa, nahisi kuna kitu kimegusa nafsini mwake.

********
‘Ndugu mwenyekiti, kwanini huyu mtu hataka kusema ukweli wa hiyo mimba ilitungwaje , sio kwa tabia zake zisizisahihi, na akaja kumrubuni mteja wangu..?’ akauliza wakili, na mwenyekiti akamgeukia mzungumzaji..,

‘Nimeshasema kuwa huyu mtoto hadi kuzaliwa kulikuwa na michakato yake, kabla hata sijafikiria hivyo, kuwa natakiwa kuwa na mtoto, kuna watu walinishauri, kuwa nipate mtoto kwa kila hali..,hata ikibidi nitembee na mume wa mtu,..mimi sikuwa na tabia hiyo kabla, wengi wananifahamu hivyo.., lakini kauli hiyo ilikuwa moja ya sababu iliyonijenga kisaikolojia kuwa kumbe yawezekana eeh..’akasema

'Ni kweli, kiubinadamu labda nisingelitakiwa nifanye hivyo, maana huyo nitakaye tembea naye kama ni mume wa mtu, ana mkewe, je huyo mkewe atajisikiaje, je kama ningelikuwa mimi nimefanyiwa hivyo ningekubali,,..’akatulia kidogo

‘Kiukweli mimi sikupenda hilo litokee hivyo, nilitamani nipate mtoto kwa mtu asiyekuwa mume wa mtu, na ingelikuwa bora zaidi awe ni mume wangu, lakini kwa bahati mbaya sikujaliwa kumpata mume wa kunioa…

‘Sio kwamba sikuwahi kutakwa, au mtu kunitaka kunioa, wapo sana na mmoja wapo ni huyo mume wa familia,lakini kuolewa na mtu asiyekuwa moyoni mwako ni jambo ambalo sikupenda kulikaribisha kwangu, huyu mume wa mtu, ni mume wa mtu nilijua fika hizo ni hadaa zake za kutaka kunitaka, nikamkataa, wapo wengi, siwezi kuwataja, niliwakataa kwasaabu hizo hizo.....'akasema

'Pamoja na ushauri huo kuwa nijitahidi kupata mtoto hata kwa mume wa mtu, lakini mimi sikuwa na dhamira ya kweli ya kutembea na mume wa mtu hususani mume wa rafiki yangu hilo halikuwepo kabisa akilini mwangu..huyu kwangu ni shemeji..’akasema

‘Shemeji eeh…’aliyesema hivyo ni mama, na watu wakacheka

‘Ni kweli mama,..nitawaelezea yote ili muweze kunielewa,..hili jambo lilitokea kwa mbinu za huyo mwanaume kama ni mkweli atalikubali hilo, sio mimi nilifanya juhudi hizo, ni yeye, sijui kama alishirikishwa kulifanikisha hilo, au ni mbinu zake za kufanikisha malengo yake, …ila hilo sio muhimu, ila yeye ndiye anabeba lawama hizo, ...'akasema

'Na sio kweli kuwa mimi nilimtaka yeye, kuwa eti mimi nilimuendea na kumwambia hivyo, kuwa nataka mtoto, na nimeshauriwa hivyo, hapana hiyo sio kweli kabisa, asema kutoka moyoni kuwa nilifika kabla na kumuambia hivyo, hayo ni maneno ya uzushi, tukio zima liligubikwa na mbinu zao, walizozipanga, yeye na ndugu zake, na huenda kama nilivyosema awali, alilifanikisha hilo kukidhi matakwa ya upande wa pili, kw kujua au kwa kutokuelewa, akatumiwa na ikaja kutokea hivyo…’akasema

'Kiukweli mimba yangu ilitokea katika mazingira ambayo sikutegemea kabisa,na mabaya zaidi ikaja kutokea kwa mume wa mtu, na mbaya zaidi kwa sehemu ambayo, najuta kiukweli,…imekuwa ni mtihani kwangu…baada ya kuipata hiyo mimba kiukweli nilikuwa na wakati mgumu sana…hata kujipa matumaini ilikuwa tu, ili nisije kupatwa na ugonjwa wa shinikizo la damu.

‘Kipindi hicho nilijaribu kujificha sana, na hata ilipokaribia siku nikatoweka kinamna lakini kwenye kujifungua ikabidi nije kujifungulia hapa Dar…na ndio ikaliweka hilo wazi kwa jamii… nahisi ni mwenyezimungu alitaka hili tukio libainike, kw avile halikufuata utaratibu ulio sahihi….’akatulia na kuhema

‘Hata hivyo mimi nilijipa matumaini kuwa, kwa vile haya yalitokea ni pamoja na ushauri wa watu, tena sio watu wa hivi hivi, ni watu ninaowaamini, washauri wangu, na wao walisema kwa kauli thabiti kuwa haijalishi, ..muhimu nipate mtoto, basi nimeshampata mtoto, wao kama ni wa kweli kwa ushauri wao wataendelea kunilinda na kunitetea kwa hilo.

'Sio rahisi, kama nilivyofikiria, ilifikia hatua nikajuta,…basi ndio imetokea hivyo sasa nitafanyaje, labda hli ndilo litathibitisha urafiki wetu kwa hao watu kuwa kweli walikuwa wakinijali mimi, au wakijali, yale ninayowafanyia, na walifanya hivyo kuniweka kwenye hali ya kuwaona kuwa wao ni marafiki zangu, naliongelea hili sio kwa kujitetea, maana hata hivyo mimi sikupenda litokee hivyo, huo ndio ukweli wa hilo, sikupenda kabia, mungu wangu ndiye shahidi nafahamu hapa hakuna atakayenielewa kwa hilo..'akasema

Baada ya tukio hilo niliwapoteza marafiki zangu, nikawa sasa naonekana mimi ni mbaya,..kwanini, kwanini, kwanza kwanini simtaji baba wa huyo mtoto,..kwanini namficha huyo mtoto, kwanini…basi ikawa ni taabu kwangu,.. urafiki sasa ukaja kugeuka kuwa ni uadui,…maana lisemwalo lipo halijajificha,..

‘Lakini jamani si nyie mlinishauri, kuwa nikishapata mtoto hiyo iwe siri yangu…na ikibidi, hata huyo baba yake asifahamu, hayo yote yakashindikana,..ni nani alifanya yasshindikane, ni mimi au ni nani, na hadi hapo alaumiwe nani, ..’akatulia

‘Najiuliza ni kwanini sasa nigeukwe, nahata kukamatishwa watoto w a kihuni, ili waje kunizalilisha, hili kiukweli limeniuma sana, lakini hata hivyo hao watoto wakihuni hawakufanikiwa,je ni kwanini hawakufanikiwa, jiulizeni kwa akili za kutafakari na kujifunza, ina maana kweli na mbinu zao, kwanini wakashindwa, maana walishaniziba pumzii na madawa ya kupoteza faamu iliyokuwa imebakia ni kutenda matendo yao maovu, lakini ..mungu akaniokoa, nasema mungu akaniokoa, si vinginevyo,…jiulizeni ni kwanini…kuna jambo la kujifunza hapo…’akasema.

‘Ila sasa najiuliza, kwanini, mumesahau urafiki wetu, mumesahau kuwa nyie ndio mlikuwa washauri wangu wa kubwa, je mliponishauri, hamkulifikiria hilo…sawa limekuwa ni kosa, lakini je hamtaki hata kunipa muda wa kutubu, …’akatulia akiwa anatikisa kichwa kama kusikitika

‘Ni sawa nastahiki adhabu, je mlimfikiriaje yule aliyefanya hili litokee, yeye mlianga adhabu gani kubwa kwake, ambayo nistahiki yake,… je mwafahamu ukweli halisi wa tukio zima hadi mimi kushika mimba hiyo, ilitokeaje, kiukweli, …hili lilitakiwa watu watulie kwanza, wajiulize kwanza, kabla ya kuhukumu,..kuna mambo mengi hapo, hata hilo la kisiasa laweza kuwa ni sababu, litizameni kwa macho mapana..’akatulia

'Kwa bahati mbaya, mungu wngu alitaka nisipate hiyo adhabu kabla ukweli haujabanika, maana kama kweli wangelifanikiwa hao watu, sizani kama ningelikuwa na ubavu wa kuja kusimama hapa hii leo..ila nina amini, hata wao wasingeliweza kuishi…haaah,..hawanijui tu, ingeliwa jino kwa jino, kabla sijafanya walichowahi kufanya wengine…’akasema

‘Siwezi kujiaminisha hivyo, maana kihabari ninayoifahamu kuhusu hao watu wao wakafanikiwa kwako, huwezi kuishi, utatamani ujiue tu, ila mimi nisingejiua kabla hawajauwawa wao kwanza, …akatulia

‘Ila mimi hapo najiuliza kama lengo hilo ni kunifundisha mimi adabu, je ingelitokea kuwa mimi nimepata hii mimba na mume mwingine adhabu hiyo ingelikuwepo pia, au ni mkuki kwa nguruwe tu…najiuliza tu hapo..’akasema

‘Ninachoshukuru ni kuwa wahuni hao hawakufanikiwa, walishindwa kufanya hivyo, baada ya mbinu zao kugundulikana na polisi, vijana hawo sasa wapo jela, na nitahakikisha wanaozea huko jela, na humo wanakipata cha moto, humo nina watu wangu wanaifanya hiyo kazi, waonje uchungu wa kile walichokuwa wakiwafanyia wengine,..na nina uhakika, wakitoka jela, sizani kama watatamani kuishi hapa Dar tena, sasa mkuki umewageukia wao...'akasema

'Nyie mliowatuma mkawatoe kabla haja-ozea huko jela, maana kumbe walikuwa wakitafutwa kwa ushahidi, sasa ushahidi umepatikana, nyie sasa...mnahitajika kuwadhamini, kiutu,..lakini kwangu mimi, wataiona hii dunia ni chungu..wamechezea kusipochezewa..’akatulia

‘Sio vyema jamani, ni kweli inauma…ni kweli kilichofanyika ilikuwa sio sahihi.., lakini hata mimi sikupenda hili litokee hivi jamani…hata hivyo, hivi sasa mimi nimekuwa, nakushukuru sana rafiki yangu uliyejitolea kwa ajili yangu hadi hatua hii, ni wewe uliyenijenga hivi, na sasa nipo zaidi ya vile ulivyonijenga, ninaweza kuishi mwenyewe, bila huo utapeli wao…’akasema

‘Kiukweli mimi sihitajii kujiingiza kwenye utapeli huo ulitakiwa kwangu mimi, lakhasha, nipo kivyangu na namuomba mungu niweze kuishi hivyo, kwenye maisha yangu ya haki, na sio dhuluma, nafahamu fika rafiki , nimekukosea sana, ila wewe ndani ya moyo wako, unanifahamu nilivyo, haya yaliyotokea ni mtihani tu, ni mbinu, na mungu mwenyewe ndiye anajua...’akasema.

‘Ni nani huyo aliyekushauri, maana naona unajitetea hivyo..kusingizia uovu wako..kwa watu wengine?’ akaulizwa

‘Hahaha, mimi sisemi kwa kujitetea, nasema ukweli wa nafsi yangu, kuwa wapo walionishauri hivyo,, kuwa nikazae kwa vile umri wangu umeshapita, hata kama huyo nitakayetembea naye…ni..ni… ,sina haja ya kumtaja huyo mtu, ni utomvu wa adabu, na mim sikulelewa hivyo,..’akasema

‘Kwanini humtaji, mbona mume wa familia, hujajali, umekuwa mwepesi kumnyoshea kidole kwa kila kitu, mabaya yote umeyaelekeza kwake,.. yeye hakuwahi kukutendea wema, wewe uliwahi kuishi kwenye nyumba yao, yeye ni mume wa familia, alikulea, leo hii umesahau fadhila zake…’akaambiwa

‘Tatizo ni kuwa mume wa familia hakubali kosa, kama yeye angelikubali kosa,haya mengine yasingelijulikana, mbona mimi nimekuali makosa yangu nimeelezeakilakitu,..’akasema

‘Lakini pia yeye kama shemeji, mlezi wangu alitakiwa kunilea katika maadili mema, lakini yeye alitumia mwanya huo kunirubuni, kunishawishi, kutumia kila mbinu za kuniingiza kwenye ushawsihi huo mbaya, je huyu anastahiki kuheshimiwa,..niambieni, ukweli, ….’akasema

‘Sasa hata baada ya hayo, kwanini hakubali kusema ukweli,.. je yeye hajakosea, kwanini hakubali sasa..kwa vile yeye ni mume wa familia, kijogoo, au sio,.., sasa hivi mimi nina ushahid hapa wa mazungumzo yake mimi na yeye , kwenye maongei hayo kajieleza alivyo, nilimchota akaongea kila kitu ..naona..eeh, sasa ni wakati wake muafaka auseme ukweli, akiri makosa yake la sivyo, ushahidi huo ufanye kazi yake…’akasema..

‘Hapana, hatuendi hivyo, …’akasema wakili

‘Kwanini, hatuendi hivyo… nyie si mnajiona hamjakosa..mpo sahihi, ngoja wayasikie yale tuliyoyaongea ili kikao hiki kibaini je ni mimi nilimshawishi hadi akanipa mimba au ni mipango yake, huenda hata hiyo mipango, ilipangwa kisiasa na mume wangu akashawishiwa kuikamilisha, kama ni hivyo basi alibainishe hilo, lakini kwa ushahidi sio kwa kujikosha,..’akasema

Mume wa familia akawa kimia…

‘Je mume wa famalia, upo radhi wayasikie au utakubali makosa yako ili kuwasaidia hawa watu, kuwa wewe kweli ndivyo ulivyo, na nia yako mbaya kwao, ili na wao wapate muda wa kukufikiria, au kama hutaki, basi, waniruhusu wasikie japokuwa kidogo, kauli zako, dhidi yao, nafahamu wakisikia hayo, watakufahamu ulivyo…’akatulia

‘Nasema na wewe… au unaogopa kwa vile wakisikia uliyoyaongea kamwe hawatakusamehe..’akasema.

‘Mwongo wewe..hizo ni mbinu zako tu….’akasema

‘Mimi mwongo, eeh,..Je niweke hayo mazungumzo bayana, watu wayasikie…?’ akageuka kumuangalia wakili wake, na wakati huo mume wa familia alikuwa akitaka kuongea jambo lakini akaghairi, na baadae akainamisha kichwa chini

‘Ndugu mwenyekiti, mimi nataka nimalize hii kazi, ili isiwe ni kazi sana kwenu, msipoteze muda wenu bure, wakati ukweli upo bayana, na mimi nashukuru mungu kwa ujuzi nilio nao, niliufanyia kazi, nilijiahidi kukusanya yote…akashika mkoba wake.

Hapa nimekamilika, na sio hapa tu,maana wengine wanaweza kufany ambinu za kuninyang’anya huu ushahidi , ushahidi huu upo sehemu nyeti, na muda wote ukihitajika, unapatikana, …tunaenda kidigitali…

‘Sasa kama mimi nimetangulia kuyasema madhambi yangu, wengine nao wafuate, aje mume wa familia akiri madhambi yake ili aokoe yale ambayo bado sijaanza kuyasema, ninao mengi, hasa sehemu ya pili, hapa ndio kwanza naanza…’akasema

Mwenyekiti akageuka kumuangalia mkewe, kuna kitu mkewe alitaka kumuelezea, wawili hao wakawa wanateta kidogo, halafu mwenyekiti akainua kichwa kuniangalia mimi, kama anataka mimi nisema jambo.

Kiukweli mimi pale nilikuwa nimeshahama kimawazo, kuna muda nilianza kujilaumu, kuna muda nilikuwa na hasira za kutaka kufanya ubaya, kuna muda...niliona sina la kufanya,, lakini hasira chuki, vilikuwa vinikinisakama kooni...pale pale nikawatupia macho watoto wale wawili

Nilimuangalia mtoto wa yule binti, alikuwa anafanana kwa kila kitu na mtoto wa rafiki yangu,...nikajiuliza hao watoto wana hatia gani, kwanini haya yametokea kwenye familia yangu...

'Upo na sisi mke wa familia,...?' nilishituka nikiulizwa na mwenyekiti, sikuelewa niliulizwa swali gani awali, nikajikuta nikisema

'Nipo mwenyekiti, tupo pamoja,...'nikasema

Mara wakili wa mume wangu akanyosha mkono, na ikaonekana kama vile mume wa familia anamzuia,....

‘Mnataka kusema nini…?’ akauliza mwenyekiti akimuangalia wakili huyo, na huku simu yake ikiingia ujumbe akawa anausoma huo ujumbe, na baadae akainu uso kumuangalia huyo wakili. Uso sasa ulikuwa umekunjamana, ina maana ujumbe huo , aliousoma mwenyekiti ulikuwa na jambo nzito...


WAZO LA LEO: Tunapopewa dhamana ya kuhukum, tuhukumu kwa uadilifu, na tunapopewa dhamana ya utetezi, tutetee kwa wema ili haki ukweli uwe bayana, na tunapotoa ushahidi tuwe na uhakika na ushahidi wetu, kwani hapo tunacheza na maisha ya mtu, tunawakilisha sehemu ya haki na ukweli , ukipindisha ukweli na haki ikaenda kusipostahiki, utabeba hiyo dhamana na mzigo huo utakufa nao.
 
SEHEMU YA 102


‘Je mume wa famalia, upo radhi wayasikie hayo mazungumzo yetu mimi na wewe, au utakubali makosa yako ili tusizidi kupoteza muda hapa…?’ akauliza mdada.

‘Wewe umekuja kutoa ushahidi, au sio, kutoa maelezo kwa ajili ya kujikosha, ili kurejesha hadhi yako, hajaitwa hapo, kumuhukumu mtu au kutoa maelezo ni nini mteja wangu afanye, timzi kilichokuleta hapo…’akasema wakili.

‘Na wewe umakuja kufanya nini, kujua ni ninikinachoendelea kwenye hiyo familia, na kukipeleka upande wa pili, au sio,..ushafahamika ndugu yangu, usipoteze muda wako wa maswali yya uchimbi…’akasema mdada.

‘Upande wa pili gani huo, usipoteze lengo..’akasema wakili

‘Unaufahamu sana, tatizo, nyie mnafikiri wote ni wajinga, hapa umeingia choo cha kike, kwa taarifa yako, na siku unaongea na bosi wako, siku ile nilikuwepo, hukuniona tu, hahaha…’akasema na kucheka, na wakili akawa namuangalia huyo mdada kama kumshangaa.

‘Hata sijui unachokiongea, tafadhali jibu maswali yetu na uache kupoteza muda, ndugu mwenyekiti, kwanini unamuachia huyu mtu apoteze muda…?’ akauliza wakili.

‘Kwani hayo aliyoyaongea mzungumzaji,sio kweli, tuambie umafuata nini humu..?’ akauliza mwenyekiti na wakili huyo sasa akashituka, na kugeuka kumuangalia mteja, kabla hajasema neno, na mume wa familia akasema;

‘Ndugu mwenyekiti huyu ni wakili wangu, nimemleta mimi mwenyewe, kwanini mnamzuia asifanye kazi yake..?’ akauliza mume wa familia.

‘Kwasababu wewe ni mjinga, hujui ni nini unachokifanya..’aliyeongea sasa ni mwenyekiti kwa sauti ya hasira.

‘Mwenyekiti, tafadhali,…’akasema mume wa familia, na mwenyekiti akasimama, na kuja hadi pale nilipokaa, akaninongoneza jambo, na alichoniambia kikanifanya nianze kuingiwa na hasira na zaidi ni mashaka kwa mume wangu, nikageuka kumuangalia mume wangu,.alikuwa hajali kabisa, nikabakia kusikitika tu, sikusema neno, na baba akarudi kwenye kiti chake na kabla hajakaa vyema, ....

‘Kama hamtaki niwepo kwenye hiki kikao chenu mimi ninaweza kuondoka…’akasema huyo wakili

‘Hilo ni juu yako wewe na aliyekuleta hapa, sisi hatuna wasiwasi na hilo, ila ni kukuarifu tu, kuwa tunakufahamu, sio kwamba nilikuwa sikujui kabla, ila mzungumzaji amejaribu kuliweka hilo wazi mapema, kabla ya muda wake, sawa wewe fanya ulichotumwa, na waliokutuma, lakini ufahamu kuwa tunakufahamu wewe ni nani..’akasema mwenyekiti, na yule wakili akawa sasa anakusanya vitu vyake kutaka kuondoka.

‘Unataka kwenda wapi wewe, mimi ndiye niliyekuleta hapa, sio wao, wao wanafanya hivyo ili kukuvuruga akili yako, wewe hulioni hilo, ina maana wewe hujawahi kukutana na kesi kama hizi, mimi nilikuwa nakuaminia sana, mbona unanivunja uaminifu wangu kwako, usiondoke tafadhali..’akasema mume wa familia.

‘Tatizo ni usalama wangu, kama wanafamilia hawa hawaniamini, je likitokea tatizo hapa itakuwaje, utaweza kunilinda, huyu mdada keshawalisha sumu hawa wanafamilia dhidi yangu na wamemuamini, hawajui kuwa huyu dada ni ndumila kuwili tu, hamfahamu vyema, nimeshawahi kupambana naye kwenye kesi nyingi mahakamani, yeye ndio zake hizo,…’akasema wakili, na mdada akasema;

‘Unataka nitoe ushahidi kuonyesha mimi na wewe ni nani ndumila kuwili, ...hahaha, kume unanifahamu, kwenye kesi hizo ni nani huwa anashinda...nikuambie ukweli, hapo nilikuwa naanza tu, kuwaonya wanafamilia hawa, kuwa humu ndani yupo mzamizi, au ‘intruder,..’ kwa msisitizo, mimi namfahamu sana huyu mtu, maana hiyo ndio kazi yangu, na pamoja na hayo yaliyotokea, mimi bado nawajibika kwa hii familia mpende msipende…’akasema.

‘Tuendelee na kikao chetu, hilo haliwezi kusimamisha sisi kuendelea na kikao chetu, hiki ni kikao halali na tunachifanya hapa ni halali, hatuna shaka, tuendelee…’akasema mwenyekiti, na mkewe akawa anamnong’oneza jambo mwenyekiti, na walipomaliza kuteta, mwenyekiti akasema;

‘Wakili unaswali la kumuuliza mzungumzaji, kabla hajaendelea na maelezo yake, usiwe na wasiwasi endelea na kazi yako tu, sisi ni watu wema, mambo ya kisiasa hayaweza kutufanya tuwe maadui, wewe ni mmoja wa wapiga kura wangu, lazima nikulinde, tuendee, ..’akasema mwenyekiti,

Wakili yule kwanza akamuangalia mwenyekiti kwa makini baadae akasema;

‘Sawa kwa vile bado mteja wangu ananitaka niendelee na kazi yangu, nitaendelea tu, ila nawaomba mnielewe, mimi ni wakili, na kazi yangu ni kwa mtu yoyote sijali kuwa huyu au yule yupo upande gani, ninaweza nikawa na watu wa kufanyia kazi , na watu hao wapo chama tofauti na huenda kisiasa ni maadui, mimi sitajali utofauti wao, ninachojali mimi ni miiko ya kazi yangu …’akasema

‘Sawa tumekuelewa, hamna shida…’akasema mwenyekiti

*************
‘Mimi bado nilikuwa na swali kwa mzungumzaji, ni kwanini hataki kuwataja, wale waliomshauri yeye kufanya hayo anayosema aliyafanya kwa mashinikizo, ikiwemo ushauri, kama nia ya familia ni kusuluhisha na kuweka mambo yawe sawa kwa kila mwanafamilia, basi ni bora kila mtu akafahamu makosa yake, kama wengine wataogopwa, sizani kama tutaweza kulifikia hilo lengo…’akasema wakili
‘Najua ni kwanini unataka niwataje …’akasema mzungumzaji
‘Vyovyote unavyojua wewe, lakini wajibu wangu ni kumtetea mteja wangu, yeye umemchafua sana kwa lugha tofauti, na yeye ana haki ya kujilinda, na kupambana na wale wote wanaotaka kumharibia jina lake, sasa ni kwanini hutaki kuwataja hao watu waliokushauri, unawaogopa, au kuna sababu gani..?’ akauliza wakili huyo.

‘Nimekuambia hivi, hapa nina ushahidi, na kuna ushahidi na mambo mengine yatatekelezwa baadae kama alivyosema mwenyekiti, kuwataja hao, ni kutoa ushahidi ambao bado muda wake,..na sio kwamba naogopa kuwataja, hapana ,mimi ndiye mtoa maelezo, na mimi ndiye ninayefahamu mpangilio wa malezo yangu , huwezi kunilazimisha niongee utakavyo wewe..’akasema rafiki yangu.

'Sio nitakavyo mimi, bali ni utaratibu wa kuelezana ukweli, ili kila mmoja ajibaini kosa lake, hatuwezi kumzonga mtu mmoja tu, kumbe na wengine wana makosa yao...'akasema wakili

Aliposema hivyo, wakili akamgeukia mwenyekiti, na mwenyekiti akawa kimia, alikuwa akiandika jambo, na kabla mwenyekiti hajasema neno, wakili huyo huyo akasema;

‘Haya endelea, ila umetufanya sisi tuelewe kuwa hapa kwenye hiki kikao, kuna watu wanaogopwa, hata kutajwa majina yao, kuna upendeleo, kuna shinikizo linatakiwa kufanyika dhidi ya mteja wangu, na yeye ana haki ya kujitetea…’akasema wakili

‘Endelea na maelezo yako mzungumzaji…’akasema mwenyekiti.

‘Samahani ndugu mwenyekiti, ningelipenda kukuliza hili, je nimekosea kuuliza maswali kama hayo ya kumtetea mteja wangu…?’ akauliza huyo wakili, na mwenyekiti akamuangalia kwa mshangao, halafu akasema;

‘Labda kwa kukusaidia tu, hapa nina mawakili wawili je umewaona wakiuliza maswali…?’ akaulizwa na akageuka kuwaangalia hao mawakili, halafu akasema;

‘Mimi siwezi kufahamu ni kwanini wapo hapa..., labda mna utaratibu wenu, lakini mimi nimeitwa hapa na mteja wangu siwezi kukaa kimia,ni lazima nitimize wajibu wangu, je kwa kufanya hivyo nimekikosea kikao..?’ akauliza.

‘Hujakosea, …ila nilitaka kukuweka wazi tu, ..’akasema mwenyekiti

‘Sawa tuendelee, au sio mteja wangu…’akasema wakili sasa akimuangalia mume wangu ambaye alikuwa kainamisha kichwa chini, na hakumjibu wakili wake, akamuashiria, jambo, sasa wakawa wanateta, baadae mume wa familia akasikika akisema

‘Muulize swali huyo mdada anayejifanya kujua kila kitu, ..’akasema mume wa familia, na wakawa kama bado hawaelewani, na baadae wakili huyo akasema;

‘Nina weza kuuliza maswali mengine muheshimiwa mwenyekiti..?’ akauliza wakili.

‘Mimi naona tunapoteza muda, na kama ulivyosikia kwa mzungumzaji ana mambo mengi ya kutuelezea, na sisi tunajali maelezo ya kila mtu, ilimradi yawe na nia njema na familia hii, na labda tuendelee naye kwanza, nitamuongoza kwa swali hili ili kufupisha mambo mengine..’akasema mwenyekiti akimuangalia huyo mzungumzaji:

'Kwa ushahidi wewe mara nyingi umeonakana na mume wa familia, mkitembea naye, mkinywa naye na hata ukawa anafika kwako usiku, na hata kulala, halafu unakataa kuwa hakuwa mpenzi wako kabla...hapo sio kwamba kuna ukweli unatuficha sisi...'akauliza mwenyekiti

Na wakili akataka kuingilia hilo swali, lakini mwenyekiti hakumpa nafasi, akawa anamuangalia mzungumzaji

'Labda niwaelezee hivi, awali kabisa mimi nilikuwa namuogopa sana shemeji yangu huyu, sio kumuogopa kihasa, hapana nilikuwa namuheshimu, kama nilivyosema awali mimi awali nilikuwa naishi na familia hiyo..’akasema

‘Na kama shemeji, ni lazima nimuheshimu mume wa dada, mume wa bosi wangu, na kwa hiyo nikawa na mipaka yangu,…, sikuwa na ukaribu sana na yeye, yeye ndio alifanya juhudi hizo za kuondoka huo uwoga wangu, alikuwa anajitahidi sana kunifanya nisimuogope, na haya hayakuanzia nje, yalianiza hata nilipokuwa naishi nao...'akasema.

‘Inategemea na jinsi ulivyokuwa unajiweka, huenda tabia na mienendo yako ilimfanya afanye hivyo…’akasema wakili kabla hajaruhusiwa kuongea

‘Afanye hivyo nini..?’ akauliza mzungumzaji

‘Hivyo ulivyosema wewe, kuwa alijitahidi kuondoa uwoga huo, na ni kawaida mtu mkiishi pamoja, utafurahi wote wakiwa sawa, je kama angelikuwa mkali tu, ungelimfikiriaje, sema ukweli wako kuwa, hata wewe ulikuwa ukimtamani, na hilo sio nazusha, kwa kauli yako ulishasema, wewe ulikuwa ukiwapenda, waume za watu, hasa huyo shemeji yako…’akasema wakili na maneno hayo ya mwishi, ‘’hasa shemeji yako’ akayakazia zaidi.

‘Ukweli hauwezi kujificha, muulize mke wa familia, pamoja na haya yaliyotokea hatashindwa kuusema ukweli kuhusu tabia yangu nilivyokuwa nikiishi nao, je mimi nilivuka mipaka yangu ya ushemeji,…’akasema

Mimi sikuwa tayari kusema neno nikabakia kimia tu.

‘Yeye hawezi kukuchunguza wakati wote, je alipokwua hayupo, labda ndio ulikuwa unafanya hivyo kuigiza wema akiwepo, akiondoka wewe unakuwa mtu mwingine, ipo hiyo, na hayo yamejidhihirisha pale ulipopata mwanya, ulipoweza kuishi kwako, ukawa unamvuta mume wa familia, hadi mkawa mnakula wote, mnakunwya wote, je kama mwanaume unafikiri yeye angalifanya nini eeh,,kwahiyi bia na mienendo yako ndiyo kishawishi …’akasema wakili.

‘Labda nielezee hapo …maana umenipeleka sehemu ya mbali ambayo nilikuwa bado sijataka kuilezea…’akasema mzungumzaji

'Ujue kuwa ofisi yangu ninapofanyia kazi ipo karibu sana na ofisini yake na katikati yetu, kuna hoteli kwahiyo nikitoka kwenda kula chakula cha mchana, ninapita kwenye ofisi yake, sasa bwana huyu alikuwa kama ananisubiria, kila nikipita hapo yeye anakuja kwa nyuma, au tunaongozana naye… je ningelimfukuza, shemeji yangu,…eeh..'akasema

‘Endelea kuelezea, ulivyomnasa…’akasema wakili na hapo mwenyekiti akaingilia kati na kusema

‘Tafadhali wakili, tufuate utaratibu, tumuache mzungumzaji aendelee na ikifiki seehmu ya maswali tutakupatia nafasi, tafadhali muheshimiwa…’akasema mwenyekiti.

‘Sawa muheshimiwa mwenyekiti,..tupo pamoja…’akasema wakili, na wakawa wanateta na mteja wake, na mdada akawa anaendelea kuongea;

'Kwahiyo ukaribu huo, na kuonekana hivyo ndio maana watu wanafikia kusema mimi nilikuwa rafiki yake kabla na mimi kama mwanamke nilishamfahamu mapema huyo shemeji yangu ana lengo gani kwangu,..namuheshimu, na ni sheemji yangu,..hata hivyo mimi sikutaka kumzalilisha, au kujizalilisha kwake, nilimpa nafasi yake kiheshima...'akasema.

'Una uhakika kuwa, wewe hukulifanya hilo kama mtego, kuwa upate ushauri kutoka kwa watu wako wa karibu, na uutumie huo ushauri kama chambo, ili iwe kisingizio, baada ya wewe kuwa mumeshajuana na mume wa familia, na inaonekana mlikuwa na sehemu mnakuatana naye kwa kificho, kwa ndugu yako mmoja..ushahidi huo upo..'aliyeongea sasa ni mama, na mwenyekiti alitaka kumzuia lakini mama alishauliza hivyo.

'Najua hilo litakuwa limejulikana hivyo, na sio kweli kuwa sehemu hiyo tuliitumia kwa nia hiyo, hapana, yeye mwenzangu ndiye aliitumia sehemu hiyo baada ya kushindwa kila namna, akamtumia ndugu yangu huyo, ili yeye afanikishe mambo yake, hapo kwa ndugu yangu alipotumia kama moja ya mitego yake..’akasema

‘Tatizo ni kuwa, yeye hakufahamu kuwa kila wanachopanga na ndugu yangu huyo, ndugu yangu huyo alikuwa akiniambia, yule ndugu yangu ni mtafuta pesa, akajua hapo ni sehemu ya kuchuma, cha mjinga huliwa na nani...'akasema mzungumzaji

'Je tukimuita huyo ndugu yako akausema ukweli, huoni kuwa hayo yote uliyoongea yataonekana ni uwongo..?' akauliza wakili wa mume, na akaongeza kusema;

‘Samahani mwenyekiti imenibidi niulize hilo swali kuongezea swali la mama, natumai sijakosea..’akasema

‘Sawa…’akasema mwenyekiti.

'Muiteni huyo ndugu yangu, hamna shida kabisa,.., nashangaa kwanini hakuitwa hapa kama shahidi..tunao ushahidi wa kuwa sehemu hiyo ilikuwa ni sehemu ya mume wa familia, kufanyia madhambi yake na hilo mkitaka naweza kuwaonyesha sasa hivi, kuna mitego mingi humo, kuna ushaidi mwingi humo, na ndio maana nasema huyo mume wa familia hawezi kukwepa lawama hizo kuwa yeye ni Malaya, tofautio na anavyotaka kutuchafulia sisi …'akasema akimuangalia mwenyekiti.

'Huyo mume wa familia, ana mengi, waulizeni hata wahudumu wa hotelini na bar, alizokuwa akilewa, waulizeni watakuambia ukweli kumuhusu yeye, na sitashangaa nikisikia pia yeye ana mtoto mwingine na wahudumu hao..’akasema na watu wakaguna.

‘Mnaguna hilo, ina maana hamjui…hahah, akane tukamuite huyo mdada na mtoto wake, tatizo ni kuwa damu yake ni kali sana, haweza kujificha, nashangaa kama hilo nalo hamlifahamu, hahaha, huyo ni kidume cha mbegu, msione kampuni inafirisika mkazani ni maeni ya kikazi tu,…ameyataka yeye mwenyewe, ulizeni maswali zaidi ili niweze kufichua uovu wake...'akasema

'Inasadikiwa kuwa wewe lengo lako na mume wa familia ni kuhakikisha kuwa mkataba huo wa kugushiwa unafanikiwa ili wewe uje kuoana na huyu mume wa familia, na hata usipofanikiwa, unajua kuwa mume wa familia atavunja ndoa yake, na wewe utachukua nafasi ya mke wa familia na kuendeleza yale mliyoyaanza hilo ndilo lengo lako, maana wewe umshakiri kuwa kweli unampenda, kweli si kweli..'akauliza mama

‘Hilo swali lilishajibiwa…’akasema mwenyekiti, lakini mdada akaendelea kuelezea

'Hiyo sio nia yangu, yeye ndiye alikuja kunitamkia hivyo, kama mnataka ushahid upo mtasikia kauli yake yeye mwenyewe, akisema hivyo kuwa lengo la mume wa familia nikuwa mkataba utampa yeye mamlaka, kwahiyo anaweza kunifanya mimi mke wake, kama mke wake atafiki mahali pa kutaka wao waachane, lakini nikaja kugundua kuwa hiyo ni moja ya lugha zake kwa wanawake wote anaowataka,...'akasema.

‘Kwangu mimi alikuja kwa mbinu hizo mapema, akinitaka, nikaona sasa amekwenda mbali, nikampasha ukweli, kuwa asinione mimi nipo karibu naye, na asinione mimi najipendekeza kwake kwa namna hiyo, mimi sio mhumi, nilimwambia wazi wazi kuwa mimi nawaheshimu sana waume za watu, na sitatembea na mume wa mtu abadani, muulize kama kweli anataka kusema ukweli…’akasema.

‘Na hata huko kulewa kupitiliza, alikuja kuniambia kuwa moja ya sababu inayomfanya alewe kupiliza ni kwasababu mimi nimemkataa na ananipenda kiasi kwamba hawezi kukaa mbali na mimi, na anapenda kila siku niwe naye, na zaidi angelipenda mimi niwe mkewe wake..’akasema na wakili akataka kuongea

‘Muulizeni yeye mwenyewe kwanza, asimtumie wakili, akatae yeye mwenyewe kwa kinywa chake..’akasema rafiki yangu akimwangalia mume wangu

Mume wangu hapo akainua uso wake na kucheka kicheko cha dharau, utafikiri linaongewa jambo la maana sana kwake, hakufahamu jinsi gani nilivyokuwa naumia.

‘Basi akawa analewa kiukweli, mwanzoni nilijua ni mbinu zake, tu, lakini akawa analewa mpaka anakuwa ni mtu wa kubebwa, na wakati mwingine tunakuwa pamoja naye, mimi sinywi kihiyo, kwahiyo ikawa tunafanya kazi ya kumbeba mimi na ndugu yake, na akilewa ndio anabwabwaja ukweli, kuwa kulewa kote ni kwasababu yangu,....anasema siku nikimkubalia tu ombi lake ataacha kabisa kulewa.

‘Hali hiyo ikawa na mimi inanitesa, kwani kimoyoni kiukweli, nilitamani nifanye hivyo ili aache pombe lakini sio kwa kuvunja udugu wetu,, na ibilisi ana nguvu sana, kuna muda nilitamani basi labda awe ni mpenzi wangu wa siri, au nyumba yake ndogo, kama alivyotaka yeye, lakini bado nafsi yangu ilinisuta…haya nayaongea kutoka moyoni…’akasema.

‘Nilijaribu sana kumfanya rafiki yangu anielewe kuwa mume wake yupo hivyo, kabdilika na kubalika huko kuna mengi, huenda chanzo kinaweza pia kutoka ndani yao wao wenyewe..kwa kujali kazi zaidi kuliko ndoa yao, lakini hata nilipotumia lugha ya busara kwake, niliona kama ananiona mtoto mdogo nisiyejua mambo ya mke na mume..’akatulia

‘Ina bidi hili niliongee hivyo, sio kwa kujitetea… samahani kwa hilo, ila ndivyo livyokuwa..’akasema

‘Hebu kidogo, unasema yeye alisema kuwa kaanza kulewa hivyo kupitliza kwa vile wewe hukuweza kumkubalia matakwa yake, kwahiyo kulewa kwake sio kutokana na mambo ya kifamilia…?’ akaulizwa

‘Jibu analo yeye mwenyewe, ila kwa kauli yake kwangu aliwahi kutamka hivyo, kuwa kaamua kulewa hivyo kwa vile mimi nimemkatalia..na atakuwa tayari kuacha pindi nikimtimizia matakwa yake…’akasema mdada

‘Wewe ni mwongo, sio kweli, kulewa kwangu kuliwa na mambo yangu mengi, ambayo hayakuhusu…’akasema mume wa familia.

‘Naona huko sasa kunatosha, …’akasema mwenyekiti alipoona wakili ananyosha mkono kuuliza swali

‘Inatosha, mzungumzaji, nataka uendelee, lakini sasa hivi ili tusipoteze muda, unaonaje ukituelezea ukweli hasa…maana uligusia kuwa mimba hiyo hukuipata kwa jinsi ulivyodhamiria, ilikuwaje.. hujatuambia uliipataje hiyo mimba..?’ akuliza mwenyekiti,…’akaambiwa

‘Sawa nilipanga kuja kuliezea hilo kwenye mpangilio wangu, …’akasema akimuangalia mwenyekiti, na mwenyekiti akaangalia saa, halafu akaniangalia na mimi, mimi nilikuwa kimia, nikiwaza hili na lile, na nilipoona mwenyekiti ananiangalia mimi nikasema;

‘Mwache aelezee, nataka kufahamu kila kitu..’akasema mama baada ya kuniona mimi nipo kimia

‘Ni kweli kwua tukio hilo lilikuja baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu wangu wa karibu, lakini sio kwamba nilikuwa na dhamira ya kufuata ushahuri huo, sio kwamba ilikuwa ni moja ya mtego wa kulifanikisha hilo..mtakaoelewa vibaya shauri lenu.’akasema

‘Siku hiyo kulikuwa na sherehe, na mume wa familia kama kawaida yake akazinywa pombe kama anashindana nazo, na mimi siku hiyo sijui ni kwanini na mimi nikanywa tofauti na siku nyingine...’akasema na kumtupia jicho wakili akitegemea nen o kutoka kwake, lakini wakili hakusema kitu,

‘Ulevi ni mbaya jamani…hapo mojaikazaa jingine, tulijikuta tupo kwangu,...na usije ukasema nilipanga mimi iwe hivyo, hapana, na wala sikujua kuwa itatokea hivyo, na hiyo sherehe, mimi sikupenda kuwepo, kuna mambo yalitokea mpaka nikajumuika....ilikuwa hivi…

Baada ya kunywa kwenye hiyo sherehe na tukawa hata kutembea inakuwa shida, aliyefanya kazi ya ziada kutusaidia alikuwa mdogo wa mume wa familia, alituchukua hadi nyumbani kwangu, tulipofika kwa vile nimelewa, nikawa sijui ninachokifanya, nilitaka mimi nikalale wao waondoke…hawakutaka kufanya hivyo.

‘Japokuwa nilikuwa nimelewa lakini bado nilikuwa na ufahamu wangu, mimi sipo hivyo, siendekezi kulewa mpaka akili ibadilike, najiheshimu, najua ni nini ninachokifanya, …sasa kilichotokea ni kuwa nilipotoka kwenda kujisaidia, nilichelewa kidogo, kuhakikisha nimesafisha tumbo, najua jinsi gani y akufanya kuondoa ulevi mwilini,..nikarudi, sasa nikiwa sijambo

‘Una maana gani kusafisha tumbo..?’akaulizwa

‘Niliweka kidole kooni na kujitapisha, labda niseme hivyo mpate kunielewa, kwenye kazi zetu hilo linaruhusiwa, ili kufanikisha mambo…’akasema

‘Endelea…’akaambiwa

‘Nakumbuka wakati narudi, niliwaona ndugu wawili wakiongea jambo..’akasema

‘Ndugu wawili nani na nani…?’ akaulizwa

‘Mume wa familia na mdogo wake…yule ambaye yupo karibu sana naye,..’akasema

‘Ina maana siku hiyo wote walikuwepo…?’ akaulizwa

‘Ndio, ndugu zake wote wawili walikuwepo..’akasema

‘Duuh…’aliyesema hivyo ni mama watu wakacheka

‘Mama sio kwamba…’akataka kujitetea

‘Endelea,…mama hana maana hiyo..’akasema mwenyekiti

‘Waliponiona wakaacha kuongea, maana huyo ndugu yake alikuwa kakaa upande mwingine, akaondoka pale kwa kaka yake na kwenda kukaa sehemu ambayo likuwepo awali,… pale pale nikahisi kuna jambo, mimi kama mpiganaji nikahisi hivyo, nikaona nijihami..lakini kama unavyojua tena kilichopangwa kutokea kitatokea tu,..

‘Mimi muda ule, hata nilipofika pale sikutaka kuendelea kunywa pombe, nilikuwa nakunywa kinywaji cha kawaida, nilishawaambia mimi imetosha sitaki kunywa tena pombe

Wakati nakwenda kujisaidia, niliacha chupa nusu…kwa muda ule sikuwa na wazo baya kuwa inawezekana wakafanya hivyo, sikuwa na shaka na hilo, nilikuwa nawazia mengine kabisa, ya kujihami,..pale kwa taratibu nikamimina na kunywa maana hapo nilikuwa na kiu…nikanywa fundo moja, la pili, ndio nikahisi tofauti.

‘Hii soda ina nini…imeharibika nini…mbona haikuwa hivi kabla’nikasema nikitamani kutema lile fundo jingine lilikuwa mdomoni…

‘Umelewa wewe….’akasema ndugu wa mume, wakawa wanacheka na kunitania, hawakufahamu kuwa mimi nilishajipunguzia ulevi kichwani kiasi fulani.

‘Hapana nina shaka na hii soda…’basi nikaiweka pembeni, nikachukua nyingine, ilikuwa imefunguliwa pia, nikaanza kuinywa

‘Mbona zote zipo hivyo…’nikasema na wao wakawa wakinicheka, ikawa ni utani tena, .. tukatulia, sijui kwanini nikaendelea kuinywa ile soda, baada ya mazungumzo, utani, kucheka..ooh, nikahisi tofauti, mwili ukawa umelegea, …nikawa sasa sijatambui kabisa.

‘Nyie kuna kitu mumenif-fa-fa-nyia…’nikasema hivyo tu, yaliyofuata hapo ilikuwa kama ndoto kwangu…, ‘akasema

‘Una uhakika kuwa sio ulevi wa kawaida, uliokufanya hivyo…?’ akaulizwa

‘Hapana mama,…nilishajiflashi…nilifanya kama nilivyosema awali, na nilirejea pale niliwa sina ulevi..sio kwamba ulikwisha kabisa,lakini kwa kiasi kikubwa mimi nilikuwa nipo sawa,…’akasema

‘Oh, ikawaje sasa…?’ akaulizwa

‘Baada ya hapo nikawa hata kuinua mkono siwezi, akilini nikajua kabisa kuna kitu wameniwekea kwenye ile soda, na kiukweli kilichoendelea hapo ilikuwa kama mtu upo kwenye njozi ya ukweli,…ndio hapo wakafanikisha malengo yao..’akasema

‘Waka..ina maana wote..?’ akaulizwa

‘Mama, hapo sijui mimi, lakini sio wote kama ninavyosema ni ..ilikuwa kama ndoto, niliyemuona ni huyo mume wa familia, kwasababu walisaidiana kunibeba hadi chumbani kwangu,..nasemea hivyo, kwa vile nilipoamuka nilijikuta nipo chumbani kwangu…’akasema

‘Kwahiyo hukujua kuwa wao walikubeba hadi chumbani kwao..?’ akaulizwa

‘Sikujua,,..ila nilijua kuna kitu wamenifanyia…’akasema

‘Je una uhakika kuwa aliyekufanyia hivyo ni mume wa familia…?’ akaulizwa

‘Ninaweza kusema hivyo, kwa vile nilipoamuka nilimkuta kitandani tukiwa tumelala naye…’akasema

‘Swali una uhakika kuwa ndiye aliyekufanyia hivyo, maana hapo walikuwepo wote, na watoto wanafanana na ndugu hao, akiwemo mume wako, ndugu hao wote wanafanana..?’ akaulizwa

‘Uhakika huo,…kinjozi, nakumbuka ni yeye,…lakini siwezi ..’akatulia

‘Kwa ufupi huna uhakika,…’akasema wakili wa mume.

‘Lakini kwa mara ya pili nilikuwa na uhakika huo…’akasema

‘Ohoo, kumbe kuna mara ya pili, kumbe sasa ilikuwa ni fungulia njia, muonja asali sio..’akasema mama

‘Hapana sio kwamba baada ya hapo niliona ni jambo sahihi, au nilijilegeza kwake, hapana kiukweli baada ya tendo hilo, tulikorofishana sana, mpaka nikataka kuwashitaki, wao kwa pamoja walikuja kuniomba msamaha, …nikaona basi tena, ni ulevi yaishie hapo tu, ila baada ya kutokea mara ya pili, tulifka kubaya, waulize kama ni nini nilikifanya,…’akasema

‘Sio kwamba ulifurahia, ndio maana ikatokea mara ya pili…’akasema mama

‘Hapana mama, sio mimi…na sio kwa njia hio, hivi hapo kuna starehe gani, ..hakuna chochote cha kufurahia, ni kunizalilisha tu, na kama nilivyowahi kusema haya mambo yana mkono wa mtu wa tatu, sio bure, haya yalipangwa yafanyike hivyo, na kama mume wa familia atakuwa mkweli tunaweza kulithibitisha hilo…’akasema

‘Ok, ikawaje…?’ akaulizwa

‘Nilikuja kuzindukana usiku nahisi ilikuwa ni saa tisa hivi,…bado mwili wangu hakuwa sawa, lakini nikajitahidi, nikatafuta dawa yangu maalimu ya kuondoa sumu mwilini…nikainywa, nilitapika sana…baadae nikawa safi.

*************
‘Kwahiyo ulikunywa hiyo dawa ya kuondoa sumu wakati gani..?’ akaulizwa

‘Nilipoamuka tu, nikakimbilia chooni, nikanawa, na nilipoona bao sipo vizuri,nikaelekea sehemu ninapoweka dawa zangu za zarura kama hiyo nikanywa, na kurudi chooni,…’akasema

‘Ndio baadae nikarudi chumbani na kumkuta mume wa familia kalala kitandani,..’akasema

‘Alikuwaje…yaaani alikuwa kava au yupo uchi…?’ akaulizwa

‘Yupo uchi…’akasema na watu wakacheka kidogo.
‘Kwahiyo ukawa na uhakika kabisa kuwa tendo lilifanyika,..?’ akulizwa

‘Ndio…’akasema

‘Utakuwaje na uhakika wakati ulikuwa hujitambui, je kumuona akiwa kalala hapo kitandani kwako kutawezaje kulithibitisha hilo…?’ akauliza wakili.

‘Nimekuambia mimi mwenyewe nilihisi kuwa nimefanyiwa jambo, pia usiku ilikuwa kaam naota nafanyiwa hivyo, ..nabakwa, au nisema hivyo…’akasema

‘Na nani..una uhakika ni nani..?’ akaulizwa walili

‘Unajua unataka nijibu utakavyo wewe…viashiria vyote vinaonyesha kuwa ni mume wa familia…’akasema.

‘Haya ikawaje…?’ akaulizwa

‘Nilipomuona huyo mtu kwanza niliogopa, nikawazia mbali, nikamuwazia rafiki yangu, kiukweli, nilihisi dhambi, nilihis kukosa, japokuwa wao walinifanyia hivyo bila idhini yangu…kwa haraka nikamuamusha, nilipoona hasikii nikachukua maji kumwagia, akazindukana, kwa hasira,..’akasema

‘Nilipandisha hasira, nikawa nafoka, mpaka mwenyewe akajua kweli nimekasirika, kwa haraka nikamwambia atoke chumbani kwangu…ili kuwa ni hasira kweli mpak ndugu zake wakaja kuamua ugomvi huo.

‘Hata hivyo hakutaka kuondoka, ikawa ni kazi kwa ndugu hao kumshawishi huyo mwanaume ili waondoke, wakaongea wenyewe baadae akakubali kuondoka, kwahiyo hapo nyumbani akachukuliwa na ndugu huyu mdogo sikujua kuwa ndugu huyu mwingine alibakia,..mimi nikarudi kulala, nikijua wote wameondoka, kumbe huyo mmoja alibakia , akaja kuingia chumbani kwangu, wakati huo nipo usingizini, nashtuka mtu huyu….

‘Unataka nini,..?’ nikamuuliza, akasema kaambiwa na kaka yake abakia kulinda usalama, wangu

‘Ondoka ndani kwangu haraka..’nilimwambia hivyo na jinsi alivyoniona nilivyoksirika, aliondoka.

Hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza, kutendekea hilo na huyo mtu, hata hivyo sijui kama ni shetani, au ndio ilipangwa hivyo, ikatokea tendo hilo siku nyingine, wakanitegea hivyo hivyo..nilikuja kugundua kuwa kumbe walikuwa wakiniwekea madawa fulani ya kulevya..ukiyanywa unaweza ukafanya mambo ukiwa hata usingizini, kama vile mtu anayeota huku anatenda jambo, na walisema yanaitwa phencyclidine, au jamii ya hizo…,’ akatulia.

‘Unasema ukinywa unafanya mambo kama unaota…mmh, kumbe, nakumbuka hali hiyo ilikuwa ikitokea kwa mume wa familia, naanza kupata picha…’akasema mwenyekiti…na akauliza swali jingine

‘Uligunduaje hilo…?’ akaulizwa

‘Niligundua hilo baada ya tukio hilo la pili, mimi nilichukua mabaki ya kinywaji kile na kwenda kukipima, na kilipopimwa, kinywaji kile kikaonekana kina madawa hayo ya kuelvya, nikaandikisha kumbukumbu kama ushahidi, siku zikaenda nikawa nimeyaacha hayo matukio kama yalivyo.

Baada ya mwezi kupita, na nusu hisi nikahisi sipo sawa, nikajua ni malaria, nikatumia dawa, lakini ile hali haikuisha, nikaone nikamuone dakitari, sikwenda hospitali ninapojulikana, ndio nikaja kugundua nina mimba...’hapo akatulia na kumwangalia mwenyekiti ambaye alikuwa mara kwa mara akiandika kitu kwenye makabrasha yake kama vile ananukuu hayo yanayoongewa.

‘Sasa kwanini hukushitakia, ukijua kuwa madawa hayo ya kulevya ni haramu, hayaruhusiwi au wewe unatumia hayo madawa ya kulevya…?’ akaulizwa

‘Sababu kubwa ni kuwa nimepata kile nilichokitaka japokuwa sio kwa njia niliyoitaka..si ndivyo unavyotaka mimi niku jibu hivyo..’akasema na kuuliza.

‘Aaah, jibu unajua wewe mwenyewe, inavyoonekana ndio hivyo…’akaambiwa

‘Kiukweli kuwa na mimba nilikuwa nakutaka sana, lakini, tatizo ni jinsi gani nilivyoipata, sio njia sahihi, kiukweli ilinipa shida,…’akasema

‘Utakuwa na uhakika gani, kwani ina maana muda wote huo hukuwahi kutemeba na wanaume wengine..?’ akaulizwa

‘Mimi sina tabia ya uhuni, ni tofauti na watu waanvyoniona, kama nilivyosema awali ukiniona na wanaume nipo kazini, au napoteza muda tu..kwahiyo kipindi chote hicho sikuwa nimewahi kukutana na mwanaume yoyote, kwani baada ya matukio hayo mawili kulikuwa na kazi nyingi sana, …’akasema

‘Tutakuwa na uhakika gani..?’ akaulizwa

‘Uhakika kwa vipi…maana mimi ndiye ninayesema, na hapa ni ukweli mtupu n au uhakika gani mwingine mtoto si huyu hapa, muangalieni mniambie hii sura ni ya nani…’akasema

‘Labda ni hao wadogo zake mume wa familia, na pili ni kwanini hukushitakia, hapo kuna kitu umetuficha…’akaambiwa

‘Lakini mimi niliona hata nikisema bado nitaonekana mimi ni mkosaji, moyoni nikasema itakuwa siri yangu, na sikutaka tena kuwa karibu na hao watu nikajitenga na hao watu kabisa…’akasema

‘Hao, watu ina maana ulikuwa na wanaume wengu au sio…’akaambiwa

‘Wewe wasema,… nikisema hao watu, ni hao niliokuwa napenda kwenda kustarehe nao, akiwemo mlengwa, yaani mume wa familia..muulizeni, asema ukweli kama hayo hayakutendeka,..yeye mwenyewe alifanya juhudi kubwa sana, lakini hakufanikiwa, na hata kuhamishiwa huko Zanzibar, ilikuwa moja ya mbinu zangu za kumkwepa…’akasema

‘Kipindi cha ujauzito kilikuwa kigumu sana kwangu, nilijitahidi sana kujizuia, na kujificha ili watu wasifahamu kuwa nina mimba, ukizingatia kuwa mimi sina mume, nilichofanya ni kuvaa manguo mapana, na kutokuonekana kwenye kadamnasi za watu..

‘Nashukuru pia kipindi chote hicho, cha ujazito wangu hakukuwahi kutokea kazi nyingi za nje ya ajira yangu, yaani kazi zangu na bosi wangu, na kama zilitokea niliweza kuwapa wasaidizi wangu, wakazifanya na kwahiyo sikuweza kukutana na mshauri wangu ambaye pia alikuwa ni bosi wangu, kwahiyo sikuwa na wakati mgumu, wa kujieleza, na siku zikaenda na hauchi hauchi , miezi nane ikafika,

Nilizaa nikiwa na miezi nane, na mambo yakaanzia hapo, na pamoja na furaha ya kupata mtoto, lakini ilifikia mahali nikaanza kujuta, kuwa kumbe nilichukulia mambo hayo kwa haraka, japokuwa sikuwa nimedhamiria hilo tendo liwe kama lilivyotokea,

‘Najua wengi watasema mimi ni mtu mzima, ningeliweza kupima kila jambo kwa uangalifu, ni sawa....lakini tuangalie na upande mwingine wa shilingi..je ni kweli mimi nilitaka litokee hivyo, ushahidi ndio huo, sikutaka , na lilifanyika kutokana na mbinu za huyo mwanaume…’akaniangalia mimi na mimi nilikuwa nimemkazia macho.

‘Sasa mimi na huyo mnayemuita mume wa familia ni nani Malaya, niambieni ukweli wenu bila kuficha, maana katuita sisi Malaya, je mimi nikimuita Malaya nina makosa, au lugha hiyo ni kwa wanawake tu. Pili mimi na yeye ni nani anayestahiki kuitwa msaliiti, tatu mimi na yeye ni nani mbakaji, mwizi, mdanganyifu,…’akasema na kuwaangalia wajumbe, halafu akamgeukia mwenyekiti alipoona watu wapo kimia

‘Najua wakili mtetezi ana maswali ya kuniuliza, ili aulinde mkate wake, je muheshimwa mwenyekiti niendelee sehemu ya pili au tumuache muheshimiwa wakili aniuliza maswali kwanza…?’ akauliza

‘Maana sehemu ya pili ndio itabainisha ukweli wa kifo cha Makabrasha, sasa hapo mwenyekiti utaamua mwenyewe, kwani hilo sio jukumu lako tena, ni jukumu la wenye mamlkaka, na mimi nawajibika kwa hilo, kama raia mwema natakiwa kuwasaidia watendaji na hapo sasa kila mtu ataubebe mzigo wake yeye mwenyewe…na mengine sistahiki kuyaeleza, labbda mwenyekiti aombe kibali..’akasema hivyo, na mwenyekiti angaalia saa, na mara akachukua simu, akawa anapiga namba, akaweka sikioni...

‘Unataka kumpigia nani mume wangu…’akauliza mama, akimuangalia baba kwa mashaka

Mwenyekiti akaashiria kwa mkono, kuwa mkewe atulie …

NB: Naona tushie hapa, kwa leo.



WAZO LA LEO: Ulevi wa aina yoyote ni hatari kwa afya zetu, ulevi, huondoa akili nzuri ya kibiadamu, na unaweza ukajikuta ukifanya jambo ambalo ukiwa na fahamu zako usingeliweza kulitenda, kama ni hivyo basi kwanini tunakunywa kitu ambalo kinatutoa utu wetu. Tutafakari kabla ya kutenda.

 
SEHEMU YA 103


‘Sasa mimi na huyo mnayemuita mume wa familia ni nani Malaya, niambieni ukweli wenu bila kuficha, maana katuita sisi Malaya, je mimi nikimuita yeye Malaya nina makosa, au lugha hiyo ni kwa wanawake tu…?’ aliuliza mdada

‘Je mimi na yeye ni nani anayestahiki kuitwa msaliiti, tatu mimi na yeye ni nani mbakaji, mwizi, mdanganyifu,…’

‘Je sasa mwenyekiti waniruhusu niendelee sehemu ya pili, sehemu hii ina sehemu mbili ya kwanza hitimisho ya kuzaliwa kwa mtoto, na sehemu ya pili yake ambayo ni tete kidogo, ni kuhusu yaliyotokea baadae ambayo yatabainisha, ukweli wa kifo cha Makabrasha…’akasema

‘Ina maana una jua jinsi Makabrasha alivyouwawa, lakini hilo sio swala la kifamilia, ni swala la kipolisi, au sio muheshimiwa mwenyekiti…’aliyeongea alikuwa ni wakili wa mume.

Na wakati wakili huyo akiongea mwenyekiti alikuwa akitaka kupiga simu,...

‘Unataka kumpigia nani mume wangu…’akauliza mama, akimuangalia baba kwa mashaka

Mwenyekiti akasimama na kusema,

‘Nipeni dakika kadhaa, kuna mambo nayaweka sawa, nitarudi,…’mwenyekiti akasema na kutoka nje kidogo, na sisi tulipobakia wenyewe bila mwenyekiti, tukawa tunaangaliana, kila mtu akiongea na yule aliyekuwa karibu naye, na kwa vile mume wangu alikuwa karibu yangu akasema;

‘Mke wangu uwe makini sana na haya mambo, haya yamepangwa ili kuivuruga ndia yetu, ninafahamu nimekosa, ..lakini ilikuwa ni bahati mbaya, na… mimi ni mume wako, na hakuna mtu atakayeweza kututengenisha, usimsikilize huyo mshenzi, huyo ni ndumilakuwili, ati anajiita rafiki yako, huyo mtu anatumiwa na watu, hata wakili wangu anamfahamu sana huyo rafiki yako, najua kabisa kakosa kote sasa hivi anataka kuharibu kabisa…’akasema na kugeuka kumuangalia wakili wake, na wakili wake akatikisa kichwa kukubaliana na yeye.

Nilimtupia macho mdada, ambaye alikuwa akihangaika na mtoto wake, alikuwa akimbadilisha nguo za ndani, na alipomaliza, akasimama na kwenda pale alipokaa mama, akawa anataka kumpa mama mtoto, na mama alikuwa kama kasinzia, akashangaa mtu kasimama mbele yake.

‘Mjukuu wako huyu…’akasema

Mama akamuangalia kwa macho ya kushangaa, hakusema neno, akawa anamuangalia yule mtoto kwa uso wa huruma, halafu akanyosha mkono kumpokea yule mtoto, akawa anamuangalia kwa makini kweli.., baadae akageuka kumuangalia mtoto yule wa bint yake wa kufikia, akatikisa kichwa na kusema;

‘Kwa haya matendo yenu mna dhima kubwa mbele ya mola, lakini hawa viumbe hawana makosa, ndio maana sitaki kusema lolote baya kuwahusu wao, vinginevyo, mimi nisingelikubali hata kumpokea huyu mtoto, yaani wanafanana kweli…’akasema

‘Ni kweli mama, lakini hayo niliyoyasema mimi ni kweli, najua mtasema, kwanini nili…kaa kimia, au kwanini ikatokea mara ya pili, na…na.. bado nikakaa kimia,..na kwanini sikuweza kuusema ukweli wote baadae, ..ni lawama kwangu kwa kweli, lakini hamjui ilivyokuwa, kiukweli baada ya hilo, nilipitia majaribu mengi sana,.. nitakuja kuyaongea hayo, yaliyotokea baadae ambayo, huenda yakasaidia kuyajibu maswali hayo…’akasema

‘Vyovyote iwavyo, huwezi kukwepa lawama kuwa na wewe ulikosea, na ulimkosea sana rafiki yako, nashangaa ukimtupia lawama kuhusu kukushauri, je ni mangapi mema alikushauri, je ni mangapi yenye kasoro alikushauri na wewe hukuyafanya, kwanini hili ukalifanya, ni kwa vile ulifahamu kuwa kuna masilahi mbele yako, huo ndio ukweli…’akasema mama

‘Mama hata sijui nisemeje…ni kweli akiri kosa, nakubali sana hilo, kuwa nimemkosea sana rafiki yangu, na sizani kama nitaweza kulilipa hilo deni.., ni yeye tu, nasubiria adhabu yake, lakini sio hiyo ya kunikamatisha watoto wa kihuni, hapana mama, huo utakuwa ni kunitaka nijiue, kaam adhabu mimi nijiue, basi iwe hivyo, sio kwa njia hiyo, …’akasema

‘Unataka adhabu gani sasa, maana sasa wewe mkosaji ndiye unayepanga adhabu gani upewe, hutaki adhabu za mkosewa, mimi nionavyo, ni kumuachia mkosewa aamua mwenyewe adhabu gani ya kukupatia, kwani hata akupe adhabu gani, sizani kama itapunguzu machungu yake moyoni, niambie kama ingelikuwa wewe ungelifanya nini…?’ akauliza mama.

‘Mama hebu fikiri, hiyo ni adhabu kweli ya kumpa mtu, tujiulize wenyewe hivi kweli hatujawahi kumkosea mtu, …ni sawa kama na wewe mzazi utaona hiyo adhabu ni sahihi…nita..oh, mama, usiombe kufanyiwa uchafu huo…’akasema

‘Nikulize umewahi kukaa ukaliwazia hilo, ni maumivu gani mwenzako kayapitia, ukizingatia kuwa wewe ni rafiki yake, ndugu wa karibu, aliyekuamini kupitiliza mpaka sisi wazazi wake akawa hatusikilizi zaidi yako, hasikii lolote kukuhusu wewe, maana sisi tulishaziona nyendo zenu wewe na mume wake, tukaambizana, je hii ni sahihi, ni kwanini binti yetu anayaruhusu haya,…yeye tulipomuuliza hilo, alisema anakuamini, wewe huwezi kumsaliti..’akasema mama.

‘Na hivyo hivyo, akamtetea mume wake kua mume wake hawezi kumsaliti kwasababu ana mkataba amabo hawezi kuuvunja, na sisi hatukuwa na ufahamu sana kuhususiana na huo mkataba, tukamuwambia, mkataba utavunjwa, na wewe utakuja kutumbia, si ndio haya yametokea…’akasema mama

‘Na tulimuambia hao hao unaowaona ni marafiki zako, ndio hao hao watakuja kukuliza, je hayajatokea…asiyesikia la mkuu, …’akasema mama.

Rafiki yangu pale akawa kainamisha kichwa chini tu, nahisi alikuwa akipambana na huo ukweli, na alipoinua kichwa, nikaona machozi machoni mwake, ..akageuka kuniangalia, na mimi nikawa nimekwepesha macho yangu tusiangaliane,..na alipoona hivyo, akawa anatembea kuja kwangu, na aliponikaribia, akataka kupiga magoti, na mwenyekiti akaingia…

‘Haya jamani tuendelee, tusiharibu utaratibu, mzungumzaji nenda kwenye sehemu yako, mchukue mtoto wako, tunataka kuendelea…’akasema mwenyekiti na huyu mdada, akaacha kitendo alichokuwa anataka kukifanya, na kwenda pale kwa mama, akamchukua mtoto wake, na kurudi sehemu yake…

Tuendelee na kisa chetu

******************
Mwenyekiti aliangalia saa, akaangalia zile ajenda mezani kwake, halafu aakgeuka kuniangalia mimi, akasema

‘Sizani kama kikao hiki kitayamaliza haya kwa leo, kuna watu wana shughuli zao, tumewasimamisha leo, kuna watu wanatakiwa kesho kusafiri, kuna mambo yangu ya kikazi, na .…’akasema

‘Mwenyekiti mimi naona tuendelee na kikao kwa vile tumeamua kulifanya hili jambo, basi ni vyema tukalimaliza kabisa, mimi hapa nilipo sizani kama nitaweza kuendelea kuliweka hili jambo moyoni tena, nimevuta subira kiasi cha kutosha, naona leo liwe ni hitimisho, ili maisha yaendelee…’nikasema

‘Hapo unajiangalia wewe mwenyewe, je umewauliza wajumbe kuhusu nafasi zao, je hawatathirika na hili, …’akasema mwenyekiti

‘Kesho ni siku ya mapumziko ya juma,..niliwauliza wenzangu mmoja mmoja kwa nafasi yake kama leo wanaweza kuitumia nafasi hii kwa siku nzima, wengi walikubaliana na hilo, ikizingatiwa kuwa tatizo hili limewagusa kila mmoja wetu hapa,na kila mmoja anataka liishe, ..’nikasema.

‘Ndugu zanguni, ..ingelikuwa ni vyema, tukafahamu , huenda kuna mtu mwenye dharura, kama kuna mtu ambaye anaona tuahirishe hiki kikao aseme, ili tuone tutafanya nini, tunaweza kuahirisha hadi kesho, kama ikibidi,..’akasema mwenyekiti.

‘Kiukweli binti wangu wa kufikia, aliniambia yeye kesho ni lazima aondoke kutokana na shughuli zake huko kijijini, sasa hiki kikao ni muhimu sana kwake, ili kufahamu hatima yake…kamuacha mama yake anaumwa,…’akasema

‘Mimi naona tuendelee tu na kikao, tuyamalize, haya, ama kwa huyo binti, mimi sioni kwamba kuna jambo ambalo halijakubaliwa juu yake, kwani mtoto keshajulikana ni nani baba yake, na baba yake ni lazima awajibike juu yake, hilo halina mjadala , mengina atakuja kuambiwa tu…’akasema docta.

‘Wewe umesema hivyo, lakini ulisikia kauli ya rafiki yako, kuwa hao watu ni watu gani,…na wamefanya hivyo kwa madhumuni gani,…sitaki kumalizia kauli yake maana kwangu inanipa mashaka..’akasema mwenyekiti.

‘Hapana, hayo aliyaongea kwa hasira tu, ukweli upo wazi, hata kama dhana yake ina mantiki kwake, mimi nafikiri rafiki yangu hawezi kukwepa hilo jukumu, huyo ni mtoto wake, haijalishi walimpata kwa njia ipi, anawajibika kwa hilo,...’akasema rafiki wa mume wangu, huku akimwangalia rafiki yake

Mume wangu alikuwa kainamisha kichwa chini, hakusema neno, na wakili wake alikuwa akipitia makabrasha yake ni kama vile hawakuwepo, na kitendo hicho kikamfanya mwenyekiti kusema;

‘Hivi nyie watu wawili tupo pamoja kweli, hamuoni kuwa kikao kinaendelea au mnataka tuwaleweje, hili ni kwa manufaa yenu, je tukitoa uamuzi mtasemaje…?’ akasema mwenyekiti.

‘Samahani sana muheshimiwa mwenyekiti, kuna mambo tulikuwa tunayapitia, ili tuje kuyaweka wazi kwenye kikao, imebidi tuongee na kuona jinsi gani tutakubaliana na hilo la mtoto…sio kwamba tumekizarau kikao…’akasema wakili

‘Kwahiyo mnasemaje..tuambieni mlichokubaliana, ili ikiwezekana tumruhusu huyu binti aondoke, tatizo pia hawezi kuondoka bila kuongozana na mke wangu kuna mambo yao wanataka kuyaweka sawa, huyu tulishamchukua kama binti yetu..’akasema mwenyekiti.

‘Tumekubaliana tuendelee na kikao, ni sio lazima kiishe leo, tunaweza kuendelea na sehemu itakayobakia tupande siku ya kuiendelea nayo, isiwe nitatizo kubwa, maana hapa ni seehmu ya kuwekana sawa kama wanafamilia…’akasema wakili

‘Sawa, sizani kama tuna muda wa kuliendeleza hili tena na tena, ni muhimu tumalizane na hili jambo ili maisha yaendelee kama kawaida, na kama kuna mengine yakufuatilia, yafautiliwe, na kama kuna kuwajibika, watu wajue ni nini wanahitajika kuwajibika nacho, naona tulimalize hili ikiwezekana leo, au mnasemaje wajumbe...’akasema mwenyekiti huku akifungua makabrasha yake.

********

‘Kwahiyo kwa sasa muongeaji wetu anaweza kuendelea na sehemu yake ya pili, kama alivyoiita yeye mwenyemwe, ila hapo nina angalizo kidogo, kwenye utangulizi wake, kasema sehemu hiyo ya pili, pia itamgusa marehemu, hapo mimi nachelea kidogo, je wanasheria wetu mnasemaje kwa hilo,...?’akauliza mwenyekiti, akiwaangalia mawakili wetu.

‘Kwasababu ni maongezi tu, hakuna jambo linaloweza kuharibu mambo ya kisheria, sizani kama hayo atakayoongelea yataharibu mambo ya polisi na upelelezi wao, naona yeye aongee tu , akizingatia hayo ya kipolisi.., kuwa hilo swala lipo kwenye mikono ya polisi, mimi namfahamu muongeaji, yeye anafahamu wajibu wake, anafahamu mipaka ya jambo kama hilo...’akasema mwanasheria wa familia yangu, na mwenzake akakubaliana naye.

‘Sawa …’akasema wakili wa mume, akimuangalia mteja wake, mume wangu alionekana kama yupo mbali kabisa.

Mara akasimama,mke wa docta, ni kama vile alikuwa mbali, na sasa kakurupuka kutoka huko alipokuwa akasema

‘Ndugu Mwenyekiti, samahani kidogo, mimi nilikuwa na ombi, nilitaka mimi nipate nafsi hiyo kwanza, kwani nilikuwa nataka kuongea jambo moja muhimu sana,…naombe mimi niongee mimi kwanza, kwani hata mimi kesho natakiwa kuondoka, kurudi kijijini, nataka nikajiandae,...’akasema mke wa rafiki wa mume wangu, na mume wake, akawa kama anamzuia, na wakawa wanateta na mume wake, lakini ilikuwa kama hali ya kusutana hivi, hakuna aliyesikia walikuwa wakiongea nini, na baadaye mdada yule, yaani mke wa docta akasema;

‘Basi aendelee tu,...’akasema

Mwenyekiti akawaangalia kwanza kwa uso wa shauku , lakini baadae akasema;

‘Tunashukuru sana kwa kutuelewa, kwasababu mwenzako alishaanza, itakuwa sio vizuri,tukiwa tunakatisha katisha haya mambo, mpangilio wa ajenda ni mnzuri, tu..itafikia muda wako, utaongea, au sio…? ‘akasema na kuuliza.

‘Sasa..unajua niwambie kitu, ni nini dhumuni la kuwaleta hawa mawakili wetu wawili, ilikuwa wao watusaidie kila tunachoongea hapa kiwekwe kisheria zaidi..tukianghalia mbele,…muhimu ni ili tuwe na kumbukumbu zenye mshiko, …na hatua zikianza kuchukuliwa tuwe na ushahidi ulio kamilika,…, ..’akasema mwenyekiti.

Yule mke wa docta akasema;

‘Sawa mwenyekiti, nimekubali kusubiria, lakini akimaliza yeye, naomba mimi ndio nipewe kipaumbele, ni muhimu sana kwakweli, sitaweza kuvumilia zaidi ...’akasema huku akigeuka kumuangalia mume wake, ambaye alikuwa akimwangalia kwa macho ya kumshangaa.

Mimi nilimwangalia huyo mdada nikahisi kweli ana jambo kubwa sana la kuongea, na kama alivyoonekana toka awali, alikuwa kama hayupo nasi kwenye kikao, na hicho alichotaka kukiongea inaonekana kakifikiria sana,..

Nikawa na mtizama kwa makini, nikakumbuka jinsi mume wake alivyosema kuwa mke wake mara nyingi ameonekana akiwa na mawazo mengi, kitu ambacho hakuwa nacho kabla, anahisi mke wake ana tatizo kubwa, ila hataki kusema ni nini kinachomsumbua.

Nilitamani mwenyekiti amruhusu tu huyo mdada aongee kwanza, kwani huenda inaweza ikafikia mahali, huyu mzungumzaji wa sasa akaongea mambo yakamfanya huyu mdada akaghairi hayo aliyoyataka kuyaongea na niliona kama mume wake hataki aongee jambo…huenda wamekwisha kuyaongea, na je hayo aliyo nayo yaanhusiana vipi na familia yangu

Nilipowaza hivyo, nikanyosha mkono..na mwenyekiti akaniangalia , na kusema

‘Vipi tena…’

‘Samahani mwenyekiti, huenda mwenzetu huyu ana jambo muhimu sana,kwanini tusimuachie akaongea kwanza…huenda hilo jambo halitaki kusubiriwa, au baadae akaja kughairi,...’nikasema

‘Hapana, mimi naona, tuendelee tu kwa mpangilio wetu, kama alivyosema mwenyekiti, twende kama ajenda zinavyosema, ili tusichanganye mambo…au sio mke wangu...’akasema docta akimuangali mke wake, na mke wake hakumjibu kitu.

Mke wa docta, akawa katulia, na alionekana kama kukerwa na maamuzi ya mume wake, akawa sasa katizama chini tu akiendelea na ile hali yake ya awali, kama hayupo vile. Na mwenye kiti akasema;

‘Basi mimi naona aliyekuwa akiongea aendelee, tusipoteze muda,… haya tuelezee sehemu yako ya pili, na sehemu hiyo kama ulivyokwisha kuonywa, isije ikagusa mambo ya kipolisi na uchunguzi wao, sisi tunahitajika kufuata sheria..’akasema

Mdada muongeaji akatikisa kichwa kukubaliana na maagizo ya mwenyekiti.

‘Ni muhimu sana , kwani hata kama hawapo hapa hao wenyewe.., lakini masikio yao ni mapana, huko walipo, wanafuatilia hiki kikao kwa ukaribu sana, wanajua humu kuna jambo ambalo linaweza kuwasaidia kwenye kesi yao, ndio maana hakuwataka kutuingilia, walitaka kuwachukua baadhi ya wajumbe, leo hii, mimi nimewatuliza kwanza….’akasema mwenyekiti

‘Mwenyekiti mbona unatutisha…’akasema docta

‘Sio kwamba nawatisha, nafahamu kilammoja anajijua yeye mwenyewe, na hakuna marefu yasiyokuwa na ncha, za mwizi niarubaini, na sisi kama wanafamilia, tutalindana pale inapobidi,lakini je kama watu wamefanyahayo nyuma ya mgongo wetu sisi tutafanyaje..’akasema mwenyekiti

Pale watu waliangaliana, kama kuhisiana, lakini hadi hapo hakuna alieymshuku mwingine..

‘Sasa jamani, tuendelee,….ila narudia tena, muongeaji, uwe makini na hilo, hatutaki kuja kuharibu sifa ya familia yetu, ongea yale yanayostahili kuongewa hapa...’akasema mwenyekiti.

Mdada akawa, anajikuna kuna kichwa kwanza kabla hajaanza kuongea, akawa anahangaika kidogo, na mwenyekiti akasema;

‘Sio lazima uongee ukiwa umesimama,…’akasema mwenyekiti.

‘Nashukuru sana, ndugu mwenyekiti, msiwe na wasiwasi na hilo, mimi nafahamu sana utaratibu huo, ninayotaka kuyaongea hapa ni mambo yanayoigusa familia yenu, ..oh, sijui nisema yetu,…kwa vile hata mimi nimekuwa ndani ya familia hii, na hata kutambuliakana kama mwanafamilia, nitajitahidi nisiharibu jina la familia yetu…’akasema na hapo akanitupia jicho la haraka.

‘Kwahiyo,…’akasema na kutoa karatasi fulani kwenye mkoba wake,..

‘Kuna mambo nitayaongea hapa...huenda mengi yamepotoshwa kwa masilahi fulani, lakini mimi kama mpelelezi, nimeshayafanyia kazi, na hivi ndivyo ilivyo, anayebisha, alete ushahidi wake...’akasema

‘Sehemu yangu hii ya pili, ambayo naona itakuwa hitimisho, la kila kitu kinachonihusu mimi, na walengwa, itaanzia nilipojifungua, maana hapo ndio nilianz kupata picha ya mambo ambayo nilikuwa siyajui,...’akasema na kuniangalia mimi kidogo, halafu akamwangalia mume wangu, na akatabasamu kidogo.

‘Mengi yalisemwa, hasa baada ya mimi kujifungua, na wengi, walitaka kufahamu ni nani hasa baba wa huyu mtoto, kama nilivyosema awali, haya yaliyotokea hadi kupata mtoto, yana mlolongo wake, achilia mbali huo ushauri, kuna kuwekewa madawa ya kulevya, hayo madawa jamani ni hatari, sijui wenzangu hawa waliyapatia wapi, na kama ningeshitaki, ilikuwa ni kesi, sio mchezo....’ akasema.

‘Ningelipenda docta atuelezee kidogo kuhusu hayo madawa kabla sijaendelea..’akasema

‘Hebu tukumbushe kidogo , hayo madawa yanaitwaje… ?’ akauliza docta

‘Kifupi chake ni PCP, na kitaalamu wamsema ni Phe, Phe-ncycline, kama nitakosea, docta unirekebishe..’akasema, na docta akasema

‘Upo sawa, ..Mhh, ni moja ya madawa yasiyorasimishwa, ni hatari sana, yanaweza yakawa ya unga unga, au vidonge, ..watumiajia wanaweza kuchanganya kwenye kinywaji, ..na yakishaingia mwilini inakuwa kama waathirika wa madawa ya kulevya, ila zaidi yake ni kuwa, mtu anaweza kufanya mambo ya ajabu, anaweza hata kuota kwa vitendo, anaweza kuona vitu ambavyo wewe huvioni, ana..jenga hisia za ajabu tu..’akasema docta

‘Mumesikia, sasa wahuni hawa waliniwekea mimi…ndio maana jamani nawaambia mimi sikuwa na dhamira hiyo, …yaliyotokea usiku ule ilikuwa nje ya uwezo wangu, najitetea tena kwa hilo,…’akasema

‘Sawa endelea, hatutaki kupoteza muda tena…’akasema mwenyekiti

‘Nafahamu kuwa rafiki yangu atanilaumu sana, na hapo alipo hataman hata kuniona, ni kweli, ilivyo, na inavyoonekana kwa sasa nimekuwa kama msaliti kwake, kwa vile niliyafanya hayo niliyoyafanya, kinyume na alivyotaka yeye ndio maana narudia seehmu hiyo…, na kiukweli nilipoongea na mama, kiukweli imenigusa sana..’akasema.

‘Haya tuendelee…’akasema mwenyewe hivyo.

‘Nilipojifungua, rafiki yangu alifika, na akagundua kuwa mtoto wangu anafanana sana na watoto wake, na kwa mtizamo wa haraka, kama angelikuwa hamuamini sana mume wake, angelijua moja kwa moja aliyefanya hayo ni mume wake, lakini akili yake ilifungwa kabisa, na hata alifikiria kuwa huenda ni mdogo wa mume wake, aliyefanya hivyo...’akasema na kuinama kama anasoma kitu kwenye karatasi , ilikuwa karatasi moja tu.

‘Kiukweli usiku ule uligubikwa na sintofahamu nyingi, naweza kukiri kuwa sikuwa na ufahamu zaidi ya kile nilichokiona baadae kuwa aliyenifanyia hivyo ni mume wa familia,..na kwa maelezo ya hizo dawa unaweza ukafanya kile ulichokuwa ukikiwaza, au ukamfikiria hata mfu kuwa upo naye, ni kama mashetani fulani…sasa hapo unaweza ukasema mengi … je ni kweli au si kweli, ushahidi ni huyu mtoto…’akasema

Mtoto huyu ni matokea ya yale waliyonifanyia usiku ule, sasa kama walitumwa au walidhamiria, mimi hapo sijapata ushahdi wa kulitosheleza hili, ila kama mume wa familia ana nia njema na hii familia anaweza kuliweka hili bayana, ili kuisaidia familia, na hapo itajulikana kuwa kweli yupo tayari, kujirudi..’akasema akimuangalia mume wangu.

Mume wangu alikuwa bado kainamisha kichwa , na wakili wake alitikisa kichwa kama kukubali,kwa niaba yake.

‘Baada ya kujifungua, mtu aliyekuwa karibu yangu, na kuniuliza mara kwa mara ni nani baba wa mtoto alikuwa rafiki yangu, bosi wangu, na ukumbuke yeye katika ushauri wake, alishanionya, kuwa ikitokea nikazaa na mume wa mtu basi hiyo iwe ni siri yangu…’akasema

‘Kwahiyo kumbe ni yeye alikushauri, uje uzae na mume wa mtu..?’ akauliza wakili wa mume wangu, na mwenyekiti akasema;

‘Sijaruhusu maswali…’akasema

‘Kiukweli sikuwa tayari kumwambia mtu ukweli, kwanza nilihitajia muda wa kulitafakari hilo, maana sasa nimepata ushahidi kuwa aliyefanya hivyo ni mume wa mtu,…ambaye ni shemeji yangu, ni aibu na sijui itakuwaje..’akasema

‘Rafiki yangu au bosi wangu ndiye aliyekuwa karibu sana na mimi, baada ya kujifungua, kiukweli nilitaka niwe peke yangu ikibidi, lakini kama walivyo marafiki, bosi hakutaka kulikwepa jukumu hilo,…ila sasa nafsi,ikawa inaombea huyu mtu asiwe karibu yangu, kutokana na maswali yake.

‘Na wakati tunaongea mimi na yeye, kila hatua nilianza kuhisi hatari iliyopo mbele yangu, awali nilitaka kumwambia ukweli ili yaishe,…, nikijipa moyo kuwa hakuna litakalotokea baya, yeye si rafiki yangu, rafiki wa kweli ni yule yupo tayari kumpa mwenziwe kile akipendacho, au sio…’akasema na watu wakaguna.

‘Nasemea jinsi nilivyokuwa najipa matumaini,..mnielewe hapo…’akasema alipoona watu wanaguna.

‘Kwahiyo kutokana na maneno yake kwa haraka nikamkatalia kumwambia ni nani baba wa mtoto..na hata pale alipojiwa na ufahamu kidogo ya kuhis kuwa huenda aliyefanya hivyo ni mume wake, baada ya kuona sura ya mtoto inafanana na watoto wake, nikamkatalia kuwa mume wake, sio baba wa mtoto wangu..’akatulia

‘Kiukweli.., kauli zake za vitisho, kuwa hatakubali mtu aje kutembea na mume wake, hatakubali mtu …na vitu kamahivyo, na zaidi akasema ambaye atawahi kuingilia ndoa yake kuna adhabu kubwa atakuja kupambana nayo. Niliogopa, na kuanza kujenga hisia nyingine ya kujihami.

‘Ni kweli inauma sana, lakini kinamna fulani, naweza kusema kuwa sikutarajia kabisa kuwa rafiki yangu ataumia kiasi hicho, sikutarajia kuwa hilo nililolifanya ni kosa kubwa kwake, , ikizingatiwa kuwa ni yeye rafiki yangu,na ni mtu anayependa kunipa ushahuri, na alikuwa anatamani sana na mimi nimpate mtoto...

‘Ni kweli kuwa mume wa familia nilikuwa nakutana naye mara kwa mara kwa rafiki yangu, …lakini baada ya tukio lile la pili nikawa simuamini tena, na akawa sasa anamtumia rafiki yangu awe mtu wa kutupatanisha…ili iweje basi, mtoto…mtoto akawa ni hamasa kubwa kwa mume wa familia.

‘Kama huyu mtu ndiye kanibebesha hii mimba nitakuwa na ushahidi gani baadae, nikaona nitafuta ushahid fulani, ikibidi, ili ije ijulikane ukweli ulivyokuwa, kwa vipi sasa.. kwa vile alishaona kwa rafiki yangu ndipo mahali pa kukutana naye ili kujenga suluhu, nikaweka vifaa vya kurekodi matukio, ili nipate kauli yake muhimu ya kuthibitisha kuwa yeye ndiye kasababisha haya bila dhamira yangu.

‘Sasa kumbe wakati nayafaya hayo,kumbe kulikuwa na mtu alishalifikiria hili mapema sana!!...’hapo akatulia kama anasoma kitu kwenye ile karatasi.

‘Ndugu zanguni haya nayaongea lakini naombeni muweni makini sana majumbani mwenu hasa nyie watu mashukuri..kuweni makini ..muwe mnachunguza nyumba zenu, dunia ya sasa ni kijiji…kimtandao,na mawasiliano…’akasema

‘Hadi hapo, bado sikuwa na ufahamu huyu mtu aliyefanya hivyo, alicheza huo mchezo na wanafamilia hao, au alikuwa na ajenda yake mwenyewe, na peleekni akili zenu mbali zaidi,…siwaambii hilo kwa hivi sasa, nitakuja kulifafanua baadae ili kuwaonyesha kuwa hili jambo, sivyo kama tunavyolifikiria kiraisi raisi, kuwa labda, au vile..’akatulia, na kugeuza ile karatasi upande wa pili.

***********
Siku moja, baada ya kujifungua, ni siku kama mbili hivi baada ya kutoka hospitalini, alikuja mume wa familia, kipindi hicho nipo kwenye sehemu yangu ya kwanza niliyopanga, akaniambia kuwa kuna tatizo kubwa limetokea, nikamuuliza tatizo gani, mara akatoa picha na kunionyesha, ...oh...shabashi,....’akatulia kama vile ndio anaziona hizo picha mbele yake, akijenga hisia za tukio lile.

‘What,..ni nini hiki, ni nani kafanya hivyo,ina maana mliyafanya haya ili …’nikawa nimekasirika kweli

‘Hapana unielewe sana, hata mimi sikulifahamu hilo, sikujua kuwa hapo kwenye nyumba yako kuna vinasa matukio,kwanza niliwazia kuwa huenda ni wewe upo nyuma ya hili jambo…’akasema

Kiukweli zilikuwa picha chafu, zilikuwa picha zikionyesha jinsi gani walivyonizalilisha siku ile,..na anayeonekana ni mume wa familia, ndio maana baada ya pale, ukichukulia na sura ya mtoto, moja kwa moja, niliamini kuwa aliyefanya hivyo ni yeye na sio ndugu zake, kwenye picha hiyo anaonekana mume wa familia, akinizalilisha, ni ushahidi usipingika, mama kila kitu kilikuwa dhahiri…’akasema akikunja uso kuonyesha uchungu au hisia ya kukasirika.

Nilishituka sana, sikutarajia kitu kama hicho, kwanza nikaziangalia zile picha, na kwa haraka nikazichana-chana, na kuhakikisha hakuna kitu kinachoonekana na yeye, yaani mume wa familia, akaniambia;

‘Hata mimi nilipoonyeshwa hizo picha nilifanya hivyo hivyo, lakini kila siku nikawa naletewe picha kama hizo na nyingine mbaya zaidi ya hizo,...’akasema na hapo akanivuta kwenye hisia nyingine kuwa waliofanya hivyo, wana nia madhubuti ya kuniangamiza mimi.

‘Alikuwa akikuleta nani hizo pichai?’ nikamuuliza kwa hasira

‘Sijui,...ila mwishoni hapa, kuna simu nimepigiwa na mtu nisiyemfahamu, mtu huyo anasema anataka kuongea na mimi, nikamuuliza unataka kuongea na mimi kuhusu nini, akaniambia kuhusu mzigo niliokuwa nikiupokea mara kwa mara, nikamuuliza mzigo gani, akasema picha..’akatulia

‘Nikamwambia hata kwenye mitandao kuna picha, watu wanaweza kuunga unga ili kumzalilisha mtu mwingine…’nikamwambia hivyo, yeye akasema

‘Picha za kuungwa ungwa zinajulikana, na hata hivyo kuna namna ya kuhakiki kama kweli picha hizo ni za kuungwa ungwa au la,..kama nabisha nichukue hizo picha kwenye studio za wataalamu, watalithibistisha hilo kuwa hizo picha ni hakika…’akasema

‘Kwanini nifanye hayo, ..?’ nikamuuliza

‘Kwasababu ushahid halisi sasa upo , hakuna ubishi tena, picha pamojana huo ushaidi umekamilisha uchafu wako…’akasema

‘Ushahidi gani..?’ akauliza

‘Mtoto…huyo mtoto na wewe hakuna ubishi, mnafanana kama vidole vyako, …’akasema

‘Sasa unataka nini..?’ akamuuliza

‘Subiri, usiende haraka, mimi nataka kuongea na wewe…nilisubiria sana, na sasa muda muafaka umefika, nataka tuongee mimi na wewe, tutaelewana tu…’akasema na kukata simu…, ndio maana nimekuja kukuona wewe kwanza...’akaniambia hivyo

‘Ina maana huyo mtu aliyekuwa akikuletea hizo picha, mlikuwa hamuonani, naye, ulikuwa unazipata vipi hizo picha, na hayo ya kupata hizi picha yalianzia lini, na kama unavyodai umekuwa ukizipokea hizi picha mara kwa mara ina maana ni siku kadhaa nyuma sijui lini…, mbona hukuwahi kuniambia kabla, na kwanini sasa umeamua kunionyesha, ..?’ nikamuuliza

‘Ni kweli,picha hizi nilishazipata kabla,mapema tu, na sikutaka kukuonyesha mambo haya, kipindi ukiwa mja mzito, nilisubiria ujifungue kwanza, niliogopa usije ukaharibu mimba, na hata hivyo, mimi nilijua nitalimaliza mwenyewe, nikijua shida yake ni pesa, nikawa nampa pesa, lakini ikawa ndio biashara, nilitamani nionane naye ni-m-malize, maana utaishije hivyo...’akasema

‘Unahisi huyu mtu ni nani?’ nikamuuliza kabla hajaendelea zaidi

‘Kwakweli nimefikiria sana, ni nani anaweza kulifanya hili, kiukweli awali nikajua huenda ni wewe ukiwa na malengo yako, lakini kila nikipima kila nikija na kukudadisi, unakumbuka nimekuwa nikikuliza maswali awali,..ukawa unanijibu kijeuri, mimi nilikuwa na lengo langu…sasa nikirejea nyuma wewe huwezi kufanya jambo kama hili, kwa jinsi ninavyokufahamu,… sasa ni nani mwingine…, ndio nikaoana nije tuongee tuone tutafanya nini…’akasema

‘Mhh..bado hujanishawishi na majibu yako, kwanini sasa, kwanini lifanyike hivi leo, na tumekuwa tukikutana mara nyingi hapa..?’ nikamuuliza

‘Nilikuwa nasubiria wakati muafaka, maana kwanza awali ulikuwa umenikasirikia, ukawa huonekani, na baadae ndio nikakutana na wewe kule hospitalini kiukweli, sikupenda kukuumiza zaidi, najua kilichotokea imekuwa ni mtihani kwako, na sio kwako tu, pia hata kwangu, ni- ni mtihani mkubwa.

‘Isingelikuwa huyu mtu, wa hizi picha kujitokeza sasa, ningelisema niache mambo yaende kama yalivyo, nafahamu muda muafaka utafika, mtoto atamuhitajia baba yake…’akasema

‘Sasa kwa hili, inaonyesha tusiposhirikiana mimi na wewe..taarifa hizi zitafika sehemu ambayo haitakiwi zifike...sasa tufanyeje..’akasema

‘Tufanyeje, wewe uliponifanyia hivi, hukulifahamu hili, ..niambie ukweli ni nani alikutuma mnifanyie hivi, nahisi una njama na hujuma fulani, sema ukweli wako, maana nikija kugundua, nitafanya zaidi ya hili..?’ nikamuuliza

‘Kunituma,!!!..Hakuna aliyenituma, haya niliyafanya kwa vile ninakupenda sikuweza kuvumilia, na nilipopata nafsi hizo, nikaona nizitumie, ndio nilifanya hivyo, zaidi nikiwa nimelewa, huenda kama ningelikuwa mzima nisingeliweza kulifanya hilo, ila pombe ndio ilinihamasisha zaidi…’akasema

‘Niambie ukweli, ni pombe au ni dhamira yako, na hayo madawa mliyapatia wapi, nina mashaka na wewe..?’ nikamuuliza

‘Kiukweli mimi nakupenda, na nimekuwa nikifanya jitihada za mara kwa mara kukuonyesha hilo, wakato upo pale nyumbani, unajua, nilikuwa nahangaika sana, ..na ilipotokea nafasi hiyo, basi..zaidi ni kwamba nimefanya hivyo ukiwa hujitambui, ..sikupenda mapenzi ya namna hiyo, nilitaka tuwe wapenzi wa kweli, na hayo madawa mbona yapo tu, ni pesa yako..’akasema

‘Hivi, nikuulize wewe si una mke wako, na mke wako ni rafiki yangu kipenzi, ina maana mke wako humpendi,..na unatarajia nini baada ya hili..?’ nikamuuliza

‘Usijali kuhusu mke wangu, hilo niachie mimi, ilimradi wewe uwe tayari, ukubali kushirikiana na mimi, ili hili tulimalize kwanza, na kuhusu mke wangu ndio nampenda kama mke wangu, huo ni upendo mwingine na wewe nakupenda kivingine usilinganishe haya mambo, nielewe tu hivyo, nakupenda…’akasema

‘Sijakuelewa, na sitakuelewa, hivi unafahamu kuwa hapo unavunja ndoa yako, na kwa hili umeshavunja ndoa yako, kutokana na mkataba wenu wa kifamilia..?’ nikamuuliza na nilipomuuliza hivyo, nikamuona akichanganyikiwa kabisa.

‘Mkataba,mkataba, mkataba….mmh, kwa kauli yako hiyo inanipa mashaka sana hivi sio wewe kweli umalifanya hili, ili uiharibu ndoa yangu..?’ akasema

‘Wewe una kicha eeh…hebu toka humu ndani kwangu, sitaki kukuona tena, na wewe na hao waliokupa hizi picha unanifahamu nilivyo,nitawatafuta,…nitawapata,..’nikasema

‘Sikiliza kwanza,…wewe ndiye pekee umesema na kulihusisha hili na mkataba wangu, na huyo aliyenitumia hizi picha kaandika ujumbe kuwa je hizi picha zikionekana itakuwaje kwenye ndoa yangu, itakuwaje, kwenye mkataba wangu wa kifamilia, na swala la mkataba lilikuwa mimi na mke wangu, ni nani.. ..’akasema, n akukatisha

‘Sikiliza, wewe na huyo mtu, mjue mumeingia sehemu isiyofaa, na kama nia yako ni kuhusu huyu mtoto, huyu mtoto hana baba, baba yake alishafiriki…’nikasema

‘Oh, kwanini unasema hivyo, mimi ndiye baba yake, huyo ni mtoto wangu tunafanana naye, nina uhakika huyo ni mtoto wangu, ni kweli , nilikufanyia vile nikiombea kuwa tupate mtoto, na niliombea atokee mtoto wa kiume, na duwa zangu zimepokelewa, kwahiyo nakuomba tushirikiane kwa hili..’akasema

‘Nakuomba utoke hapa nyumbani kwangu, sitaki nikuone ukikanyaga hapa nyumbani kwangu tena, unasikia, sitaki kusikia mambo yak ohayo..sitoshiki na huo ujinga wenu, picha zinatengenezwa, na…na sitaki kusikia.. , kuwa wewe ni baba wa mtoto wangu, unasikia,, huyu mtoto hana baba…’akasema

‘Sasa hizi picha zina maana gani, ..hujasoma ujumbe nyuma ya picha…’akasema na wakati huo nilikuwa nimeshazichana-chana zile picha

‘Ujumbe huo unasema nini..?’ nikauliza

‘Kuwa yeye anafahamu tukio lote la kukutana mimi na wewe, na kwa jamii, wakiona kitu kama hiki sizani kama kuna cha kujitetea eti kuwa, nini na nini..’akasema

‘Bwanaee, niache..’nikasema

‘Sikiliza,..huyu aliyefanya hivi alitaka ushahidi na keshaupata, ushahidi ambao akiufiksiha kwa mke wangu anajua nitamalizwa, nitaumia, na kwa wakwe zangu hatawaweza kulivumilia hili, hii ni kashfa kubwa sana,..sizani kama walikiliona hili watavumilia, na hata kama mke wangu atanitetea vipi ..’akasema

‘Wewe unahisi ni nani huyo mtu…?’ akaniuliza

‘Bado sijaweza kumtambua, ..kiukweli nimekuwa kwenye wakati mgumu,nilipanga kuwa mimi sitalewa tena, ulevi na mimi basi, kwa vile ulishanipatia kile nilichokitaka, lakini kwa hali kama hii…hapana nikitoka hapa nitakunwya mapaka nsipate muda wa kuwaza, …ni matatizo…’akasema

‘Kwahiyo wao wamesema wanataka nini…?’ akniuliza

‘Ndio maana nimekuja kwako, kwanza nilihisi inawezekana ukawa ni wewe ulifanya haya yote kunikomoa, mimi, ..kwahiyo kuja kwangu hapa, ilikuwa nikuulize unataka nini kwangu, mali labda, au…, lakini nilipokuona tu, akilini, nikaingiwa na mawazo ya kulipinga hilo, sio wewe, sizani kama ni wewe…na kama sio wewe ni nani basi,…mmh, huyo ni mtu asiyejulikana…’akasema

‘Naomba uondoke , na sitaki kukuona tena…’nikasema kwa hasira, na yeye akaniangalia kwa mshangao, na hakuondoka, akawa kasimama tu, baadae akasema;

‘Ina maana wewe upo tayari, taarifa hizi zifike kwa rafiki yako, ukumbuke wapi ulipotoka wewe na yeye, na ukumbuke wewe una mipango ya kwenda kusoma nje…’akasema

‘Hayo yanahusiana nini na huu ujinga wenu, ni nyie mlionifanyia haya, sikupenda iwe hivi…’nikasema

‘Una uhakika..wewe hukuwa unataka mtoto, kama ilivyo mimi, niambie ukweli wako, ..umri umekutoka, utazaa lini, ..eeh, hujashauriwa hivyo…?’ akaniuliza

‘Ni kweli nilishauriwa hivyo, ..lakini sio kwa hivi livyotokea, sikutaka iwe hivi, na sijui kwanini sikwuashitakia…’nikasema

‘Ndio..kwa vile unanipenda, au sio…?’ akauliza

‘Siwezi kupenda mume wa mtu, …wewe ni shemeji yangu, na kwa hili hata sijui jamii, itanielewaje…’nikasema.

‘Jamii, jamii..mmh, kiukweli mimi nilifikia mahali nikasema …ahsante mung, hatimaye nimepata nilichokitaka, nilijua na wewe utsema hivyo hivyo, au sio…lakini kwa hili sasa ..sijui kuna nafasi hiyo tena…’akasema

‘Mimi nakuomba uondoke ..nitajua mwenyewe jinsi gani ya kulitatua hili…unajua, natamani ni….’hapo sikuweza kumalizia, na yeye akasema

‘Kunifukuza kutasaidia nini…mimi najaribu kukumbusha tu, kuhus tatizo lilipo mbeel yako,..hebu kwanza fikiria, je hili tatizo utaweza kulitatua mwenyewe, achilia mbali matunzo ya mtoto, kumbuka,..ni nani alikusaidia na atakaye kulipia kila kitu, eeh, na ukumbuke ulipotoka, …,’akasema

‘Una maana gani..?’ nikauliza

‘Ni kuhusu hizo picha,… je yeye huyo mfadhili wako, akija kuziona, ..akiona kitu kama hicho, hivi kweli bado atakuwa na nafasi ya kukusaidia, ….na je maisha yako ya baadae yatakuwaje,…huoni huo utakuwa ni mtihani mkubwa kwenye maisha yako, utakimbilia wapi, eeh,… mimi nakuomba tushirikiane ili tuweze kulimaliza hili jambo…’akasema

‘Kwa vipi..?’ nikamuuliza, nihisi kiukweli kuwa kweli kuna mtihani mbele yangu.

‘Kwanza, …kuna mtu namshuku, lakini …sijawa na uhakika naye, wewe ni mtaalamu sana wa kuchunguza mambo, tukiwekeza nguvu zetu kwa pamoja tunaweza kumshika huyo mtu, lakini kwa hivi sasa anataka pesa, tena pesa nyingi tu..’akasema

‘Anataka pesa, mimi nitazipatia wpi hizo pesa, unajua nilivyo, au wewe unahisi nitazipataje hizo pesa…?’ nikamuuliza

‘Tukishirikiana tutazipata tu..hilo sio tatizo…,kwanza ni muhimu kupatiakane kiasi fulani, ili tuweze ku-m-poza huyu mtu…, na huku tunaendelea na uchunguzi, ujue sio kwangu tu kutaharibika lakini hata kwako pia, umeonaeeh, ..’akasema

‘Kwahiyo unatakaje..?’ nikamuuliza nikitaka kujua huyu mtu ana lengo gani, maana hadi hapo japokuwa nafahamu nimekosea, lakini sikuwa bado nimefikiria kwa hali mbaya kiasi hicho, …baada ya kuziona hizo picha ndio nikajua sasa kuna tatizo,..

‘Tushirikiane bila kujali haya yaliyotokea, pili, hili jambo liwe siri kubwa, tatu, hakikisha hata iweje rafiki yako asiweze kuliona hili, je mtoto ameshamuona..?’ akaniuliza

‘Ndio…’nikasema

‘Alipomuona kashuku jambo..?’ akaniulia

‘Anasema anafanana na watoto wako..’nikasema

‘Mhh..mtihani huo, hukutakiwa kumuonyesha yeye, sasa utafanya mambo yazidi kuwa magumu…’akasema

‘Sasa ulitaka mimi nifanye nini..?’ nikamuuliza

‘Sikiliza, kwanza cha muhimu, usije kumuambia mke wangu, fanya ufanyavyo, mke wangu asifahamu kuwa huyu mtoto nimezaa na wewe, hilo liwe siri, nakuonya hilo tena tena, humfahamu mke wangu akikasirika anavyokuwa,...'akatulia

'Sawa...'nikasema

'Sasa ni hivi, kuna wazo limenijia akilini, na..nafahamu hutamuamini huyo mtu, wengi hawamuamini, kihivyo, lakini kwa mmabo kama haya hakuna mwingine anayeweza kupambana nayo zaidi yake, mimi namuamini sana, kwa vile huyo mtu ni rafiki yangu mkubwa sana, yeye anaweza kutusaidia kwenye hili tataizo, nakuomba kwa hili umuamini …’akasema

‘ Ni nani huyo…?’ nikamuuliza sasa nikiwa na mashaka, kila nikiwaza na kuwazua, naona hata mimi nipo kwenye mtihani.

‘Kwanza ukubali kushirikiana na mimi, ….tuwe marafiki,na hata baada ya hili..’akatulia kidogo.

'Marafiki, haaaah, ..'nikasema na kutikisa kichwa kumkatalia

‘Nakuahidi …hata kama itashindikana, japokuwa hakishindikani kitu mbele ya pesa, nakuahidi kwa hili, kwa vile mimi kweli nakupenda, natamani uwe wangu wa milele..lakini tuyaache hayo, …hayo yatakuja baadae, ila hili, kwa hili hata wewe huna ujanja kama nilivyo mimi, unasikia, na mtu peke yake wakutusaidia hili ni huyo rafiki yangu…’akasema

‘Ni nani huyo rafiki yako, sasa …?’ nikamuuliza

‘Ni jamaa mmoja hivi , ni mjumvi wa haya mambo, nimeshamtumia kwenye mambo yangu mengi, akanisaidia sana vinginevyo, ningeumbuka..na kwa hili bila yeye, hatuwezi kuponyoka,…ninachojiuliza ni kwanini mimi, maana, kila nikimaliza tatizo moja, linazuka jingine…sasa kwa hili , limenishika pabaya..’akasema

‘Ni nani huyo mtu..?’ nikamuuliza, sasa nikionyesha kukasirika, maana badala ya kunitajia anazidi kuniweka kwenye hofu, na mimi sio mtu wa hofu japokuwa hapo hofu ilishaniingia.

NB: Tutaendelea na sehemu ijayo. Msione kama tunarejea nyuma, hapa ndio tunakwenda kufikia kwenye ukweli halisi.


WAZO LA LEO: Mara nyingi uwongo haudumu, ni swala la muda tu, wapo watu wanahisi ni wajanja kwa kuishi kiujanja ujanja,..wanahisi hali waliyo nayo, na maisha waliyo nayo, waliyoyapata kwa ujanja ujanja, watadumu nayo, na kwahiyo wataweza kuishi milele, je ni nani aliishi milele,kiukweli hakuna atakayeishi milele, walikuwepo , wamepita,…na sisi tutapita vile vile..cha muhimu ni kujiuliza huko tuendapo tumejiandaaje..niwatakie ijumaa njema.

 
SEHEMU YA 104



‘Ni wakili mmoja hivi wa kujiegemea,..sio muhimu kumfahamu jina lake kwa sasa…’akasema

‘Kwangu ni muhimu sana…’nikasema

‘Unajua cha muhimu ni wewe kukubaliana nami, halafu mengine niachie mimi, maana hili janga bila mimi kushirikiana nawe, halitaweza kufanikiwa, na ujue lolote baya likitokea halitaniathiri mimi tu,…’akasema

‘Kwanza nikuambie kitu, siogopi majanga, hayo ni sehemu ya maisha yangu, sawa naweza kukubaliana na wewe kwa vile kuna huyo mdudu mtu kaingilia maisha yangu, na mimi hilo ni changamoto, …nataka kumfahamu huyo mtu ni nani..’nikasema

‘Ndio hapo nikaona tushirikiane, ili tuweze kumnasa huyo mtu…’akasema

‘Achana na huyo mtu, mimi nataka kumfahamu huyo wakili ambaye yupo tayari kukusaidia ni nani…?’ akauliza

‘Sijakubaliana naye baddo kwahiyo siwezi kukuambia…’akasema

‘Ok, kama hutaki kuniambia tuachane tu, ondoka zako…’nikamwambia

‘Sikiliza nitakuuambia nikirudi huko nilipoitwa, nina uhakika , haya mambo yalivyo, yanahitajia mtu kama yeye, yeye huo ni uwanja wake, hutaweza kumchukua wakili wa aina nyingine akakubaliana na sisi, na kwa hili, hatutakiwi kwenda polisi, unaona eeh, maana ukifanya hivyo, nyuma yake utakutana na waandishi wa habari..’akasema

‘Ok, so unataka mimi nifanye nini…?’ nikamuuliza

‘Kwanza unakubaliana na mimi kuwa kuanzia sasa hili la mtoto iwe siri, hakuna wa kufahamu baba wa mtoto ni nani, na rafiki yako asijue hili kabisa ..unanielewa hapo, maana akifahamu hilo, sio mimi tu, hata wewe utakuwa umejiharibia…’akasema

‘Sawa…hilo halina shida, tangia mwanzo hili nilitaka liwe langu tu, tatizo ni huyo kidudu mtu, na nakuonya, kama wewe upo nyuma ya hilo jambo, utanitambua mimi ni nani, unanifahamu sio…’akasema

‘Kwanini huniamini…nisingelipoteza muda wangu kuja hapa kwako,…sasa ngoja mimi niende, nikaonane na huyo mtu, nikitoka kwake nitakuja kukufahamisha ni nini tulichoongea naye ,sawa ilimradi wewe umeshakubaliana na mimi ..’akasema akitaka kuondoka

‘Pamoja na hayo, sitaki uwe unakuja hapa kwangu, pili..tusizoeane kihivyo, mimi sio mpenzi wako na haitatokea kuwa hivyo, maana tangia awali sijataka mahusiano na wewe, wewe ni mke wa mtu,..na kwa hili imetokea bahati mbaya, na tatu, msimamo wangu ni ule ule, huyu mtoto ni wangu peke yangu, hana baba…’akasema

‘Usiseme hivyo kuwa hana baba,..hata hivyo, hayo tutakuja kuongea, kwasasa sio ya muhimu, tusianze kugombea mtoto, au sio…umenielewa hapo, muhimu ni kuona jinsi gani ya kulikwepa hili, hivi wewe huoni hatari iliyopo mbele yetu…naogopa sana mkwe wangu akija kulifuatili,a yule mtu ni hatari, …’akasema na kuanza kuondoka.

Na alipoondoka tu, simu yangu ikaita, alikuwa ni rafiki yangu anasema yupo njiani kuja kuniona, hapo nilihisi mwili ukinicheza, maana kuja kwake nilishamuahidi kuwa nitamuambia kila kitu, lakini kutokana na haya yanayoendelea sizani kama nitaweza kumuambia.

‘Nduguzanguni, …naongea haya ili muone kipindi hicho jinsi nilivyokuwa na wakati mgumu , mnaponilaumu kwanini sikusema mapema, baada ya tukio hili, yaonekana kabda mimi nilifanya makusudi,..hapana kulikuwa na changamoto zake.

‘Na pia naomba mnivumilie kwa mahojiaono yatakayo kuja kuendelea baadae nia ni kuja kuwafichulia kile kilichokuwa kimejificha ndani yake, hili tukio sio rahisi kma lilivyo, kuna mambo yamepangwa,..na huenda hata wahusika wengine hawalifahamu hilo..’akasema bila kuonyesha hao wahusika wengine ni nani.

*********

Baadae alikuja rafiki yangu tukawa tunaongea na hoja yake ikawa ile ile ya kutaka kufahamu ni nani baba wa mtoto wangu, sikuweza kumwambia, nikijua kuwa kuna huyo mdudu mtu, ni lazima nimpate, pili, ni hali halisi ambayo, nahis nikimuambia rafiki yangu ndio urafiki utakufa kabisa, na kwahiyo sitaweza hata kwenda kusoma kabisa.

Sasa wakati rafiki yangu yupo hapo, simu yangu ikaingia ujumbe wa maneno, na nilipoangalia, kabla sijaufungua nikahisi ni hao watu, kwa jinsi ujumbe wenyewe ulivyokuwa kuwa kuna kitu kimebebeshwa kwenye huo ujumbe na ni picha au video…sikuweza kuisoma ile simu nikapotezea.

‘Mbona huangalii , nahisi kuna ujumbe umetumiwa, akaniambia rafiki yangu, na kwa haraka nikaufungua huo ujumbe, maelezo, kidogo tu, halafu, fungua hizo picha kama ushahidi, nikafungua, mamamamah!….nilitamani niirushe hiyo simu chini, nilibadilika kwa haraka, lakini akili ikanicheza, kwa haraka pale nikasimama kupotezea, nikasema;

‘Vipi kuna nini…?’ akauliza rafiki yangu

‘Mhh..kuna mtu ana mzigo wangu kasema niende sasa hivi, ni mzigo muhimu sana, na muda umeshapita,… samahani dada, sio nakufukuza, ila ni muhimu niende..’nikasema

‘Na mtoto…?’ akaniuliza

‘Usijali, nipo na ndugu yangu hapa, …’nikasema na rafiki yangu akanielewa akaondoka, na alipondoka nilishukuru mungu, maana nilichotumiwa kwenye simu, kilitaka nipoteze fahamu, ni picha zile zile, lakini hii ilikaa vibaya zaidi..kwanza sikuifuta kwa haraka, nikampigia mtu mmoja wa studio, ili anisaidie, nikamuelezea kuwa kuna mtu ananichezea je unaweza kugundua kuwa picha hii ni kweli au ya kutengeneza

‘Akasema anaweza…na sikupoteza muda nikaenda kwake, akaichunguza akasema picha hiyo ni ya kweli na imechukuliwa kwenye kamera za kujificha, haina shaka,..

‘Unaweza kugundua ni kamera za namna gani ..?’ akasema

‘Hii ni mitambo ya kisasa, inaweza ikawekwa sehemu yoyote, ikachukua matukio, ni kidude kidogo tu, …’akasema

‘Nawezeje kugunduaje kama bado kipo ndani ya nyumba yangu..?’ nikamuuliza

Akanielekeza jinsi gani ya kukigundua kwa kutumia simu yangu tu ya mkononi, akaniwekea program fulani kwenye simu yangu, ambayo itanisaidia kugundua hicho kifaa, basi nikarudi nyumbani, nikajaribu kufanya kama alivyonielekeza, lakini sikuweza kukigundua hicho kifaa, ina maana kilishaondolewa.

‘Sasa ni nani huyu mtu…’nikajiuliza na kabla sijapata jibu mara simu yangu ikaita, kuangalia nikagundua kuwa ni mume wa familia,

‘Unasemaje…?’ nikamuuliza nikiwa naona kama ananipotezea muda tu

‘Umetumiwa ujumbe wowote..?’ akaniuliza na hapo nikashtuka, yeye kajuaje hilo, nikasema hivi tu

‘Na nani…?’ nikauliza

‘Mimi nimetumiwa ujumbe hapa wenye picha, wakasema na wewe wamekutumia, unaona hizo picha zilivyo, wanataka tuwalipe pesa nyingi, na mimi sina pesa za kutosha, tufanyeje..?’ akaniuliza
‘Ni nani hao…?’ nikamuuliza

‘Hawajajulikana bado…’akasema

‘Kwahiyo unaniambia mmi nifanye nini, mimi sina pesa, unafahamu fika mimi namtegemea mke wako, anilipe mshahara na kazi hiyo ya ajira pesa yake ndio kiduchi hata sisemi ni kiasi gani…’nikasema

‘Sikiliza mwambie rafiki yako umekwama, una tatizo kubwa sana, kama anaweza akukopeshe milioni kumi hivi…’akasema

‘Milioni kumi!!.Wewe una wazimu kweli mimi sio kama wewe unayemiliki kampuni pesa kama hiyo kwako ni ndogo au sio…, kwangu mimi ni pesa nyingi sana.siwezi kufanya kitu kama hicho, hata rafiki yangu atanishitukia..’nikasema

‘Umesoma huo ujumbe kwenye hizo picha, ulivyosema..?’ akaniuliza

‘Mimi sijali, wafanye watakavyo, mimi sina hizo pesa…siwezi kujiingiza kwenye mtego kama huo…’nikasema ila kiukweli moyoni nilikuwa na wakati mgumu, yaonekana huyo mtu alishajipanga, na sio rahisi kumnasa kwa njia rahisi, iliyobakia ni kushirikiana na huyo huyo mume mtu.

‘Kwenye hizo picha kweli kulikuwa na ujumbe wa vitisho, uliandikwa hivi; je unataka kwenda kusoma, je unataka urafiki wako na rafiki yako udumu, je rafiki yako akiziona hizi picha utafanikiwa hayo…tutawasiliana nawe baadae..’’ wakamaliza hivyo

‘Ninakuja kwako nataka kukuelezea nilichokutana nacho huko nilipokwenda…’akasema, sikuwa na ujanja, nikakubaliana naye tu . ila nikampa tahadhari kuwa asije na gari lake..

Baadae kweli alifika:

‘Unajua kuna mambo ambayo huwezi kuamini..’akasema

‘Kwanini..?’ nikamuuliza

‘Unafahamu sikuamini hata mimi,…sikutarajia unajua nilikwenda kuonana na huyo mtu, na nikafuata maagizo yake, ni kwenye mgahawa fulani hivi, mara akaja mtu, akaniambia naitwa niende sehemu nyingine humo humo, nafika nakutana na mtu ambaye sikutegeemea kukutana naye hapo…

‘Mtu gani huyo, …?’ nikamuuliza

‘Makabrasha…’akasema

‘Makabrasha anahusikanaje na hili..?’ nikamuuliza

‘Hahusiki, lakini ilikuwa ni bahati kukutana naye hapo…’akasema

‘Kwa vipi..?’ nikamuuliza

‘Kwasabau ndiye wakili niliyepanga nionane naye …’akasema

‘Wewe, ina maana huyo wakili uliyesema anafaa, ndio huyo,.. hahaha, wewe kweli huna akili , kama ndio huyo mimi simo…?’ nikamuuliza

‘Sio kuwa ni yeye anahusika, hapana, yeye anasema kaniona nikiingia akawa anataka tuongee mambo mengine nikamkatiza kuwa mimi nipo matatani, ..nilishampigia simu awali, akasema niende ofisini kwake, lakini nilimuambia hilo jambo sio la kiofisini..’akasema

‘Mjanja huyo ndio huyo huyo kakufanyia hivyo…’akasema

‘Hapana sio yeye, yeye alikuwepo hapo kwa mambo yake tu, ndio ikaabidi nimuambie, maana bado nilikuwa sijamuambia tatizo lenyewe..’akasema

‘Akasemaje sasa…?’ nikamuuliza

‘Nimpe yeye hiyo kazi ya kukutana na huyo mtu, na yeye atajua jinsi gani ya kulimaliza hilo tatizo, maana watu wote wenye kazi hizo anafahamina nao,…nikaona basi nimemaliza tatizo…’akasema

‘Ukakubali…kirahisi hivyo…?’ nikamuuliza

‘Sasa ningelifanya nini,kwa hali kama hiyo, unajua nilichofanya kweli nlikubali,nikasema sawa kama ana nia kweli ya kunisaidia anisaidie, na kama ana nia mbaya, nitamgundua tu,… sikuondoka kwa haraka.

Nikajifanya nimeondoka pale, lakini sikuondoka nilikwenda kwenye duka moja na nikanunua nguo za haraka nikabadili na kuvaa mawani ya kuficha sura, nikarejea pale na kujificha sehemu ambayo ningeliweza kuiona ile sehemu niliyotakiwa kukutana na huyo mtu…’akasema

‘Basi kweli,…kwasababu Makabrasha alikaa sehemu ile niliyopanga nikae mimi, na huyo jamaa akaja kwenye ile meza, unajua,….. ndio maana nasema sio kweli, jamaa alipogundua kuwa aliyepo hapo ni Makabrasha…kwa haraka akasimama kuondoka,

Makabrasha akajua jinsi gani ya kumweka sawa, wakaongea na mwishoni wake nikaona wakikubaliana kwa kushikana mikono, …’akasema

‘Walikubaliana vipi…?’ nikauliza

‘Baadae Makabrasha akanipigia simu ndio akaniambia kuwa kaongea na hao watu, na wao wamekubali kuachana na hizo picha kama watapata mafaso yao, na gharama za huo mradi, wamesema mradi huo umewagharimu pesa nyingi, kwahiyo wao, kwa haraka wahitajia hisa kwenye kampuni yangu, asilimia kumi na ishirini, akashushana nao hadi kumi na tano, ndio mwisho…na pesa taslimu, milioni hamisini…’akasema

‘Mungu wangu, mbona ngumu hiyo kwanini hisa za kampuni, huoni hapo ni mtego, na watu kama hao huwezi kuingiana nao makubaliano ya hisa, watakuja kuua kampuni…’nikamwambia,

‘Ndio hapo, siwezi kwakweli, lakini sasa nifanyeje…kiukweli hapo nimechanganyikiwa, hata sijui nifanyeje…’akawa kweli anaonyesha kuchanganyikiwa, mimi sikuweza kumsaidia kwa hilo, nikasema;

‘Mimi sitaki upuuzi wenu, huyo makabrasha ndiye anakuchezea akili, wewe hujui tu, mimi hado hapo nimeshaiona hiyo picha, ni swala la kupata ushahidi tu…’nikasema

‘Sio yeye bwana, yeye hawezi kunifanyia hivyo, yeye pamoja ya kuwa ni rafiki yangu lakini pia yeye ni kama ndugu yangu tumetokea kijijini kimoja, kama angelitaka kitu kama hicho angeliniambia, na yeye mbona tunafanyiana kazi mara kwa mara ...’akasema.

‘Sasa sikiliza umeshanifahamisha hilo, sasa ankuomba, niachie hilo jambo, mimi nitafanya kivyangu, lakini kwangu hapati hata senti moja, wewe fanya ufanyavyo, wewe si una pesa, …tumia pesa zako, na hisa zako, shauri lako,..mimi nitatumia mbinu zangu, huyo mtu kaingia kubaya..’nikasema

‘Ndio maana nimekuja kwako, na nakufahamu wewe ni askari, unaweza kupambana na mtu kama huyu, kwa mbinu zako za uchunguzi na mimi nitatumia kila hali, pesa , na kila njia, ili tuweze kupata mwanya wa kumshinda huyu mtu na mambo mengine yaenda kama kawaida,...’akaniambia

‘Hili sio swala la uaskari, huu hapa ni utapeli, wa kishenzi, na mbinu kama hizi mwisho wake ni mbaya, sipendi kabisa kujiingiza huko, najua ni nini kitatokea baadaye, ...tamaa ya namna hiyo inaweza kugharimu maisha ya watu, na ukiingia huko, ukanaswa kwenye mitegi yao, kuja kujinasua itakuwa vigumu sana, ..haya baada ya hapo mkakubaliana nini?’ nikamuuliza

‘Mimi sijakubaliana naye bado, maana walichokitaka ni kikubwa sana kwangu, kwa hivi sasa kwanza sina pesa, pili kampuni ina madeni mengi, na ukumbuke baba mkwe anafuatilia kila kinachoendelea kwenye kampuni kwa vile kampuni hiyo imeanzishwa kwa mkopo wake,…..’akasema

‘Hujapanga kitu na yeye unakuja kwangu, mimi sina pesa, mimi kwa hivi sasa nipo maternity, na zaidi unajua mke wako kaniganda kama ruba, unataka mimi nifanye nini..?’ nikamuuliza

‘Nafikiri hunielewi na huniamini, nimekuambia kila kitu nimekiacha mikononi mwa huyo wakili, kaongea naye wakaja na makubaliano hayo, sasa, mimi nashindwa la kufanya,..na huyo wakili anasubiria jibu langu, nilitaka ushauri wako hapo, nifanyeje…?’ akaniuliza

‘Ushauri wangu eeeh, waambie, ‘go to hell’ unasikia, najua unafahamu kiingereza sawa sawa,….unanielewa waambie wafanye wanalotaka, mimi siwezi kukushauri jambo hapo, huwezi kuwapa hisa nyingi hivyo, bado wanataka pesa kiasi hicho, kama unazo wape..’nikasema

‘Basi, ngoja nikikutana naye tena nitajua la kufanya, huyo wakili atanisaidia tu, anafahamu njia ya kupambana na hao watu, atawafanya washuke shuke, kwa hisa sikubaliani nao kabisa…’akasema

‘Umesema kuwa uliwahi kufanyiwa hivyo, na aliyekusaidia ni huyo huyo wakili , alikusaidiaje… ?’ nikamuuliza

‘Nikuambie ukweli, yaani sasa nachanagnyikiwa, kwani siku za nyuma, kama miezi kadhaa nyuma..yawezekana mwaka sasa, sina uhakika.., nilitakiwa kumlipa binti mmoja pesa nyingi tu, baada ya vitisho vinavyofanana na hivi, sikuweza kufahamu ni nani, ila huyo binti aliniambia kuwa huyo anayeshirikiana naye ni mtu wa usalama wa taifa...’akasema

‘Mtu wa usalama wa taifa!, hapana wewe, ulijuaje kuwa huyo mtu ni mtu wa usalama wa taifa?’ nikamuuliza

‘Ndivyo alivyoniambia hivyo huyo binti...’akasema

‘Usiwe mjinga, ni huyo huyo wakili wako anakuchezea, keshaonja asali sasa anataka kuchonga mzinga, naona hapo kuna jambo, nahisi wewe unafahamu zaidi ya hayo...je huyo binti ni nani?’ nikamuuliza

‘Mhh, ni binti mmoja muhuni tu, haina haja kumfahamu, si unajua zangu, pombe zikinitinga nakuwa sio mimi tena, ilitokea bahati mbaya tu...’akaniambia

‘Au ni yule binti wenu wa ndani mliyesema katoroka..hivi kweli ilikuwaje, sijamsikia kabisa, sio yeye kweli?’ nikamuuliza na yeye akageuka pembeni,na kukaa kimiya.

‘Sikiliza, kama unataka kushirikiana na mimi kwa hili, hunabudi kuniambia ukweli wote je huyo binti ni yule binti wenu wa ndani, na kwanini alitoroka?’ nikamuuliza.

Hapo alikaa kimia, nikahisi kuna jambo hapo na hapo naweza kugundua mambo, na huenda huo ndio mchezo wao, na sasa anataka kunitumbukiza na mimi kwenye huo mtego.

‘Sikiliza unafahamu mimi ni mpelelezi, na kwa hilo naweza kulifanyia kazi na kuligundua, ..ninaweza kumtafuta huyo binti na kuufahamu ukweli wote, sasa ili tusipoteze muda niambie ukweli kilichotokea kwa huyo binti..?’ nikamuuliza

‘Wa nini huyo binti, sitaki kabisa kumuona tena huyo binti, maana nikimuona nitamweka ndani..hata hivyo yule binti ni wa kijijini tu.., anahusikanaje na hili…’akasema

‘Una uhakika na hilo…sio yeye uliyempachika mimba ndio akaanza kudai mapesa mengi…, niambie ukweli au nianze kazi ya kuwapigia simu watu wangu,wanaomfahamu huyo bint..?’ nikamuambia

‘Unataka nikuambie nini kumuhusu yeye…?’ akauliza sasa akionyesha wasiwasi fulani. Hapo nikakumbuka kipindi fulani nilizoeana na huyo binti, ikawa mara fulani akiwa na nafasi ananitembelea, na hapo akilini mwangu ikawa inaniuliza ni nani angeliweza kufika kwangu kwa uhuru na kuweka vifaa kama hivyo, ni shuku shuku tu.

‘Kila kitu…ilitokeaje mpaka akatoroka, maana yawezekana ni yeye kaamua kukuchezea huo mchezo, ili kukukomoa, je ilitokeaje kwa huyo binti, je ndio yeye aliyesema anashikrikiana na usalama wa taifa, ..na huyo usalama wa taifa ni nani, nikipata majibu hayo nitaweza kusema neno…’nikasema

Akaa kimia kama anawaza na baadae akaanza kuongea;…

NB: Ngoja niishie hapa kwanza, maana hapa kuna maelezo marefu msichoke kwanza, lakini hapa hapa mtagundua jambo muhimu kwenye hiki kisa…


WAZO LA LEO: Dunia ya sasa ilivyo, sio vyema kumuamini kila mtu, watu wengine wanapenda kuwaingiza watu wengine kwenye biashara haramu, hasa wakishaona mtu mwingine yupo kwenye hali ngumu. Halingumu zetu, maisha magumu yetu, mitihani mbali mbali ya isiwe ni sababu ya kujitumbukiza kwenye biashara haramu, tukauza utu wetu na heshima zetu,..tukaja kuachana na familia zetu, kwa kutumbukizwa jela au kupoteza maisha,…Tuwe na subira kwani mapito hayo, kwani mitihani hiyo maisha, ni ya muda tu, muhimu ni kujaribu kutafuta njia halali za sababu ya kupata riziki na pato halali, tukumbuke baada ya dhiki hiyo, itakuja faraja.
 
SEHEMU YA 105


.....huyo bint ndio yeye aliyesema kuwa anashirikiana na usalama wa taifa…?’

‘Hapana, unasikia ….’akatulia kama anawaza jambo

‘Yule binti aliyekuwa mfanyakazi wa nyumbani yeye aliondoka kwa sababu zake binafsi, aliiba pesa, na pesa hizo nilikuwa nimezichukua kwa mke wangu, kwa kazi maalumu ya zabuni kubwa ya kibiashara, sasa huyo binti akazikomba zote, na sikupenda hilo jambo mke wangu alifahamu kabisa, nikatafuta njia ya kuzirejesha kivyangu..’akasema

‘Kwanini sasa, kama mtu kaiba, kwanini wewe ubebe gharama zake, hiyo sio kweli, niambie ukweli, huyo binti aliondoka hapo nyumbani kwenu kwa sababu gani, nahisi kuna kitu ulimfanya huyo binti, na huenda ni uzinzi wako, na ndio maana ukalipa hizo pesa, na hukutaka mkeo afahamu, hiyo ndio tabia yako, na leo hii unataka mimi nikusaidie, hayo ndio maisha yako au sio...’nikamwambia.

‘Sio kweli yule ni mwizi, na akirudi tena hapa Dar, tunamweka ndani, tatizo hajulikani wapi alipo…’akasema

‘Wewe sikuamini, au nikusaidie kumtafutahuyo bint alipo, nipe hiyo kazi japokuwa sina muda, mimi nitamleta hapa na atausema ukweli wote…’nikasema

‘Hapana achana naye, huyo nilishamalizana naye, muhimu ni hili tatizo lililope mbele yetu, mbona hulitilii maanani, hivi, ..’akasema

‘Sizani kama tutaelewana kwa hali kama hiyo…’nikasema

‘Sasa kama huniamini mimi utamuamini nani,..ndivyo ilivyokuwa,..na mimi ndiye muhusika,…’akasema

‘Sasa sikiliza, mimi nikionana na huyo mtu atakayetusaidia, kama mambo yatakwenda vyema nitakuja kukuambia, vinginevyo, kama unaona huwezi kunisaidia, au tusaidiane, haya,…lakini hili tupo wote..hatari niliyo nayo mimi haina tofauti na yako…na hao jamaa inavyoonekana, lengo lao ilikuwa kupata pesa kote kote, ila wameshindwa…’akasema

‘Mimi siwezi kukubaliana na wewe mpaka nifanye uchunguzi wangu nihakiki haya mambo, siwezi kukubali upuuzi kama huo, mimi sio kama unavyonifikiria wewe, na ole wenu nikiwagundua kuwa mna njama zenu za kitapeli, .....’nikasema

‘Hakuna utapeli hapa..unielewe hivyo…’akasema

‘Miminilivyo eeh, nipo tayari hata hizo picha zifike kwa mkeo lakini nitahakikisha nalisafisha jina langu kuwa hata mimba wewe ndiye sababu, nyie ndio mlifanya mbinu zenu na sijui mlikuwa na malengo gani, mlitumwa, au…sawa usiposema ukweli hili litakuwa lako,....’nikamwambia.

‘Ukinitisha mimi utajisumbua bure, sijui lolote, hata mimi najiuliza ni kwanini, sijui kitu, wakati mwingine nahisi kuwa sipo sawa sawa..lakini haya niliyokuambia ndio ukweli wenyewe…na hata kuamua kuja kwako, nilijua tutaweza kushirikiana , sasa wewe unazidi kunichanganya tu hapa’akasema

‘Niambie huyo Makabrasha mlijuana naye kivipi, ndio umesema mlikuwa wote kijijini sawa…, je ilitokeaje mpaka mkawa na usuhuba wa karibu kwenye mambo yenu ya kazi, na haya…, ?’ nikamuuliza

‘Usiweke hivyo …usuhuba na huyo mtu ni mpaka kuwe na masilahi kwake, ..’akasema

‘Ni kusema kabla ilikuwaje …’nikataka kuongea na yeye akaanza kuongea

‘Kujuana kabla, ni hivi, yeye mwenzangu alitangulia kidunia na kimaisha, ni mkubwa kuliko mimi, na aliwahi kufika mjini muda mrefu tu, na kutokana na kisomo chake, alikuwa akifahamu mambo mengi sana...nilipenda sana tabia yake ya kujua kila kitu, akawa kama mwalimu wangu...akija kule kijijini, ananisimulia mengi, na alipenda sana kusoma vitabu, na moja ya mambo aliyokuwa akinisimulia ni kama hayo...’akasema

‘Mambo gani hayo, unayosema kama hayo…?’ nikamuuliza ili kujua zaidi

‘Yakusomea sheria, na kuja kupambana na watu matapeli, kama hao, ambao kazi yao ni kutaka kupata pesa kwa matajiri kwa njia hii, ya kuchukua picha mbaya na kuwatishia matajiri, na wanatoa pesa ili siri zao zisivuje yeye alisema anataka kuwakomesha hao watu...’akasema

‘Kwahiyo akakufundisha na wewe jinsi gani wanafanya, au anafanya, au alipenda kufanya, na wewe sasa ukaamua kunifanyia mimi, au sio?’ nikamuuliza

‘Kukufanyia wewe…!!! Hapana, alikuwa akinihadithia hivyo visa tu, mimi nilikuwa nikimsikiliza tu, ikatokea nikamuoa mke wangu, na akalifahamu hilo kuwa nimemuoa mke mwenye uwezo, na hapo ndio akaanza kunifua fuata, kwanza alikuja na ajenda ya kunilaumu kwanini nimekimbilia kumuoa mke mwingine nikamuacha mchumba wangu,…’akasema

‘Mchumba wako!!! Ina maana ulikuwa na mchumba wako, mwingine, kabla ya kukutana na huyu mkeo ?’ nikamuuliza

‘Kila mtu anakuwa hivyo, au sio, unakuwa na wachumba wengi lakini mwisho wa siku unaamua kumuoa mmojawapo, ni kweli nilikuwa naye, sikuwa na mwingine zaidi yake, wengine walikuwa wakupotezeaan muda, kila mtu alijua hilo, hilo kiukweli siwezi kukudanganya…’akasema

‘Ok…nimekuelewa hapo…, sasa lakini bado najiuliza, kwanini huyo wakili akulaumu kwa hilo..?’ nikamuuliza

‘Unajua yeye, alitaka awe wakili wetu, lakini sikupendelea awe hivyo kwa vile namfahamu sana tabia yake, hata hivyo alivyozidi kunifuatilia, nikaona bora niongee na mke wangu niona kama ataweza kunikubalia tumpe kazi hiyo, lakini mke wangu akasema tayari yupo wakili wake anamuamini sana.

‘Sasa kwanini azidi kuja kwako, bado haijaniingia akilini, kwanini wewe, asiwe mwingine, sawa yawezekana ni katika kutafuta wateja au sio, lakini kwako…mmh, kuna sababu au sio…’nikasema

‘Yeye nahisi alikuwa na ajenda zake za siri, maana baadae alikuwa akija kunishawishi nifanye mambo fulani ili huyo wakili wa mke wangu aonekane hafai, ili yeye aje kuipata hiyo nafasi, unaona ilivyo… ina maana alikuwa na jambo anataka kulifanya, na mimi sikumkubalia ..’akasema

‘Kwahiyo…kwahiyo…sizani kama ni ajira tu alikuwa anataka kwako, kuna msukumo hapo,..kwanza lawama, pili ajira, na tatu….niambie ukweli?’ nikauliza

‘Tukawa hatupatani, lakini kuna muda tunaelewana, nikiwa na kazi fulani za haraka unajua tena hizi kazi zetu za biashara, sio kila kitu kinakwenda kwa mkono wa sawa, inabidi wakati mwingine upindishe mambo, basi huwa namtafuta yeye, na yeye hashindwi kitu, anajua njia zote za kupindisha pindisha mambo na siku zinakwenda, unafanikiwa kile ulichokitaka ndio maisha..’akasema.

‘Nimjuavyo Makabrasha katika uchunguzi wangu, alijengwa, hata kusomeshwa na yule mwanasiasa mpinzani wa baba mkwe wako, …na sasa kuona anataka kujiunga upande huu, …tatizo lako hutanielewa,…huyo Makabrasha ana zaidi ya hilo unalolifikiria wewe…’nikasema

‘Hayo ni mawazo yako, maana pia mimi nilimuuliza hilo, akasema yeye ni kama taksi dereva, abiria wake wote ni sawa, haijalishi wapo kwenye imani au chama au kabila gani, muhimu wanamlipa ujira wake…’akasema

‘Ukaamini hivyo..hahaha, huyo mtu yupo kwenye orodha ya watu wasiofaa, nikisema hivyo nina maana yangu, …na siwezi mimi kuwa naye chungu kimoja, hatutakuja kuelewana kamwe, na anaifahamu….ila kwasasa anahisi kanipata, hajanipata bado, haweza kuja kuonana na mimi uso kwa uso…ndio maana anakutumia wewe…’nikasema

‘Mimi hayo siyajui, kama mna uadui ni wenu nyie wawili, mimi yule ni ndugu yangu rafiki yangu, tunaivana sana, …kama ana ajenda ya siri, labda ni ya kimasilahi, lakini nina imani kubwa, kuwa hawezi kunitupa..’akasema

‘Hahahaha…sasa hebu subiri, usiondoke, ..’nilisema hivyo nilipoona anataka kuondoka.

‘Huyo mchumba wako na Makbrasha, wana ukaribu gani, udugu labda hivi..maana ni kwanini akaja kukulaumu wewe kwa hilo, kuwa umemuacha mchumba wako na kukimbilia kumuoa mchumba tajiri..?’ nikamuuliza

‘Unajua alichonilaumu mimi, sio kwa vile tu nimemuoa binti tajiri na kumuacha huyo mchumba wangu, wa awali, yeye alisema nimemuoa mke tajiri, lakini siwezi kuwa na akili ya kuona mbali, siutumii huo mwanya kujiimarisha na kuwa kama baba mkwe wangu ….’akasema

‘Kama baba mkwe wako…unakuja taraibu, au sio…’nikasema

‘Kwani, ..ndio hivyo…yeye alisema hivyo, na pia mimi nimekuwa kama mtumwa fulani hivi wa mke wangu..siku hiyo tulikosana naye, anafikia kuniambia eti mimi ni mjinga, mtumwa wa mke wangu.. sio kweli…’akasema..

‘Ngoja, ngoja..hapo hapo,.. nikuulize kwani kwa mkeo unakosa nini, mbona mkeo ni mtu mnzuri tu, hajali kuhusu maisha yako, una kampuni yako, na hiyo kampuni imetokana na baba yake,..?’ nikamuuliza

‘Unajua tena, wakati mwingine nayawazia mawazo ya huyo rafiki yangu kuwa huenda ni kweli naweza kufanya hivyo na mimi nikawa mtu mwenye mamlaka yake, ni ndoto za kimaendeleo au sio, hata kama utaharibu hapa, lakini kwa vile mwisho wa siku utafanya jambo kubwa la maendeleo, hakitaharibika kitu, ndio hivyo…sasa sikiliza, ngoja mimi niondoke…’akasema nikahisi kuna kitu ananificha na mimi sijamalizana naye.

‘Subiri mimi sijamaliza na wewe,…hili neno la kutaka wewe uwe kama baba mkwe wako, ni lako, ..au lilitoka kwa Makabrasha..?’ nikamuuliza

‘Mhhh, yeye ndio alianza kuniambia, lakini hata mimi nilikuwa na wazo hilo…’akasema

‘Kwanini hakukuambia uwe kama yule mpinzani wa baba mkwe wako, na yule si mtu mkubwa, tajiri…eeh, kwanini…huoni kuna kitu hapo, au akili yako bado inafikiria hapa tu…?’ nikamuuliza

‘Tatizo wewe unakuza mambo, …unataka kulifanya hili la kisiasa au sio, makabrasha na siasa wapi na wapi…’akasema

‘Yeye si mbwa wa bwana, anatumwa, anaelekezwa, tatizo wewe humfahamu makabrasha kwenye uwanja huo…wewe unamfahamu kwa mahusiano ya karibu, mimi namfahamu kitaifa na kimataifa, huyo mtu sio mchezo, anajua kuingia anaga zaote na akafanya uaharibifu..ni mtu hatari, kuliko unavyofikiria yeye, akiwa vitani hana udugu,…nakuonya hilo ulifahamu…’nikasema

‘Wasiwasi wako tu, mimi namfahamu sana, ni mtu wa kijijini, tumeishi naye sana..sema mud mwingi alikuwa huku mjini…’akasema

‘Ok…najua naongea na mtu …ok… nikuulize kwanza, ina maana wewe ulimuoa mke wako kwasababu ya utajiri au ulimpenda eeh,..?’ nikamuuliza na hapo akacheka, na kutikisa kichwa, na kuonyesha furaha fulani hivi…akasema;

‘Unajua swali lako hilo ni kama kunitega, lakini nikuambie kitu hata rafiki yangu huyo ananilaumu kwa hilo na hata kufikia kusema kuwa mimi sikustahiki kumuoa mke tajiri, eti sijui jinsi gani ya kuendeleza huo utajiri, na mke akaniamini, eti mimi nilitakiwa nimuoe mpenzi wangu huyo wa siku nyingi, maana yeye tunaendana, lakini mimi sio kuwa nimemuoa mke wangu kwa vile ni tajiri tu, pia nampenda …’akasema

‘Unampenda pia, hahaha… sasa kwanini umemsaliti, au mapenzi kwako yana maana gani..?’ nikamuuliza na hapo, akawa kimia kama anawaza jambo, na nilipoona hataki kujibu swali langu hilo nikamuuliza swali jingine;

‘Huyo mpenzi wako unaweza kumlinganisha na mkeo, mkeo ana kila kitu, kwanza yeye ni mzuri, mpenzi wako anaweza kumfikia mkeo kwa uzuri, zaidi ya hayo yeye ni msomi ana pesa, amatokea kwenye familia yenye uwezo,....kwanini hutulizani na yeye mkasonga mbele, sasa angalia ulichokifanya, haya yasingelitokea kwasababu ya tamaa zako?’ nikamuuliza

‘Usinilaumu kwa hilo….kwanza haya yameshatokea, lawama haisaidii…,najua nimekosea, lakini sio kwa kupenda, unajua mengine nikikuambia hutanielewa, ndoto yangu kubwa, ilikuwa kumpata mtoto wa kiume, na pia hiyo ya kutaka na mimi nijikweze, niwe mtu wa kuheshimiwa, kama mume wa familia,…’akatulia

‘Una uhakika kwa kufanya ulivyofanya unaweza kulifanikisha hilo…?’ nikamuuliza

‘Ndio kitu …nilitaka kukifanya, haya mengine yamtokea na kuharibu kila kitu,..haya sio ajenda yangu, …hapana, ndio maana nasema wakati mwingine nahisi kama sipo sawa sawa, ..kuna hali inanitokea na kuwa kama nimechanganyikiwa,…na sijui, kuna dawa nilipewa zinanisaidia saidia..’akasema

‘Unahisi…haupo sawa kiakili..una tatizo la akili labda, au ..kwani ulipimwa hospitalini..?’ nikamuuliza
‘Hospitalini walisema ni mawazo tu…nikaonana na jamaa yangu mmoja akaniambia hata yeye ana matatizo hayo, kuna dawa anatumia zinamsaidia…’akasema

‘Rafiki, sio docta, wewe…si umesoma wewe, halafu dawa za matatizo ya akili..?’ nikamuuliza

‘Unajua ukitegemea hospitalini, unaweza ukapata shida, kwanini hamuamini dawa za kienyeji..’akasema

‘Kwahiyo ni madawa ya kienyeji ulitumia…ya miti shamba au sio..?’ nikamuuliza

‘Ya kienyeji lakini ya kitaalamu..yapo kividonge hivi…’akasema

‘Ni nani huyo docta, au huyo rafiki yako ni docta..?’ nikamuuliza

‘Kwanini unaiuliza hivyo, nimeshapona, inatokea tu , sio tatizo sana, ila kuna muda inatokea, ikitokea natumia hizo dawa…’akasema

‘Hebu kwanza,..hili la afya yako tuliweke pembeni…. unajua mimi siwezi kufanya jambo bila kufahamu kiini chake, kukuhoji hivi ni kutaka kufahamu kiini cha haya yote,..unasikia, sasa twende kwa huyu rafiki wako wa zamani…’nikasema

‘Wanini, huyo achana naye, hana tatizo kabisa, usimuhisi vibaya, huyo namuamini sana, na …sitaki mtu amsema vibaya,…’akasema

‘Kwasababu unampenda sana au sio…?’ nikamuuliza hivyo

‘Hahaha, sio hivyo, ndio kumpenda ni sawa tu, kwa vile alikuwa mtu wangu, na ndio hivyo, hata hivyo, kwa hivi sasa yeye ana mume wake, na mimi nina mke wangu, hayo yalipita, japokuwa tumetoka naye mbali, sio kwamba kwa vile sijamuoa, ndio nimseme vibaya, hapana, huyo …hapana, ..sipendi kwanza kumuongelea vibaya, kabisa kabisa..’akasema, na mimi nikamuangalia moja kwa moja usoni na kusema;

‘Kwangu mimi ili nikusaidie hili, itabidi umuongelee, nimfahamu, kuna kitu nahisi anahusika,…’nikasema

‘Wewe unahusikanaje, uwongo kabisa, ungelimfahamu huyo binti, hana tatiz na mtu…’akasema

‘Sikiliza mimi ukiniambia ukweli kumuhusu yeye, basi mimi nitafahamu kama kweli anahusika au hahusiki, unielewe hapo, hebu niambie ukweli kuhusu huyo mpenzi wako wa siku nyingi, ni kitu gani maalumu kinakufanya umpende sana?’ akaniuliza

‘Mpenzi wangu wa siku nyingi nampenda sana, na yeye anafahamu hilo, lakini mke wangu ana kitu cha ziada, ana mali au sio, hata wewe unalielewa hilo,. Kwahiyo hivi ni vitu viwili huwezi kuvilinganisha kama unavyotaka wewe.’akasema

‘Hujanijibu swali langu bado..’nikasema

‘Huyo mpenzi wangu wa zamani, yeye kwa kulinganisha na mke wangu, yeye kiukweli, anayafahamu mapenzi ya kweli, na penzi letu mimi na yeye ni la kutoka moyoni,…nilishakuambia ni penzi la asili, hilo halitaweza kufutika moyoni hta ukimuuliza yeye, …lakini eeh, mtaishije, maisha yanahitaji kujiongeza, au sio..? hamuwezi kulala njaa, huku mnasema mnapendana, au sio, ilibidi iwe hivyo, baada ya kumpata huyu mke wangu basi tena, ikawa ni bahati …’akasema

‘Kwahiyo,eeh,..ngoja kwanza, ulipompata huyo mkeo, maana sio kazi rahisi kama nijuavyo, kwenye swala la mapenzi,…sasa wewe uliwezaje kumshawishi huyo mpenzi wako hadi akakubaliana na wewe au wewe ulimsaliti tu kivyako, maana nakuona ndio tabia yako …?’ nikamuuliza

‘Hapana mbona tulikubaliana tu kwa wema tu.., tulikaa tukaongea ,tukakubaliana iwe hivyo..unajua ilitokea bahati, yeye naye alimpata mwanaume mwenye uwezo,…na..alimpenda kwa hali kama ilivyo yangu, tukaona tusiziachie hizo bahati, unaona eeh, nakuelezea haya, kwa vile nakuamini,sikutaka kumwambia mtu mwingine haya yalikuwa baina yangu mimi na yeye tu...’akaniambia hivyo.

‘Hahaha, mnanishangaza sana, ..yaani muache kuoana nyie mnaopendana kiukweli, mkakubaliana muachane ili mpata wenye mali, ajabu kabisa,, sasa hauoni kuwa mlijidanganya..’nikasema

‘Kwa vipi…?’ akaniuliza kwa mashaka.

‘Sasa wewe huoni, ndio maana hutosheki kwa mkeo, wewe hulioni hilo..?’ nikamuuliza

‘Hapana…sio hivyo,..sisi wawili tulielewana, na hakuna atakayeweza kutuelewa kamwe, ndio maana nasema huyo mpenzi wangu wa zamani muache kama alivyo, hahusiki na lolote,..na isingelikuwa uyu mtu , aliyekuja kutughasi baadae, sisi tulishamalizana,..’akasema

‘Aliyewaghasi ni huyo Makabrasha au sio..?’ nikauliza

‘Ndio,…, maana hakuishi kwangu tu, alikuwa akienda hadi kwa huyo… kumsumbua..’akasema

‘Anamsumbua kwa lipi sasa..?’ nikamuuliza

‘Eti na pia huko yeye awe wakili wao wa familia, yeye alitaka apenyeze mambo yake kila mahali, lakini hakuafahamu misimamo yetu sisi wawili, na akija kwangu anajaribu kunishawsishi kwa maneno yake ya kunikera kuwa mimi sio kama mume, mimi ni kama nimeolewa na mambo kama hayo, ni maneno ya kuniumiza moyo tu…’akasema.

‘Kwani ni kweli, kuwa wewe upo upo tu, sio kama mume…?’ nikamuuliza

‘Aah, hayo tuyaache bwana, kwani yanasaidia nini kwa hili…’akasema

‘Sikiliza unajua hapa najaribu kutafuta ukweli, inawezekana huo ukweli ukawa na sababu na hili tukio, mimi kwanza simuamini huyo rafiki yako, nahisi anahusikana na hili jambo, nimeshaanza kuhisi hivyo…, kuna mambo kidogo bado sijaelewa, nikielewa tu, nitakuambia ni kwanini simuamini huyo rafiki yako…’akasema.

‘Mambo gani hujaelewa, sikiliza haya ni mambo mawili tofauti, niamini mimi…’akasema

‘Sikiliza, mimi kazi hizi za upelelezi nazifahamu sana, sisi huwa tuna hisia zetu, hisia ya tatu,..kama kuna jambo linahusiana, akili hucheza, na mara nyingi, ikitokea hivyo, inakuwa kweli..hisia ya tatu, usiifanyie mchezo na hisia ya tatu,.. mashaka kidogo yanakutuma kwenye sehemu ambayo hutegemei, na huko huko ndio unaupata ukweli, mimi nahisi huyo mpenzi wako, ana kitu na Makabrasha..sasa niambie ukweli, …wewe kuna kitu unanificha, au …’nikasema

‘Unataka nikuambie nini sasa…?’ akaniuliza

‘Kila kitu, ..mfano, Huyo Makabrsaha alikushauri nini, baadae, ..?’ nikamuuliza

‘Ushauri wake, ni kuwa yeye anaweza kunisaidia, nikawa mume mwenye nguvu, nikaweza kuzitawala hata mali zetu za ndani..vitu kama hivyo…’akasema

‘Kuzitawala…!!! Mhh..kwa vipi sasa…?’ nikamuuliza, nikiwa bado na maswali mengi kwake.

‘Unajua mimi na mke wangu tuna mkataba,…’akasema

‘Mkatabaeeh, ..yapu huo ndio unakuweka roho juu, je huyo rafiki yako aliwahi kukusaidia ukaukwepa huo mkataba, au sio…’nikasema

‘Ndio… sikutaka kukuambia hili…, kuna kipindi ilitokea nikamjaza binti fulani mimba ..’akasema na kushtuka akakatiza , hakuendelea kuongea.

‘Mwingine huyo,au yule yule…?’ nikauliza

‘Sikiliza sasa,…ilikuwa ni bahati mbaya, huyo binti akaja juu, anataka kunishitakia, ..sasaa liyenisaidia kwa haraka ni huyo rafiki yangu, na ndio hapo akagundua kuwa mimi na mke wangu tuna mkataba,..na ndio akaniomba aupitie huo mkataba, aona kama kuna kitu cha kunisaidia…’ akasema

‘Duuh, kwahiyo ndio hapo huyo jamaa akafahamu kuhusu mkataba wenu, kumbe alishalifahamu hilo…sasa huoni hapo, huyo jamaa alishakutega, alishajua siri zenu, na sasa keshakuweka kiganjani,…’nikasema

‘Sasa ningelifanya nini, maana asingelikuwa yeye, mimi ningelichukulia haya mambo kiubabe, na binti angelienda mahakamani, ina maana mke wangu angelilifahamu hilo, na mkataba wetu ungelinifunga, hebu wewe angalia hilo, ndio maana namthamini sana huyo rafiki yangu…’akasema

‘Na wewe huoni kuwa huyo rafiki yako alingojea nafasi kama hiyo, na sasa imetokea, ndio maana anatumia mbinu za namna hiyo, hivi sasa keshakunasa, ana kila ushahidi wa kukuweka kubaya..ndio maana akalifanya hili..hapo alichokifanya ni kutafuta mtu mwingine, kumbe huyo mtu mwingine wamepangana naye, hizo ni mbinu zake tu…’akasema

‘Huyo jamaa haamini watu bwana kwenye kazi zake, sijaona msaidizi wake zaidi ya binti mmoja anyechapisha barua zake, mimi ninamfahamu sana, achana na mawazo hayo..’akasema

‘Kwahiyo kwa kifupi, huyu rafiki yako kakushauri nini kwenye hilo, atakusaidiaje, si lazima mlijadili afanye hiki na hiki, au sio..?’ nikamuuliza

‘Anasema kuna jambo alitaka alifanyie kazi likifanikiwa sitakuwa kwenye matatizo tena, ila ni gharama sana, zaidi ya gharama, …lakini yeye hana tatizo, hata kama ni gharama hawezi kunifanya nilipe kwa mkupuo, atajua jinsi gani mimi nitamlipa…’akasema

‘Hajakuambia ni kiasi gani..?’ nikamuuliza

‘Hajasema , si mpaka afanikishe hilo jambo,…’akasema

‘Hapo sijakuelewa, hilo ni pamoja na hizo picha au hilo ni jingine…?’ akauliza

‘Hilo ni jingine bwana, hili la picha ndio imekutana naye leo tukajadili , ila kasema hata hili la picha ataweza kulimaliza, kwa huo mpango anaoufanya, ukifanikiwa basi mimi nipo huru, maana picha zikifika kwa mke wangu, ina maana ni ushahid tosha au sio..kwahiyo akasema nimpe muda alifanyia kazi….’akasema.

‘Kwahiyo hilo la kulifanyia kazi lilitokea lini, kabla ya hili tuko la picha au sio..?’ nikamuuliza

‘Kabla, ndio…na sasa tulipokutana ndio akasema ule mpango uharakishiwe maana utasaidia hata kwenye hili tatizo la picha..muhimu ni mimi nihangaike kutafuta pesa, maana inahitajika pesa nyingi sana..’akasema

‘Hahaha, wajinga wakubwa nyie…hapo nimekunasa kilaini, ..haaa, sawa bwana, ngoja tuone…’nikasema, na yeye alikuwa bado hajanielewa, na sikutaka anielewe, kwa muda huo, ila kwangu mimi nilishagundua ni nini kinachoendelea

‘Umeninasa kwa vipi..?’ akauliza, na mimi nikasema

‘Kwahiyo wewe sasa unataka kufanya nini, kwa hivi sasa, maana mwenzako kakutega, na kwa hili umeshaingia kwenye mikono yake, sasa nikuulize ni kitu gani hicho alitaka kukifanyia kazi, ..?’ nikamuuliza

‘Hakuniambia, …cha muhimu kwangu ilikuwa ni jinsi gani ya kuikoa ndoa yangu,..’akasema

‘Yeye alikuambia hichoakikifanya ataiokoa ndoa yako, ..?’ nikamuuliza

‘Hicho kitu, kitasaidia mambo mengi tu, pamoja na hilo…’akasema, na kuendelea kusema
‘Kiukweli mimi na mke wangu tunapendana, na sitaki kuja kumuumiza mke wangu, sitaki watoto wangu waje kupata shida, wakiulizia baba yao yupo wapi, ni bora nife kabisa nijue moja…’akasema

‘Ni nini maamuzi yako mpaka sasa tusipotezeana muda hapa, maana nakuona akilini hufikirii mbali, hapo kila kitu kipo wazi,..?’ nikamuuliza

‘Mimi nina uhakika huyu rafiki yangu atanisaidia, alishanisaidia sana, na hili hawezi kunitupa,atapambana na hao watu, sasa tatizo ni pesa…’akasema

‘Sawa tatizo ni pesa, na wao lengo lao kubwa ni kupata pesa, na wameshakuambia pesa unazo unazikalia, sasa inuke wazichukue, hahaha, unajua wewe ni mjinga sana, unajua nikuambie, usipende kujifanya mjanja, kwa hili utaumbuka sana, hapa wameshakushika kubaya, utoe wakitakacho au wakuumbue, na kwa hali yako hiyo, huna ujanja…’nikasema na yeye akaniangalia kwa mashaka

‘Kwanini unasema hivyo..?’ akaniuliza

‘Sio kitu…’nikasema nikiwaza kidogo, na yeye akasema;

‘Unajua huyo rafiki yangu aliwahi kuniambia mimi nakusaidia sana, lakini ipo siku utanikumbuka, utayakumbuka maneno yangu kuwa matajiri hawana wema, na ukiwa nao bora ujue njia ya kuwekeza mapema kabla hawajakufukuza, kwani kukuchoka kwao ni rahisi sana , na wao wana mbinu za kukutega, ili wakikuchoka tu wanakutema kirahisi…’akasema

‘Una maana gani hapo sasa, sijakuelewa mbona..?’ nikamuuliza

‘Hebu angalia hili tukio, unafikiri likifika kwa mke wangu itakuwaje, ina maana ndoa yangu hakuna tena, na mimi sina changu, maana kutokana na huo mkataba wetu wa kifamilia, ikipatikana ushahidi, hata kampuni yangu nitanyang’anywa, nitabakia mikono mitupu, na makosa ni ya kibinadamu tu,..wote tunakosea, mbona mimi nafahamu kuwa yeye ana mpenzi wake wa siku nyingi, lakini sina ushahidi,..’akasema hivyo

‘Kwa mawazo ya rafiki yako huyo, wewe uliyafanyia nini,maana unavyoongea ni kama uliyakubali mawazo yako, ukamruhusu afanye anachotaka kukifanya bila kujali ni kitu gani,.. au sio,…sasa wewe ulichukua hatua gani..?’ nikamuuliza nikitaka nimfahamu zaidi.

‘Awali mimi sikumjali sana rafiki yangu, ..lakini siku zilivyozidi kwenda, naona ni kweli, matatizo yanazidi kuniandama, kila nikifanya kosa , najikuta kwenye wakati mgumu,..unajua kitu kingine huyu rafiki yangu hafanyi kazi bure bure, nina madeni mengi kwake, sijamlipa,...’akaniambia hivyo

‘Linaongezeka jingine la madeni,…hahaha,….kuna kitu anakufanyia kazi na hicho kitu kikikamilika hutakuwa hakuna tatizo tena, ni kitu gani hicho…wewe unasema hukijui, au sio, na huku una madeni mengi kwake, nab ado yanaongezeka, nab ado hujaelewa,…mjinga sana wewe…mimi sio mtoto mdogo, unasikia, sasa sikiliza..nijibu haya maswali yangu halafu nitakuambia ni kitu gani hicho…’nikasema

‘Maswali gani hayo tena…?’ akauliza kwa mashaka.

************

‘Hebu nikuulize huyo jinsi gani huyo mpenzi wako wa zamani, alikukubalia umuoe huyo binti tajiri?’ nikamuuliza mume wa familia tena hilo swali , sijui kwanini, nilihisi kuna maungano fulani hapo.

‘Alikubali, kwa shingo upande, tulikuwa hatuna jinsi, lakini alifanya hivyo, kwa vile, na yeye alishampata mwanaume mwenye mwenye nazo pia, kwahiyo tukaona tukubali ili na sisi tuyajue maisha ya kitajiri, mimi nikamuoa binti mwenye hali nzuri, na yeye akaolewa na mume mwenye nafasi yake, na maisha yakaendelea nikijua kuwa pesa ni kila kitu...’akaendelea kunisimulia mume wa familia.

‘Kwahiyo kwa kauli hiyo inaonyesha kuwa huna raha na mke wako?’ nikamuuliza

‘Raha ya kipesa ninayo, lakini kwa mapenzi..mmmh…, yale ninayoyataka mie, unajua mke wangu ni mtu wa kazi, hana muda wa starehe, ndio maana nahangaika na watu kama nyie, ..lakini sio tatizo sana, …tuyaache hayo, maana , kila mtu na uwalakini wake, ...unafahamu mke wangu hajali kuangalia hisia za wenzake, ndio tatizo lake jingine, yeye anaona utajiri ndio mapenzi yake,...’akaniambia

‘Nikuulize kitu, ina maana wewe na mpenzi wako wa zamani, huwa, mnakutana, mnaonana, au ulipo-oa mkakata wenu wa mahusiano…ndio mkawa hamuonani tena,ili kulinda heshima zenu, ili msije mkagundulikana kuwa mlikuwa wapenzi na bado mnapendana?’ nikamuuliza

‘Hili swali gani, hilo siwezi kulijibu, maana huko unakokwenda una nia ya kunichimba,huko unapokwenda hakuna maana usiniulize maswali ambayo hayatatusaidia kitu, sanasana ni kuniumiza moyo wangu, mengi yamepita na haya yaliyopo mbele yangu,yataharibu kila kitu,sema utanisaidia au niondoke, .?’akaniuliza

‘Mimi ninakuuliza hilo swali nikiwa na maana yangu muhimu, inawezekana huyo jamaa anashirikiana na mpenzi wako wa zamani, atakuwa anakufanyia hivyo kwasababu maalumu, ’nikawambia.

‘Hiyo hoja yako haina mshiko, yeye anifanyie hivyo ili iweje, ...ili nikose, nimuache mke wangu, nikikosa yeye yeye atapa faida gani kumbuka tuliacha kuoana mimi na yeye kwasababu gani, ..na mali aliyo nayo yeye iende wapi, hapo umakosea, hiyo hoja yako haina mshiko...’akasema

‘Binadamu anaweza kukutwa na jambo, au kushawishika na jambo akilenga jambo fulani, na nyie mnaonekana akili zenu ni fupi…, au hata mume wake anaweza kumtumia kwa masilahi fulani, huwezi jua, ufahamu wewe upo kwenye sehemu ambayo kila mtu anaimezea mate, na kwa ajili hiyo, utegemee maadui wa nje na ndani...’nikamwambia lakini yeye akatingisha kichwa kutokukubaliana na mimi.

‘Hapana yule hawezi kunifanyia hivyo hata siku moja, ananipenda sana, hawezi kuniumiza, kama ilivyo mimi, …tumeamua iwe hivyo, na tunaaminiana kihivyo, kwa vile tunafahamu wapi tulipotoka, kila mmoja ana mipango yake ya kimaisha na mwenza wake,tulishawekeana ahadi kuwa tusiingliane...’akasema mume wa familia.

‘Ina maana ulivyoniambia mimi kuwa unanipenda ulikuwa unanidanganya..?’ nikamuuliza na hapo akatulia ni swali ambalo hakulitegemea

‘Ok, sawa nimekuelewa, wewe ulitaka mtoto wa kiume, na sio mtoto wa kiume, bali hilo ni kizingizo, kuna zaidi ya hilo, ...na kwahiyo kwangu mimi, kwasasa kazi yako imekwisha, naomba tusijuane…umenisikia..’nikasema kwa ukali

‘Sio kwamba sikupendi, mimi nakupenda, lakini kila mmoja nampenda kwa nafasi yake, mke wangu nampenda kwa nafasi yake ya kwanza…, na ni mtu muhimu sana kwangu, ndio maana sitaki nimkose kwa hali na mali, na wewe nakupenda kwa nafasi yake, lakini mpenzi wangu wa zamani penzi lake ni la asili, siwezi kuliweka sawa na wengine…’akasema

‘Penzi lake ni la asili kwa vipi..?’ nikamuuliza

‘Hahaha, tatizo lenu hamfahamu mapenzi, penzi la asili kamwe halifutiki moyoni, hata iweje,..penzi hilo huwezi kulilinganisha na kitu chochote, na kama ikiwezekana, kama ikiwezekana zunguka kote lakini mwishowe mtakuja kukutana…’akaniambia

‘Kiukweli ulivyonieleza hapo, haya ya ulevi, kujifanya hupati mapenzi, kuhangaika huku na kule ni kwa vile akili yako bado ipo kwa mpenzi wako huyo wa zamni mpenzi mwenye penzi lako la asili, au sio..wewe ulikuwa unatafuta upate ili baadae mje kukutana na kurejesha mahusiano yenu, na wengine wakawa wanawatumia kufanikisha mambo yao..au sio?’ nikamuuliza

‘Kwani hayo, yatasaidia nini kwenye hili tukio, hivi hujafahamu hatari tuliyo nayo, hulioni hilo…’akasema

Nilikaa kimia kiukweli mimi akili yangu ilishazama kumuwazia huyo mpenzi wake wa asili, sijui kwanini alitokea kumpenda hivyo, na kwanini akawa karibu na Makabrasha, na kwanini..nikahisi hawa watu wana kitu muhimu sana, na kupitia kwao nitaweza kugundua jambo, ambali litamaliza haya matatizo..

Sasa akawa anataka kuondoka, na kabla hasogeza hatua mbili, nikasema

‘Hebu subiri kwanza, ili tuelewane..nataka uniambia ukweli wako,..Ni nani huyo mpenzi wako wa zamani?’ nikamuuliza.

‘Siwezi kukuambia,…’akasema sasa akiwa anaondoka.

‘Sikiliza wewe si unataka tusaidiane kwa hili, kama kweli una nia hiyo, niambia huyo mpenzi wako ni nani…akili yangu inanituma huyu mpenzi wako wa zamani ana jambo na huyo wakili , ukiondoka hapa bila kuniambia hilo usirudi tena hapa, ..NI NANI HUYO MPENZI WAKO WA ASILI…

Hapo akasimama…taratibu akageuza kichwa kuniangalia.....

NB: Ni nani huyo mpenzi wake wa zamani, tukutane sehemu ijayo mungu akipenda tuombeane uzima na changamoto za kimaisha.



WAZO LA LEO: Wapo wana ndoa wapo kwenye ndoa kwasababu ya mali, lakini ndani ya nafsi zao wana wapenzi wao wa zamani, waliowapenda sana, hata wakifany ajambo, wanakuwa kama wanalinganisha,.., hilo ni kosa kubwa sana, huko ni kumsaliti mwenza wako, tukumbuke kuwa mapenzi ya kweli yanatoka moyoni, tukijidanganya kuwa tunapenda eti kwasababu ya pesa, au mali, ipo siku hivyo vitu vyote vitakwisha, je ndio mwisho wa mapenzi yenu. Kama mumeamua kuoana kwasababu ya mali, au sababu fulani, basi jifunzeni kupendana kiukweli. Mungu atawasaidia na mapenzi yenu yatakuwa na baraka.
 
SEHEMU YA 106


‘Sikiliza wewe si unataka tusaidiane kwa hili, kama kweli una nia hiyo, niambia huyo mpenzi wa zamani ambaye unasema mna mapenzi naye ya asili,…?’ nikamuuliza

Ilikuwa ni kama kitu kimemusa moyoni, akasimama, na taratibu akageuka kuniangalia, akasema;

‘Kamwe siwezi kukuambia ni nani, hata hivyo nimekuambia mengi ambayo sikuhitajika kukuambia, tulipatana mimi na yeye mapenzi yetu ya nyuma yawe ni siri kubwa sana,…kumuongelea hapa, ni kama kumsaliti..kwaheri…’akasema na kuondoka zake.

Tuendelee na kisa chetu

************
Siku zikazidi kwenda na mimi nahitajika kwenda kusoma, na hali ya hatari inazidi kuniandama, na kama nisipokuwa makini hata huko kusoma sitaweza kwenda kusoma tena, na nikikwama hilo, basi malengo yangu ya mbeleni yangelikwama kabisa.
Kilichokuwa kikinikwaza ni kuwa bosi wangu yaani mke wa familia, anataka nimuambie ukweli kuwa huyo mtoto nimezaa na nani, nahisi kuna kitu kilikuwa kinamsukuma hivyo, huenda, ameshanishuku.

Siku rafiki yangu ananitamkia kuwa siku akimgundua mtu anayetembea na mume wake atamkamatisha kwa wale wahuni hatajali kuwa ni ndugu yake au ni rafiki yake ndio siku aliyofunga kauli yangu ya kumuambia ukweli, …hapo nikaomba zoezi la kwenda kusoma lifanyika kwa haraka.Nilichofanya ni kuongea na wale watu wanaosimamia mchakato huo mnzima wa masomo yangu ili uwe tayari iwezekanavyo. Ilikuwa ni kazi rahisi kwangu.

‘Ninachoshukuru, pamoja na yote hayo , mke wa familia hakuwa akilifuatilia hilo, ilikuwa kama kalisahau, kwahiyo mipango yangu ya kusoma ikawa inakwenda vyema, japokuwa sikuwa na amani,…na nilishukuru mungu kuwa muda ulipofika tu, nikaondoka kwenda kusoma.

Sasa kabla sijaondoka, nilitaka nifanye mambo fulani ya kuniweka kwenye amani, kwanza kuna huyo mdudu mtu, ambaye alishaingilia maisha yangu, sikutaka hili la picha liishe hivi hivi, japokuwa mume wa familia alishasema kazi hiyo keshampatia Makabrasha, lakini ni nani huyu Makabrasha,..ni mtu asiyeaminika!

Ukumbuke kabla sijaondoka, rafiki yangu au bosi wangu, mke wa familia aliwahi kunipatia kazi, kuwa nimtafuta mtu anayemzuzua mume wake, kwani kasikia kuwa mume wangu ana mwanamke, ambaye anamfanya asiwe na amani, ..na anasikia kuwa huyo mwanamke kazaa na mume wake…sasa hiyo kazi nilitakiwa nimpatie mume wa familia kwa haraka.

‘Atakuwa ni huyo mpenzi wake wa asili…’ niliweka mikakati ya hivyo, ndio maana nilitaka kumfahmu huyo mpenzi wa asili wa mume wa familia, nilijua nikimfahamu tu, mizigo yote ataibeba yeye, tatizo ni hilo, la kuwa kazee na yeye, je kama hana mtoto,..lakini muhimu ni kumfahamu huyu mtu ..maana asipopatikana yeye, basi huyo mwanamke atakuwa ni mimi..’nilijisemea hivyo.

Mikakati ya kwanza na muhimu kumpata huyo mpenzi wa asili,..mikakati ya pili, kumpata huyo mdudu mtu, hapokuwa kwa akili yangu ya haraka, nilishaanza kumshuku huyo Makabrasha

Hapo nilikuwa na siku moja ya kuyafanikisha hayo, sio kazi rahisi, nikaona kwa vile mikakati ya safari imeshakamilika, hiyo hakuna wa kuzuia tena, labda mdada, bosi wangu kama angeliamua, kufanya hivyo, angeliweza, lakini ingemchukua muda,…
Usiku huo nikapanga jambo, ...
Usiku huo, nikawaza sana, na hatimaye nikaona haina budi, ni lazima nimpate mtu, ninayemuamini, nikaanza kuwachuja rafiki zangu ninaowatumia kwenye kazi zangu, nikagundua kuwa kuna mtu wangu mmoja wa karibu sana ambaye nikimpa hiyo kazi anaweza kuifanya bila matatizo.

Tatizo la huyo mtu wangu wa karibu, yeye, kikazi ni mtu kivuli, huwezi kufahamu kabisa kuwa anafanya kazi na mimi, napenda sana kumpa kazi huyu mdada, nilishafanya kazi naye za siri, alitokea kuipenda hiyo kazi, lakini alikwama kusonga mbele, mimi nikamuwezesha kisiri, ..na kiukweli huwezi kujua kabisa kuwa huyu mtu anafanya kazi hizo, kabisa,…tatizo yeye alishaniambia kuwa hataki tena hizo kazi,…

‘Mimi hizi kazi sitaki tena, nataka kutuliza maisha yangu na familia yangu, sitaki kujipa presha…’siku moja aliniambia hivyo.

‘Lakini kazi ninazokupatia ni zile ambazo, huwezi kujulikana kabisa, muhimu iwe hivyo hivyo, siri ndio ufunguo wa kufanikisha hilo, usije kulogwa kumuambia mtu kuwa uanafanya hizo kazi, unasikia, sasa niambie ni kwanini unaogopa kuendelea kuzifanya, ina maana juhudi zangu hadi kukusomesha hazina maana tena..?’ nikamuuliza

‘Nina maana yangu kubwa, na sitaki mtu afahamu hilo, hata wewe, haya nayafanya kwa ajili ya maisha yangu ya baadae, mimi nataka kuwa mke wa familia muadilifu, na hili litakuwa linavunja uaminifu wngu kwa mume wangu…’akasema

‘Sio bosi wangu kakushauri uache kazi hizi au sio , kwa vile bosi wangu keshaanza kunichukia mimi..,?’ nikamuuliza

‘Hapana , wala mimi sina ukaribu naye, unajua kazi zetu zilivyo, sizani kama yeye anafahamu kuwa nafanya kazi kama hizo, ukumbuke hili ulinionya wewe mwenyewe, na ndivyo nilivyo, …’akasema na kweli nilimuamini.

Unapofanya kazi kama zangu unaweza ukawa na watu wako, hata muajiri wako asiwafahamu hata kama huyo mtu ana mume wake , huyo mume wake pia anaweza asijue kuwa mke wake anafanya kazi kama hizo…inakuwa baina yangu mimi na yeye, na yeye anafahamu ni kwanini inatakiwa iwe hivyo. Na malipo yake sio mchezo.

Huyu msaidizi wangu ni mdada, na sio mchezo, kwenye kazi kama hizo namuaminia, anaijulia kazi, anajua mbinu za kila namna za kupata siri fulani zilizojificha, na ni msiri mkubwa sana, na kilichonipa nguvu na kumuamini, ni kuwa kweli hata mume wake alikuwa hajui kuwa mke wake anfanya hiyo kazi.

Siku aliponiambia hataki hizi kazi , nilipata shida sana,maana ni mtu niliyekuwa nikimtegemea kwenye kazi zangu za namna hiyo, sio kwamba sikuwa na watu wengine,lakini huyu nilimuamini sana kwenye hizo kazi, na hata aende wapi nikimuita atafika hapa mjini hata bila kujulikana, akafanya kazi, na akatoweka bila mtu kumfahamu kuwa alikuwa hapa jijini, ni mbinu zetu za kujibadili.

Nilipomkumbuka hapo hapo nikamtafuta kwenye simu, nikampata, nikamwambia,namuomba anisadie kazi mbili muhimu sana, akaniuliza kazi gani, hakusema nilishakuambia sitaki kazi, nikajua huenda sasa hivi huyo mdada hana pesa.

Mimi nikamwambia, moja kwa moja bila kuficha, kuwa kuna mtu anatakiwa yeye amchunguze, kwa ukaribu nahisi huyo mtu anataka kuingilia maisha yangu..

‘Mtu gani bosi, unajua nilishakuambia…’akataka kujitetea

‘Ni Makabrasha, …’nikasema kwa haraka

‘Mungu wangu, huyo mtu tena…’akasema

Hilo neno ‘tena’ nikahisi lina jambo, lakini sikutaka kumdadisi zaidi, mimi nikasema;

‘Sizani kama unamuogopa huyo mtu, ni saizi yako kabisa, mimi nakuaminia,..nafahamu kuwa watu wanamvumishia ujasiri ambao hana, wewe ni jasiri zaidi yake, unaweza kuzivunja nguvu zake kwa siku moja tu, au umeshalainika, na mume wako, usiniangushe, nakuamini kwa kazi hiyo..’nikasema

‘Kwanini unamtaka huyu shetani....’akasema, na alivyotamka hilo neno ‘shetani’ nikahisi kweli kuna jambo kati yake na huyo Makabrasha. Mimi nikamwambia kwa kifupi;

‘Huyu mtu anataka kuniingila kwenye maisha yangu binafsi,…usiniulize ni kwa vipi, muhimu kwako, ni kumfuatilia, kumchunguza, na utakuja kugundua ni nini kipo anakifanya ili kutaka kuangamiza maisha yangu, na ni ni lengo lake, hakuna mtu ninayemuamini kwa kazi hii zaidi yako wewe, malipo yatakuwa zaidi ya unavyofikiria…’nikamwambia.

‘Nilijua tu, ....huyu mtu anataka kumjaribu kila mtu, nahisi anataka kufanya jambo kubwa sana,… na kinachonishangaza ni kuwa hata polisi wanashindwa kumkamata huyu mtu, ana ulinzi gani huyu mtu, kiukweli yeye, ni… ni mjanja kupita maelezo, lakini …mimi naona hapo alipofikia kavuka mpaka, kuna haja ya kumuwahi kabla hajafika mbali...’akaniambia.

Hapo nikajua kweli nimelifikisha kwa mtu ambaye huenda naye katendwa, huenda alishaingizwa kwenye mitego ya huyo mtu, na jamani sio kwamba namteta vibaya marehemu, huyu mtu alikuwa mbaya sana, na kama angeliendelea kuwa hai, sijui tungelizunguza nini leo, alishafikia kubaya…’mzungumzaji akaendelea na maelezo yake.

‘Kwahiyo unasemaje, upo tayari kuifanya hiyo kazi, ...au?’ nikamuuliza

‘Umesema kuna kazi mbili, hiyo ni ya kwanza , hiyo kazi nyingine ya pili ni ipi, na unataka niifanyeje, na kwa hiyo ya kwanza, umesema unataka nimchunguze, kuwa kuna jambo kakufanyia, au anataka kukufanyia, au niwekezeje nguvu zangu kwa hiyo kazi …?’ akauliza na hapo nikajua kakubali hiyo kazi.

‘Kumchuza nyendo zake, na kujua ni nini kakifanya dhidi yangu, nahisi kuna kitu anakitaka kwangu, sasa wewe fuatilia ujue ni kitu gani,na kwanini anafanya hivyo, je ni kwa ajili yake au kuna mtu kamtuma, mengine utajua mwenyewe lakini nataka iwe siri…’nikasema

‘Toka lini kazi zako kwangu zikawa sio za siri, najua kabisa kila kazi ukinipa ni ya siri, au sio…’akasema

‘Hii ni ya siri zaidi…’nikasema

‘Upo wapi Dar, au Zanzibar, na lini utasafiri…?’ akaniuliza

‘Nipo Dar, natarajia kusafiri kwenda kusoma hivi karibuni, ila nitakuwa nikiwasiliana nawe, wewe ndiye utakuwa mawasiliano yangu, nilitaka nikuachie majukumu yangu lakini wewe haupo ofisini ulishaacha kazi, ila kwa kazi hii inabidi nikuachie…’nikasema

‘Ile safari yako…, imeshafika sio umeweza kuruka vihunzi,..sawa nenda kasome uje uanzishe kampuni yako, uachane na hizo kazi za kutumwa…huenda huko baadae , lakini sijui, nimechoka na hizi kazi, …naweza kuja kwako kuomba kazi,… lakini sio kwa sasa…’akasema

‘Usijali, wewe ni mtu wangu ninayekuamini sana, ni wewe tu kukimbilia kuacha kazi ngoja nimalize masomo, utarudi tu..’nikasema

‘Najua..hilo usiwe na shaka kabisa…nataka tu unielewe, siwezi kukuambia hili, kuacha hizi kazi nina maana yangu kubwa, kwahiyo unasema tutawasilianaje sasa…’akasema na kutulia

‘Unajua hii kazi inahitajia uharaka fulani, mimi nitakupatia namba ya kuwasiliana na mimi, ikifanikiwa haraka nitashukuru zaidi, na malipo yake kama kawaida yetu..’nikasema

‘Swala la malipo sio tija, wakati wote nikiwa na shida, ni wewe unanisaidia, hiyo nitaichukua kama kulipa fadhila tu…ila msimamo wangu ni ule ule, kwa hivi sasa sitaki ajira, sitaki kazi za mikataba, nitafanya kimia kimia, na tutamalizana hivyo hivyo…’akasema

‘Usijali, ni lazima nikulipe…’nikasema

‘Na hiyo kazi ya pili ni ipi…?’ akaniuliza

‘Huyo mume wa familia, mke wa bosi wangu, eeh, ana mpenzi wake wa zamani, kabla hajaoa, walikuwa naye huko kijijini, nakata unitafutie huyo mpenzi wake alikuwa ni nani,..’nikasema

‘Unasema nini, mmh, kwanini unataka kumuingilia bosi wako, kuna nini, ..?’ akauliza kama hajasikia vyema, na ilinipa mashaka huko kuitikia kwake, kama kushtuka, na maswali yake hayo

‘Unitafutie huyo mchumba wake alikuwa ni nani, ni muhimu sana kwangu kumfahamu, ilikuwa siri kubwa,, hakuna aliyelifahamu hilo, nimelifahamu lakini sijamfahamu huyo mchumba wake ni nani..’nikasema

‘Subiri kwanza kuna mtu ananisumbua hapa…’akasema na kukata simu, basi nikasubiria na baadae nikampigia simu, simu yake ikawa haipatikani. Nilimpa muda, kama masaa mawili nikampigia tena..

Alipokea na nikamuuliza kwanini alikata simu, akaniambia kuna mtu alifika, na hakutaka asikie anaongea nini na mimi, mimi nikamuelewa maana kiukweli kazi zangu mimi na yeye ni za siri kubwa.

‘Ni hivi, mimi nataka umtafute huyo mtu ni nani, na nimegundua jambo, kuwa mume wa familia, (hapo nilimtaja jina lake) ana ukaribu na Makabrasha, nataka kufahamu ni kwanini wapo na ukaribu hivyo, na pia, nahisi huyo mchumba wa huyu mume wa familia, anaweza akawa na ukaribu na huyo Makabrasha, nataka kufahamu ni kwanini, na je kuna kitu mume wa familia kafanyiwa, sasa sina uhakika kama ni Makabrasha au kuna mtu mwingine..’nikasema.

‘Sikiliza rafiki yangu, bosi wangu, mara nyingi mimi napokea kazi zako bila masharti, nikijua ni nini ninachokifanya, ila hii kazi, sio sitaki kuifanya, ila …inanipa ukakasi, huyu mtu anayeitwa Makabrasha sio mtu mwema, nilishamchunguza kabla, huyu mtu haaminiki , pili inaonekana ni kazi ndefu, maana hapo umeshamgusia hata mume wa familia, ni zaidi ya watu watatu hapo, natakiwa kuwachunguza, no, wanne...’akasema

‘Kwahiyo utazifanya hizo kazi mbili nilizokupa, au ndio unanikatalia hivyo..kwangu mimi ni muhimu sana, na wewe ndiye mtu wangu wa karibu wa kazi zangu za siri, na nilitaka chochote utakachogundua kiwe siri kati yangu mimi na wewe, unasikia..?’ nikamuuliza

‘Siwezi kukukatalia, lakini …mmh, kumchunguza huyu mtu, ni kunitaka mimi nihatarishe maisha yangu na familia yangu, nilishakorofishana naye na akanitegea, si unajua mambo yake,…’akasema

‘Mambo gani yake..?’ nikamuuliza

‘Huyu mtu anaendesha biashara za mlungula(blackmaili), na akitaka akupate kwa jambo fulani, atafanya kila hila ili akuingize kwenye biashara hiyo, na ..bila kukuficha alishanitega kwa hilo…’akasema

‘Mhh, ndio maana unaogopa..hujamalizana naye ?’ nikauliza

‘Sio kwamba naogopa, ila nakuelezea ni kwanini nasita kuifanya hiyo kazi..mtu kama huyo kumalizana naye sio rahisi, kila akikutaka atatumia vitisho, …si unajua biashara hiyo ilivyo,…ila nitapambana naye nione mwisho wake ni nini.’akasema

‘Sasa utaifanya hiyo kazi au hutaifanya…maana kumbe ulishaianza au sio?’ nikamuuliza

‘Bosi unajua , sitaki kufanya kazi hizo tena, nilishakuambia, lakini pia sipendi kukukatalia, na nikikutolea udhuru, ujue kuna sababu ya umuhimu...’akasema

‘Na mimi ukiona ninakupa kazi hiyo wewe peke yako ujue ina umhimu sana kwangu, tafadhali, ..huwa wakati wote natoa amri kwako, lakini hii ninakuomba, ni muhimu sana kwangu..’nikamwambia.

‘Mhh,.... ama kwa Makabrasha, hiyo kazi ninaweza nikaifanya,..kwa vile… lakini sio kwa hiyo kazi nyingine, ya kumchunguza huyo mchumba wa mtu, naona huko kuna safari, kuna mambo mengi, na sitaki kushikilia kazi zaidi ya hii, na hii ni kwa vile inanigusa na mimi..’akasema hivyo na kunifanya nishangae kidogo.

‘Kwahiyo kumbe kuna kitu kakufanyia,..ok, huwezi kuniambia ni kitu gani…au umeshaingia kwenye ajira yake nini…?’, nikamuuliza .

‘Hapana sina hisa naye kabisa, lakini sitaki kuchukua kazi mbili kwa sasa, nina majukumu mengi, na..nimekubali hiyo moja tu , kwa vile wewe ni rafiki yangu, na unanidai sana, fadhila zako kwangu ni nyingi sana…vinginevyo sina sababu nyingine ya msingi, ya kuikataa kazi hiyo ya pili, na zaidi ya kwanini, siwezi kukuambia, unielewe tu…’akasema.

‘Hizo kazi zote mbili kwangu ni muhimu sana, unajua mimi nakwenda masomoni, sitakuwa na muda wa kufuatilia, na wewe ndiye unyeweza kuzifanya kazi hizo kwa uamakini na kwa siri kubwa,..Nakuomba sana...’nikajaribu kumsisitizia, na yeye akasema;

‘Sitaweza kukufanyia kazi zote mbili hiyo moja sawa, maana Makabrsha namfahamu na nilishawahi kuifanya kazi inayomuhusu, lakini hiyo nyingine hapana, sitakuwa na muda huo, nielewe hivyo,...’akasema.

‘Kwahiyo hiyo kazi kumuhusu Makabrasha, utaifanya, lakini kwa kunisaidia kumtafuta huyo mtu mwingine, ndio umesema hutaiweza, unanipa mashaka ujue, je nikikuambia uiache hiyo ya makabrsha uifanye hiyo nyingine je…?’ nikamuuliza, na yeye akasema.

‘Hiyo ya makabrasha nitaifanya tu kwa vile nimeona huyo mtu na mimi namtafuta sana, nataka nimfahamu vyema, nije kulipiza kisasi kwake,,...japokuwa kwa ujumla sikutaka niifanye kazi zozote za namna hii tena, lakini kwa vile na wewe una muhitaji, basi ndio nikaona niichukue hiyo, ...’akasema.

‘Kwani kuna nini kikubwa huyo Makabrasha alikufanyia mpaka utake kulipiza kisasi kwake niambie ili nijue huenda ni yale yale..?’nikamuuliza.

‘Unaona, ....sitaki mtu kuniingilia hayo mambo yangu, kama unataka niifanye hiyo kazi, sitaki kuniuliza-uliza maswala kunihusu mimi binafsi, nitakuambia yale unayoyataka kuyafahamu kwenye kazi yako, ya kwangu niachie mimi mwenyewe, nina maana yangu na sitaki mambo yangu yaje kuwaumiza wengine...’akasema

‘Mhh, safari hii nakuona mwenzangu unaniacha njia panda, sijui kuna nini kinaendelea kwenye maisha yako, ujue mimi nipo tayari kukusaidia, tusaidiane ndio urafiki wa kweli ...’nikasema.

‘Kwa hili huwezi, hutaweza kunisaidia, haya ni maswala binafsi tu sipendi yakumguse mtu mwingine, sipendi…’akasema

‘Haya sawa nimekuelewa…’nikasema

‘Wewe nenda kasome, kwa kazi inayomuhusu huyu jamaa, anayejiita wakiliw a kujitegemea wa kimataifa, nitaifanya..ila nimjuavyo mimi huyu mtu ni mbaya, na hatari,kuliko unavyofikiria wewe, hata hivyo, siwezi kukuambia lolote mpaka nimalize uchunguzi wangu, na sikutaka niyaongee haya kwenye simu na kwa mtu yoyote, mpaka nimalize kazi yangu...’akasema

‘Ok, itakuwa vyema, kama ulishaianza…’nikasema

‘Saana, niamini kwa hilo, utapata taarifa nzuri tu…’akasema

‘Basi ukiwa tayari kuhusu huyo mtu tutaongea ili nijue tufanye nini, ni muhimu sana kwangu,..na nakuomba ulifanyie kazi hilo kwa haraka iwezekanavyo, na kwa huyo mtu mwingine nitajua ni nini cha kufanya, hata hivyo nina ombi moja kwako zaidi...’nikamwambia

‘Ombi gani hilo...’akaniuliza

‘Nina mikakati ya kazi kubwa baadae…, nina mipanglio mingi ya kimaisha, nikimaliza elimu yangu huku nataka tuwe wabia mimi na wewe.,.kwahiyo ninakuomba ujiandae kwa hilo, weka kumbukumbu za kazi zetu za zamani, kusanya ukweli wa kusaidia kwenye kazi zetu, tengeneza maktaba fulani yenye kumbukumbu za kesi na matukio, hasa za watu mashuhuri, nk..si unajua ninachotaka kukuambia..’nikasema .

‘Hilo halitawezekana..hujanielewa mimi sitaki tena hizi kazi,..nilikuambia ukija utaniajiri awali nilikuwa nasemea tu, nataka kubadilika, kuwa mtu mwingine kabisa, kama uhai bado upo, kiukweli kazi hizi sio nzuri, zinamuweka mtu mashakani muda wote, mimi sitaki kujishughulisha na haya mambo tena, kwa manufaa yangu ya baadae...’akasema.

‘Sawa nimekuelewa, lakini mimi nina imani kuwa tupo pamoja, hata kama kuna mambo yametokea ya kukwaza, bado tuna mafungamano ya kikazi, unafahamu kazi zetu hizi zilivyo, unaweza ukasema humuhitaji mtu, baadaye ikatokea jambo ukamuhitajia sana mtu wako wa zamani, usitupe mti na jongoo wake..’nikamwambia

‘Kwa maisha haya ninayopambana nayo, sizani kama kuna mashikamano na mtu kwenye kazi kama hizi, naomba tuishie hapo ,na ni vyema usitake kujua mengi zaidi kunihusu mimi, usiniulize tena , samani sana....’akasema akitaka kukata simu

‘Sawa kama unataka iwe hivyo…’ nikasema

‘Kiukweli nataka iwe hivyo..’akasema

***********v
Ndugu mwenyekiti ili uweze kuipata hii picha vyema, nawarejesha kidogo nyuma, nilishaliongelea hili kabla, awali, jinsi gani nilivyoweza kurejea nyumbani kwa dharura, lakini kuna mambo sikuweza kuyaongea awali, kwasababu za msingi.

Sasa hivi nitafichua yale yaliyojificha kwenye kurejea kwangu, ambayo sikuyaongea awali , hayo ninayoongea sasa yanafichua ukweli mwingine ambao utahitajika sana kama nilivyogusiwa, sitakiwi kuingilia maswalaya mauaji ya Makabrasha, nitajaribu kufanya hivyo.…’akasema.

‘Sawa endelea, lakini ni muhimu ukalichunga hilo, swala la mauaji halipo kwenye kikao chetu hiki, hilo swala lipo mikononi mwa polisi….’akasema mwenyekiti

Siku nilipokuwa masomoni, wakati najiandaa kufanya mtihani fulani muhimu, nilipokea ujumbe kama huu… ‘

‘Utahitajika ‘’Dar kwa haraka, kusaini mkataba wa hiari, dhidi yako na mzazi mwenzako, lakini bado ninamdai pesa nyingi sana, kama itatokea sitalipwa pesa zangu, sitakuwa na jingine bali kuwakilisha hizi picha kwa rafiki yako,…’’ ule ujumbe ukaambatishwa na picha, mojawapo ya picha mbaya, ambazo zilionyesha yale niliyokuwa nikifanya na mume wa familia, hiyo ikiashiria vitisho, kuwa nisipofanya hivyo, picha hiyo itafikishwa kwa walengwa.

Nilipopata huo ujumbe nikampigia simu huyu mtu wangu wa karibu, nikamwambia anifanyie uchunguzi, ni kitu gani kinachoendelea kati ya Mume wa familia na mke wa familia, na hapo mtu wangu huyo, akaniambia hilo ameshalifanyia kazi, na kusema;

‘Mume wa familia kaingia kwenye mtego na adui yetu,..’akasema

‘Una maana wakili Magumashi..’nikamwambia
‘Huyo huyo, …. kwahiyo inabidi afanye kila anachotakiwa kukifanya , na mengi ni kwa ajili ya masilahi ya huyo adui yetu, ikiwemo kukubali kuingia na adui yetu kwenye mkataba unaoidhinisha adui yetu kupata hisa kwenye makampuni ya bosi..’akaniambia.

‘Haiwezekani...ooh, mbona hilo ni gumu sana…unauhakika na hilo..?’nikasema kwa mshituko mkubwa.

‘Ndio hivyo, kuna mengi yamefanyika, na mshika usukani ni huyo adui yetu, inavyoonekana ni kuwa huyu adui yetu kaingilia mambo mengi, lakini nia na lengo lake ilikuwa kuingiza makucha yake kwenye mali za bosi wako…’akasema

‘Una uhakika na hilo…?’ nikauliza

‘Zaidi ya uhakika… na ukumbuke kuwa bosi wako na mume wake hawapo kwenye mahusiano mazuri, hawajui yote hayo yalipikwa na huyu adui yetu, ingawaje hadi sasa wana ndoa hao, wapo kwenye kutimiza wajibu wa kibinadamu, kutokana na huo wajibu, itawabidi waendelee kuwa wanandoa, vinginevyo, kitu kinachoitwa ndoa ni kama hakipo...’akasema.

‘Hali gani hiyo ya kibinadamu?’ nikamuuliza.

‘Mume wa familia kutokana na hiyo ajali, kuna matatizo mengi yanazidi kutokea, kuna dalili za maradhi ya kuota kwa vitendo, kuna kuchanganyikiwa, …unaona..na inaonekana hali aliyo nayo sio ya kupona leo, na mke kama mke hatakiwi kumtelekeza mumewe kwenye hali kama hiyo.., nahisi kama isingelikuwa huo ugonjwa sasa hivi tungeliongea mengine...’akasema.

‘Kuna nini kikubwa ulichokigundua, kilichosababisha hadi hiyo ndoa iingiwe na tatizo kubwa kiasi hicho, ni mambo yao ya ndani kwa ndani au kuna msukumo mwingine kutoka nje...?’ nikamuuliza.

‘Hayo unayafahamu sana wewe, sioni haja ya mimi kukuambia, japokuwa kuna mbinu zilizotoka nje, zilizojengwa kitaalamu sana na wajanja, ili ionekane hivyo ilivyo, kwa muda niliofanya uchunguzi wangu, nimegundua mengi, kumbe hata wewe upo kwenye mchakato huo, sikutegemea, kumbe unanipa kazi ambayo unaifahamu ...’akasema

‘Mimi kwa vipi..sielewi kitu ndio maana nikakupa hiyo kazi..niambie kwa vipi?’ nikamuuliza

‘Hahaha..usijali, ..japokuwa imeniuma sana, kuwa kumbe nafanya kazi kwa mtu ambaye ni mmoja wa watu wanaonichoma kisu moyoni mwangu...’akasema akiongea kwa sauti yenye huzuni.

‘Una maana gani, ‘mimi kukuchoma kisu..’ ?’ nikauliza

‘Usijali, utakuja kujua , lakini sio sasa…’akasema

‘Ni kwanini sasa hutaki kuniambia ukweli...nimekufanyia nini mimi kibaya , niambie ukweli, kama kuna jambo nimekukosea, ni bora uniambie, huenda kuna sababu ya msingi ya mimi kufanya hivyo, ila wewe hufahamu’ nikamuuliza na kujaribu kumuelezea, ili nifahamu ni jambo gani hilo, nililolifanya hadi mwenzangu afikie kuumia kiasi hicho.

‘Ukweli unaoufahamu wewe unatosha, na nakushauri ufanye kama wao walivyotaka, na watakavyotaka, kwa hivi sasa…hakikisha umefika huku nyumbani bila kukosa,…, ufanye kama watakavykuambia, baada ya hapo, mengine yatafuata, kwa hivi sasa wameshikilia mpini, ukikosea kidogo utakuja kujuta,..’akaniambia.

‘Ina maana hata wewe upo kwenye huo mchakato au umeligundua hilo kutokana na ule uchunguzi niliokuambia…?’ nikamuuliza

‘Hata siku moja siwezi kushirikiana na hao mashetani, hili ninalokushauri ni kutokana na uchunguzi wangu, nifanyavyo kazi zangu hutaweza kunielewa, lakini mwishi wa siku nitakupatia taarifa yako..’akasema

‘OK…’Nikasema hivyo, halafu akasema

‘Siku nikimaliza hii kazi, kila kitu kitakuwa hadharani, na nitahakikisha kuwa kama kuna kundi, kama kuna njama, basi zitafikia kikomo chake...kama ni kundi, nikitoka kwa huyu mtu, basi nitamuendea mwingine, mpaka nihakikishe nimemaliza kazi...’akaniambia

‘Unaposema kundi, au watu wengine ni akina nani, inaonyesha umeshawagundua hao watu au sio?’ nikamuuliza

‘Mhh, ,,kwa hivi sasa siwezi kukuambia kitu, nipe muda kidogo, cha muhimu ni kuhakikisha kuwa hili jambo nimeliweka sawa, nataka kuhakikisha kuwa hawa wananitesa moyo wangu, wanasambaratika, na hakuna kitu kama hicho tena, na kama ni njama, zinazofungamana na mwenza wangu, nitahakikisha nazifahamu, na kama yeye anahusika,…oh, hata yeye mwenyewe atajuta kufanya hivyo, ..’akasema

‘Mhh, sasa hapo unazidi kunichanganya, na huyo mwenza wako ndio nani tena, ndio huyo mume wako ?’ nikamuuliza

‘Usinidadisi sana kuhusu hilo, ila yeye ndiye moyo wangu, unasikia, ni, ni....’ simu ikakatika, na ilikatika kama vile mtu kapatwa na tatizo, ikanibidi nipige simu, kwa mtu wangu mwingine, yeye ni msaidizi wake, katika mambo yetu ya utendaji, nikamhoji,

‘Unamuulizia bosi, mbona alishaacha zile kazi zetu…’akasema

‘Yupo salama ..ebu mfuatilie hata kwa simu tuone kama yupo salama..’nikasema na ikachukua muda, halafu akawa hewani na kusema

‘Yupo salama bosi..’akasema

‘Je kwa hivi sasa anafanya kazi gani..?’ nikamuuliza

‘Hajulikani sana bosi, nahisi yupo nyumbani…’akasema

‘Kwahiyo hana kazi yoyote yupo nyumbani tu, au ana kazi gani maalumu anaifanya kwa sasa y akumuingizia kipato..?’ nikamuuliza

‘Si kwamba yupo nyumbani, si unajua alivyo, anaweza kuacha kazi hii, kumbe ana kazi nyingine, kuna sehemu anafanya kwa muda,…anakwenda huko mara chache chache, ila mara nyingi anaonekana yupo peke yake, yaonekana kuna jambo linamtatiza, anakuwa kama kachanganyikiwa hivi..’akasema.

‘Kwa mtu gani huyo anapoonekana akifanya kazi ...unamfahamu huyo bosi wake mpya?’ nikamuuliza

‘Ndio namfahamu huyo bosi wake, japokuwa awali alifanya ni siri, lakini nilimfuatili mpaka nikaja kugundua wapi anapofanyia hiyo kazi, japokuwa sio kwa siku zote,...’akasema

‘Au labda anafanya kazi hapo kwa ajili ya kupata taarifa, ..?’ nikamuuliza

‘Mhh, sizani,…hapo sina uhakika bosi …’akasema

‘Ni kwa nani hapo anapofanyia kazi, nipe taarifa kamili, sio unanipa taarifa kama unaogopa, ni kwa mtu gani anapofanya kazi kwa sasa?’ nikamuuliza kwa hasira

‘Ni kwa Makabrasha bosi, ...mara nyingi anaonekana ofisini za siri za kwa Makabrasha, inaonekana kaajiriwa na Makabrasha, au kuna kazi maalumu anaifanya kama ulivyosema, sina uhakika na hilo...’akasema na hapo hapo nikakata simu.

Sikupoteza muda nikapanda ndege na kuja Dar,ndivyo ilivyokuwa kuja kwangu Dar, kwa ghafla .... na sasa safari yangu hiyo iligundua nini, na ukumbuke ndicho kipindi Makabrasha aliuwawa, ukumbuke ndipo kipindi mume wa familia anaumwa…kuna mambo mengi hapo yamejificha…akatulia pale alipoona mwenyekiti akiongea na simu

‘Niendelee mwenyekiti…’akauliza



WAZO LA LEO: Mambo yanayohusu imani za watu , hisia za watu, upendo wa watu…, mambo hao ni nyeti sana, ni vyema, ukikutana na vitu kama hivi uwe makini sana kuviingilia. Mtu akiamini, akapenda, huona vingine vyote havina maana, anaweza hata akafumbia macho elimu yake, na akafanya mambo ambayo kwa elimu yake, hastahili kuyafanya hayo. Ndio maana wanasema, mwenye kupenda haoni, hata akiona kibaya kwake, ni kizuri, akiona chongo ataita ni kengeza.
 
SEHEMU YA 107


Niliyoyakuta Dar, yalinikatisha tamaa, kwani sikutegemea kuwa kuna watu wamefikia kiwango hicho cha uhalifu wa kimataifa, maana hayo yaliyofanyika sio uhalifu wa kitoto, na hao watu waliofanya hivyo, wamefanya kwa kujiamini,hawakujali kabisa kuwa kuna usalama, kuna polisi,… sikuamini..

Kama nilivyoambiwa nisigusie huko, lakini nataka muone jinsi gani tukio nzima lilivyotokea, hadi mimi nakaamua kukubali kuingia kwenye makubaliano ambayo baadae nimekuja kulaumiwa na kuonekana kuwa mimi ni miongoni mwao, huenda sitaweza kuthibitisha kwa mia kwa mia, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa, mkiniamini sawa msiponiamini, mimi nimetimiza wajibu wangu…’akasema na kutulia.

Mwenyekiti alikuwa katulia hakusema neno, nahisi mzungumzaji alitarajia mwenyekiti atasema neno…

Niwaambie ukweli baada ya uchunguzi wangu niligundua jambo, huenda halijagundulikana hilo, huenda limeshagundulikana lakini nia na amdhumuni kwa sasa ni kuwajibishana, lakini kuna mambo ambayo hamjayaweka kwenye mtizamo wa kihekima…samaahni kwa kusema hivyo.

Hamjui kuwa, malengo na mbinu za hili, kwanza ilikuwa ni kuondoa nguvu za ulinzi, akili na mawazo ya kikazo yaondolewe kisaikolojia, kuharibu ulinzi na usalama wa familia, hilo hakuna aliyelifahamu, sijui naeleweka hapa, na…na pili kuondoa, mshikamano…familia iyumbe, ikose udhibiti, ni nani kiongozi na ni nani wa kutiiwa, hilo lina umuhimu wake.

Lakini la tatu ambalo ndilo huja kuharibu kabisa, ni kujenga chuki…ukiliangalia hili utaona mfano wake, ni nini kilifanyika kwenye familia iliyolengwa,…na je hili halikufanikiwa, chuki ziliandaliwa kitalamu, kukajengwa matabaka mawili ya mume upande wake na mke upande wake..je hili halikufanyika…?’ akawa kama anauliza

Ilihakikishwa kwua hilo lawezekana, chuki ikasambazwa, kwa marafiki, makundi, ..kundi mume n akundi mke, ushabiki ukajengwa, watu hawalioni hili ubaya, wake, ushabiki wenye mlengo wa chuki ni mbaya sana,…haujengi, familia ikawa sasa kila mtu na lake,…sijui naongea na watu wanaolewa, au ndio bado makundi hayo yapo hapa.

Mzee mimi nayaongea haya kwa nia njema, sina nia ya kuwagawa hawa watu sina nia ya kuingilia hii familia na sina nia mbaya ya kuchukua chochote kwenye hii familia, mimi ni mtu wa kuja tu, wenye familia wapo, wenye mali wapo, kwanini mimi nije kujiingiza humo,…sina fani yangu, na sio lengo langu, lengo langu ni kujitegemea, kufanya kazi yangu kwa malengo mema.

Tuyaache hayo, nahisi mtaniona najitetea kwa vile nimeharibu, ni kweli najuta sana kwa hiki lichotokea imeniuma sana,…lakini yameshatokea nitafanya nini…’akaweka mikono kama anamuomba mungu wake.

‘Namuomba mungu sana anisaidie kwa hili….’akatulia kwa muda

‘Ndugu mwenyekiti, …haya yalipangwa kitaalamu sana, na kila tukio lilikuja kutokea baadae lilichukuliwa kwa uzito wake, maana kashfa inaweza kuwa ni ndogo tu, lakini jinsi itakavyokuzwa na vyombo vya habari, midomo ya watu, inaweza ikawa kubwa kuliko kashfa yenyewe, ni kweli si kweli..hili lilipangwa na maadui wa mzee, na kinara wa kulifanikisha hilo mnafahamu wenyewe…’akageuka kushoto na kulia.

Sasa oneni hili, siku nilipofika uwanja wa ndege kulitokea nini..na onenani ujanja wa mwenzetu, ulivyo, yupo mbali kabisa na hili, na huwezi kabisa kumdhania, yeye anachofanya ni kutia mafuta kwenye ule moto ulioanza kuwaka..kidogo kidogo…

Nasimulia hili nitajitahidi kutokuingilia kazi ya polisi…

*******a

Nilielezea kidogo yaliyotokea awali kwa ufupi, lakini sivyo ilivyokuwa kwa undani wake, mimi nilitekwa nyara mapema tu, na nilikuwa ndani ya mikono ya hao watu kwa siku mbili, hakuna anayelifahamu hilo…’akatulia

Nilipotoka uwanja wa ndege kaam nilivyosema awali mtoto wangu nilimkabidhi mtu, nikijua huku huenda kukawa na jambo, na sikutaka kabisa mtoto wangu aguswe, nilikuwa tayari kupigana hadi kufa, kama mtu atamgusa mtoto wangu.

Nilijiamini kuwa mtoto wangu atakwua salama, nikatangulia kutoka, na mtu niliyemuachia mtoto wangu alibakia nyuma, japokuwa hata nilipotoka macho yangu kwa siri yalikuwa yakihakikisha kuwa mtoto wangu kaondoka uwanjani pale salama, nikabakia mim, na yaliyonikuta

Baada ya ukaguzi wa mizigo yangu, sikuwa na mizigo mkubwa, ni kiasi cha nguo za mtoto na zawadi kidogo, sasa wakati natoka, nje, ..uon ilivypopangwa kumbe …hahaha maana huyu mtu aliyekuwa nyuma yangu sikuwa na ..yaani hapo ndio nasema hawa watu sio wa kawaida, huyu mtu sikuwahi kumuona kwenye ndege,..

Ukitoka pale uwanja wa ndege,unatembea kutoka, huku wapo watu wanasubiria jamaa zao, wamejipanga, mstari, nyie mnapita ile sehemu ya kutembea, huyu mtu alitokea wapi hadi kuwa nyuma yangu na mimi kwenye ndege sikuweza kuiona sura hiyo.

Sasa namaliza ile sehemu ya kutembea nataka kufika ile sehemu ya watu walijipanga mtu nyuma yangu ndio akanigusa na kitu kikali, ina maana huyu mtu alikwua nyuma yangu wakati wote, haiwezekani akatokea miongoni mwa watu na kuja kuniwahi kwa nyuma ..hapana…sijui naeleweka hapa…’akasema

Ilikuwa ni kisu kikali maana nilihis maumivi yake, sauti ikasema;

‘Fuata tutakavyokuelekeza, kuna taksi ile pale mbele yako, mlango wake upo wazi, ingia, na mizigo yako tutakuchukulia, hatutaki kukuumiza...’akaniambia, na baadaye akanipa bahasha, akaniambia

‘Fungua hiyo bahasha...’kwa mikono ya kutetemeka, nikaifungua,..nilitetemesha ile mikono kwa makusudi, kumteka huyo mtu akili , ili ahisi kuwa mimi nimeogopa, ni ujanja mdogo tu…nikafungua ile bahasha, na kwa mbali nikaona yule mtu aliyekuwa an mtoto wangu akitoka, akawa anaendea gari, sikuona dalili ya watu kuwa nyuma yake

Na kuwa muda huo ndio nimefungua ile bahasha na kuona zile picha mbaya, le nilizozoea kutumiwa, na huyo mtu akaniambia

‘Siku hizi hapa bongo kuna magazeti mengi yanazitafuta picha kama hizo, hatutaki kukuharibia jina lako, na kukuharibia maisha yako ya baadaye, na kumpoteza mtoto wako, yote hayo yanawezekana, au sio…ila sisi tunataka kulijenga jina lako uwe karibu na wenye pesa, wewe unafaa kuwa kiongozi mwema, tunataka kulifanikisha hilo…tunaweza…’nikaambiwa

‘Sasa ili uwe salama, ili mtoto wako awe salama, timiza masharti yetu madogo tu, tutakuwa sambamba na wewe...’wakasema na mimi sikutaka kubishana nao, nikaingia kwenye gari, na gari likaondoka, sasa linatoka, na wakati huo niliona gari lililombeba yule mtu na mtoto wangu wakiondoka..

Kwa pale sikuona dalili kuwa na wao wametekwa, na hata wakati tunatoka, wao walielekea njia ya kawaida ambayo nafahamu wanapokwenda, ila sisi tukageuka upande wa kuelekea Pugu…unaona, na gari halikutembea mwendo mrafu tukawa tumeshafika ahpo walipotaka kunipeleka mimi.

‘Tumefika mpendwa, tunachokuomba ni wewe kuwa mstaarabu, hatutaki wewe uonane na mtu mwingine yoyote bila idhini yetu, kwahiyo tutakupeleka mahali maalumu utakaa hapo, hadi lengo letu likamilike, mambo mengine utakuja kuendelea nayo baadae..’wakasema

‘Ama hilo tataizo la kibali chako cha kwenda kusoma, usiwe na wasiwasi nalo, limeshashughulikiwa, utapata muda mdogo tu wa kuweka sahihi yako pamoja na mambo mengine,…utuelewe, sisi hatuna nia mbaya na wewe, ...’akasema huyo mzungumzaji

Mimi sikuongea kitu adi hapo, sikutaka kwanza kuongea chochote,…na wakati huo tulikuwa tunaingia kwenye jengo moja, ni jengo kwa nje linaonekana kama halijakamilika , lakini kwa ndani limeshakamlika, sijui kwanini walifanya hivyo.

Tuliingia ndani kama watu wa kawaida, na jamaa yule akaenda kuongea na mlinzi, na mlinzi akatuelekeza wapi pa kwenda, kumbe pale kuna njia mbili ya kwenda juu na nyingine ya kwenda chini…kuna jengo la chini ya ardhi, humo humo lakini huwezi kuligudnua hilo .

Unajua mimi kule ilipangwa niondoke baada ya siku mbili hivi, lakini kwa haraka nikaamua kuondoka mapema, hawa watu walifahamu vipi, na mawazo hayo yalinijia usiku na usiku huo nikawasiliana na watu w ndege, na kukubaliwa kuwa nafasi ipo naweza kubadili tarehe,..yawezekana ndio, kama wana watu wao, lakini sio kwa haraka kihivyo.

Kwahiyo hapa Dar nilifika siku mbili kabla ya ile tarehe iliyojulikana kuwa nitafika, ila hadi leo watu wanafahamu nimefika siku ile ile ya tarehe iliyokuwa imepangwa, hadi leo hakuna anayelifahamu hilo…’akasema

Tuliteremka ngazi chache hadi chini..na kufika kwenye ghorofa ya chini ya ardhi,…tukatembea na kuingie kwenye chumba chenye kila kitu, ...ni chumba cha kifahari, nikaambiwa hapo nitakaa mimi hadi nitakapopewa maagizo mengine...’msemaji akasema na kuondoka zake.

Kitu cha kwanza nilitaka kujua ni nani yupo nyuma ya haya yote, sikujua ni nani kwa muda ule,.japokuwa kwa mtizamo wa haraka, toka awali, nilijua kuwa anayefanya haya yote huenda akawa ni Makabrasha, kutokana na maaelezo ya watendaji wangu.

Nilipoingizwa mle na kuona hicho chumba nikawa na mashaka, huenda sio makabrasha au kama ni yeye, basi kuna mtu anamtumiwa huyo Makabrasha, …maana hicho chumba ni cha kifahari, kuna gharama kubwa imetumika kukiweka vile.

Kwanza ikabidi nijimwagie maji kidogo, na kutuliza akili, ...nikatulia na ukumbuke mtoto wangu alikuwa mikononi mwa mtu niliyemuamini, na huyo mtu alinihakikishia kuwa atamfikisha mtoto wangu kwa jamaa yangu mmoja, lakin je alimfikisha, ndio nilikuwa nawaza jinsi gani nitawasiliana naye kulihakiki hilo..

Simu yangu hawakuichukua, nikasema basi ngoja nipige simu kwa mtu mwingine yoyote kwanza nione kitakachotokea, kiukweli hakukuwa na mawasiliano ya simu, mawasiliano ukiwa humo ndani hayafanyi kazi, wamezuia namna yoyote ya kuwasiliana, kuna simu ya mezani…nikaiendea na nilipoinua tu, ujumbe ukasema

‘Kuna tatizo tunaweza kukusaidia…/’ nikaulizwa

‘Nataka kupiga simu nje…’nikasema

‘Unaweza kunitajia namba ya mtu unayempigia nikusaidia tafadhali..?’ nikaulizwa na mimi nikakata simu.

Wasiwasi wangu kwa mtoto ukawa sasa umethilika, je ni kweli kafikishwa hiyo sehemu salama, nikawa sina amani…nikaona ni lazima nifanye jambo, ni lazima niweze kujua kama mtoto wangu yupo salama au la…

Ilipofika muda fulani, nikasikia mlango ukifunguliwa, na akaingia dada mmoja akiwa kabeba vifaa ni vyakula na vifaa vingine vya kuongeza kwenye jokofu.., alikuwa kafunga uso wote, haonekani sura, kaacha sehemu ya macho tu, inaonekana ni muhudumu, aliwekea vyakula, hakuniangalia, alifanya hiyo kazi, na alipomaliza, akanijia, na kuniuliza

‘Una shida yoyote?’ akaniuliza

‘Ndio , nataka kutoka nje...’nikasema

‘Mhh, fuata maagizo , kama ulivyoambiwa, ..’akasema na kuondoa vyombo, akaacha kijiko, lakini ni kijiko cha plastiki, ni kama kakisahau,…mimi sikuwa na mawazo yoyote nacho, akatembea hadi mlangoni , na kabla hajafungua mlango akasema;

‘Ukweli wewe unaoufahamu, nakushauri ufanye kama wao walivyotaka, na watakavyotaka…’akasema na kuondoka. Kwa mpelelezi ujumbe huo ulinitosha kujua ni nini kinachoendelea humo, lakini kwa muda huo, akili yangu haikuwepo, akili yangu ilikuwa kwa mtoto wangu,..mama na mtoto wake sio kitu cha kubahatisha.

Nikawa nimetulia, kwanza niliangalia zile kamera juu, nikawa nawaza jinsi gani ya kuharibu mawasiliano yao, ili wasijua kinachoendelea humo ndani, …na mara macho yangu yakigundua kitu kwenye kile kijiko cha plastiki, sikukichukua kwa haraka maana yoyote anayenichunguza juu, ataligundua hilo, nikavua koto langu na kulirusha mezani kama najisikia joto, nikajinyosha, nikatembea hatu kadhaa za mtu anayawaza.

Nikajivunga vunga na kujinyosha, halafu nikaliendea lile koti, kwa haraka nikalizoa, na kuhakikisha kuwa kile kijiko kipo mikononi mwangu

Nilienda chooni, na baada ya kuhakikisha kuwa hakuna kamera, nikachukua kile kijiko, kama nilivyohisi ilikuwa sio kijiko tu, bali kulikuwa na zaidi ay hicho kijiko…

Kulikuwa na karatasi nyepesi imekunywa vyema na kunatishwa kwenye kile kijiko, na nilipokitoa kile kikaratasi nikaona maandishi;

‘Tupo pamoja..’ nikakigeuza nyumba nikaona namba ya simu, nikaikariri halafu nikakitafuna kile kikaratasi.

Nikarudi kule ndani, …kuna hali isiyo ya kawaida nilihis hali ya hewa ni nzito, mwili ukanisihia nguvu, na kabla sijadondoka nikajirushia kitandani, ..na hapo hapo nikazama kwenye usingizi mnzito

Nilianza kuhisi hali ..nahisi nililala sana, lakini hadi hapo sikuweza hata kujiunua,ila nilihisi sipo peke yangu. Nikajipa moyo, kuwa nipo salama, ni baada ya akili kutulia.

Nililala kwa muda wa nusu saa hivi, baadae sasa hali ikajidhihirisha kuwa kweli kuna mtu mwingine humo ndani, hapo kitandani, lakini hadi hapo, mwili wangu ulikuwa hauna nguvu hata kuinua mkono siwezi,…oh, wamenifanyia nini hawa watu

Hali hiyo ikanikumbusha siku ile nilipobakwa na ..na..mume wa familia…’akatulia kuongea na kumuangalia mume wa familia.

‘Lakini hii ilikuwa zaidi, maana hata kuwaza kitu, inakuwa vigumu, akili ni kama imefungwa hivi…’akaendelea kusimulia.

Kwa muda huo cumba kilikwua ni giza, na ni giza nene, …sijui taa ilizimwa saa ngapi,.nio nikaanza kukumbuka, nikakumbuka wakati nataka kujipumzisha chumba kilikuwa na mwanga, nikajisikia hewa ni nzito, ..na nikajirusha kitandani, nikazama kwenye usingizi mnene, nikakumbuka yoet hayo

Kwa vile mwili ulikuwa bado hauna nguvu, sikuweza kuinuka, nikawa nasubiria litakalokuja kutokea, nikasubiri, mara nikahisi kitanda kikitikisika, kuwa huyo aliyekuwa karibu yangu, akajiandaa kufanya jambo, au kama alifanya jambo anataka kuondoka,

Hapo nikawa najaribu kuvuta hisia za nguvu, nguvu ziweze kunirejea, japokuwa siwezi kuinua hata mkono, au kukunja kidole, mwili umelegea, nikahisi mkono ukinipapasa sehemu ya tumboni, nikatulia nione lengo la huyo mtu,..

Aliposogeza mkono chini zaidi, ule mkono ukasita, na mara nikaona kitu kikiletwa mdomoni, ni kijiko, kina kitu kama dawa au maji, yakawekwa mdomoni mwangu yakapenya, nikameza..nilihis mwili saa ukisimuka,. Na mara ule mkono ukawa unashika tena tumbo langu, ukielekea chini zaidi.

Nilihisi sasa nguvu zimenirejea, hasira, zikanipanda, nilisubiri, kabla mkono haujaenda mbali zaidi kwa haraka nikashusha mkono wangu ukaudaka mkono huo ulioshiaka tumbo langu, nikajirusha,..ni mbinu zetu za mapigano, nilichoskia baadae ni kilio cha maumivu, na jamaa alikuwa sakafuni akilalamika maumivu.

‘Aaah, umeniumiza mkono, ooh,, ...nini unafanya wewe, sikuwa na nia mbaya, nilikuwa nakusisimua ili damu ifanye kazi, aaah, watu wengine bwana...’sauti ikaniuliza,. Ujue humo ndani kukizimwa taa ni giza kweli,

‘Kwani wewe nani na lengo lako ni nini?’ nikamuuliza

‘Usijali sikuja hapa kwa nia mbaya, kwanza sina muda wa kufanya lolote na wewe, nimeshachoka, nilikuja kukusalimia tu, nikawa napendezewa kushika mwili wako uliojengeka kimazoezi, una mwili mzuri sana, na nilitaka kukusisimua, ili uondake na hiyo hali...’akasema

‘Wewe ni nani,…nijibu kwanza?’ nikamuuliza

‘Wala usijisumbue kutaka kufahamu mimi ni nani mimi ninachokuomba ni wewe upumzike tu, usiwe na wasiwasi upo salama...’akasema.

‘Nipo salama, wakati mumeniteka nyara, na kupulizia madawa ya kupoteza fahamu…’nikasema na kwa haraka nikawa naelekea sehemu ya kuwasha taa.

‘Wala usisumbuke kuwasha, nimekuja kukusalimia, tu, kesho asubuhi nina kikao na wewe, ajenda ni moja, kukubaliana na hayo tuliyoyapanga, wewe utatusaidia kutupa taarifa chache, na huenda tukakutuma mahali, ukimaliza kazi yetu, utaenda kuendelea na madhumuni ya kuja huku kwa dharura, unasikia sasa hii ni amri, vinginevyo....’akasema.

‘Hujanijibu swali langu, wewe ni nani…?’ nikamuuliza

‘Utanifahamu labda hiyo kesho, samahani kwa usumbufu, nashukuru kwa kuwa mvumilivu, ukifanya hivyo, na kufuata masharti yetu, ukatii yote tunayohitajia, hutapata taabu, na haya tunayafanya kwa ajili yako, na familia yako,...mwenyewe utaona, kwa hivi sasa lala,..usijali..’akasema na kuondoka, sikutaka kujishughulisha zaidi, nikarudi, na kulala huku bado nikimuwazia mtoto wangu.

‘Mtoto wangu yupo wapi…’nikawa naweweseka, maana nilihis kuzama tena kwenye usingizi mnzito

Nakatiza kidogo, tutaendelea na sehemu hii, muhimu ambayo inatupeleka kwenye mshukiwa wa mauaji

WAZO LA LEO: Maisha ya mtu yana thamani kubwa sana, na ni lazima kila mtu atafikia umauti, lakini tujitahidi sana tusiwe sisi ni sababu ya uamauti wa mwingine , dhambi yake ni kubwa sana, ni kama umeua dunia nzima…je ni nani anaweza kubeba dhambi za dunia nzima…Tuwape pole wale wote waliofikiwa na misiba, maana msiba uusikie tu kwa wengine, msiba unauma, hasa akiwa ni ndugu yako wa karibu. Ila mwisho wa yote tusema tu, yote ni mapenzi ya mungu, na mwenyezimungu anajua vipi atalilipizia hilo.
 
SEHEMU YA 108

'Aaah, umeniumiza, ...nini unafanya wewe...’sauti ikaniuliza,. Ujue humo ndani kukizimwa taa ni giza kweli,

‘Kwani wewe nani na lengo lako ni nini?’ nikamuuliza

‘Wala usisumbuke kuwasha, nimekuja kukusalimia, tu, kesho asubuhi nina kikao na wewe, ajenda ni moja, kukubaliana na hayo tuliyoyapanga,…’akasema

Tuendelee na kisa chetu..

**********
'Kikao na wewe, kama nani kwangu...?' nikauliza kwa hasira

‘Utanifahamu tu, ila kifupi mimi ni mjumbe tu , mjumbe hauwawi...au sio...'akasema

'Nyie ndio mbwa wa hao mabwana zenu...'nikasema

'Vyovyote iwavyo...muhimu ni wewe kutii amri, unasikia, hutajutia kwa hilo, ukikubaliana na kila kitu, wewe utakuwa bosi wetu, hilo lipo kwenye ajenda, sikufichi hilo, kwahiyo hapa nakuelekeza ila baadae nitakwua nikitii amri kutoka kwako, huoni jinsi watu hawa wanavyokupenda.

'Wananipenda au ni tamaa zenu.

'Sio tamaa madamu, haya ni kwa manufaa yako..kiukweli baada ya hapa, wewe utabadilika kabisa, kutoka kwenye kuita wengine mabosi, na wewe kuitwa bosi, tena muheshimiwa, unafaaa sana,..hilo ujiandae nalo, wewe utakuwa mtu mashuhuri na tajiri,..'akasema

'Mimi ni mjumbe tu , lakini hayo yameshawekwa wazi, unaandaliwa kuwa kiongozi , sifa unazo, na muhimu ni wewe tu ukubaliane na hayo utakayotakiwa uyafanye, mengine kwa hivi sasa ni kwa manufaa yako, kukuhakikishia kuwa wewe na familia yako mpo salama, kiufupi huyu mtoto alikuwa anawindwa na watu wengi, wewe hujui tu.

'Nahisi hata wewe uliliona hilo ndio maana ukamuacha nyuma, lakini sisi tulijiandaa kabla ya hapo, kuwa mtoto hatapata madhara, atalindwa kwa nguvu zote, na hadi unaondoka hapa mtoto atakuwa salama, lakini sis tumeona atakuwa salama akiwa nasi, sio akiwa na wewe,...zaidi ni masilahi yako na mtoto huko mbeleni....’akasema.

‘Hujanijibu swali langu, wewe ni nani…?’ nikamuuliza

‘Utanifahamu kesho, samahani kwa usumbufu, nashukuru kwa kuwa mvumilivu, ukifanya hivyo, na kufuata masharti yetu, ukatii yote na kuyafanya yote tunayoyahitajia, hutapata taabu, wewe na mtoto mtakuwa salama hadi hapo ukirudi huko masomoni, na tutazidisha elimu yako ikibidi...'akasema

'Sina haja..'nikasema

'Haja unayo, sema hujafahamu nia njema yetu...na hujafahamu kuwa haya tunayafanya kwa ajili yako, na familia yako, hebu jiulize hao waliojifanya wanakupeleka kusoma kweli wana nia njema na wewe, utakuja kuona siku ukimaliza masomo yako , kama kweli wanakujali, hapo walipo wanatafuta njia ya kukumaliza, sis ndio wenye nia njema na wewe,...mwenyewe utakuja kutushukuru kwa hilo . ..’akasema

‘Nimeshakuambia sina haja na msaada wenu, …’nikasema

‘Kwa hivi huwezi kuliona hilo, subiria mdua utafika utaliona hilo, sasa lala kwa amani, usingizi mororo....usijali..’akasema na kuondoka...

Ndugu mwenyekiti kauli yao hii, kama ningelikuwa nataka kuwaamini wao, ningeliwaamini, nilikuwa najiuliza ni nani walifanya namna mpaka nikaja kuokolewa na hao watukutu waliotaka kuniharibu ....ni hawa walilijua hilo kabla, na ..huko tupaache kwanza au sio...

**********

Kiukweli baada ya huyo jamaa kuondoka, bado mwili wangu ulikuwa haujawa sawa, mwili ulikuwa hauna nguvu, viungo vilikuwa kama sio vyangu, nahisi huyu jamaa alipulizia tena ayo madawa yao ya kunivunja nguvu,ili nilale u nisiweze kufanya lolote, kwani kweli pale nilipojilaza kitandani tu, usingizi mnzito ulinichukua, hadi pale nilipozindukana, ..

Ilikuwa ni asubuhi...

Nilipofungua macho, niliona mwanga wa kawaida hakuna giza tena, nikajaribu kukumbuka matukio ya usiku wake, nilijua kabisa hao watu walikuwa wamenipulizia hayo madawa yao ili nilale, walinijua kama wangeliniacha huru, ningelifanya jambo, hata hivyo pale nilipozindukana tu akili yangu ilikuwa kwa mtoto wangu.

'Mtoto wangu yupo wapi, je ni kweli yupo salama...' ilikuwa hali hiyo, na ilinifanya nisiwe na amani.

Kwa haraka nikatoka na kuingia bafuni baada ya mazoezi kidogo nikijua sasa nipo vitani,..nikaoga kwa haraka na kurudi pale chumbani, kwa umakini nikagundua kuwa kuna mtu aliingia wakati nipo bafuni, kuna mabadiliko, kuna vitu vimeondolewa, hali ya hewa haikuwa nzito tena, hali ya hewa ilikuwa shwari, utahisi kama upo ufukwenu mwa bahari, upepo mwanana, na humo ndani hakuna dalili ya kipozoe hewa!

Kwa vyovyote vile kuna mtu aliingia humo nikiwa bafuni, akafanya jambo kwa haraka sana, sikujali hilo, mimi nikavaa nguo zangu kwa haraka na kuanza kutoka, kuelekea ile sehemu ya maongezi, nisubirie kitakachofuata. Huku akili yangu ikiulize 'mtoto wangu yupo wapi, na je kweli yupo salama...

Kabla sijashika mlango wa chumbani ili kutokea sehemu hiyo ya chumba cha mapumziko, mara nikasikia sauti ikisema;

‘Habari za asubuhi mpendwa, tunatumai umelala salama, japokuwa haupo na amani , na tunajua hilo ni kutokana na kutokuweza kuwasiliana na mtu wako uliyempa mtoto ukiwa ndani ya ndege, usijali kuhusu hilo, mtu uliyempa mtoto wako, anafahamu kabisa wewe ndiye uliyemuhitajia mtoto wako, na mtoto wako akaletwa hapa kwetu sehemu salama zaidi..’akasema

‘Ssshit…’nikasema

‘Kwahiyo kuhusu mtoto wako, unakuhakikishia kuwa mtoto wako yupo salama, atapata kila kitu anachohitajia apate, tunafahamu huduma zake zote..., cha muhimu ni wewe kufuata masharti yetu, vinginevyo, mtoto wako unaweza usimuone tena katika maisha yako yote na hilo tunaweza,...’sauti ikasema

Nilikuwa nimeganda pale mlangoni nikisikiliza hiyo sauti, sikuona sehemu inapotokea ni kama sauti hiyo ilitokea kila sehemu ya hicho chumba.

‘Ina maana hawa watu walifanya mbinu wakamchukua mtoto wangu, mmh sitawasameeh kwa hili na anayehusika, siku nikipata muda, nita-m-maliza huyo mtu kwa bastola,..’ nikajisema moyoni, na kweli nilidhamiria kufanya hivyo.

Nilitaka mtu kama huyo asiwepo tena hapa duniani, na kusumbua watu, japokuwa nitakwua nimechukua sheria mikononi mwangu.

‘Huyu atakuwa ni Makabrasha tu…hakuna mwingine siku nikikutana naye siampa muda wa kujitetea hafai kuishi huyu mtu...’nikajisema hivyo.

Baadae nikatuliza kichwa, nikahisi kama ..yaani, naanza kuona jinsi wanadamu tulivyo, kuwa hatuna maana, pindi tu nilikuwa na mtoto wangu, sasa hivi hayupo, sasa hapo yupo hai, na sina uwezo wa kumuona..je...yaani niliwazia mbali sana...

Kiukweli hapo ilibidi nimkurubie mwenyezimungu...nilimuomba sana,.... mtoto wangu awe salama, hata ikibid mimi nife lakini mtoto wangu awe salama...kiukweli mimi sio mtu wa dini sana, lakini kwa muda ule, dini ikanijaa moyoni. Nikatambua bila mola wetu, bila rehema za mola wetu, hatuwezi...hebu angalia tukio lilivyokuwa, wewe kama wangelitaka waneglifanya lolote, ningefanya nini pale...

Nikafika ile sehemu ya maongezi, ...na nikakuta kila kitu kipo tayari mezani kifungua kinywa cha kila namna, kuonyesha kuwa wanajiweza…. , lakini kiukweli sikuwa na amani, nilikula kidogo tu, nikasogea kwenye magazeti nikawa nasoma kupoteza muda..

Mara mlango ukafunguliwa, ….aliingia mdada, huyu sio kama yule wa kwanza, kwa wajihi, japokuwa na yeye alijifunika usoni, watu wote hawa hawajionyeshi sura zao, kuanzia wanaume hadi wanawake,...yeye akachukua vifaa, halafu akasema;

‘Tuongozane tafadhali…’akasema na mimi nikawa namfuata nyuma,..

'Tunakwenda wapi...?' nikamuuliza

'Wewe nifuat tu, usiwe na wasiwasi...'akasema huku tunatembea hadi sehemu ya mwisho ya eneo hilo la gorofa ya chini, na baada ya hapo, unatakiwa kupanda ngazi kwenda juu, na huyu mdada akasema

‘Subiria hapa…’akasema na hapo hapo akapanda ngazi na kuondoka, na haikupita muda mara akatokea mtu kwa nyuma yangu, nikahisi unywele wa nyuma ukisisimuka kuwa kuna adui nyuma, nikasubiria..mara sauti ikasema

‘Haya twende…’sauti ikasema nyuma yangu

‘Twende wapi..?’ nikamuuliza kisauti ya kibabe kumuonyesha kuwa siogopi, lakini sio kweli, kwa hali kama ile ni lazima uwe na mashaka.

‘Panda ngazi, utaambiwa wapi pa kwenda tukifika huko juu…’akasema

Nilisita kidogo, lakini baadae nikaona haina haja, ngoja kwanza nitoke eneo hilo, nikafanya kama alivyotaka,..tukatembea hadi juu, nahisi ni ghorofa ya pili juu, sikuwa na uhakika kwani tulikuwa tunatembea kwenye ngazi tu.

Tulipofika juu , akasema;

'Subiri...'akasema na yeye akapita mbele yangu, maana kipindi chote hicho yeye alikuwa nyuma yangu...akawa ananikagua na mashine alipojirizisha akawa anaongea na simu kwa suati ndogo sikusikia kitu.

'Haya tembea twende mbele...'akasema na mimi nikafuata maelekezo yake, tukawa tuantembea kupita ofisi mbali mbali kuna majina yake mlangoni, hadi kwenda ofisi moja, haikuandikiwa kitu mlangoni, nilijua ni ofisi pale tulipoingia ndani,.

'Ingia huko ndani na kaa kwenye kiti, na kuna chochote unachohitajia, ukitaka maji, vinywaji, chai, unaweza kujisaidia, ni ofisi yako kwa muda...'akasema na hakutaka kusema zaidi huyo akaondoka zake, na mimi nikaingia humo ndani.

Kilikuwa chumba cha ofisi chenye kila kitu cha kiofisini, nikaambiwa nikae hapo nisubiri, na akma naihitaji chai, kinywaji, chochote kile naweza kujisaidia...lakini sikutaka kitu , nikaa kimia tu kusubiria, na mara

Sijakaa sana, mara mlango ukafungulia, akaingia jamaa mmoja kama kawaida zaidi usoni kavaa mawani makubwa, kuficha uso,na hata ndevu za bandia, niliona hilo kwa uzoefu wangu, akasema;

‘Samahani bosi, nimeleta huu mkataba, nimeambiwa uweke sahihi zako, lakini kabla ya kuweka sahihi una dakika kama tano hivi, za kusoma kilichoandikwa, ili uwe na uhakika kuwa watu hawa hawana nia mbaya na wewe, natumai, unaelewa wajibu wako, mtoto wako yule salama ...’akasema na kuniwekea hilo faili mbele yangu, nikalichukua na kuanza kufungua ukurasa mmoja mmoja, nikawa nasoma;

Ulikuwa mkataba wa hiari, ambao mimi nakubali kuwa nitafanya kazi, chini ya kampuni iliyotajwa jina, na nitakuwa nikimtii kiongozi wake, hapo kwenye kiongozi wakaacha nafasi , hakukuweka jina la huyo kiongozi. Sehemu nyingine, inataka mimi nikubali kuwa mtoto huyo ana baba yake, jina , sehemu ya jina hakuna kitu, mbele yake, ikasema,baba huyo ndiye mwenye mamlaka na huyo mtoto, na mtoto atapata haki zake zote kutoka kwa baba huyo...na yeye kama mama atapata haki zake.

‘Hivi ni mkataba gani huu wa kutegeana, kampuni gani, sioni jina, baba wa mtoto simuoni jina lake..unataka niweke sahihi kitu ambacho hakipo kamili, ni sheria gani inasema hivyo…?’ nikauliza

‘Hawajaandikwa hapo kwasababu maalumu, lakini ukiweka sahihi, ..naweza kuja kukuonyesha wataonekana…muhimu ni usalama wa mtoto wako au sio…’akasema

Kukawa na maelezo mengine mengi, ya hisa, na mimi nitapewa sehemu ya hisa, kama nitakubaliana na yote hayo, na kutimiza maagizo yote, na nilitakiwa nisimtambue mtu mwingine yoyote kama bosi wangu zaidi ya huyo aliyetajwa hapo,....huyu aliyetajwa hapo ni nani, nilitaka kuuliza lakini nikaona haina haja

Nikamaliza, kusoma, nikainua kichwa kumuangalia huyo mtu aliyeleta hayo makabrasha, nikamuuliza

‘Kwanza mtoto wangu yupo wapi?’ nikamuuliza

'Samahani bosi, ...Mimi sijui maswala ya mtoto wako yupo wapi, niamini hilo, nilichoambiwa nikuhakikishie ni kuwa mtoto wako yupo salama, ..ukimaliza kuweka sahihi, mimi nimemaliza kazi yangu...'akasema na kutulia kidogo, na aliponiona nipo kimia akasema

'Je umemaliza kusoma huo mkataba, umeona ulivyo, mengi ni kwa masilahi yako..sasa kama umemaliza kusoma, tafadhali…,weka sahihi yako, tumalize kazi, ukizidi kuchelewa ndivyo utakavyozidi kuchelewa kumpata mtoto wako bosi.....’akasema

‘Mimi siwezi kuweka sahihi yangu mpaka nimuone mtoto wangu...sijui kama kapata maziwa sahihi, muda kama huu alitakiwa kupata maziwa yake maalumu.’nikasema na kabla sijatulia mara ukutani kukatokea maandishi, na taswira ni kama vile unaangalia runinga, na mara mtoto wangu akatokea, akiwa kabebwa na mwanamke, na huyo mwanamke alikuwa akimpa huyo mtoto maziwa ya mpira, yale yale ninayompa kila siku, na mtoto wangu alikuwa katulia

Pale nilihis machozi yakinilenga lenga…nilitamani nisimame na kufanya jambo, ili mtoto wangu afahamu kuwa mama yake nipo…lakini ningelifanya nini, na huyo mtu akasema;

‘Natumai umemuona mtoto wako..yupo salama, na kila kitu anapata kama ulivyokuwa ukimpatia, sasa sikiliza...sahihi yako ndio itakayofanya mtoto wako aendelee kuwa salama, na ndio itakayokufanya umpate mtoto wako, ili mambo mengine yaendelee…’akasema

Na mimi kwa haraka nikachukua peni, na kuweka sahihi yangu, hiyo ni sahihi maalumu, ambayo, naitumia kwa wakati kama huo, huwezi kuona tofauti, lakini mimi mwenyewe nafahamu wapi nimebadili.

Nilipomaliza kuweka sahihi, nikaweka peni chini, na yule mtu akanishika mkono, akaniambia;

‘Hapa kuna sehemu ya kuweka dole gumba hapa tafadhali kidogo,…’akasema na kunishika mkono, akaweka kidole gumbe mbele, ili niguse kitufe cha wino, kidogo nilitaka kugoma.

‘Usilete ubishi madam,..mtoto wako…’akasema

Baadae nikaona haina haja, akakiweka kidole changu kwenye wino, na kidole hicho akagandisha kwenye zile karatasi, hakufahamu kuwa mimi nilishajiandaa kwa hilo, hiyo alama itakayoonekana hapo, haiwezi kuonyesha usahihi wa dole gumba langu.

‘Nafikiri tumemaliza, subiri kuna sehemu unatakiwa kwenda...’nikaambiwa, nikasubiri kidogo mara akaja mtu na kuniambia nijiandae, kwani tunatoka nje ya jengo, na ninatakiwa kufuata masharti kama namjali mtoto wangu.

‘Hivi nyie watu mna ubinadamu kweli…’nikasema

‘Kwanini madam, kuna kitu umefanyiwa kisicho sahihi, niambie ..?’ akauliza

‘Mimi ni mama wa mtoto, na mtoto wangu bado mdogo, anahitajika kuwa karibu na mama yake…’nikasema

‘Wakati ukiwa huko unasoma, mtoto wako aliweza kukaa masaa mengi bila ya wewe au sio, akawa anahudumiwa na mtu mwingine, yaya…au sio…na isitoshe wewe humnyonyeshi mtoto wako, au sio, maziwa yako yana matatizo au sio…, ulishauriwa usimnyonyeshe na docta, nipo sahihi…’akasema huyo jamaa kama ananiuliza

Sikuelewa hayo yote aliyafahamu vipi , maana kiukweli sikuweza kumnyonyesha mtoto wangu maziwa yangu, ilitokea chuchu zangu kuvimba na nikimnyonyesha mtoto wangu napata maumivu makali, docta akanishauri nisimnyonyeshe. Kwahiyo mtoto wangu alianza kutumia maziwa ya mpira bado mapema tu.

‘Hiyo haijalishi,…mimi nahitajia kumuona mtoto wangu, angalau mara moja kwa siku.. mimi sitaweza kufanya lolote mpaka nimuone mtoto wangu, nimguse, awe karibu na mimi...’nikasema na mara kwenye ukuta nikaonyweshwa mtoto wangu, sasa akiwa kashikiwa kisu kooni...

‘Shsssiti...nyie ni mashetani..’nikasema, sikutaka kusema jambo, nikaondoka na hawo watu, tukashuka ngazi , sasa tukitoka nje ya jengo, na tulipo fika nje ya jengi, karibu kuingia kwenye gari, huyo muongozaji akasema;

‘Tumechelewa, lakini haina shida, tunatakiwa kwenda kumuona mgonjwa…’akasema,

‘Mgonjwa gani..?’ nikauliza

‘Mzazi mwenzako...’nikaambiwa hivyo, sikutaka kuuliza zaidi, nikahisi ni nani, tukaingia kwenye gari, na gari likaondoka, hadi hapo nikaona niwe mpole tu, ili nione mwisho wa haya mambo ni wapi.

Na kweli tukafika hospitalini, ni ile hospitalini alipokuwa kalazwa, mume wa familia, nikaongozwa hadi sehemu alipolazwa, na kwa muda ule ilikuwa sio muda wa kuona wagonjwa, lakini mimi nikaruhusiwa, nikaingia ndani alipolazwa mume wa familia, alikuwa chumba cha peke yake.

Kiukweli nilipomuona huyu mtu, nilitaka nimvamie na kumparura na makucha maana nilihisi kuwa ni yeye au hata kama sio yeye, kiongozi, lakini ni miongoni mwa hao watu wabaya wangu. Nilishawachukia kikomo cha kuwachukia, we acha tu..

‘Vuta subira…’nafsi ikaniambia hivyo

Nikasogea hadi pale kitandani, na jamaa nilimkuta akiwa kalala, lakini sehemu hii ya juu imeinuliwa kama kukaa hivi, akageuza kichwa kiniangalia na tabasamu likajaa tele mdomoni mwake, mimi sikutabasamu,.

Na alitarajia kuwa nitamsalimia, mimi sikufanya hivyo, na wala sikuuliza anaendeleaje, swali langu likawa hivi;

‘Ina maana na wewe upo kundi moja na hawo watu, hao watu waliomteka nyara mtoto wangu…?’ nikamuuliza. Na nilimuona akashtuka, unaona kabisa mtu akishtuka, kuonyesha kuwa hajui au labda anaigiza kufanya hivyo.

‘Eti nini!!!, wamamteka nyara mtoto wetu, haiwezekani, ngoja niongee nao...’akasema akionyesha mshangao, na sasa akawa anachukua simu, na mimi nikamzuia na kusema;

‘Haina haja, ila nakutahadharisha, kama upo kundi moja na hawo watu, ujue, kitakachotokea baadaye hutaweza kuamini kuwa mimi ndiye huyu unayeniona hapa mbele yako, unasikia...’nikasema

‘Una maana gani kusema hivyo, mimi sijui chochote….’akasema akitikisa kichwa kukataa hivi

‘Haya yaliyotokea sitaweza kuyasahau,..maishani mwangu, kuniweka roho juu, mpaka sasa sijui mstakabali wa mtoto wangu, sijui yupoje, mnataka nini kwangu, nakuambie ukweli hili utakuja kulijutia, wewe na hao wenzako, ...’nikasema

‘Unanilaumu mimi bure,…Mimi nimeletewa taarifa kuwa umefika kutoka huko masomoni kwa dharura, sijui ni dharura gani, na baadae leo naambiwa utakuja kuniona,…sasa..’akasema na mimi nikamkatisha na kusema;

‘Unajifanya hujui kinachoendelea huo mkataba wa hiasri kuwa mimi nikubali kuwa wewe ni baba wa mtoto wangu, na utawajibika naye umetungwa bila yaw ewe kufahamu..?’ nikamuuliza

‘Hayo nimeambiwa leo hii, alipokuja huyu mtu kunipa taaarifa hiyo, na mimi sikuwa na pingamizi na hilo, mimi nimekubali kuwa nipo tayari kuwajibika kwa ajili ya mtoto wetu, kwani hapo kuna kosa, kwanini nikate hilo, nikifahamu hiyo ni damu yangu..na pia nikaambiwa umekubali kuweka sahihi ..kwanini mimi nikatae, sasa tatizo lipo wapi hapo...’akasema

‘Tatizo ni kuwa nyie hamnifahamu kuwa mimi ni nani...sawa mimi sina zaidi, nashukuru kuwa nimekuona, na naona umepona, tofauti na nilivyoambiwa kuhus hali yako, najua ni janja yenu, uzidi kuonekana unaumwa, au so...’nikamwambia na yeye akawa kama kakumbuka jambo, na kujiweka kitandani kama mgonjwa aliyezidiwa.

‘Usijabarague ndugu, kujiigiza huko itafika mwisho wake, hata kama unaumwa, lakini sio kivile au sio, ipo siku mtaumbuka na haya yote yatasikika kwa kila mtu na hata wale ambao hukutaka wasikie huu ukweli...’nikasema

‘Janja gani lakini, naumwa, na sijasema naumwa kivile, niliwaambia hii hali yangu naweza kukaa nyumbani na kuendelea na kazi zangu, lakini wao wakasisitiza kuwa ni muhimu nikae hapa kwa uchunguzi zaidi…’akasema.

‘Ok, sawa, endeleeni tu, na dhuluma zenu, tuone mtafikia wapi…’nikasema

‘Sikiliza mpenzi, haya tulishayaongea na hadi hapo natumai utaelewa ukweli halisi kuwa hata mimi nayafanya haya kwa vile sina jinsi, hapa ilipofikia sina jinsi ya kuzuia, ngoja yafanyike ya kufanyika na muda ukifika utasema…’akasema

‘Tatizo lako ni tamaa, wewe na Makabrasha, na hao wanasiasa, mnafikiri mtaweza kufanikisha mambo yenu kirahisi hivyo, wakikutumia wewe kama chambo, haya yatafika kwa mkeo, na itakuwa mwisho wa ndoa yako na mwisho wa ndoto yako ya utajiri wa haraka haraka..’nikasema;

‘Chunga ulimi wako, sikiliza hivi sasa wewefanya wtakavyo, kwa masilahi ya mtoto wako, vinginevyo utanifanya mimi nichanganyikiwa, hivi yule mtoto akipata madhara, unafikiri mimi nitaweza kuvumilia, usifikiri ni wewe tu utaumia..’akasema

Aliposema hivyo, mimi sikutaka kuongea naye, nikageuka kutaka kuondoka.

‘Sikiliza jitahidi ,...usiondoke bila kuniaga...’akasema na mimi sikugeuka kumwangalia nikatoka nje.

Nilipofika nje, akaja huyo muongozaji wangu, akaangalia sasa na kusema;

‘Mbona haraka mumemaliza kuongea..?’ akauliza

‘Kuongea kuhusu nini, sina cha kuongea na huyo mtu, …’nikasema kwa hasira na huyo jamaa akanitupia macho ya mashaka, akashika simu yake akaongea na wenzake, na mara gari likaja.

‘Sasa inabidi turudi mjengoni…’akasema

‘Sawa narudi huko, lakini nimuone mtoto wangu, kwani mtoto wangu yupo wapi..?’ nikamuuliza

‘Wewe ulipoteremka pale uwanja wa ndege mtoto wako ulimuachia nani, ..hukujali hilo, kwanini kama ulitaka mtoto wako muwe naye mbona ulimpa mtu mwingine, huyo mtu unamuamini vipi…?’ akaniuliza

‘Ina maana huyo mtu ni mtu wenu pia..?’ nikamuuliza

‘Sijasema hivyo, …nazungumzi hiyo hali yako ya kutaka kuwa na mtoto wako karibu, kuwa kama ungelikuwa na tabia hiyo tungelijua hutakiwi kuwa mbali na mtoto wako, je nikuulize huko ambapo ulitaka akakae, eeh, ulitaka akae muda gani, si mpaka ukiondoka, au sio..?’ akaniuliza

‘Hayo hayakuhusu, nilijua mwenyewe ni muda gani wa kumchukua..’akasema

‘Usijali kuhusu mtoto wako, yupo salama na ataendelea kuwa salama, ushukuru kuwa kwa hivi sasa yupo sehemu analindwa hakuna kitu kitamgusa, kitu kitamgusa kama wewe hutafuata masharti..’akasema

Basi mimi nikaendelea kufanya wanayoyataka wao, ilimradi mtoto wangu awe salama, kwahiyo nilifuata kila wanachokitaka, bila kupinga, hadi siku ya pili yake ndio nikaambiwa nitatoka mle mjengoni muda ambao ndege yangu ya kutoka huko masomoni itakapotua hapa Dar.

‘Una maana gani kusema hivyo..?’ nikamuuliza

‘Unasikia kwa kumbukumbu zako, siku gani ulitakwia ufike hapa Dar, eeh, si umekata tiketi kwa haraka ukarudisha siku nyuma, basi siku ambayo uliweka taarifa kuwa ndio utafika dar, ndio itatambulikana hivyo, leo ndio undio unafika hapa Dar…umenielewa…?’ akaniuliza

‘Ujinga mtu huo..’nikasema

‘Kila kitu kimeshawekwa hivyo, leo ndio unafika Dar, muda ndege ikitua na wewe utafikishwa pale uwanjani, na hapo ndio, utachukua usafiri kuelekewa huko nyumbani kwako, ulipopanga kufikia haya yote ni kwa usalama wa mtoto wenu, uhakikishe kila mtu unamuambia hivyo,..tunakufuatilia kwa hilo, kosa dogo, mtoto hutamuona tena..’nikaambiwa

‘Ina maana mtoto wangu siwezi kumuona, nakumchukua..?’ nikauliza

‘Kwa usalama wa mtoto hutaweza kumuona, maana sio sisi pekee wenye haja na huyo mtoto, unielewe hapo…mtoto wako utamuona siku ya kuondoka, wewe si ulipanga iwe hivyo, una wasiwasi gani, kila kitu mtoto wako atakipata, hata hivyo, ni muhimu mtoto aonane na baba yake, hilo tutaangalia jinsi itakavyowezekana…’akasema

‘Yule mtoto hana baba, mnawazimu nyie watu,s itaki mtoto wangu aje kuonana na huyo mpuuzi, mnasikia, mkitaka tuelewane mtoto wangu asionane na huyo mtu mnasikia..’nikasema

‘Usijali kwa vile umeshaweka sahihi mkataba kuwa baba yake ana mamlaka na mtoto,..na huo mkataba umeshapelekwa kwenye ngazi za sheria, utahifadhiwa huko kama makubaliano halali ya kisheria, huna jinsi madam, kama ningelikuwa mimi ni wewe nisingelisumbuka zaidi kwa hilo..kwani unakosa nini hapo, hayo yote nikwa masilahi yako na mtoto au sio…’akasema huyo mzungumzaji.

‘Huyo bosi wenu yupo wapi…nataka kuonana na yeye..?’ nikauliza

‘Huwezi kuonana na yeye, yeye anatimiza wajibu wake kwa ajili ya kusimamia familia zenu, kama unahitajia hilo, ni baada ya kila kitu kukamilika, mengine yote utakuwa ukiongea na mzazi mwenzako..’akasema

‘Hili jengo analimiliki nani..?’ nikamuuliza

‘Hata mimi sijui madam, mimi natimiza wajibu wangu tu, maswala ya jengo na utawala sio kazi yangu…’akasema.


Unajua walikuwa wakinitesa kiakili, maana sina tofauti na mfungwa, ..kwa hasira, nikachukua bakuli iliyokuwa na mboga, ile mboga nikaimimina sehemu nyingine, niliona uzito wake, unaweza kufanya hicho ninachotaka kukifanya, nikageuka kwa kwa haraka sana nikairusha ile bakuli hadi kwenye kile kitufe nilichojua ni cha kuangalia matukio, kwa shabaha ile kikavunjia ...na taa.

Nilitarajia mlio wa tahadhari, lakini sikuusikia, nikaona nimefanikiwa jambo muhimu, kwa haraka nikasogeza meza nikapanda juu, na kuvuta nyanya zake, kuhakikisha hakuna mawasiliiano kwenye hicho chumba, nikatoka nje, na kuanza kutembea bila kujua nielekee wapi, nikaiachia hisia yangu iniongoze, nilipanda hadi juu, nikaanza msako, wa kumtafuta mtoto wangu.

NB: Mdogo mdogo, ni hatua ya ushahidi na ukweli


WAZO LA LEO: Ni muhimu wakati mwingine tuwe na subira na mambo, tukiwa katika halali na taratibu zilizokubalika. Tusikimbilie pupa pale tunapoona kuna hatari, au kuna sintofahamu. Pupa ya mambo, uharaka wa kutaka kupata, hasira na tamaa ndizo hufanya watu wakafanya mambo yasiyo sahihi. Kwanini tusifuate utaratibu, kwanini tusitimize wajibu wetu kwa mujibu wa sheria, kwanini tusichume chumo halali, kihalali, …tukumbuke subira huvuta heri.
 
SEHEMU YA 109


Sikuweza kuvumilia tena niliona liwalo na liwe, nataka kumpata mtoto wangu…

Tuendelee na kisa chetu..

**************

Kuna kitu kimoja tunajifunza kwenye kazi zetu, hata siku moja usitake hasira ndio zikutawale ukashindwa kuhimili nafsi yako, ukijua kuwa adui yako ana kila kitu. Ni muhimu sana kuwa makini, kwani adui wengine hawajali, kutoa roho za wengine sio kitu kigumu.

Kwahiyo pamoja ya kuwa niliondoka mle ndani kwa hasira, bado utaalamu wangu wa kiupelelezi niliulinda, nilitoka kwa tahadhari, na kuhakikisha kuwa sitafanya makosa yatakayo mgharimu mtoto wangu.

Ujue kwa muda ule nilikuwa kwenye ofisi niliyopewa, ofisi yangu eti kama bosi mtarajiwa, kwahiyo nilipotoka pale nilikuwa kwenye ofisi za ghorofa ya juu, sio kule chini sehemu ya kulala…na anilijua siku hiyo sitakubali kwenda kule tena, mpaka nijua hatima ya mtoto wangu.
Nikatoka mle ndani ya ile ofisi nikawa natembea nikipita ofisi ya kwanza, ofisi ya pili nikasikia sauti, kwanza nilihakikisha mbele au nyuma hakuna mtu anayenifuata, nilijua huenda maeneo yote hayo yana video za kuchukua matukio, sikujali kwa hilo

Nilijifanya kama nataka kuingia kwenye ile ofisi, huku nikitegea siku kubahatisha tu, hao watu humo ndani wanaongea nini…

‘Nimeshakufanyia kila kitu unachokitaka, nimekutii, nimekusaidia na sasa umefanikisha kile ulichokitaka,kwanini bado waendelea kunifanya kama mtumwa wako, ...’sauti ya kike ikalalamika.

‘Ndio wewe ni mtmwa wangu ulielewe hilo, japokuwa nafahamu kuwa nakuonea, lakini ni kwa vile wakati mwingine hutaki kunitiii amri yangu, inabidi nifanye haya ninayoyafanya sasa hivi..’sauti ya kiume ikasema

‘Kiukweli nimechoka..’sauti ya kike

‘Sikiliza ninachotaka mimi kutoka kwako ni utii, nikitaka hiki ukifanye, basi ukifanye mara moja, ndivyo makubaliano yetu yalivyo,...hata hivyo nisamehe, leo akili yangu haijakaa sawa,...nisamehe mtumwa wangu eeh,..’sauti ya kiume

‘Sitaweza kukusamehe kamwe..’sauti ya kike

‘Nisikiliza basi…mimi nakuhakikishia kuwa, hili likikamilika, wewe na wengine wote mtakuwa huru, usiwe na wasiwasi na hilo…haya mambo nataka yamalizike ili hata mimi nitulie, na kuanza kula raha za dunia,….habu nikuulize kwa hivi sasa kuna kitu unanidai...’sauti ya kiume ikauliza.

‘Nipe hizo kumbukuzi zote za mapicha machafu uliyochukua kutoka kwangu na kwa watu wengine, niziharibu, hapo ndipo nitaamini maneno yako, ili watu wawe na amani na ndoa zao...’ sauti ya kike.

‘Hilo kamwe lisikutie wasiwasi, ndoa zenu zitakuwa na amani kama nyie wenyewe mtajituliza na waume zenu, tatizo nyie mumekimbilia kuolewa kwa kutaka mali, na sio upendo, kwahiyo hilo sio kosa langu..au nimekosea…’sauti ya kiume

‘Sio kweli, sisi pamoja na hayo tulishaamua kutulia na waume zetu, mengine uliyatengeneza wewe, ili yatokee na upate unachokitaka..’sauti ya kike

‘Hapana sio kweli, mimi nilijua tu hamutaweza kutulia, hamtaweza kuwa mbali mbali, ipo siku mtakumbukana, na sikufany aharaka kwa hilo, taratibu kama yule ndege tai…anavyovizia mizigo,..kwahiyo sio kosa langu, ila mimi nawahakikishia kuwa kazi hii ilikuwa na mipaka na muda wake, ikikamiliza, haina haja tena, hizo picha, video, nitaviharibu, mbele yako, wewe nipe mud unimalize kazi hiyo iliyobakia,...’ikasema sauti ya kiume

‘Na malipo yangu je…?’ sauti ya kike

‘Malipo gani zaidi, ..bado kazi haijaisha unataka malipo, malipo yako utapata usiwe na shaka…’sauti ya kiume

‘Kazi gani imebakia,..mikataba si imeshakamilika su sio, sasa hivi unamiliki hisa, kuna mipesa kibai umeshalipwa na wahanga wako wa milungula,..bado huajtosheka unataka nini wewe, kiukweli wewe ni shetani asiyeshiba madhambi..’sauti ya kike

‘Hahaha napenda sana hiyo lugha yako, kumbe unafahamu kuwa mimi ni shetani, basi mambo bado…kuna mambo bado hayajakamilika..’sauti ya kiume

Mara nikahisi kuna suti nyuma yangu…haraka nikajifanya kutembea hadi ofisi za mbele na nilipohakikisha hakuna mtu, nikarudi tena kusikiliza kwa muda kama ule ulikuwa mchana watu wanapita, lakini siku ile sikuona watu wakipita pita na hata wakitokea ni mtu anatoka kwenye ofisi fulani na kuelekea chini au juu.

Niliporudi pale nikasikia

‘Mimi nayaelewa hayo yote, kuwa ni mabaya na hayana mwisho mwema, ndio maana njiandaa kuachana na tabia hiyo, nikikamilisha hili, natulia, ....nitakuwa na haja gani tena, wakati nitakuwa mkurugenzi mkuu wa makampuni kadhaaa, yenye mabilioni ya pesa, ....tatizo anayenichelewesha ni huyo mtu wako wako, ngoja akija kesho kutwa, eeh…’akatulia

‘Kesho kutwa au kesho..?’ sauti ya kike ikauliza

‘Kesho nina mambo mengine ya kufuatilia, kuhakikisha hiyo mikataba imefika sehemu husika, na kwenda kukutana na wafadhili wangu, kuwahakikishia kuwa mambo yapo kama ilivyotakiwa iwe, kwahiyo ushindi ni lazima…’sauti ya kiume

‘Sikiliza…mimi sihitaji kuingie kwenye siasa, nataka kuwekeza kijijini, mimi sitaki kuishi mjini, nataka maisha yangu yawe huko kijijini, hadi hivi sasa mume wngu anafahamu nipo huko…’sauti ya kike

‘Najua sana ni nini unakifanya huko, na hayo yote ulifanya kwa kuogopa au sio…sasa hutakwua an hajaya kuogopa, usitishike na wanaume akitaka kukuacha, muambie afanye hivyo, hataweza maana hai hapo atakuwa hana kitu…’akasema

‘Tatizo wewe unajiaminisha sana, unafikiri wao ni wajinga wakae kimia tu..’akasema

‘Ndio maana nilikuambia hivyo kuwa muda wa kuziharibu hizo picha na video bado, hukunielewa, hivyo vitu havijamaliza kazi zake, zitamaliza kazi zake pale tutakapohakikisha hao watu hawana kitu na hawana namna ya kufanya,..na wafadhili wangu wameridhika, na kushika hatamu…na mimi huku niwe na mamlaka ya vitega uchumi vyote..’sauti ya kiume.

Kukawa na ukimia fulani hivi…halafu sauti ikasema

‘Kuna nini, mbona umesimama kuongea, una mashaka gani na maneno yako au umeona nini…?’ sauti ya kike ikauliza

‘Kule ofisi ya bosi wako, hakuna ishara,…unaona hapa, kuna alama nyekundu kuashiria kuwa huko kuna tatizo,.. yaonekana kamera za kuonyesha matukio za kule hazifanyi kazi, kuna nini..unajua huyo bosi wako simuamini, ni hatari sana, yawezekana kafanya jambo…’sauti ya kiume ikasema

‘Huyo mnamsumbua bure, yeye ni mzazi, na sioni umuhimu wake kwa hili… muachieni akasome, na mpeni mtoto wake, hana tatizo na nyie..yeye kawakosea nini..unajua hadi hivi sasa mimi kama mimi sioni umuhimu wake….’sauti ya kike ikasema.

‘Wewe utakuja kuona umuhimu wake….na unanishangaza sana,…haya yaliyotokea hadi yeye kuweka sahihi hujaona umuhimu wake, wewe hujui kuwa huyo ndiye kiongozi wao wa usalama, huyo tukimweka mikononi, hao watu hawana ulinzi, hawana mtu wa kumtegemea…sikiliza kama haupo upande wangu niambie, nifanye vitu vyangu…’sauti ya kiume ikasema

‘Kwani mimi nilikuwa upande wenu, mimi mumenilazimisha na sina la kufanya, nitakutii, ili utimize mambo yako, lakini mkimaliza …hapo na mimi nitakuwa huru, na kiujumla mimi sitaki kujishughulisha na jambo lolote hata bosi wangu nilishamuambia hivyo…’sauti ya kike.

‘Wewe au mwingine, ukiishiwa pesa hukumbuko ulichosema, sikiliza wewe uwe upande wetu, sehemu ambapo pesa hazikauki, unasikia,..oh, unaona hapa, hii alama bado inaonekana, na sioni chochote kule alipo huyo bosi wako, yule mlinzi kaenda wapo, nampigia simu hapatikani..’sauti ya kiume

Kukawa na ukimia kidogo, halafu sauti ikasema tena.

‘Nahisi mitambo ya pale imeharibika, kama sio yeye kafanya jambo basi kuna tatizo, ngoja niongee na mtu wangu…’sauti kasema na kukawa na ukimia fulani baadae sauti ikasema

‘Na huyu mshenzi sijui kaenda wapi, simu yake haipokelewi, sasa sikiliza hebu nenda wewe, kaangalie kinachoendelea unasikia, …’sauti ya kiume ikamsema

‘Sawa nitaenda, ila usiwe na wasiwasi na huyo mdada, nilishamuweka sawa, anajua madhara yake anampenda sana mtoto wake, hawezi kufanya jambo la ajabu, hebu angalia tena labda ni mitambo yako tu hiyo..’sauti ya kike ikasema.

‘Nisikiliza amri yangu…unasikia wewe nenda,…’sauti ikasema

‘Sawa bosi,…’kabla hajaondoka suti ikasema

‘Kabla hujaondoka,ule mkataba niliokuambia uuchukua kwa mume wako upo wapi, unajua kesho, ndio siku nataka kwenda kuufanyia kazi,..unafikiri nimesahau eeh..’sauti ya kiume

‘Nilikuambia bado sijaupata, na nitaupate na mimi sipo naye, unajua mimi nipo wapi, unaniuliza kitu ambacho hata wewe unakifahamu, mimi nipo wapi, si nipo kijijini, au umesahau,..hata hivyo, mimi naona hayo ya mume wangu achana nayo, hayafai, hayana umuhimu, wa nini kwanza..?’ akauliza

‘Ina umuhimu sana, tunamuhitaji sana huyo mtu, achilia mbali na kazi yake lakini pia kisiasa, ana umuhimu wake,…ngoja nikimalizia hii kazi mimi mwenyewe nitamfuatilia, utaona nilivyo, …yeye mwenyewe atasalami amri, kuna video yake mbaya nikimuonyesha ni lazima atanitafuta…’akasema

‘Video yake!! Video gani hiyo..?’sauti ya kike ikauliza

‘Siwezi kukuonyesha wewe…ukiiona unaweza ukachanganyikiwa, na sitaki uende kuleta fujo,..wewe una umuhimu sana hapa, tatizo lako ulimuamini sana, hakuna msafi hapa, mimi wote nawafahamu madhambi yao, asikudanganye mtu, wewe tulia na mimi ule nchi,…’sauti ya kiume.

Niliona nikiendelea kukaa pale ninaweza kushukiwa kwahiyo nikasogea hadi kwenye mlango, nikausukuma ule mlango kwa taratibu,.. nikaona unafunguka…mimi kwenye begi langu nilikuwa na kifaa, nikakitoa na kuchukua kitufe kidogo, kama kitenesi, nikakiweka hicho kifaa,..ni kidogo, huwezi kudhania ni kitu muhimu sana, nilipohakikisha kuwa mlango upo wazi, nikakitumbukiza kile kitenesi, kikawa kinaserereka kulekea ndani.

‘Umedondosha nini…na mbona mlango kama upo wazi,..’sauti ya kiume ikauliza

‘Kumedondoka kitu, !! ni kidude cha kuwekea peni, mmh, na wewe una msikio, umesikiaje na wewe upo unaangalia mitambo yako huko..?’ sauti ya kike ikauliza

‘Kila kitu kinachofanyika kwenye maeneo yangu ninakiona hapa.., ila huyu bosi wako kawa mjanja…kwa hivi sasa simuoni kabisa, .., haya wewe nenda kamuangalie..hivi sasa ni mchana sitaki mimi kuonana naye,.., hiyo kazi ni yako, na akifanya ujanja tu..mtoto wake kiukweli atampoteza, sitanii hili, unanifahamu nilivyo.’sauti ikasema

‘Sawa bosi…ngoja niende..’sauti ya kike

Na mimi niliposikia hivyo, nikageuka na kuondoka, kwa haraka nikitaka kurudi ofisini kwangu, lakini kabla sijageuka, nikahisi mtu yupo nyuma yangu…

‘Unafikiri unafanya nini hapa…’ilikuwa sauti nyuma yangu na kabla sijamjibu kitu mara mlango ukafunguliwa akatokea mdada,…mmh, sijawahi kumuona huyu mdada kabla, muonekano wake ni kama mzungu fulani hivi, aliponiona kwanza alishtuka baadae akasema

‘Kwanini hujapiga hodi,…nilikuambia ukija upige hodi, sasa sikiliza bosi hana muda wa kuongea na wewe, twende huko huko ofisini kwako..’akasema huyo mdada.

Na jamaa yule aliyekuwa nyuma yangu akabakia kaduwaa, …tukawa tunatembea kuelekea kule ofisini kwangu na huyo jamaa sasa akawa anataka kufungua mlango kuingia kwenye hiyo ofisi aliyotoka huyo mdada, huyu mdada akasema;

‘Wewe, Bosi alikuwa akikuulizia muda mrefu, kakasirika sana, ukienda kuonana naye sasa hivi utalikoroga, wewe katulie kituoni kwako kwa muda, baadae ndio uende, kama atakuhitajia tena..’akasema mdada

‘Poa….kwani hukumuambia kuwa nilitoka kidogo..’jamaa akasema na kuondoka kurudi huko alipotoka.

Na sisi tukarudi ofisini kwangu, na huyo mdada aliyejiweka kama mzungu akasema;

‘Wewe vipi kwanini unataka kuharibu…?’ akaniuliza

‘Sina amani nataka kuonana na mtoto wangu..’nikasema

‘Sikiliza nimeshakuambia kila kitu kitakuwa sawa, wewe hakikisha unafanya kila wanachokita wao, kwanini hunielewi, utaharibu na utakuja kujijutia, …’kabla hajamaliza akaona kazi niliyoifanya kule juu..

‘Mungu wangu, huyu mtu akija kuona hiki kwanini uemvunja hiyo taa,…?’ akauliza,

‘Wewe muite fundi, aje arekebishe kwa haraka lakini asirudishe hiyo video kamera, wewe huoni kuwa hiyo video kamera ilikuwa imefichwa kwenye hiyo taa,, je waweza kumuita fundi akarekebisha hilo tatizo kwa haraka..?’ nikamuuliza huyo mdada

Huyo mdada kwa haraka akachukua simu na kumpigia fundi, haikupita muda akaja fundi akapata maelekezo, na haikuchukua muda, kila kitu kikawa sawa.

‘Safi kabisa,…’nikasema

‘Sasa wewe rudi kwa jamaa yako endelea kuongea naye, nataka kupata ushahidi zaidi..’nikasema

‘Kwa vipi, ok, bosi nimekuelewa, ila tafadhali usifaney tena hivyo, fuata wanavyokuambia, mengine niachie mimi, …’akasema huyo mdada na kuondoka.

Nilisubiria kidogo, baadae nikachukua simu yangu na kugeuza upande wa nyuma nikatoa kitu fulani kweney begi langu, nikakiweka kwenye ile simu, baadae mitambo yangu ikaanza kufanya kazi….nikawa sasa nasiiliza kile wanachokiongea kule kwa huyo jamaa,, mpaka muda huo nilikuwa sijafahamu ni nani, huenda ni Makabrsha, lakini sikuwa na uhakika huo.

‘Umemkuta bosi wako, kafanya nini mbona bado mitambo haionyeshi kitu..hivi yeye hajui haya yote ni kwa jili yao, yeye akiwa mmojawapo..’sauti ikauliza

‘Yupo lakini hana amani, anamtaka mtoto wake…’akasema

‘Mtoto wake wa nini, hajui hayo ni kwa usalama wa mtoto wake, wewe unafikiri kama hao wenzetu wangelimchukua huyo mtoto ingelikuwaje, wangempima kwanza DNA, halafau ikawa ndio sababu ya kuharibu kila kitu…’akasema mwanaume

‘Ni kawaida kwa mzazi yote hasa mama wa mtoto, huwezi kumlaumu kwa hilo, ila nimeongea naye, baadae atarudi kule chini kujiandaa kwa ajili ya kile mlichomuagiza au sio..’sauti ya kike

‘Sawa hakuna shinda baadae nitakwenda mwenyewe kuona kuna tatizi gani..lakini sitaki akiwemo humo ndani..’sauti ya kiume.
.
‘ Sawa bosi, jihangaishe tu, lakini hawo hawo unawasumbua, ..hasa huyo docta, na wengineo, watakuja kuwa mashahidi siku ukiwa umesimama kizimbani...’ikasema sauti ya kike.

‘Thubutu, labda kizimba cha kaburini, lakini nikiwa hai , hivi hivi, hanipati mtu, wewe hunijui tu, kila kitu kina plan A na B, ..kwa hivi sasa wameshasambaatika na hakuna wa kumfunga paka kengele,…’sauti ya kiume.

‘Sawa bosi…’sauti ya kike.

‘Sawa bosi, sawa bosi,..unajifanya mtiifu kumbe kigeu geu…nakuambia ukweli baada ya haya, utakuja kuniona umuhimu wangu, …hata hao watu wa usalama sasa hivi wananiheshimu, kuna tatizo kidogo, nasikia, huko kwa mdhamini wa mikataba, kuna kitu kimetokea, ..lakini nitamaliza hilo tatizi ..’sauti ya kiume ikasema.

‘Haya wewe jidanganye tu, umesema kuwa docta naye umepata video ya mapicha yake mabaya, ulimpataje madhambi yake, maana namuona ni mtu mtulivu sana,...?’ sauti ya kike ikauliza.

‘Hawo unaowaona watulivu, ndio balaa, wana mambo yao ya chini kwa chini, na wakati mwingine ni uwoga tu, nilimkamatisha kabinti kamoja karembo, ...huyo binti alifika kwake kama mgonjwa, na huyu bint anajua kazi badala ya matibabu, ikageuka kuwa kitu kingine,..sitaki uone hayo, hayo ni kwa ajili ya kazi, msamehe tu, hata ingelikuwa ni mimi nisingeliweza kuvumilia, hahaha…’akasema

‘Mjinga mkubwa wewe kumbe sio yeye, ni wewe ulimkamatisha kabinti, sasa unatarajia nini, kuwa utanitishia mimi, kuwa mimi nikiona hiyo video na mapicha hayo mabaya,tutaachana na mume wangu…, hahaha, hata kama nitamfuma akiwa mbashara, mimi sitaumia saaana…, maana najua mimi nina madhambi zaidi yake..’sauti ya kike.

‘Ni wewe, lakini sio yeye, docta ni muoga wa kufumaniwa, anajali sana ndoa yake, ila kwa …huyo mdada, alishindwa, na pia, …ile ya yeye n mpenzi wake wa zamani, pia ninayo, siwezi kukuonyesha,..japokwua sio mbaya kihivyo, lakini inaonyesha hisia za kuwa hao watu bado wanapendana, mimi kwangu inatosha akbisa kama ushahid..hao watote hawaniwezi ..kila mmoja nimeshamuwekea kinaso chake, …na wafadhili wangu watafurahi sana…’ akasema na mara sauti ikasimama.

‘Kiukweli mimi sitishiki tena na huo uchafu wako, fanya utakayo, lakini mimi nina imani ipo siku utaumbuka, na ...’akatulia kidogo, hapo nikaingiwa na wasiwasi, nikifikiria huenda wamekishitukia hicho chombo nilichokipenyeza mle ndani.

‘Mbona unasita kuongea, ongea tu..mimi nakusikiliza..’sauti ya kiume

‘Ni wewe nakuona kama unaangalia angalia chini, umeona kitu gani....’sauti ya kike.

‘Kuna kitu hakipo sawa, una uhakika yule mdada hajafanya kitu, ..?’ akauliza

‘Kama wewe huniamini, nenda ukaone mwenyewe..’sauti ya kike ikasema

‘Siwezi kwenda kweli kwa hivi sasa, ila nitakwenda, ni lazima kuna kitu kimefanyika, nitakwenda kuhakikisha, huyo mdada ni hatari....’sauti ya kiume.

‘Sasa mimi naondoka…kuna zaidi la kufanya..?’sauti ya kike

‘Usiondoke kwanza, nataka wewe uhakikishe huyo mdada akiondoka umemuweka sawa, unasikia, asije akaharibu,…nilitaka muende naye hadi uwanja wa ndege, lakini wewe utabakia huku nyuma kuhakikisha mambo fulani fulani, na mtoto tumemuhamisha, kwa usalama zaidi..’akasema

‘Ina maana huyo mdada hataondoka na mtoto wake..?’ akauliza

‘Hapana huyo mtoto atampata siku ile akiondoka, siku akirudi masomoni baada ya kuhakikisha kila kitu kipo shwari, huyo ndiye ndoana yetu kwa hivi sasa, na ni kwa manufaa yake, ili wenzetu wasije kumuona huyo mtoto maana mpaka sasa hawajahi kumuona sura yake..’sauti ya kiume

‘Na zaidi ya hapo utanihitajia kwa lipi zaidi au ndio nitakuwa nimemaliza kazi na wewe..?’ sauti ya kike ikauliza

‘Unahitajika kuwepo pia na huyo mwenzako akija, nataka huyo kidume wako, akubali kila kitu, aweke sahihi kwenye mikataba yote ikishamalizika hiyo kazi imekamlika, yeye hana kitu, atakwua chini yangu, na wewe utamfanya utakavyo, maana …usione kuwa mimi ni mbaya, nafanya hivyo, kwa vile yeye akibakiwa na hizo mali hana akili ya kuziendeleza, umeona anavyofanya , …tunahitajia watu kama mimi na bosi wako, na wewe…umenielewa, yeye ndio ataendelea kuwa na hisa, lakini mamlaka,hayawezi…unasikia…’akasema

‘Mimi sitaki kuonana na yeye, unajua mimi sijulikani kuwa nipo hapa Dar, unalifahamu hilo, pili, sitaki kuwa karibu na yeye kwa hivi sasa, uzalendo utanishinda, kanisaliti vya kutosha, nita…’hakumaliza

‘Najua najua hilo, pole sana….lakini usimlaumu sana, maana yote hayo yamefanyika ili kuhakikisha hili zoezi zima limekamalika, sizani kama wewe una haja ya kuwa na wivu, au sio…’sauti ya kiume na kukawa na ukimia fulani baadae akasema

‘Unaona eeh…nimegundua kitu kwenye hii mitambo, kule chumbani kwa mdada, ile kamera imevunjwa, na waya zimeharibiwa ni nani kafanya hiyo kazi, nahisi unalifahamu hilo..’sauti ya kiume

‘Mimi sijui..na mbona niliona ni taa tu imeharibika..’sauti ya kike

‘Mbona hujaniambi,..na ni nani alitengeneza..?’ akauliza

‘Ni yule yule fundi wetu, sasa vitu vidogo kama hivyo ni mpaka nikuambie au umenileta hapa kwa kazi..?’akaambiwa

‘Basi kwa ujinga wake…huyo fundi sijui lakini…atakuwa kaharibu zile waya za kamera…itabidi baadae niende kuifanya hiyo kazi mwenyewe…’sauti ya kiume.

‘Sawa..mimi sikulijua hilo…’akasema

‘Acha ujanja wako wewe, nakufahamu sana, wewe ni mnafikii …usifikiri mimi nakuaminii sana, hakuna kitu kama hicho,…sikiliza alichofanya huyo bosi wako hakiwezi kuniathiri kamwe, mweneywe utaona, najua kuna kitu kakipandikiza mahali, kama sio kwako basi kuna mbinu katumia, huko alipo anatusikiliza..’akasema

‘Mimi sijui hayo… na sizani kama kuna ukweli wa hilo, hawezi kufany ahivyo akijua kuwa mtoto wake yupo hatarini…’akasema mdada

‘Ni kweli, mimi sitasita kufanya lolote kwa mtoto wake, akijifanya mjanja,atakuja kujuta,…ngoja nione la kufanya..’sauti ikasema na mimi pale pale nikaharibu mawasiliano na kile kitufe kwahiyo hataweza kukigundua wapi kilipo. Hata akikigundua ataona kama kitenesi tu kisicho na uhai

Mimi pale nilipo, sikutaka kupoteza muda, kwa haraka nikachukua vitu vyangu, na kujiandaa kurudi chini, ili nikajiandae kwa ajili ya kwenda uwanja wa ndege, nilikuwa radhi sasa kufanya kama walivyotaka, kwa usalama wa mtoto wangu, sikuona kama kuna lolote zaidi, ilimradi nimepata uhakika wa usalama wa mtoto wangu.

Nilikaa kidogo pale chumbani, na ulipofika muda ambao ndege inayotoka huko inafika, akaja mtu kunichukua hadi uwanja wa ndege na kama walivyotaka ndivyo nilivyofanya…

Mzungumzaji hapo akatulia akimuangalia mwenyekiti na mwenyekiti alikuwa kimia, kama akiwaza jambo, na mdada akaendelea kuongea;

‘ Na yaliyokuja kuendelea hadi siku ile ya tukio ni kama nilivyowaambia awali..zaidi ni mambo ambayo sitakiwa kuyaongea hapa…maana hayo ni ya kazi za polisi, ila kama mwenyekiti ataruhusu hilo, kwa kibali cha polisi, kwanini tusiweke wazi, mnasemaje wajumbe

Mwenyekiti akatikisa kichwa kukataa.

*********
Mwenyekiti akachukua simu na kupiga namba akawa anaongea kidogo na huyo aliyempigia halafu akasema;

‘Je mume wa familia hayo yaliyoongelewa hadi hapo na huyu askari kanzu wenu au rafiki wa mke wako ni kweli,..unakubaliana nayo..?’ akauliza mwenyekiti na mume wa familia akabakia kimia

‘Natumai sasa kama wewe ni muungwana, na …mimi nakushangaa sana, hivi hadi hapo hujioni kuwa una makosa,…au wajumbe mnasemaje,..nilijua huyu mtu, utaungama nasisi kama familia, akiri kosa, na tuwe kitu kimoja ili kupambana na huyo adui yetu, eti jamani…’akasema mwenyekiti.

Mume wa familia akawa kimia tu, na wakili wake naye akawa kama anafungua makabrasha yake, hakusema neno.

‘Mume wa familia, tunaongea na wewe hapo sio sehemu ya wakili wako, maana ukweli sasa upo wazi, na muongeji aliyepita ni mtu wako wa karibu, na zaidi ya hayo ni mtaalamu wa upelelezi, unasemaje mume wa familia...?’ akauliza mwenyekiti, na mume wangu akatulia kimiya kama sio yeye aliyeulizwa na baadae wakili wake akawa anamuongelesha jambo, lakini mume wa familia akawa anatikisa kichwa kukataa.

Baadaye sana mume wa familia akasema;

‘Tatizo sio mimi kukubali hayo yaliyoongewa, au kukiri kosa, wangapi hadi hapo wana makosa, ni mimi tu mwenye makosa, hapana,… tatizo hapo ni huyo muongeaji, mengi kayaongea kutilia chumvi ili nionekane mimi ni mbaya, haya..si mumeshaona mimi ni mbaya, nina makosa, na wengine je, …mnataka mimi niseme nini hapo…’akasema

‘Tunataka wewe uthibitishe kwa kauli yako je hayo yaliyosemwa ni kweli au sio kweli, ili tuendelee..?’ akaulizwa

‘Kaongea mengi, kamuongea marehemu, kawaongelea watu wengi, na wengi ni kama mimi, kila mmoja ana makosa yake, hata yeye muongeaji ana makosa yake mengi , na mkumbue hayo aliyoyaongea nikipindi mimi nilikuwa mgonjwa, sasa mimi nitawezaje kukiri kosa wakati sikuwa na ufahamu…’akasema

‘Unajua hueleweki, ina maana muda wote alichokuwa akiongea muongeaji hakuwa na sisi, swali nakuuliza tena, haijalishi yaw engine je hayo yanayokuhus wewe ni y akweli au sio ya kweli, maana hapa kikao kipo kwa ajili ya familia yenu,…je ni kweli au si kweli labda nikuulize hivyo..?’ akaulizwa

‘Niwaambie ukweli wangu kutoka oyoni au sio, kwanza ..huyu mtu muongeaji kwanza mimi simuamini, ndio ni mtaalamu wa kupanga hoja, lakini hakuwahi kutoa ushahidi au shahidi wa yoet hayo aliyoyaongea, ni nani shahidi wa kumuunga mkono hayo, ndio mimi au sio…ndio mnataka mimi niwe shahidi wake,..lakini mjue jambo moja kuwa huyu mtu ni mnafiki mkubwa, msaliti, na hayo aliyoyasema…’akasema

‘Kwahiyo hayo aliyoongea sio ya kweli..?’ akaulizwa

‘Ndio mengi sio ya ukweli, yapo ya ukweli hayaana ubishi, lakini mengine kaongezea uwongo wake, na kafanya hivyo, kwa vile keshajua kuwa rafiki yake kamshitukia, na akaona njia ya kujikosha na kutunga huo uwongo,, ...na kwa uwongo wake huo, nitahakikisha, kuwa unawajibika,..’ akasema huku akiwa kamwangalia mwenyekiti, na baadaye akamgeukia rafiki yangu na kusema;

‘Wewe, unafikiri kwa kuongea hivyo, umesalimika, unajidanganya, hata siku moja tajiri hamuangalii masikini mara mbili, ukikosea ujue huna maana kwake, umechezea shilingi kwenye shimo la choo, umenisaliti na mimi…, na kwahiyo wewe huna maana kwao, na huna maana kwangu......kabisa huna maana kabisa...’akasema

Wajumbe walimuangalia kwa macho ya kushangaa na alipoona hivyo, haraka akisimama, na wakili wake akawa anamuangalia kwa alama ya kuuliza machoni, yeye hakujali hilo, akaanza kutembea kuelekea mlangoni, na watu wakabakia kimia tu, baadae kabla hajafika mlangoni mwenyekiti ndio akasema;

‘Mjumbe unajua unachokifanya ni kukidharau kikao, unakwenda wapi, wakati kikao hakijaisha, unanidharau hata mimi mwenyekiti...’akasema mwenyekiti,

‘Siwezi kuendelea kukaa hapa kuzalilika, kila mmoja aliyesimama ananisimanga mimi tu, wengine wana mabaya yao, hamtaki waambiwe, mnajua na mimi ninafahamu kiasi gani kuhusu mabaya ya wengine, kiukweli mimi siwezi kuvumilia tena, uwongo wenu umevuka mipaka najua kwa hivi sasa sina langu au sio, na mumejitahidi kuni dhalilisha, kunivua nguo sina thamani tena hapa..na ushahid upo wapi, eehe, niambieni...’akasema na kabla hajamaliza sauti ikatokea kutoka kwa mmoja wa wajumbe, ilikuwa sauti ndogo iliyochoka…’, ikisema;

‘Mimi ni shahidi wa hayo yaliyosemwa, ndugu mjumbe kabla hujaondoka, ningelipedna mimi kuyathibitisha hayo, aliyoongea mjumbe aliyepita...’ sauti hiyo ikasema na wakati huo wajumbe wengi walikuwa wakimuangalia mume wa familia, akitaak kutoka nje, na aliposikia sauti hiyo akasimama

Na wajumbe wote wakageuka kumuangalia huyo muongeaji mpya, ni nani, na hata mwenyekiti akafanya hivyo.

NB: Ni nani huyu tena, anataka kusema nini


WAZO LA LEO: Ni kawaida kwa binadamu, kulalamika, pale anapotendewa ubaya, lakini binadamu huyo huyo, akimtendea mwenzake anaona ni jambo la kawaida tu,...ni bahati mbaya, ni ibilisi, nk , sio vizuri tukijenga tabia hiyo, kwani sote ni binadamu hakuna mwenye moyo wa sugu, usiohisi maumivu, ndio maana wahenga wakasema mkuki ni kwa nguruwe,...
 
SEHEMU YA 110

Mwenyekiti akaangalia kule sauti ilipotokea, kwanza alihisi sauti ni ya mtu mwingine kabisa, kwani sauti ile ilikuwa ndogo zaidi tofauti na sauti liyotambulikana, na ilionekana ya kuchoka,.., lakini alipoangalia pale ilipotokea akafahamu huyo mtoa sauti ni nani…

Na kwa muda ule wajumbe wote walikuwa wamegeuze vichwa vyao, kumuangalia mume wa familia na sasa wakageuza vichwa kumuangalia huyo aliyetoa sauti, ili kuwa na uhakika kuwa ni yeye au ni sauti ya mtu mwingine, hata yule aliyekaa karibu naye alifanya hivyo. Ilikuwa sio sauti yake ya kawaida...

Na wakati huo huo, mume wa familia alikuwa bado kasimama kama kapigwa ganzi, kama kaamrishwa 'simama!' akatii..., akaganda, lakini bado akiwa katizama huko mlangoni, ni kama vile anatafakari sauti hiyo ni ya nani....

Mwenyekiti akakohoa halafu akasema;

‘Najua wewe ulitaka kuongea awali, nikakuzuia, ...ili mwenzako amalizie maelezo yake, na ingawaje bado kama alivyodai, lakini sio mbaya, ...'akatulia mwenyekiti akiteta na mke wake kidogo.

'Sio mbaya kama tutampa nafasi ... 'akasema akigeuka huku na kule

'Lakini niliona kabla ya kuendelea tufanye hicho nilichokitaka kwanza,...kupeana nafasi ya kukiri kosa, kutubu nk..., maana vyovyote iwavyo, sisi ni wanafamilia, sisi ni wanandugu, na zaidi ya hayo sisi sote ni wanadamu, tunatakiwa tusameheane, lakini utasamehewa vipi kama mwenyewe hujakiri kosa au sio..., ndio maana nikajaribu kumpa nafasi hiyo mume wa familia..’akasema mwenyekiti.

Mume wa familia alikuwa bado kaganda tu...

'Je mimi sikutimiza wajibu wangu..?' akauliza mwenyekiti na wajumbe wakaguna na ikawa kama sauti ya kuguna guna tu.., hakuna kilichosikika,

'Kiukweli nimelitimiza hilo, na nini kimetokea,..mumeona wenyewe, mume wa familia anataka kukimbia, kama alivyofanya mdogo wake, maji hufuata mkondo...'akasema na hapo wajumbe wakacheka kidogo

‘Lakini ndugu yangu mkwe wangu, mjumbe wa hiki kikao , mume wa familia,... hilo, unalotaka kulifanya unajisumbua bure, huwezi kuondoka hapa...'akasema mwenyekiti.

Hapo mume wa familia akageuka na kuanza kusema kwa hasira...

'Ninani anaweza kunizuia...mimi sio mfungwa, mimi sijashikiliwa na polisi hapa..mimi nipo hapa kwa hiari yangu mwenyewe, na ninaweza kuondoka kwa hiari yangu mwe-nye-we..'akasema mume wa familia, na mwenyekiti akageuka kumuangalia yule aliyetoa sauti, na hakusema neno, aliyesema neno ni huyu ...aliyetoa sauti awali.

'Mimi nitafanya hivyo, ...'sauti ikasema na mume wa familia akamgeukia kama kushtuka vile, lakini hakusema neno, alionyesha uso wa kutahayari tu, kama haamini hicho anachokisikia. Na huyo msemaji akasema;

'Ndugu mwenyekiti, huyu mtu hawezi kufanya mnavyotaka nyie, maana akifanya hivyo ndoto yake yote itayeyuka..nafahamu hilo, ...kiukweli kufanya hivyo inahitajia ujasiri, imani na utashi ulio sahihi, ukizingatia kuwa mikakati mingi ya miaka mingi ilishafanyika, na..kiukweli...hataweza kukiri kosa, ...'sauti ikasema.

'Kwanini..sijaelewa...?' akauliza mwenyekiti.

'Kwanini hawezi kufanya hivyo...eeh, kwanza anaogoa huenda atakiuka yale tuliyokubaliana mimi na yeye, lakini hilo sio kweli, ..' akatulia kidogo.

'Sio kweli kwa maana alishakiuka hayo tayari...hata hivyo, ukweli upo wazi, kama ingelikuwa ni mtu wa kutubu na kuomba msamaha angeshalifanya hilo mapema na mkewe...'akatulia

'Mimi nina imani mke wa familia kwa upendo wake na huruma zake angelimsamehe tu, nina uhakika na hilo, lakini wapi, sikio la kufa halisikii dawa, sasa labda, nasemea labda, huenda mwenzetu huyu bado anasubiria ushahidi, bado anajiamini kuwa hayo aliyoyafanya hakuna anayeweza kuyazuia,...

'Sasa kwa vile anahitajia mashahidi, basi mimi ni shahidi,..na akitaka ushahidi utatolewa, au sio ..’akasema huyo mzungumzaji mpya, akimuangalia muongeaji wa kwanza, na huyo muongeaji wa kwanza akatikisa kichwa kukubali.

Hapo sauti ya mume wa familia ikatokea sasa kwa jaziba, ikisema;







‘Ina maana hata wewe, unaungana na huyo mzandiki, ..hata wewe unataka kunisaliti mimi..' akasema sasa akiweka kidole mdomoni kama kuzuia kuongea zaidi...’

Sasa mume wa familia alikwua kasimama akiwaangalia wajumbe, lakini akiwa kainamisha kichwa chini. Na wajumbe wakasubiria kauli ya huyo mzungumzaji mpya ambaye bado alikuwa hajapewa kibali rasmi cha kuongea;

‘Rudi ukae mume wa familia, …’aliyesema sasa hivi alikuwa ni mwenyekiti, na mume wa familia akawa bado kasimama pale pale karibu na mlango, sio karibu ya kuweza kuushika ule mlango, lakini karibu ya kuukaribia, lakini akiwa kawageukiwa wajumbe.

‘Hiki kikao ni rasmi, na baada ya hiki kikao, kitakachofuatia ni polisi kufika hapa kufanya kazi yao, unavyokimbia hivyo unatupa wasiwasi, kuwa huenda ndio wewe unayetafutwa na polisi..’akasema mwenyekiti

‘Kwa kosa gani..?’ akauliza mume wa familia kama anashangaa, akawa anageuza kichwa kwa kujiiba kumuangalia mwenyekiti

‘Hilo swali watalijibu wao, hao polis sio mimi..mimi sijui..., ila kwa taarifa yao waliyotupatia ni hivyo, kuwa sisi sote tuliopo hapa kwenye hiki kikao tupo chini ya ulinzi, sikutaka kuwaambia hilo kabla ..hata tunavyozungumza hivi sasa, tunafuatilia kama nilivyowaambia awali, polisi wametuzingira,.. je unafahamu wapi alipo huyo mdogo wako aliyetoroka hapa na kukimbia,..?’ akaulizwa

‘S-s-sijui, ina maana wameshamkamata…?’ akauliza sasa akionyesha uso wa kushangaa na kama kuogopa fulani hivi

‘Na wewe ukitoka hapo nje, utafanyiwa hivyo hivyo, kwahiyo ni bora urudi ukae kwenye kiti chako ili uwe miongoni mwetu na hata likitokea la kukamatwa tutajua sisi ni wanafamilia kwahiyo tutaangalia jinsi gani ya kusaidiana kama wanafamilia…’akaambiwa

'Hahaha, kama wanafamilia, ...hahaha, usinione mimi kama mtoto mdogo mwenyekiti, hapa mnachotafuta ni ushahidi wa kutufunga, bila hata ya kutaka zaidi kutoka kwangu, ukweli halisi ninao mimi...mnazunguka tu,..nia ni nini, kuhakikisha nadidimia na kuzama kuzimu,...niende nikawa hohehahe kule kijijini, hiyo ndio furaha yako,..maana ukitaka kumuua mbwa kwanza si lazima umuite majina mabaya au sio, ndicho ulichokitaka, haya sasa fanya utakavyo,...'akasema akinyosha mikono kama ya kusalimu amri.

'Mjumbe usipoteze muda, maana hata useme nini, haya yatafanyika tu,..kikao kitaendelea na wewe utakuwepo, upende usipende, ukitaka kwa hiari yako,..sawa kakae, ila kama unataka nguvu itumike sawa ..sisi tutawaachia wenye mamlaka,...'akasema mwenyekiti.

'Haina haja ya nguvu ndugu mwenyekiti,...mwenyewe atakaa tu,kwasababu mimi ndiye mtu wake wa karibu, mimi ndiye ninayweza kumrejesha akae...sasa kama anataka kuondoka ondoke tuone,... uniache mimi nikamatwe na polis, si ndio pendo lake hilo, si ndivyo alivyotaka au sio, haya ondoka bwana...'akasema mzungumzaji

Sasa taratibu mume wa familia akageuka kuangalia mlangoni kama kweli anataka kuondoka, halafu akiwa kama anarudi kinyume nyume,...huku akiongea, kwa sauti ya huzuni akasema;

‘Kumbuka tulipotoka, kumbuka ahadi yetu, kumbuka mimi na wewe ni nani, usije kunisaliti tafadhali, nakuomba …’akasema..na sasa akiwa kageuka kumuangalia huyo mzungumzaji.

Mzungumzaji alikuwa kimia, na kitendo kile cha kukaa kimia, kilimfanya mume wa familia, sasa atembee kwa haraka hadi pale alipokaa huyo mzungumzaji mtarajiwa, ili mwendoo wa hatua kadhaa, maana zilikuwa za hasira kama vile anataka kwenda kufanya jambo.

Ili ufike pale kwa huyo mzungumzaji, inabidi umpite docta, kwahiyo alipofika pale alipokaa docta akasita, akageuza kichwa kumuangalia docta, na docta akawa anamuangalia, wakaangaliana, na docta akatikisa kichwa cha kusikitika, na mume wa familia, akainamisha kichwa chini, ..halafu baadae akainua kichwa na kusema;

'Samahani docta...'akasema hivyo, halafu akamgeukia huyo mzungumzaji..

‘Ni kweli hata wewe unataka kuungana na mzungumzaji wa kwanza, kuyathibitisha maneno yake ya uwongo, maneno aliyoyatunga ili kujihami,...au , hata siamini,…..?’ akauliza...hapo akiwa anazungumza kwa sauti ya chini, kama vile hataki wengine wasikie, lakini ni sauati ya kusikika na watu.

Mdada akatikisa kichwa kukubali.

Kutikisa kichwa huko kuashiria kukubali, kulimfanya mume wa familia kuinamisha kichwa upande, hakuweza kuamini hayo,…hakuamini huyo mdada anaweza kuwa kama alivyoita yeye, 'kumsaliti..', sasa wakawa wanaangaliana, mume wa familia, akasema;

‘Ina maana ni kweli, unataka kufanya hivyo,... hapana siamini haya, wamekupa nini hawa watu,....haiwezekani, usidanganyike mpe---'hapo akasita na kumuangalia docta, halafu akaendelea kuongea

'Hizo ni hadaa zao hao watu, hawatakujali baada ya hapa, nakuambia ukweli, na ilivyo, baada ya hapa huenda ukaishia jela, huenda mimi na wewe tukaishia jela, maana hata mimi najua hilo ...’akasema huku akionyesha uso wa kukata tamaa, na huzuni, lakini shahidi huyu mpya akasema;

‘Hapa sio swala la mimi kukusaliti, tatizo ni kwamba nyani haoni kundule,…na kama ni ubaya , ubaya huo umeuanza wewe, na haijalishi kama nitaongea au nitakaa kimiya, lakini ni bora niongee ili ukweli ujulikane kwa manufaa ya wengi, kabla mambo hayajaharibika zaidi, hawa ndio wataweza kutetea au kukuangamiza..’akasema shahidi huyo mpya.

Mume wa familia taratibu akarudi kwenye kiti chake na kukaa, alikaa karibu yangu na hakutaka hata kuniangalia mimi machoni, na aliyeweza kumsemesha alikuwa wakili wake akawa anamuongelesha jambo, yeye akamuashiria kwa mkono anyamaze, na wakili wake akafanya hivyo.

'Je mwenyekiti nianze...?' akauliza mzungumzaji, na mwenyekiti akaniangalia mimi, na kusema neno, mwenyekiti akatikisa kichwa kukubali, hakutoa sauti...

Mzungumzaji mpya akasema;

‘Naongea haya nikiwa nimeshaongea na mume wangu...kwahiyo nina kibali rasmi japokuwa awali alionekana kunizuia, alifanya hivyo, akiwa bado haamini, lakini baada ya haya mazungumzo, ataamini...haina shaka kwa hilo...’alianza kuongea mzungumzaji

‘Endelea kuongea na kuruhusu sasa rasmi,...nilikuwa napata ushauri kutoka kwa msaidizi wangu hapa... ila nakuomba kama alivyofanya mwenzako na wewe iwe hivyo hivyo, …’akasema mwenyekiti.

***********

‘Mhh…kama ni hivyo utanifanya nishindwe kufikisha ujumbe ninaotaka kuufikisha hapa, kiukamilifu wake, na kwa hivyo ukweli utashindwa kubainika, na mimi sitaki ukweli uje kupotoshwa na watu wengine hasa hao maadui wasionitakia mimi mema,...’akasema

‘Jitahidi kufanya hivyo …’akasema mwenyekiti.

‘Sawa nitajitahidi kufanya hivyo…’akasema shahidi

‘Mimi namwambia mume wa familia kuwa hatima yangu na mume wangu imeshajulikana, kwahiyo kwangu hakuna cha ajabu, tatizo ni yeye na mke wake..'akasema na sasa akamuangalia mume wa familia akisema

'Kama wewe umeshindwa kuukubali ukweli, kama wewe umeshindwa kukaa na mke wako mkaongea mmkayayamaliza, ukasubiria kitu kama hiki, ujue wewe una matatizo, tena matatizo makubwa,...maana haya yasingelijulikana na kila mtu,..na kwa kufanya hivyo, wewe unashinwa kuwajibika kama mume, na huo sio ujasiri,na huo sio upendo wa kweli..na kwahiyo , wewe ndiye msaliti wa kwanza…’akasema mzungumzaji na mwenyekiti akatabasamu.

‘Mimi nimeteseka sana, ..hujui ni kiasi gani nilivyoteseka, nimekuwa katika wakati mgumu sana, hujui tu, nimekuwa nikijiuliza je hili ninalofanya ni sahihi, unaishi na mume ndani hakufahamu, unawalinda watu hawakujali , unafanya mambo, kiukweli mimi…imekuwa ikiniumiza sana..’akasema

‘Sasa ni wakati wa kujitakasa, …'akasema akimuangalia mume wa familia, na mume a familia akawa sasa kakunja uso kuonyeha hasira.

'Mume wa familia hebu jiulize hivi haya mpaka lini, ..au bado ulikuwa na ndoto za ushindi,...kwanini tuendelee kuishi katika maisha haya ya sintofahamu, ya kudanganyana, maisha ya kuigiza, ...mimi bwana nimeamua, ni heri kusema ukweli, ili haki itendeke, hata kama nitakosa kila kitu, lakini nitakuwa nimepata kitu cha kudumu, ..ambacho ni haki na ukweli.

Mume wa familia hapo akainua kichwa na kumuangalia mzungumzaji halafu akageuka kwa mwenyekiti, halafu akainamisha kichwa chini hakuniangalia mimi bado.

‘Wewe unanifahamu sana mimi nilivyo, jinsi gani ninavyokupenda, unafahamu sana jinsi nilivyojitolea kwa ajili yako, jinsi gani nilivyoweza kuvumilia, na kuyafanya yale ambayo sikupenda kuyafanya yote hayo niliyafanya kwa ajili yako..’akatulia

‘Hata huko kujizalilisha nilifanya hivyo kwa ajili yako kukulinda wewe na familia yako.., hebu niambie ni mapenzi gani unayoyataka,kutoka kwangu, je mimi ni tofauti na hawo wanawake wote uliwahi kutembea nao…’akawa kama anajiuliza

‘Sio lazima unijibu, lakini ukweli upo wazi, ..lakini kwanini, je ina maana mimi sikutakiwa nipate raha, sikutakiwa niwe na amani, ina maana mimi sio binadamu kamilifu,..na zaidi ina maana mimi ni nani kwako!...’hapo akatulia

Mume wa familia akageuza kichwa na kumuangalia muongeaji, sasa wakawa wanaangaliana, na muongeaji akaendelea kuongea…

‘Au ina maana mimi ni njia ya kufanikisha starehe zako tu…, hapana, nasema sasa iwe basi, iwavyo na iwe, na kama kweli ulinipenda kwa ukweli basi turudi kijijini, tukaanze maisha mapya, kama hilo litawezekana,..lakini haliwezekani au sio,..unajua ni kwanini haliwezekani, su sio.......’akatulia na wakawa wanaangaliana.

Mume wa familia akasema;

‘Sikiliza, sikiliza mpendwa,...usiendelee tafadhali, unajua jinsi gani unavyonitesa moyoni…unayoongea hapa hayataweza kukusaidia wewe au mimi, hayo sana sana yanazidi kutuumbua tu, na hayo ni furaha ya mkizi…’akasema mume wa familia.

‘Mimi ninajua ninachokifanya, na nafahamu njia sahihi ya kunifanya mimi niwe na amani ni kusema huu ukweli,…’akasema mdada.

‘Hahaha, ukweli, haya fungua hilo bakuli uone kama utafanikiwa...unawafahamu hawa watu, unavyoongea hivyo unawapa faida, ya kutufukuzilia mbali, haya utaondoka na nini sasa, wao wanachotaka ni ....uwaambie huo wanaouita ni ukweli, ili wapate ushahidi, na mwisho wa siku waweze kutumia huo ushahidi kukutimua, au kukutia kitanzini…’akasema mume wa familia

‘Kwangu mimi siogopi kutiwa kitanzi, au kukosa haki yoyote, mimi nina imani kama nina haki yangu hiyo haki nitakuja kuipata tu, lakini sio nitumie ujanja kuipata wakati haijatambulikana kuwa ni haki yangu, ni kweli ujana na utoto ulitudanganya sana, na sote tulikuwa na ndoto hiyo, lakini kwa jinsi umri unavyokwenda, tunajifunza.

‘Namshukuru sana bosi wangu na wale wote walionijenga, wakanisomesha wakanifanya nibadilike na kuujua ukweli wa maisha,..nashindwa kuelewa kwanini wewe mwenzangu ulisoma na bado hukubadilika, ina maana hiyo elimu ilikusaidia nini, maana wewe umesoma au sio..., na sio elimu ndogo, hiyo elimu yako imekufundisha nini, kwanini uhadaike, kwanini ukubali kudanganywa, hapana mimi siwezi kurudia uchafu.

‘Sasa sikiliza wewe mume wa familia,… hakuna ukweli zaidi ya ukweli unaoufahamu wewe mwenyewe, ukweli ni mkataba wako wewe na mwenyezimungu wako,…jiulize hayo unayoyafanya ni sahihi, je ungelifanyiwa wewe ungelifurahi, ..ukifika hapo kama ni muungwana utageuka nyuma,.....’akasema.

‘Siamini…’akasema mume wa familia

‘Huwezi kuamini, maana mimi sio yule mdada wa kijijini tena, japokuwa moyo wangu wa upendo kwako upo pale pale,…ninachoweza kukuambia ni hivi, mimi sitaki chochote kutoka kwao, nimerizika na maisha yangu na umasikini wangu, ninajua ni vipi nitapata halali yangu, na kazi niliyotaka kuifanya nimemaliza, …’akatulia

'Hahaha, utaimalizia jela...'akasema mume wa familia akicheka kwa kukata tamaa

‘Tatizo hunifahamu mimi ni nani kwa sasa, mimi siogopi kwenda jela, kama kweli nilitenda kosa na likadhihirika kuwa ni kosa, kwanini niogope kwenda jela, ….kama niliogopa kwenda jela kwanni nilifanya hayo yanayompeleka mtu jela, huo ndio unafiki, …uliousema wewe..sasa je mimi na wewe, ni nani anatakwia kuitwa hivyo.

‘Sikiliza wewe mtu, baada ya kusikia hayo yote uliyoyafanya wewe, ambayo nilikuwa nayasikia tu, sikuwa nimeyafuatilia kabla, sio kwamba nilishindwa kufanya hivyo hapana, muda ulikuwa hautoshi tu, kuwalinda, na kuyafanya hayo ya kuhakiki ukweli huo,..kwa namna nyingine, nilijua ni katika kuyaweka maisha yako yawe bora zaidi, lakini ya kwako yamezidi mpaka,..’akatulia


‘Je uliyafanya kwa mujibi wa kazi yako, hapana, je uliyafanya kwa nia njema ya kuinua maisha yako na katika kufanya hivyo, ilibidi ifanyike hivyo, kwa nia njema hapana, je ulifanya hayo kwa vipi basi, jibu rahisi ni tamaa, au utasingizia nini…kiukweli umeniumiza sana…’akamuangalia mume wa familia

‘Hivi wewe upoje, unadiriki hadi kubaka bint wako wa kazi, unamfahamu vyema yule binti, amatokea wapi, ..binti wa watu alikuwa akihitajia sana msaada wenu, jamani, yule sio sawa na, na…binti yako, je hayo yangelitokea kwa bint yako ungelifurahia, kiukweli kitendi hicho kimeniuma sana…

‘Sasa mambo kama hayo mimi nikae kimia tu, niendelee kuumia tu moyoni, sawa, labda utasema mbona wewe umefanya hivi na vile, ..mimi niliyoyafanya ni katika uwajibikaji wangu, kazi zangu…na kila jambo naweza kulitetea kuwa nililifanya kwa minajili gani..japokuwa nimekiuka sheria za ndoa, na hayo nimeshaongea na mume wangu.

Je wewe uliwahi kukaa na mke wako ukamuelezea yote, ukweli, kwanini unayafanya hayo, au ulimtegemea marehemu ndio akuongoze au sio, haya keshakuongoza, sasa hivi hayupo duniani, utamtegemea nani sasa...ni huyo wakili wako, hizo pesa zako..kiukweli hadi hapa ni lazima niuseme ukweli wote..na mke wako ataamua, lakini ukweli ni ukweli tu....’akatulia kidogo, akimuangalia mke wa familia.

‘Mke wa familia kwanza nikuombe msamaha kwa haya yote yaliyotokea , pamoja na hayo, mimi nimekuwa nikifanya kazi zako kwa kupitia kwa …rafiki yako, nimekuwa mtiifu kwako, bila hata ya wewe kunifahamu, ..na zaidi hata mume wangu mwenyewe alikuwa hajui hilo..'akatulia

'Nia na madhumuni yangu ilikuwa kukulinda wewe na mabaya, kwa vile wewe unaishi na mtu ninayempenda, sikutaka nyia kama familia yake yawakute mabaya, ndio ilikuwa kazi yangu, na katika kufanikisha hayo nilipitia changamoto nyingi tu,..kuna muda nakaa nalia,..siolii machozi, nalia ndani ya nafsi yangu.....je huo wema ni nani anaufahamu..’akatulia akigeuka kumuangalia mwenyekiti

Halafu ndio akamgeukia mume wa familia, mume wa familia bado alikuwa akimuangalia mdada huyo kwa mshangao, kama haamini hayo …

‘ Mimi nilishakuambia toka awali, njia tunayopitia sio sahihi, ukanikatalia, ukamsikiliza marehemu, ukisema yeye ni msomi anayeona mbali, je hicho alichofanya ndio kuona mbali huko,...'akasema

Mume wa familia akanyosha mkono kama kumzuia, na yeye akasema

'Usinizui,... naanza kuelezea sasa, je kuna haja ya kuyaficha haya, hapana ni lazima kila kitu kiwe wazi, unasikia wewe mume wa familia, ...?’ akawa kama anauliza lakini ilionekana kuwa hakutaka kujibiwa akaendelea kusema;

‘Mimi nilitumai kuwa umeshajifunza, kwa hayo yaliyotokea, kama kweli ulikuwa na nia njema, kama sio kunitumia, nichakae,na baadaye uendelee kuzaa na wanawake wa kila namna.Kama kweli unanipenda…sasa nakuambia hivi.., turudi kwetu kijijini tukajipange upya, tuachane na maisha yasiyona mpangilio..’akasema na mume wa familia akatikisa kichwa kama kukataa.

‘Unaona eeh, unakataa, kwanini…, hebu angalia, alichokuwa akikihangaika Makabrasha kipo wapi, kapata nini na sasa yupo wapi sasa hivi..,je wewe una uhakika gani na maisha ya kesho na kesho kutwa, kuwa wewe utakuwa mjanja kuliko huyo aliyemkatiza maisha huyo mtaalamu wako, kama ni mtaalamu kweli mbona kashindwa kutetea uhai wake ...’akatulia akiwa anamwangalia mume wangu.

‘Mimi nimechoka, siwezi tena kuvumilia, siwezi tena kutumikia watu.., yaliyotokea yametokea, na yaliyofanyika yamefanyika, hakuna faida iliyopatikana, sana sana ni kujiweka kwenye maisha ya utata....mimi na mume wangu tumeshaelewana, na anajua ni nini cha kufanya, baada ya hapa, anaweza kutoa kauli yake au vyovyote atakavyotaka, mimi sio stahili yake, ...akubali sikubali huo ndio ukweli,....’akageuka kumwangalia mume wake

Mume wake alikuwa kainamisha kichwa chini tu, na taratibu muongeaji huyo akamshika mgongoni docta, na docta akashtuka ni kama vile alikuwa mbali kabisa.

‘Pole sana docta,..unisamehe tu…’akasema hivyo na hapo docta akainua kichwa na kumuangalia muongeaji, lakini hakusema neno.

********

‘Hivi ni nani anaweza kuyafanya haya yote niliyoyafanya, wakati mwenzake, anastarehe, na wanawake tofauti-tofauti, anazaa watoto, mimi mpaka sasa sina mtoto hata mmoja, eti kutimiza ahadi na mipango isiyofikilika, hivi ni nani, ataweza kuvumilia hayo yote uliyoyafanya mimi kuwalinda wana ndoa hao huku roho ikiniuma

Hahaha…, ina maana mimi nimeumbwa na moyo wa jiwe, niweze kuyavumilia hayo yote, sina wivu, sina tamaa, … je hivyo ndivyo tulivyokubaliana mimi na wewe mume wa familia, tulikubaliana kila mtu aaishi na mwenza wake kwa heshima na adabu mengine tumuachie mungu au sio...’akamwangalia mume wa familia, ambaye alikuwa naye amemwangalia kwa macho ya kukata tamaa.

Mume wa familia akageuka kuwaangalia watu, na akiwa kama vile mtu anayeogopa au kutaka kukimbia, aligeuka huku na kule, halafu akamwangalia muongeaji na kwa sauti ya unyonge akasema;

‘Sikiliza nikuambie, hapo panatosha usiendelee, utania kwa kihoro, kwanini unarudia rudia huko…haya yatakwisha tu, na mambo yatakuwa sawa, usiogope vitisho vya hawa watu, usilainike kwa propaganda zao, mbona mambo yapo shwari tu,...’akasema

‘Hahaha bao tu unajidanganya au sio, nimerudia rudia haya ili yakuguse ili usema imetosha, nakiri kosa, nimejirudi, kumbe naongea na jiwe…’akasema mdada

‘Wewe nisikilize kwanza, usianze kuongea ovyo....utaumbuka, watakufunga hawa watu, hawana ubinadamu hawa.....’akaongea na kukatiza maneno ni kama vile kaongea sichokuwa kakidhamiria kukiongea.

Na mara mjamaa akasimama, sasa akatembea hadi pale aliposimama huyo mdada muongeaji, akanyosha mkono kumshika huyo mdada mkono, na kusema;

‘Haya simama twende tukaongea kwanza mimi na wewe, tuyamalize haya mambo, ukiendelea kuongea hapa, utaharibu kila kitu..’akasema

Mwenyekiti wakati huo alikuwa akiangalia matendo hayo kama anaangalia picha ya kuigiza, huku akitabasamu au kutikisa kichwa, hakutaka kuingilia kwanza.

‘Sikiliza mtu wangu,…mimi na wewe tumetoka mbali, ina maana yale yote tuliyowahi kupanga ndio iwe mwisho wake hivi..tutakwendaje kijijini, tutaishije huko, kwanza mimi ni mume wa mtu, wewe ni mke wa mtu, hulijui hilo, tulia na maisha yaendelee..’akasema mume wa familia, ni kama vile kachanganyikiwa.

‘Nimesema nipo tayari kuthibitisha hayo aliyoongea mwenzangu, kwani mimi ndiye niliyekuwepo toka mwanzo hadi mwisho wa mipango yote hiyo, japokuwa sio kwa kuitunga, lakini kwa kutumiwa.Mimi nafahamu mipango yote toka kijijini hadi kuja hapa Dar, mimi namfahamu marehemu, kuliko mtu yoyoye humu ndani, na mimi namfahamu mume wa familia kuliko watu yoyote humu ndani, kwahiyo mimi nawajibika kulimaliza hili jambo moja kwa moja, ...’akasema

‘Mume wa familia tafadhali rudi kwenye kiti chako, tusipotezeane muda..’hiyo sasa ilikuwa kauli ya mwenyekiti, na mume wa familia akiwa kakata tamaa akageuka kumuangalia mwenyekiti, na hakutaka hata kuniangalia mimi.

Mwenyekiti akawa anawaangalia wawili hao kwa hamasa kubwa, alikuwa akitaka kusikia mengi kutoka kwa huyo muongeaji, na alifahamu huyo shahidi ataongea kile alichotaka kukusikia, na iwe mwisho wa kikao, wamalize kazi
.
Mume wa familia akanyosha mkono kutaka kumshika huyo muongeaji, lakini huyo muongeaji, akauona ule mkono na kuusukuma mbali na..na hapo mume wa familia,akasema kwa sauti ya ukali;

‘Hivi wewe umechanganyikiwa unataka kuwapa nini hawa watu faida, unataka kujizalilisha au kunizalilisha mimi, hayo yaliyosemwa bado hayatoshi ....’akasema mume wangu akimsogelea huyo muongeaji, na muongeaji akamsukuma pembeni, na kumwangalia mwenyekiti, kama vile anaomba msaada, na mwenyekiti akasema;

‘Mume wa familia, nimeshakuamuru, urudi sehemu yako, ....mpe nafasi shahidi wetu asema ukweli, tumekupatia sana wewe nafasi uongee lakini ukakaidi, kwa sasa hivi huna mamlaka ya kumzuia shahidi wetu huyo…’akasema mwenyekiti.

‘Mwenyekiti nilikuwa naomba nafasi tuongee na huyu mtu kabla hajaanza kuongea, tafadhali..’akasema akiwa kama anaomba.

‘Nafasi hiyo haipo tena, huyu sasa hivi ni shahidi wa muongeaji aliyetangulia, wewe si ulitaka shahidi na ushahidi, sasa subiria huo ushahidi ufanye kazi…kwa hivi sasa tunachohitajia ni ushahidi wa ukweli uliotanguliwa kuelezewa, hata ukijaribu kumzuia haitasiaidia kitu, mimi namfahamu yeye kama ninavyokufahamu wewe, kwahiyo sogea pembeni, muachae mwenzako aongee....’akasema mwenyekiti.

Mume wa familia, akabakia akiwa kaduwaa, hakujua afanye nini tena, akakaa kwenye kiti kilichokuwa karibu na huyo muongeaji, hakurudi kwenye kiti chake, akawa kaka huku kainamisha kichwa chini kama alivyokuwa kainamisha kichwa rafiki yake docta, ..

********

‘Kila jambo lina mwanzo na mwsho wake, mimi nimeona mwisho wa haya yote ni hapa, na hakuna jingine ila nikuelezea ukweli, na nyie mtaamua ,mtakalolifanya....’akasema muongeaji.

‘Lakini ndugu mwenyekiti mimi nawaomba , muwe makini na mamauzi yenu, msikimbilie polisi,, kama mtakimbilia polisi, mnaweza msifanikiwe, kwani huko kote niliwahi kupitia, nikakatishwa tamaa, ndio maana nikaamua kufanya nionavyo mimi, na sitaweza kuacha kuusema huu ukweli kwenu, hata kama nitakuwa nimekiuka utaratibu wa polisi....’akasema.

‘Ili kupata ukweli,na kumlinda yule asiyependeka, nilijitolea maisha yangu, hata kuzalilika,.., nikaamua kuwa na adui yangu, uso kwa uso, hata kulala naye kitanda kimoja, ili niupate huo ukweli, hii ni moja ya kazi zangu msije kunidhania vibaya, wanaojua ukweli wa kazi zangu hawataniona ni mtu wa ajabu,…haha, samahani kwa kauli hiyo,...eti kumlinda mpenzi wangu, jamani, ....hivi ni binadamu gani angaliweza kuyafanya haya yote, kwa ajili ya mtu kama huyu...nimakata tamaa, ndio maana nimeamua niseme ukweli, ili jamii isikie, na watakaojifunza wajifunze, ..’akasema

‘Hapa nilipo natafutwa na polis, ndio mimi natafutwa na polisi au sio, sitafutwi na polis tu,, ..bali hata wale wanaotaka ukweli huu usilijulikane,..na mimi ushaidi wangu nitaugawa sehemu mbili, kama alivyofanya mwenzangu aliyetangulia

‘Sehemu ya kwanza ni lazima nielezee historia na chimbuko la haya, na pili, jinsi mauaji ya ya amrehemu yalivyofanyika, haya ni lazima niyaelezee ili haki itendeke, ni kazi kwako wewe mtetezi wa wanyonge ulifanye hili kama kweli ndivyo ulivyo,....’akasema na kumuangalia mwenyekiti.

Mwenyekiti akwa anamuangalia huyu muonegaji bila kusema neno.

Aliposema hivyo mume wa familai akainua kichwa na kumwangalia huyu mdada, kwa uso uliokata tamaa, lakini hapo hapo akionyesha ishara ya chuki..lakini hakwua na jinsi, afanye nini sasa….

‘Kwanini niwaaambie nyie, badala ya kwenda polisi, ...kwasababu, jamii ndiyo inahitajia ukweli kwanza, na sheria, itachukua mkondo wake, baadaye, kama watathibitisha kuwa mimi ni mkosaji sawa…’akatulia hapo

‘Mimi nina-amini jamii ndio yenye mamlaka,na ukificha ukweli kwao, unaikosea, na bora kusema ukweli kwa wale uliowakosea, kuliko kuiacha sheria ambayo huenda, ikakutaka ufiche ukweli, sheria ambayo wakati mwingine wenye mali wanaweza kupata mawakili wakafanya haki iwe batili, watendaji ambao wanaojali masilahi zaidi kuliko haki, nawaogopa sana hao watu....’akatulia.

‘Kuna watu wananitafuta ili waniue,...ili siri isivuje, ili ukweli usiwe bayana, na hata hii ajenda ya kusema maswala ya mauaji ya Makabrasha yasiongelewe hapa, ni moja ya ajenda zao,…hamjui tu…’akasema na mwenyekiti akatikisa kichwa kama kukataa hilo.

‘Sasa kwanini tufiche ukweli, kwanini kama familia tusiuone huo ukweli, ili mwisho wa siku kila mtu atoke hapa akiwa huru, kwanini tusujue ukweli ili familia zilizofarakana ziwe na amani, ili wenye haki wapate haki yao, na wenye kuwajibika wakawajibike..’akatulia
Mfano mnzuri ni kwa huyo kijana wetu aliyetaka kuusema ukweli hapa, hamjui ni kwanini alikimbia, ..aliona hata angelisema ukweli wote msingelimuamini, maana mumeshahukumu kutokana na propaganda za aliopanga haya yote yatokee, lakini atakimbilia wapi, eeh, niambie, najua baada ya hapa wengine tutaandamwa, lakini mpaka lini,....’akatulia huku akiwa kamwangalia mwenyekiti, na mwenyekiti akawa anamwangalia bila kupepesa macho,

‘Ndugu mwenyekiti, mimi ndiye mpenzi wa asili wa mume wa familia...’aliposema hivyo watu wakahema, na wengine wakaguna. Najua wengi walikuwa wakijiuliza hilo au wakitaka waupate ukweli halisi, ukweli ndio huo…

‘Mume wangu alikuwa halifahamu hilo, kiundani wake, na huenda yalitokea hivyo wengine watafaikiria kuwa huenda yaliyotokea yalifanyika kama kulipizana kisasi, kati ya mume wa familia na rafiki yake, hayo wanayajua hao watakaoongea hivyo, lakini undani wa hayo yote ulikuwa kati yangu mimi na huyu bwana hapa..mume wa familia. ...’akasema na kugeuka kumwangalia mume wa familia ambaye alikuwa hataki hata kumwangalia.

‘Nafahamu, kikweli kuwa wazazi wa familia ya mke wa familia, wanatufahamu sana, lakini sio kiundani kihivyo, wao wanatufahamu kutokana na historia za mababa zetu, na walijua kuwa hata sisi hatutaweza kubadilika, au sio..

Yawezekana kutokana na hulka ya mtu, kiukweli hata ndoa yangu na docta haikubarikiwa kivile, hata upande wa mume wa familia ilikuwa hivyo hivyo tu, na wahanga wa haya ni watu wasio na hatia kama mke wa familia na docta..wao walitaka kubadili hilo kuwa yawezekana, kuwa watu wanaweza kubadilika, sasa je yawezekana hilo……….’akasema na kuinama chini kama anayesoma kitu.

Wengi wanajiuliza ni kwanin matajiri wasitake watoto wao kuolewa na masikini, ni kwanini..kiukweli hii sio halali, upendo wa kweli hauangaliii maisha ya kifedha, ...umasikini kisiwe kikwaza ya kuwanyima watu haki zao, za kupendana, ..’akatulia

Naombeni msinichoke maana baada ya hapa huenda tusikutane tena, huenda mtaniona kwenye kizimba cha mahakama, au mtanisikia nimefungwa au..nimeuliwa yote yawezekana maana sisi kama sisi hatuna haki,..toka lini masikini akawa na haki…mmh. Nina imani kama isingelikuwa hizo ajenda za siri, kuwa kuna watu walikuwa wakilisubiria hili , ili wapike fitina na kufanikisha malengo yao huenda maisha yanegliendelea…. Mimi na mume wangu tungelikuwa tunaishi kwa raha na amani....

Sasa ni hivii, ngoja niwaambie kidogo historia za maisha yangu yalipotokea…
**********

‘Mimi na mwenzangu tumezaliwa kwenye familia za kimasikini, familia duni, iliyogubikwa na mitihani ya kila namna, sitaweza kuisema , ila ninachoweza kusema hapa ni kuwa mimi natoka kijiji karibu na kijiji cha mume wa familia, wote mnalifahamu hilo, na familia zetu ni zile familia zalili sana huko kijijini.

Na huena ndizo familia za kutolewa mifano, kuwa ni familia duni, zalili , enye tabia mbaya,…ni nani angakubali kuolewa au kuoa kwenye familia kama hizo, inayobakia ni ndoto za Alianacha, kuwa siku moja nitamuoa, au kuolewa na binti mfalme, au mtoto wa mfalme,...na ndio ilikuwa ndoto yangu na mwenzangu!

‘Lakini kwa mipango iliyopangwa, na makubaliano, kati yangu na mwenza wangu, tukajikuta sote tukiingia kwenye familia zenye uwezo, kutokana na zile njozi zetu,.. japokuwa kiundani mimi na mwenzangu tunapendana sana, pendo la asili, ambalo tuliwahi kulifunga kwenye handaki la umasikini....baada ya kuvikana pete ya uzalili, na umasikini, tulikaa na kujadili hili, hivi sisi mpaka lini.

Mjadala ulikuwa wa kulalamika, ...ina maana sisi tutakuja kuishi kama walivyoishi wazazi wetu, ina maana watoto wetu watakuja kuzalilika, na kuishi maisha ya umasikini kama tulivyourithi kwa wazazi wetu, tukasema hapana, ..

Hapana sasa tufanyeja wakati kweli tunapendana,..tufanye nini ili nafsi zetu zije kufurahia, tukaota ndoto, tukamuomba mungu, …tukasubiria ndoto hiyo ya aalinacha,.....oh..’hapo akatulia kwa muda akiwa kainamisha kichwa chini kama anawaza jambo, na alipoinua kichwa machozi yalionekana machoni, akasema;.

‘Samahani mimi sio mtu wa kulia lia ovyo, huwa nalia moyoni, na ukiona machozi yananitoka usoni, ujue kuna jambo nzito kuliko uzito wenyewe,..haya yamenitoka tu kwa bahati mbaya,...hayatarudia tena...’akasema na kufuta yale machozi, akaendelea kuongea;

‘Tulijadili sana, jinsi gani ya kuwapata matajiri, je inawezekana kweli, mimi niolewe na tajiri, utawezaje kumshawishi tajiri kuja kunioa mimi, au utawezaje kumshawishi binti wa geti kali kuja kuolewa na mlalahoi kama mwenzangu alivyokuwa...huwezi kulazimisha pendo, au sio, lakini bahati nzuri ikatokea kama dhamira zetu zilivyokuwa, kila mmoja akapata tarajio lake kwa nyakati tofauti, huena ilitokea hivyo ili iwe sababu ya watu kujifunza....

‘Wa kwanza kumpata mwenza ilikuwa ni mimi, nikampata mume mwenye uwezo, na nikamwambia mwenzangu kuwa nimempata mume mwenye uwezo sasa tufanya nini,..’akageuka kumuangalia mume wa familia.

‘Mwenzangu akapagawa na kukasirika, wivu ukamjaa, siunawafahamu wanaume kwa wivu, akasema haiwezekani, akawa kasahau makubaliani yetu, na wakati tunapingana, tukiwa tumenuniana siku mbili tatu,, mwenzangu akiwa hataki hata kuongea na mimi akakutana na binti wa kitajiri kwa mazingira yaliyokwisha kuelezewa huko nyuma..wakajikuta wame...mtamalizia wenyewe..’akacheka kidogo.

Haraka akaja kwangu na kuniambia kuwa hata yeye kampata mwanamke, tajiri, kwahiyo tupange mipango yetu,....mwenzangu kwa haraka, akamwelezea mshauri wake…mnamfahamu eeh…?’ akauliza na ajumbe wakaguna tu.

‘Mshauri wake, ni jamaa mmoja msomi, kijiji kizima wanamfahamu msomi wa hadi nje ya nchi. Na huyo jamaa alipoambiwa hivyo, akamwambia mwenzangu ampe huyo jamaa muda wa kulifanyia hilo kazi. Akalisafiria hatujui huko alifanya nini, alikutana na nani, …alipokuja akaongea na mume wa familia, walichoongea wanakifahamu wenyewe.

Basi siku yake akatuita, na kutuweka kikao, akasema;

‘Mnafahamu hiyi ni bahati kubwa sana, sasa umasikini bai-bai, kama mtafuata masharti yangu, mtafanikiwa lakini mkiwa wajinga, makajikanganya kuwa ..ooh, nimeolewa, ooh, nimemuoa, tajiri, mtakufa na umasikini wenu, kaeni mkijua kwa tajiri hakuna urafiki wa kudumu...’hiyo ilikuwa kauli ya huyo mshauri wetu, nikaona hapo tumefika.

Sasa ngojeni kuna mambo yanafanyiwa kazi, ..hiki ni kipindi cha kujiandaa na kampeni, kwahiyo tuvute muda kwanza, mimi nikajiuliza kampeni na mapenzi yetu yanahusikanaje,…sikumuuliza ila tulimkubalia tu..

Baada ya muda akasema anasafiri na akija atakuja na mambo mazuri, na pesa za maandalizi ya harudi, ili na sisi tuonekane tumeolewa, au kuoa, sio kuchukuliwa kama mzigo tu..tukakubali, …

Baada ya siku mbili, huyo mshauri akaja na mikakati ya jinsi gani ya kufanya....

NB: Tuishie hapa kwa muda

WAZO LA LEO: Ukweli unauma, lakini ukweli ni njia ya kujisafishia njia ya uhalali wa mafanikio, tusiogope kuongea ukweli hata kama katika kuongea huo ukweli utajiumiza hata wewe mwenyewe. Ukweli ni haki, na haki yataka ukweli.
 
SEHEMU YA 111

Kiukweli kipindi hicho nilikuwa na furaha sana, furaha ya kuwa naolewa kwenda kuishi mjini na mtu mwenye uwezo, kwa muda fulani sikufikiria sana mapenzi yangu na mwenzangu, akili hiyo ilinitoka kidogo.

Lakini kabla ya hapo, nilikuwa nimekutana na mdada mmoja, ilikuwa ni bahati, tu,…nataka kulielezea hili najua wengi wanajiuliza ni kwa vipi nikawa nafanya kazi hiyo hatari ya upelelezi.

Nahisi ilikuwa imepangwa iwe hivyo…, unajua mwenyezimungu humkadiria kila mtu na namna yake ya kutokea, riziki imepangwa hivyo, japokuwa ni muhimu kutafuta sababu, lakini iwe na uhalali fulani, ..siku moja alitokea kibaka, akamkwapua dada mmoja mgeni, sijawahi kumuona huyo mdada kabla,..ulikuwa mkubwa mnzuri, na kiukweli nihisi utakuwa na vitu vya thamani kama sio pesa.

Pamoja na maisha ya umasikini pale kijijini, mimi niliwachukia sana wezi,…basi yule kibaka alipomkwapua huyo mdada, akaanza kukimbia, akanipita mimi, nikaingiwa na hamasa, kwanini nisifanye jambo, kwanini watu hawaangaiki kumkimbiza yule mwizi, hapana lazima na mimi nifanye jambo

Nikaanza kumkimbiza, sasa watu wakawa wanaangalia kwa hamasa, mimi kama mwanake nitafanya nini…na huyo kibaka ni mwanaume, na mwanaume kweli, anavyooneka, ana nguvu,…kiukweli kama angejizatiti, nisingeliweza kupambana naye kwa uonekano wa hivi hivi, lakini nilijiamini.

Kwa kukimbia mimi sio mchezo,…, yule kibaka alipoona aliyekuwa akimkimbiza nyuma yake ni mwanamke, mdada tu,…akasimama

‘We mdada unataka kuumia…’akaniambia nilimpomkaribia

‘Nipe huo mkoba wa watu, na wewe uwe salama, usitutie aibu hapa kijijini ..’nikasema

‘Hahaha, kwanza mkoba sio wako , pili wewe ni mwanamke tu, huwezi kunifanya chochote na tatizo lako, hujui unayepambana naye, unajileta hadi huku,..kwenye mikono ya fisi utajuta kufanya…’akasema, sasa akiniangalia kwa macho mengine ya kutaka kufanya baya kwangu.

Nikawa nimeshamkaribia, hakuelewa kabisa malengo yangu, yeye akawa sasa kazarau, kasimama, ananiangalia mimi nitafanya nini kwanza, … hakuamini, maana nilichomoka kwa kasi na kuudaka ule mkoba mkononi mwake, na kuanza kukimbia, kuelekea mbele, na hata alipojaribu kunifuata hakuweza kunipata.

Baadae mbele nikageuza na kurudi kule kituoni na kumkuta huyo mdada aliyeibiwa mkoba bado kashikwa na bumbuwazi, nahisi kulikuwa na vitu vya thamani sana, nikamkabidhi mkoba wake, hakuamini, alisema

‘Oh, umewezaje wewe au…’aliishia hivyo, nikajua labda kahisi kuwa mimi ni miongoni mwa huyo mtu.

‘Uwe makini sana maeneo haya, …kuna vibaka..’nikasema

Na mara kwa mbali nikamuona yule jamaa akija,hakuogopa kurudi tena hakujali, nahisi maeneo ya pale wanamuogopa sana, sasa …alipofika pale akataka kunivamia mimi, kabla hata hajaniwahi mimi, akajikuta akipambana na huyo mdada, ilikuwa dakika mbili hivi, ..yule kibaka akawa kalala kwenye vumbi, mdomo unatoa damu, ilibaki historia.

Mimi pale nilipo nikawa na hamasa ya ajabu, alifanyaje, aliwezaje kumviringa na kumbamiza mwanaume yule …hadi jamaa akasalimu amri, nikawa najaribu kufanya kama yeye,..wakati huo watu wamejaa sasa..

‘Mwizi mwizi..sasa hata wale waliokuwa na hasira na huyo mtu wakawa wanatoa hasira zake, yule mwizi alipigwa na alikuja kuokolewa na mgambo wa kijiji..

Kiukweli tendo lile likawa mwanzo wa kunibadili, pale pale nilimuambia huyo mdada, wakati akiwa ananishukuru kwa kuweza kumuokolea huo mkoba , mimi nilisema tu

‘Napenda sana niwe kama wewe..’nilitamka hivyo tu, na huyo mdada akasema

‘Ombi lako limefika kwenyewe,..’akasema

Ni kweli kumbe huyo mdada alikuwa na ziara yake maalumu na katika harakati zake za kikazi akawa anatamfuta mdada jasiri anayeweza kumsaidia kwenye kazi zake na ndio ikawa mwanzo wangu wa kuanza kujuana na huyo mdada.

‘Ngoja nimalize hii kazi, lakini nitamtuma mtu aje kukupa mafunzo maalumu, tutawasiliana..ila nataka iwe siri, unajua kutunza siri wewe..?’ akaniuliza

‘Sana…’nikasema.

Basi huyo mwalimi kweli akaja, nikawa napata mafunzo maalumu, kwa siri..na ndani ya mafunzo hayo, kitu muhimu nilichojengewa ni usiri, asijue yoyote hata mpenzi wangu,..kuna namna walinijenga, nikakubaliana na hilo,.

Kiukweli hutaamini, nilitii, nikafanya hivyo, nikawa nimejiandikisha pale kijijini kwa mafunzo ye ushonaji, lakini humo humo, nakutana na huyo mwalimu wangu, napata mafunzo, asubuhi sana ni mazoezi, na jioni, akanijenga kiakili , ujasiri wa mwili ..na hayo yalifanyika kabla sijafika huku mjini.

Hivyo ndivyo nilivyoweza kuwa mdada mwingine, …mengine sio muhimu kuyaelezea hapa, au sio.. turejee sasa nirejee kwenye msingi wa maelezo yangu..

Aliporudi huyo mshauri alituambiaje,…..

‘Nawabariki mkaolewe lakini ndoa zenu ziwe na lengo moja la ndoa tu ya makaratasi, mnanielewa…lakini ndani yake tuwe na mikakati mingine mnasikia, nataka kuwafundisha jinsi gani ya kutengeneza maisha ya baadae..mnielewe, sina nia mbaya kabisa,nia ni kuhakikisha na nyie mnakuwa watu, au sio…….. ‘akasema

‘Baso mimi sijakuelewa…’nikasema

‘Muhimu kwanza hilo lifanikiwe..la ndoa, mkipata ile hati ya ndoa, mengine niachieni mimi,…baada ya hapo, baada ya ndoa, nitakuwa na vikao vya mara kwa mara,..kwa mmoja au kwa wote wawili, nitawapatia mikakati muhimu, ila cha kwanza mpate hizo hati za ndoa, ni muhimu sana kwangu……’akasema

Basi ndoa zikafanyika…kwa sherehe na gharama ilikuwa juu yake, kiukweli ilitoa fora, sio kwamba tulifanya siku moja, hapana, kila mtu ilitokea kwa jinsi ilivyopangwa, ila sisi tulishazipanga siku hiyo,

Nipo ndani ya mume wangu naambiwa kuna mgeni, kutoka na kutana na mzee mzima, akaniambia …nina haraka, ila nataka kitu kimoja, fanya ufanyavyo, upate hati za biashara za mumeo..

‘Nini..?’ nikauliza , maana nilishasahau
‘Umesahau eeh, fanya hivyo…’akandoka.

Sikuweza kufanya hivyo, baadae ndio akapanga tukaja kukutana kikao akiwemo mwenzangu, kila mmoja alishajisahau, ndio akatukumbushia ile ajenda yetu

Alituelezea mikakati mingi sana, ukumbuke kipindi hicho mimi nilishaanza kujengekea kivingine, nilikubali tu pale …, lakini akili yangu ilikuwa na mtizamo mwingine wa maisha..mwalimu wangu alikuwa kajaribu kila awezavyo kunifanya binti wa kisasa, mwenye elimu nyingine, na nilishaanza kusoma masomo ya jioni, ndani yake kuna hayo masomo.

Pamoja na hayo moyo wangu hakuwa huru , haukuwa huru kwa vile bado nilikuwa nampenda sana mpenzi wangu wa asili, kile kitendo cha kuishi na mwanaume mwingine ambaye moyoni hayupo, ilikuwa kazi..kwa kipindi cha wiki moja hivi lakini nashukuru sana docta aijitahidi naye akanibadili kifikira ..yeye alikuja kugundua kuwa mimi sipo sawa, nakuwa nipo kam sipo,..aliligundua hilo mapema sana.

Mtu wetu hakuchoka na siku moja akatuita tena, akasema;

‘Sikilizeni kwa hivi sasa sahauni yaliyopita mnasikia, muwe na akili za kuona mbele, ili muonekane na hili lindi la umasikini, fanyeni ninavyotaka ..tafuteni hizo nyaraka haraka kabla sijaondoka..alisema anataka kusafiri.

Basi mimi nikajitahidi nikapata baadhi ya nyaraka ili tu kuona anachotaka kukifanya, na mwenzangu halikadhalika,..

‘Hizi sio muhimu sana…nitakuja kuwaambia ninazotaka..’akasema na hapo nikaona huyu mtu hana maana, kila ukimleta hiki anasema hicho sio chenyewe, tafuta hiki, nikaona ni ujanja ujanja wake, nikaja kumuambia kuwa mimi siwezi tena kufanya hivyo

Kuna jambo kubwa alipenda kutushauri, tujizuie kupata watoto,ili watoto wasije kuwa ni kikwazo, na ikiwezekana tukutane sisi wawili kisiri tupate mimba, na hizo mimba tuwabambikie waume zetu hiyo ni moja ya mikakati yake aliyokuja kutushauri baada ya ndoa, ambayo haikuweza kufaulu.

‘Na muhimu zaidi mpate watoto wa kiume, mkiwapata hao, mimi nitakuwa mwalimu wao..’akasema na sikuelewa ana maana gani

Mipango yake mingi aliyokuwa akituelekeza haikuweza kufaulu kwa vile kama mlivyoona, mwenzangu alianza kupata watoto na mke wake, na hilo lilimuuzi sana mshauri wetu, lakini hakukata taamaa akawa bado anatuelekeza mengine ya kufanya.. .na alisema, huyu kaharibu, lakini hata hivyo, kapata majike, hayo hayawezi kutuzuia kwenye mikakati yetu, muhimu nyie wawili mpate madume, na hayo madume myajenge yaje kuwa warithi wenu.

‘Ndoto ya madume ilimgusa sana mwenzangu, sijui aliambiwa nini na huyo mtu, na hayo yakiendelea, wao hawakujua kuwa mimi nimeshajengwa upande wa pili, nikiwa nao, nakuwa kama wao, nikitoka kwao nakuwa mwingine, na nikiwa na mume wangu nakuwa mke wa nyumbani, hayo niliyaweza..

‘Jingine kubwa ilikuwa, kutafiti undani wa familia tulizoolewa, tujue jinsi gani walivyopata utajiri wao..familia za wazazi wao,..alisisitizia sana kwa mwenzangu mimi hakuwa na mambo mengi kwangu, hayo nilikuja kugundua ni kwanini baadae.

Asikudanganye mtu, ukishaolewa au kuoa, akili yako yote inakuwa kwenye ndoa yako, ndoa inanoga,asikuambie mtu, hasa kama umeingia kwenye sehemu unayopata kila kitu, ndoto, na mipango tuliyopanga ikawa kama inayeyuka, na kila tukikutana kila mmoja anakuwa na dharura zake utaona tu, hata huyo mshauri tukawa tunampiga chenga, na hilo zoezi likawa kama limekufa, na kila mmoja akawa na malengo na ndoa yake.

Ni kweli moyoni bado kila mmoja alikuwa akimkumbuka mwenzake, lakini ki hali halisi, ni nani angekubali kuachia hali aliyo nayo, akarudi kwenye umasikini, hakuna, tulipokutana tena, akiwemo mshauri wetu, tukalibainisha hilo wazi kuwa ile mipango ya awali isitishwe, kwani haiwezekani. Ndani ya ndoa kuna vikwazo vingi, kwahiyo hayo tuliyoyapanga yasiwepo tena, kila mmoja kesharizika na ndoa yake.

Kauli hizo zikamkatisha tamaa mshauri wetu akatuona sisi ni wasaliti, akatuona sisi hatuna maana, na akaapa kuzisambaratisha ndoa zetu, na kusema hazitadumu, maana tumeolewa au kuoa, kwa ajili ya mali tu, na sio kwa ajili ya upendo.

‘Nyie mtaona, sizani kama ndoa zenu zitadumu, nawafahamu sana nyie mlivyo, kunguru hafugiki...mnafikiri mimi siwajui eeh, nitawachunguza juu chini, na ipo siku mtanikumbuka…’ikawa kiapo chake.dhidi yetu

Ndoa ya mwenzangu ilianza kuonyesha nyufa…, baada ya kuzaa watoto wale wawili, na katika makubaliano yetu ya awali ilitakiwa mtu asizae, kwani ukizaa watoto watakuwa vikwazo, mwenzangu yeye akazihirisha wazi kuwa yeye hayupo tena kwenye makubaliano hayo, akavunja miiko, mimi sio kwamba sikutaka kuza nasema ni mungu mwenyewe alinipa huo mtihani, sikuweza kushika mimba mapema.

Kiukweli mimi sikuwa hivyo sana, yaani kujali hayo ya huyo mshauri, kama nilivyosema nimeshajengwa kinamna, kitu ambacho sikuweza kukiacha,..ni mapenzi yangu ya moyoni, sijui kwanini, japokuw akiuwazi nilishaona kuwa mwenzangu hayupo nami tena, lakini sio mimi, moyoni muda mwingi nilikuwa namuwaza yeye,..hata hivyo kutokana na mafunzo yangu nikaona hakuna jinsi… nijipange kivyangu.

Baada ya mwenzangu kupata watoto wawili, nikaona mambo yanageuka, na mara mwenzangu akaja kunikumbushia ile mipango yetu, nikashangaa, na kumuuliza iweje sasa, na wakati yeye ana familia yake tana ana watoto wawili tayari, akasema, hana raha kwenye ndoa yake,..

Aliniambia hivyo,..hana-raha-tena-kwenye-ndoa- yake…yeye anaishi tu kwa vile ni sehemu yenye utajiri, lakini ndoa yake anaiona kama jela. Ohoo nikakumbuka ule usemi usemao, utasema hakifai, au hakitoshi kwa vile unacho, wakati ulipokuwa huna, ulikitamani.....sasa ndio yakawa kwa mwenzangu…sasa hana raha tena kwenye ndoa yake…

‘Sasa unataka tufanye nini?’ nikamuuliza

‘Tumtafute Makabrasha atusaidie,..’akasema

‘Hahahah, hapana, sikiliza achana kabisa na huyo mtu, huyo mtu sio mtu mwema, atakuangamiza, na kukuacha ukiumia, nimegundua kuwa huyo mtu ana malengo yake binafsi,...’nikamwambia,na kweli mwanzoni akanisikiliza.

Kumbe mwenzangu alishaingia kwenye mambo mengine ya ndani zaidi., akawa hawezi kuvumilia, akaanza kutembea na mfanyakazi wao wa ndani kwake, na sikuamini, mfanyakazi wake wa ndani ni mtoto mdogo sana kwake, ni lile umbile kubwa tu ndilo lilimponza, ..hayo alinificha kabisa, sikuyafahamu hadi huyo binti alipofika huko kijijini na mimba.

Huyo binti alipofika hakuonekana nilisikia tu yupo, nikajitahidi hadi nikaonana naye, kwasababu anatoka sehemu ambayo mtu wangu wa moyoni yupo nilitaka kufahamu ukweli nikamuuliza kulikoni, akasema ana mimba , mimba ya nani, awali hakukubali nilipotumia ujanja wangu akaja kuniambia ukweli, sikuamini, ikabidi niwasiliane na mwenzangu, mwenzangu akanikatalia, kata kata…lakini ukweli ukaja kufahamika binti alipojifungua, maana sura haijifichi.

Nikakutana na Makabrasha, na yeye akajifanya hajui, lolote, kumbe mwenzetu alishapata upenyo wa kuingiza mambo yake..hapo hapo kwenye hilo tatizo,.., akawa kapata nafasi ya kupata taarifa zetu za ndani, na aliyewezesha awali kulifanikisha hilo, yaani kupata taarifa za ndani, alikuwa ni huyo binti …

Huwezi kumlaumu, maana marehemu alikuwa ni mjanja sana, jinsi gani alivyoweza kuingia ndani ya kuwekeza vitu, ni,..kwa vile binti wa watu hakuwa mjanja wa kuligundua hilo, kwahiyo ikawa ni rahisi kwa mtaalamu kupandikiza vitu vyake,..na baadae binti alipopata mimba, na yaliyotendeka humo ndani akaja kuyapata kama ushahid wake wa kumnasa bwana mzee.

Kwangu mimi ikawa ngumu, na alipoona mimi ni mgumu na mjanja kwake, ndio akatafuta njia nyingine,kwasababu hadi hapo alishaniona kama tishio kwake, kwani najua njama zake, na pili sitoi ushirikiano anaoutaka yeye..

Na jingine huyu Makabrasha alinifahamu toka siku nyingi, kuwa mimi sio mtu rahis sana wa kuingilika, kama alivyokuwa mume wa famila, na alinifahamu kuwa mimi ni mpinzani wake, kwahiyo akaona aniweke kwenye makucha yake kwanza, alichofanya ni kufuatilia nyendo zangu, kila ninalolifanya yupo nyuma yangu, na alinipatia kwenye kazi nilizokuwa nikipewa. Hakujua kuwa mimi nipo kazini.

Kuna kazi nyingine ilibidi ujifanye wewe ni changudoa, na inabidi wakati mwingine ujitolee kufanya hata yale yasiyowezekana kufanya ili kuupata ukweli, yeye akachukua kumbukumbu za matukio hayo, kama kinga yake, ujue kazi hiyo nilikuwa naifanya hata mume wangu hajui, hadi leo mume wangu hafahamu kuwa mimi nilikuwa siadii wa kujitegemea.

Kiukweli nilijitahidi sana kujificha, na ndicho bosi wangu alikipendea hicho, na siri ya hayo yote ni kuwa sikuwahi kumuambia mtu naifanya hiyo kazi zaidi ya bosi wangu..na kwa mume wangu yeye alijua nafanya kazi za kawaida za biashara za hapa za pale za mikononi, mali kauli, na hivyo, kumbe mwenzake nilikuwa na kazi za ushushu. Na alichoweza kukipata kwangu, huyu mtu ilikuwa sio kwa madhambi yangu, yeye hakulijua hilo, ila niliogopa je mume wangu akipata ushahidi huo itakuwaje..

Ukumbuke kuwa mimi na mpenzi wangu wa zamani pendo letu lilikuwa kama linaanza kufifia hivi, lakini sio moyoni, na mimi niliona tukiendelea kuwa karibu naye sana, hata yale ya siri yatakuja kujulikana, kwahiyo siku mume wa familia akikwazika huko kwa mke wake, hana pa kwenda anakuja kwangu, tulikuwa tunakutana sehemu ambayo tuna uhakika hatutaonekana na hata tukionekana nisitambulikane.

Kama nilivyosema awali mimi nilishakuwa mtu mwingine, kuwa naweza kujibadili, naweza kujiweka kinamna ambayo mtu huwezi kunigundua, na nikifika kwa mtu wangu najirudisha kwa hali yangu..ni utundu tu kidogo wa kucheza na mavazi, ..na vipodosi , hata kuvaa ngozi za bandia, ..ni vitu vya kawaida , wala sio uchawi.

Lakini pamoja na hayo, mimi kwa vile nilishajitambua na nilishaona haya yanayoendelea hayana mwisho mnzuri, nilianza kutumie hekima ya kumweka mwenzangu katika njia sahihi, kuwa yeye ni mume wa mtu na mimi ni mke wa mtu, inabidi hilo tuliheshimu sana, vinginevyo tutakosa kote,…hilo likawa sasa linamkwaza mwenzangu.

Mimi nikawa najitahidi kulinda ndoa yangu yeye akitoka hapo hawezi kuvumilia tena, anatoka kwenda huko anapokwenda, kulewa na kufanya mambo ya aibu,.. nilikuwa naumia sana, maana wakati mwingine nayaona, ila sikutaka sana kumfuatilia kwenye mswala yake, kwasababu nilijua nitaumia,…kuna wakati mwingine unamuonea huruma, unafikia kumweka sawa, na hapo ..ndipo Makabrasha akapata ule ushahidi alioutaka yeye..

Ina maana aliweka vifaa vya kuchukua kila tendo tunalolifanya, nia na lengo lake ni kufanikisha kile alichokitaka...akilini na mafunzo yangu yalikuwa bado machanga ya kugundua vitu kama hivyo, japokuwa nilikuwa nafahamu vitu hivyo vipo, lakini sikuwa na….sikutilia maanani kuwa anaweza kutifanyia hivyo, kabisa…

Makabrasha, alipoona pia kuwa hayo aliyakusanya kama ushahidi wa kuninasa mimi hayampi mwanya wa kuyafanya yale anayoyataka yeye kuyafanya, akaamua kuingia ndani zaidi, alimshawishi mume wa familia ajitahidi kuwa name, alivyomshauri ili tupate mtoto wa kiume,..kumbe nia yake tendo halihis lionekane na liwe ushahid.

Alikuja kuweka seehmu ya sisi kukutana, hatukuelewa lengo hilo, kumbe humo alishaweka mitambo yake na bila kujielewa tukaja kunaswa..unajau tena huruma yangu iliniponza, nikafanya kile ambacho nilikipiga vita sana, ..na makabrasha akapata kitu cha kuninasa…

Ndani ya familia ya walengwa huko akaja kugundua hiyo mikataba, aliigundua katika mazungumzo yao, ..sasa jinsi ya kuipata ..ndio akatumia mbinu hiyo ya video za matukio, akagundua wapi ilipo, na..ilikuwa kazi rahisi kumshawishi mume wa familia kutoa ufunguo…

Akawa sasa kafanikiwa kwa kiasi kikubwa,..na iliyobakiwa ikawa ni lugha za vitisho,akitaka kitu usipompatia, basi anaonyesha hayo madhambi, kuwa atayafikisha kwa mume wangu au kwa mke wa jamaa..

Hapo mume wa familia ikabidi afanye kila anachoambiwa, angelifanya nini sasa, kwangu mimi bado ..japokuwa alikuwa na ushahidi lakini sana sana alitaka huko kwa mume wa familia,..baadae akafanikiwa kutimiza hatima yake ya kuingilia nyumba hiyo ya mume na mke wa familia kama alivyotaka yeye, kama alivyoelezea mwenzangu.

Kuna mengi aliyoyafanya keshayaeleza aliyetangulia japokuwa kuna mengi mimi nayafahamu zaidi ya hayo…ila hadi hapo utaona kuwa ilifikia muda, mume wa familia akawa hana jinsi, ikabidi akubaliane na kile anachoambiwa na marehemu.

*********
Nashukuru mungu kuwa hadi marehemu anaondoka, hakuwahi kunitambua upande wa pili wa kazi zangu, na hilo lilinisaidia sana,…nakumbuka siku moja alituita mimi na mwenzangu,..

‘Nduguzanguni, najua tulifikia mahali tukawa hatuelewani tena,..tukaondoa udugu wetu, urafiki wetu, nilijua itafika mahali mtakwama mtarudi tena kwangu, kwa hiari au kwa nguvu..sasa mumerudi kwangu, au sio..’akasema

‘Nawafahamu sana, kuwa huko mlipo hampo kwa mapenzi, na sasa nimepata ushahid huo, kuwa ndoa ya mume wa familia na mkewe haipo kwenye msimamo mwema, hiyo ni kuashiria kuwa siku yoyote ndoa hiyo inaweza kuwa marehemu, ..’akasema

‘Kwahiyo kabla ya hiyo ndoa haijafikia ukingoni, basi ni bora kuwa na mpango wa pamoja, kuhakikisha mali zote za familia zinakuwa mikononi mwa mume wa familia, lakini kwa vile mume wa familia ana mauchafu yake yakibainika atanyang’anywa kila kitu, sio vyema ikawa mikononi mwake, basi itafutwe namna mali hiyo itakuwa salama zaidi, kwahiyo mipango iwe ni namna gani mali hiyo itakuwa mikononi mwake

‘Mimi nayafanya haya kwa ajili yenu, ..mnasikia, nina uhakika ikiwa hiyo mali ikiwa kwangu kwanza kama wakili wenu , lakini pia kwa kumiliki hisa zaidi ya nusu, itakuwa ni salama zaidi.

Hapo kwenye hisa mume wa familia akapinga, lakini akaja kuambiwa kama hili analiona gumu, basi alipe madeni ya huyo marehemu yote, kama ana uwezo huo..hakuwa na pesa, alishakuwa mtu wa madeni, alishafanyiwa mengi, ya kutoa pea ili apate picha au video, akakamuliwa hadi tone la mwisho, sasa akawa mtu wa madeni, isingelikuwa mke wangu angeliuza hata magari yakampuni..sasa akawa anakopeshwa na marehemu, hakujua anayefanya hayo yote ni marehemu,..

‘Marehemu alip[opiga mahesabu ya madeni anayomdai jamaa ikawa ni makubwa sana, jamaa hana uwezo wa kulipa,. Sasa afanyeje.., basi marehemu akasema njia ni rahis ni yeye kuyageuza hayo madeni kuwa hisa..alipe kwa kumuuzia hisa…ilikuja kuwa ngumu awali, lakini mwisho wa siku mume wa familia akawa hana hoja,..ikabidi auze hisa kwa kulipa madeni ya marehemu..’akasema.

Kila mume wa familia akipinga jambo, anakuja kuonyeshwa uchafu wake, anadaiwa madeni, ..basi akawa mtumwa wa jamaa…na ikafikia muda sasa kashindwa akaja kwangu kuniomba msamaha, na kuomba ushauri…na alikuja kipindi ambacho hata mimi marehemu ananindama,..na ningemshauri nini mimi…, nilimuambia ukweli hayo umeyataka yeye mwenyewe iliyobakia kwasasa umuache huyo jamaa afanye atakavyo

‘Mimi siwezi nitamuua…’akasema

‘Wewe una ubavu wa kupambana na Makabrsha, hilo sahau, labda kama unataka kujitakia matatizo..’nikamwambia, lakini jamaa siku hiyo alitoka na ajenda ya kutafuta namna ya kumuua Makbrasha, na hata tulipokutana tena na tena akawa na ajenda hiyo hiyo, kuwa atatii yote, ila siku ya mwisho wa kusaini huo mkataba wa kukabidhi kila kitu hapo ndipo siku atafanya kile alichokidhamiria…

‘Mimi sipo, ..kama unataka kufanya mauaji, usinihusishe mimi kabisa..’nikamwambia

‘Nimekuambiatu..’akasema na siku zikawa zinakwenda nikaona wao sasa wapo sambamba, mikakati ya pamoja, ikawa inafanyika, hadi wakafikia kukubaliana kuwa hayo yafanyika kwa masilahi ya pamoja,..ndio ikapangwa mikakati ya kubadili huo mkataba wa familia, hayo yalifanyika bila ya mimi kushirikishwa.

‘Unajua pamoja na yote hayo mimi niliendelea kujitolea kuhakikisha familia ya mke na mume ipo salama, ilikuwa moja ya kazi angu kutoka kwa bosi wangu, kwa siri ajabu, lakini sikuweza kulitatua hilo, unauma na kupulizia, huku unafahamu mbaya ni nani.. nikawa sasa nafanya kazi mbili kwa waakti mmoja,

Kumlinda mpenzi wangu, na kuilinda familia na huyo shetani, asizidi kuleta madhara, na ili hilo lifanikiwe ikanibidi na mimi sasa niwe mtumwa wa huyo jamaa..


Nikaja kugundua kuwa sio marehemu tu, kumbe hata marehemu alikuwa akitumiwa, na kwa jinsi alivyofanya, isingelikuwa rahis kumdhibiti, ndio nikaongea na bosi wangu kuhusu hilo, lakini sikuwahi kumuambia kuhus mahusiaono yangu na mume wa familia, hilo lilikuwa siri kubwa sana kwetu anayefahamu ni marehemu na ili marehemu aendelee kulificha hilo,..ni mimi kuwa mtumwa wake

Katika kuhangaika nikajikuta mikononi mwa wapinzani wa mzee, sijui walinijuaje ila bado walikuwa hawana uhakika..na sio kwamba walinijua kutokana na kazi zangu ila wanasema wameona mimi nina kipaji cha kuwatumikia, umbo, sura..ujanja, kuongea, ..unajua tena,, wanakiniomba waniajiri kwao..

Kiukweli mimi niliwakatalia, japokuwa walikuwa tayari kunilipa mapesa mengi, ili niajiriwe na wao, ..walipoona kuwa mimi ni mgumu ndio wakamtumia Makabrsha, makabrasha akaja kuniambia hao watu wananihitajia, na hao watu ni hatari sana, wakikutaka uwafanyie kazi zao ukikataa, wanakuua, hawasiti kumuua mtu.

‘Sasa mimi nifanye nini..?’ nikamuuliza

‘Cha kufanya nitaambia utakuwa na mimi, nakuandaa ili baadae uje kuajiriwa na wao..’akasema

‘Mpaka lini..?’ nikamuuliza nikiwa na malengo yangu kichwani

‘Mpaka nitakaporizika mimi, maana nakuhitajia kwa kazi zangu, zikiisha basi, itabidi uende huko..’akasema.

‘Hapo una ujanja tena..ikabidi kwanza niandike barua ya kuacha kazi kwa bosi wangu, lakini sikuweza kumuambia dhumuni langu ni nini, ila nilitaka hata nikiingia huko, niwe na mikakati ya kulimaliza hilo kundi kwa namna yangu mwenyewe japokuwa najua hiyo ni hatari kubwa sana kwangu.

Nikamwambia Makabrsha nimekubali, lakini kwa masharti, kuwa aachane kabisa na familia ya mke na mume, aachana na kazi yake hiyo mbaya..

‘Hahaha, unajua hilo haliwezekani..’akasema

‘Kwanini…?’ nikamuuliza

‘Nitakuja kukuambia pale unakaposaini mkataba wa ajira kwangu, na mkataba wa kukubali kuwa umeachana na familia hiyo ya mpinzani wa bosi wangu..

‘Mpinzani wa bosi wako..?’ nikauliza kama mshangao

‘Ndiyo mambo ambayo utakuja kuyafahamu baadae..’akasema

Wakati huyu mdada anaendelea kuongea, kukasikika sauti, ya mtu kama analia..mdada akatulia kuongea na akitulia sauti hiyo inapotea badae akaja kugundua ni nani analia..

‘Sasa unalia, utalia sana, hapa ndio nimeanza, nilikuwambia leo ndio siku ya hukumu, upende usipende, hukuniamini, hapo ndio nimeanza…’akasema mzungumzaji


NB: Naishia hapa kwa muda,


WAZO LA LEO: Ukweli unauma lakin ukweli ndio njia sahih ya kutatua magumu yote, tujifunze kuwa wakweli kwa watu wenye kuaminika, …
 
SEHEMU YA 112

Kuna mtu alikuwa analia, ikaja kugundulikana kuwa ni mume wa familia, ..na ndipo shahidi aliyekuwa akizungumza akasema, ;

‘Utalia sana,na hapo ndio nimeanza…’

Tuendelee na kisa chetu

*********

‘Wewe niache nilie, ujue mwanaume akilia kuna mazito, wewe hujui tu, wewe hujui ulivyoharibu, mumeniharibia maisha yangu, na kwa hili utakuja kunikumbuka, …hutafanikiwa kamwe, na hiyo mipango yako na waliokudanganya, utakuja kujuta.. ’akasema mume wa familia.

‘Kufanikiwa, au kujuta kwangu sio hoja, hoja ni ukweli wote ubainike, ili haki iweze kutendeka, ndicho mimi ninachokitaka, baada ya huu ukweli … kila mtu atabeba mzigo wake yeye mwenyewe,na maisha yataendelea tu…’akasema mzungumzaji.

‘Nilijua tu…haya sawa ngoja tuone…’akasema mume wa familia kwaunyonge.

‘Kwani.., wewe ulitakaje, kuwa haya yaendelee hivi hivi, wakati ukweli upo bayana, na ukweli ni kuwa dhuluma haitadumu, ni lazima mwisho wa siku utagundulikana tu, na ni heri nusu shari kuliko shari kamili. Kama nilivyosema awali mimi sio yule binti wa kijijini asiyejua kitu, asiye na ufahamu, ..elimu niliyopata japo kidogo, imenizindua, naifahamu sheria, naifahamu haki, ..na kwa hili nafahamu kabisa huna lako, utegemee huruma za mke wako tu..’akasema muongeaji.

‘Sawa…endelea kufungua bakuli lako, tuone mwisho wake utakuwaje,…ukitoka hapa unaelekea jela, unafikiri ni nani wa kukusaidia….hao watu eeh, hahaha unajidanganya tu..’akasema mume wa familia.

‘Ndugu mwenyekiti….’muongeaji akawa anataka kulalamika, ili aweze kuendelea maana mume wa familia anamkatiza kila akitaka kuendelea. Na kabla mwenyekiti hajasema kitu, mume wa familia sasa akasimama.

Wakili wake alipoona hivyo, akawa anajaribu kumzuia huyo mume wa familia, haikueleweka lengo la huyu mume wa familia kusimama ni nini, kuwa laba anataka , kuondoka au kumzuia muongeaji asiendelee kuongea.

‘Sikiliza,..niamini mimi haya yatakwisha, nakuambia ukweli haya yatakwisha, si unataka turejee kule tulipotoka, sawa, haya lakini tatizo polisi wanasubiria, jela inanukia…’akasema

Hapo mwenyekiti akaamua kuingilia kati na kusema;

‘Mume wa familia, usivuruge utaratibu, hebu kaa chini, nakuona sasa unaleta vurugu, kitu gani unaogopa, muache shahid aendelee, hapa kila mtu anataka kusikiliza ushahidi wake,..sitarudia tena kukuonya, kwasababu kikao hiki kina kibali kisheria, hatukufanya tu kama kikao cha mitaani, unasikia,….’akasema mwenyekiti.

Hapo mume wa familia, akageuka na kukaa kwenye sehemu yake na wakili wake akawa anamnong’oneza kitu, wakawa wanaongea sasa kwa taratibu, nikaona kama wanakubaliana jambo. Na kabla muongeaji, shahidi hajaendelea wakili akanyosha mkono, kutaka kuongea, na hata kabla mwenyekiti hajamruhusu wakili huyo akawahi kusema;

‘Samahani mwenyekiti…kuna ombi kidogo kwa mume wa familia, naomba tumsikilize…’akasema wakili na kabla wakili hajamaliza kuongea, nahis walishafahamu kuwa hawataruhusiwa kuongea, akasema;.

‘Kwa vile umesema mdogo wangu kakamatwa na polisi, na mimi ndiye kaka yake, ninaomba mimi na wakili wangu tuende tukafuatilie utaratibu wa dhamana yake…’akasema hivyo akauliza

‘Nani kasema kakamatwa na polisi, mimi nimeuliza unafahamu wapo mdogo wako alipo, yawezekana kakamatwa..sawa. mimi sina uhakika na hilo, hayo ni maswala ya polisi. Walichoniambia nikuwa tusiwe na wasiwasi na huyo mtu, …kwahiyo huenda anaisaidia polisi..na watatoa taarifa kama kakamatwa au la..’akasema mwenyekiti

‘Kwani Polisi wamesemaje hasa..?’ akauliza wakili.

‘Polis walisema wanamfuatilia, pale nilipotoa taarifa kuwa huyo kijana ametoroka, maana ilikuwa niw ajibu wetu kutoa taarifa…wakasema watalifuatilia hilo.

‘Na baadae nilipooongea nao tena, ndio wakasema wameshayaweka mambo sawa tuendee na kikao,na wakatahadharisha kuwa kikao chetu kisingilie maswala ya mauaji, ina maana kuna jambo kijana kaongea huko…’akasema mwenyekiti.

‘Kwa kauli hiyo mpaka hapo ina maana mdogo wake mteja wangu yupo mikononi mwa polisi …au sio?’akasema wakili

‘Yawezekana, ndio..sina uhakika huo, huenda yupo mikononi mwa polis lakini akiisaidia polisi, kama atakuwa kakamatwa kwasababu kadhaa, ni lazima watatufahamsisha, sisi ndio ndugu zake…’akasema mwenyekiti

Hapo mume wa familia akasimama, na wakili wake akamzuia wakawa wanaongea na wakili akasema;

‘Mteja wangu anasema kama yeye haruhusiwi kutoka, bas I ngoja mimi kama wakili wake nilifuatilie hilo, kwa niaba yake..’akasema wakili.

‘Hivi tunaelewana jamani,..huyo ni ndugu yetu, sote tunawajibika naye, kama ni swala la kufuatilia, sote tutaungana na kuona vipi tutamtetea, ..eeh, lakini hadi hivi sasa tupo chini ya amri ya polisi, kuwa asije akatoka mtu na kikao kikimaliza wao watakuja hapa, …’akasema mwenyekiti

‘Lakini mimi siwezi kuzuiwa maana, mimi ni wakili tu, kama mteja wangu kaniruhus mimi nitoke nifuatilie hilo, ni wajibu wangu kutii, mimi nipo kwa mamlaka yake sio kwa mamlaka ya hiki kikao..’akasema wakili

‘Haijalishi wewe ni nani mimi nafuata amri za watu wa usalama, …, kwani wewe wakili hauwezi kufanya makosa, muhimu tusubirie, tukimaliza kikao, wenyewe watafika hapa na kitakachoendelea baadae tutaambiwa, sawa, …shahid endelea…’akasema mwenyekiti.

********

Shahidi akaendelea…

‘ Baada ya Makabrasha kumweka sawa mume wa familia, bado kulikuwa na mambo hayajawekwa sawa kwa utaratibu wake, kwa upande wa wadhamini wake, hao waliomtuma alishafanya kazi yake, lakini sasa alikuwa akikamilisha mambo yanayohusiana na masilahi yake.

Aliniambia kwua katika mipango yake alihitajia kundi la watu, ambao ataweza kufanya kazi nao, kuachilia mbali sisi ambao tunakutana mara kwa mara, akasema bado anahitajia kiongozi ambaye atakuwa akiongoza hilo kundi.

‘Wewe si ndio kiongozi..?’ nikamuuliza

‘Hapana, mimi sitakiwi niwe kiongozi wa moja kwa moja, maana mimi ni mtu wa sheria, kazi yangu kubwa itakwua kuhakikisha sheria zipo sawa, hata hivyo …inavyoonekana mimi ndiye nitakuwa mkurugenzi mkuu kutokana na hisa zangu…lakini nahitajia mtedaji mkuu, kiongozi wa kusimamia mambo yote.

‘Ni nani huyo..?’ nikamuuliza

‘Ndio namtafuta,..ungelifaa kuwa wewe, lakini bado ..wewe bado unahitajia muda, yupo ambaye anafaa sana, lakini sijaweza kumshawishi…’akasema

‘Ni nani huyo..?’ akauliza mume wa familia

‘Haina haja kumfahamu kwasasa…ila zaidi ya hayo, tunahitajika kumuandaa huyo mtu kuja kuwa kiongozi wa baadae, wewe mume wa familia utakuwa na mamlaka yako, lakini hutaweza kuongoza hili kundi, hili kundi ni jingine, linahitajia mtu mwenye uelewa wa mambo mengi na jasiri ..’akasema

‘Kwanini mimi sifai, usielete watu wako hapa kwanza kampuni ni yangu, nay a mke wangu, bado unaona sisi hatufai, kwanini....?’ akauliza mume wa familia

‘Mimi ninakufahamu sana, kiongozi tunayemuhitajia anatakiwa mtu tofauti na mkeo kwasababu atakuwa mpinzani wa familia ya mkeo, …sihitajiki kujieleza sana kwa hilo, muhimu muelewe hivyo tu…’akasema

‘Hapana mimi sitakubaliana na hilo…’akasema mume wa familia.

‘Kumbuka mimi ndiye mkurugenzi mkuu, ninayemiliki zaidi ya nusu ya hisa, nina kura turufu…na uniamini, mimi nina maana yangu kubwa sana kulifanya hilo, mwenyewe utakuja kuona,… tuombe mungu tu nizidi kuwepo..’akasem

‘Una maana gani kusema hivyo, kumbe mwenyewe unajua kuwa hutafanikiwa au sio..?’ akauliza

‘Kazi kama hizi ..ni za hatari, ..vyovyote iwavyo, lolote laweza kutokea, hilo siwezi kulipinga, ila kwangu mimi ..kisheria nimeshaanza kuweka kila kitu sawa, hata hivyo maisha hayana ujanja, leo nipo kesho sipo,..ila nawahakikishia , kama nitaendelea kuwepo, mali zote hizo zitakuwa kwenye miliki yetu, mikakati yote imekwenda sawa ni nyie tu kushirikiana na mimi ili muwe na uhakika wa maisha mazuri, …’akasema.

‘Sisi tutakuwaje na maisha mazuri wakati hisa karibu zote unachukua wewe..?’ akauliza mume wa familia

‘Je ni kipi bora kukosa kabisa au hata kupata kidogo, eeh, maana kwa hali ilivyo ungelikosa kila kitu, hunishukuru mimi, …acha ubinafsi hapa,..’akasema kwa ukali.

‘Kama ni ubinafsi unao wewe sio mimi…’akasema mume wa familia.

‘Sikiliza…hivi unajua kashafa uliyotengeneza, ..kashifa hiyo ingekugharimu wewe kutimuliwa kwenye hiyo familia kwa fedheha, …pili ukumbuke kuwa kutokana na kashfa hiyo familia hiyo ipo kwenye wakati mgumu…’akasema

‘Kwa vipi…?’ akauliza mume wa familia.

‘Unaona, ndio maana nikasema uongozi unahitajia mtu anayeona mbali, anayefahamu mambo mengi kwa wakati mfupi, siwezi mimi kukufafanulia kila kitu, unasikia,..au nikuulize wewe ulitakaje, …?’ akauliza

‘Sisi mimi nilitakaje, wewe umetumia ujanja wa kuhakikisha unanifirisi mimi, na familia yangu, unafikiri mke wangu atakubali kirahis hivyo, eeh, na..hapana hilo la kutafuta watu wengine kuja kuongoza hata mali za mke wangu sitakubaliana nalo..’akasema mume wa familia.

‘Tatizo bado hujanielewa,…unasikia,…kundi hilo, kwa namna moja halitamuhusisha mkeo moja kwa moja, maana mkeo ni familia ya kundi pinzani, mkeo ataingia pale tu tutakapogusa mali..mbazo na yeye anazimiliki..vinginevyo yeye atakuja kuwa kama picha ..familia hiyo itafirisika, na wewe utakuwa juu…’akasema

‘Hizo ndoto….hahaha..’akasema mume wa familia.

‘Ndoto, ni kwa vile wewe huwezi kufuatilia, mambo ya hisa, kushuka na kupanda kwa tahamni za hisa za wawekezaji wakubwa, mkweo sasa hivi anayumba, kisiasa na kiuchumi, ..hilo kwako tuliache, kidogo kidogo utakuja kunielewa..’akasema

‘Mimi nakubali tu kwa vile sina jinsi, kwa vile unanitishia amani, vingnevyo nisingelikubali kabisa…’akasema mume wa familia.

‘Hizi jamani wewe mtu unataka nikupe nini,..ulitaka mimi nikusamehe madeno yote, ina maana mim iwe kazi yangu kukufanyia kazi zako,..nipate hasara, hebu niambie hayo madeni yangu yote ungeliwezaje kuyalipa, hebu jaribu kuwa na akili pana…’akasema wakili.

‘Nitakuja kuyalipa na hisa zangu zote utazirejesha, ..hilo na kuahidi ..’akasema mume wa familia

‘Hahaha, kwa hali uliyo nayo, sizani,labda mimi niwe sipo duniani, ..unafikiri hayo madeni ni kitu kidogo, ..eeh, hutaweza hilo sahau na ujipange nnavyotaka mimi, nataka nyie muwe matajiri, kwanini hutaki kunielewa…’akasema wakili huyo.

*********

Mikakati ikawa mingi, na mingine mimi sikuhusishwa kabisa niliweza kuigundua hiyo mikakati, wakati nikiwa kwenye kazi zangu, na nikiwauliza wanasema nisiwe na wasiwasi mane mengine sio lazima mimi nifahamu, ila kila kitu kimeshafanyiwa kazi, iliyobakia ni mambo machache ya kukamilisha, na hayo hayanihusu sana.

Kwahiyo mimi nikawa nasubiria, na wakati nasubiria ndio ikaja taarifa hiyo ya ajali…

‘Ile ajali ya mume wa familia, ilitokea katika harakati zile za kuchukua mkataba ule wa zamani ili ikabadiliswe na huo mpya wa kugushiwa, na hayo yote yaliwekewa muda maalumu kwa mume wa familia kuhakikisha nakala zote za zamani zmechukulia na kuharibiwa, na kuhakikisha kuwa hakuna nakala yoyote itakayobakia.

Tatizo sasa mume wa familia akawa na ziada ya kazi ya kuongea na mama mzazi, ili mtoto huyo aje kuwa sehemu ya warthi wake, aweze kutambulikana, na hilo lilitegemea sana mama yake, kwahiyo pamoja na mihangaiko ya kubadili hiyo mikataba bado alitakiwa kumshawishi mama wa mtoto huyo akubaliane naye. Mambo yote hayo yakapangiwa muda,…sijui ni kwanini, nahisi ni moja ya mbinu za marehemu kuhakikisha jamaa hapati muda wa kutafakari tena.

Muda, ukawa ni sehemu kubwa ya kufanikisha malengo hayo, muda pia ukatumiwa kama namna na kumfanya mume wa familia awe na wakati mgumu ili asipate nafasi ya kutafakari zaidi, muda ukawa namna ya kuwaogofya wale wote wanahusika, kuwa wakichelewa kashfa zao zinatumwa kwa walengwa..mume wa familia,..hakujua hayo yote yote wenzake wameyaweka kwasababu maalumu.

Siku hiyo mambo yalianza hivi----

Akiwa ofisi akapigiwa simu na Marehemu kuwa zile nakala zote za mikataba yao, zinahitajika kwa haraka, …na pia akaulizwa vipi mama wa kichanga keshamuweka sawa, maana yote ni muhimu sana, kwani asipomuweka sawa mama wa kichanga, huyo mtoto anaweza asiwe na nafasi kwenye mipangilio ya watoto wanaotakiwa kumiliki mali halali.

‘Kwanini, kwani hata asipokubaliana kwa sasa baadae si inawezekana, kuna tatizo gani hapo..?’ akauliza

‘Tunahitajia sahihi ya mama,..tunahitajia kukubali kwake, hatuwezi kupitisha jambo kama mama wa mtoto hajakubali, hiyo ni kazi yako kama kweli unampenda huyo mtoto na kama kweli unamuhitajia kama mrithi wako wa baadae basi fanya juhudi ..’akaambiwa

‘Sawa…’akasema mume wa familia, hapo kichwa kinamgonga kweli, akachepuka na kumeza zile dawa, alizopewa, ..muda mchache baadae akajihis mwingine, akili ikawa na changamoto za dawa. Anarudi kwenye kikao hajaa vyema zimu ikalia, akaambiwa;

‘Lakini pia zile nakala za mkataba wenu , wewe na mkeo, zinahitajika kwa haraka, zoezi hilo halitaweza kufanyika kama hizo nakala zote hazipo, msimamizi anayesimamia idara hiyo, kasema hataweza kukamilisha hilo mpaka nakala zote ziwepo, ili ziharibiwe mbele yake..’akaambiwa.

‘Sawa…’akasema na kupekua kwenye briefcase yake, ndio akakumbuka nakala mmoja haipo, ..akakumbuka alipoiacha, hapo kwa haraka akawaambia wajumbe;

‘Jamani endeleeni na nikao, nipo, …msikatize kikao, kuna kitu cha haraka nakichukua hapo nje…’akasema akitoka na briefcase yake, akaingia kwenye gari, mbio, barabarani.

Akiwa barabarani, Makabrasha akaendelea kumsumbua na simu, ni kama anamuona anavyohangaika,…akamwambia;

‘Na ukumbuke hiyo ndio salama yako, maana mkataba wa zamani ukiwepo, na kashfa ulizokutwa nazo zikibainika basi hutapata kitu… umeelewa, hiyo ni kwa faida yako,…’akaambiwa

‘Ni kweli…’akasema, na ni kweli, kutokana na hizo kashfa, mbele ya mkataba wao alitakiwa akose kila kitu, na zaidi ni ndoa yake kufa, na ndoa ikifa yeye ana faida gani tena,,,;akatulia kidogo mzungumzaji, halafu akasema

Kama mtausoma vyema huo mkataba, utaona hadi sasa mume wa familia hana ndoa, sisemi hili kwa uzushi, au kutilia fitina, mkataba wao unasema nini kuhusu madhambi kama hayo, na ushahidi upo wazi…au amkane huyo mtoto kama sio wake, je anaweza kufanya hilo, hawezi kumkana, sasa chukulia hali hiyo, na ndio umepata mwanya kama huo, ungelifanyaje, ndio maana mume wa familia akakurupuka, hana amani, akili sio yake,….

Kwahiyo ndio akapanga akitoka hapo kwenye kikao chake cha kikazi…kikao ambacho alikiacha kikiendelea,..ili iwe ni ‘kinga’ kwake kama ikitokea jambo kuwa yeye siku hiyo alikuwa na kikao ofisini, …kwa usafri wa gari, alijua atakwenda kwa haraka, na kurudi na kuendelea na kikao.

Ili kukamilisha mambo yote hayo akaona ampitie mzazi, mama wa mtoto ili amuhakikishie mikakati yote na amshawishi kuwa mambo sasa yapo sawa, na kutokana na shinikizo la yule mtu asiyejulikana, mtu wao..yaani wakili, ambaye ni marehemu.., atalimaliza..

Alipofika huko akashangaa kumuona mke wa familia yupo na huyo mdada aliyejifungua, na hili hakulitegemea kabisa, yeye alijua kuwa mke wake atakuwa kazini, sasa iweje awepo pale, na kwa muda huo huo akapokea ujumbe wa simu ikimuhimiza kuwa nakala za mikataba yote ya zamani, zinahitajika kwa haraka iwezekenavyo. Na muda ni leoleo, ikishindikana ndio basi tena..

Hapo akili ikazidi kuchanganywa, alijua kabisa mkewe akitoka hapo atarudi nyumbani, na hataweza tena kuchukua ile nakala ya mkewe , ambayo aliisahau kwa bahati mbaya usiku, yenye shida ilikuwa ni nikala moja ya mkewe maana yake alishaichukua anayo…

‘Sitaweza kuongea na huyu mtu kwa leo, lakini ni lazima niwahi kuzipata hizo nakala za mkataba ..kwa manufaa yangu..’alikuwa akisema hivyo, alinihadithia jinsi siku hiyo ilivyokuwa na wakati mgumu kwake..

Ya mungu mengi, …wakati Makabrasha keshafanikisha namna ya kumweka sawa msajili wa hiyo mikataba, na wakati huo wanasubiria nakala hizo walizokuwa nazo wahusika wakuu,akaja taarifa jamaa kapatwa na jail, yupo kwenye hali mbaya..

Ukumbuke kabla ya hilo zoezi, Makabrasha alishafanya vitisho vingi ambavyo vilizidi kumchanganya mume wa familia,…na mume wa familia kuna muda akawa analalamika kuumwa na kichwa Makabrasha ndiye aliyemtafutia dawa, akasema hizo dawa zitamsaidia sana hayo maumivi ya kichwa, mimi nilikuja kuzipeleka hizo dawa kwa wataalamu baadae lakini zikaonekana ni dawa zakuharibu akili…’akatulia kidogo.

‘Kiukweli Makabrasha anaifahamu kazi yake vyema, kwenye kucheka atacheka, kwenye kazi, vitisho, atakutisha kweli,...alijipanga vyema,kwahiyo kila muda kwake ilikuwa ina mbinu zake na kila jambo lilikuwa na plani A na B, ikishindikana moja nyingine itachukua nafasi yake, hakuwa mtu wa mchezo.

Hizo dawa alipewa kabla ya ajali na baadae akawa anaendelea nazo baada ya ajali mwenyewe anasema akisikia kichwa kinauma sana, akinywa hizo dawa kichwa kinapona, lakini hakujua hiyo ahueni ilikuwa inazaa tatizo jingine. Na ndio hayo yakawa yanatokea baadae ni sababu ya hizo dawa, .hata mimi sikuwa na ufahamu wa hizo dawa, nimekuja kuligundua hilo baadae sana...

Sasa alipogundua kuwa mkewe hayupo kazini, yupo kwa rafiki yake, na anatakiwa kuwahi kuchukua zile nakala azifikishe kwa walengwa, si ndio akatoka hapo kwa mwendo kasi, akili pale ilikuwa sio yake tena, keshapata vitisho, kamuona mkewe na muda hautoshi, na zile dawa huenda alizitumia asubuhi,zilikuwa bado kichwani akilini ikawa inaota mengine, haoni kabisa kama yupo kwenye mwendo kasi, tahamaki ndio hiyo ajali..ilikuwa ni ajali mbaya sana.

Ajali haina kinga….!

Ajali hiyo ingelichelewesha mambo mengi, lakini kwa Makabrasha ikaonekana ni bahati nyingine nzuri tu kuitumia, tunaweza kusema kwake ilikuwa ni bahati nzuri ya kufanikisha mambo mengine.., japokuwa ilikuwa ni ajali kwa rafiki yake..

Hutaamini ajali hiyo ikaja kutumiwa kama kisingizio cha kufanikisha mambo mengine mengi tu, kama mlivyosikia kwenye maelezo yaliyotolewa awali. Mtu anaumwa yupo hospitalini, mara yupo uwanja wa ndege, mtu anaumwa, yupo hospitalini mara yupo nyumbani….inaeleweka kweli….! Lakini kiukweli ajali ile ilikuwa mbaya, na kuna madhara makubwa aliyapata kwenye uti wa mgongo, hili halina shaka.

Sasa baada ya ajali ni nani anaweza kutumiwa ili kufanikisha hayo yaliyopangwa, nakala za mikataba ile ni muhimu sana, akatafutwa mtu wa haraka, ambaye yupo karibu na mume wa familia ambaye anaweza kuficha siri, hata kama…na akipewa maagizo atayafanya kwa haraka..

Uwe na kujali fulani,…, ndio hapo wakamchukua mdogo wa mume wa familia, yeye kwa asilimia kubwa hakufahamu chochote kinachoendelea zaidi ya kutumwa , na hakutakiwa afahamu kitu gani kinachoendelea, kazi yale ilikuwa kumtii kaka yake,na kaka yake ahakikishe hilo. Sizani kama alikuwa anafahamu undani wa hayo yote, kwani nimjuavyo, kama angelifahamu undani wake, mengine asingelikubali.

‘Sasa hapo utajiuliza iweje wakati mtu hajiwezi yupo hospitalini, maana hadi anafikishwa hosp alikuwa hajiwezi, sasa huyu marehemu alijua ampe dawa gani ili aongee kila kitu cha kusaidia, na maongezi yake yasaidie…dawa hizo zilitumika pia.

‘Na ajali iliyopotea mtu wa kwanza kufika kwenye hilo gari alikuwa ni marehemu alifuata nini, na alijuaje kuwa ajali hiyo itatokea,… marehemu alikuwa sio mtu wa mchezo..sijui siku ile walipokutana wakati mgonjwa yupo taabani, waliongea nini...hilo tutamuuliza mume wa familia.

Nisije kulisahau hili….Kuna mtu mwingine ambaye alikuwa kinara wa hayo yote, akiwa kama msaidizi wa Makabrasha, ambaye hadi sasa watu hawajamgundua…huyu mtu ni hatari kuliko watu wanavyomfikiria…’hapo akatulia kidogo.

Huyu mtu ni hatari hata kuliko Makabrasha mwenyewe maana tatizo lake kunwa ni kuwa ana papara, hajatulia kama alivyokuwa akitulia baba yake kabla hajaingia kwenye mapambano, mtu huyu ni nyoka yenye sumu, ni mbaya sana, si mwingine ni mtoto wake mwenyewe marehemu.

Huyu aliweza kupenya kwenye sehemu mbali mbali na kupata taarifa nyeti. Huyu anajua siri nyingi tu za baba yake,..na ndiye alitarajiwa kuwa mrithi wake mkuu, kwa mtizamo wa wengi lakini ikaja kutokea tofauti, ..hapa hatuna uhakika ni kitu gani hasa kilifanyika…maana imeshangaza kuona aliyepewa majukumu hayo ya kifamilia ni mtoto mwingine.

Ni kweli mtoto huyu kisheria ndiye aliyetakiwa kuchukua hayo majukumu, lakini mtoto huyu hakuwa karibu na baba yake, hawakuwa wanaelewana kutokana na tabia za baba yake, mtoto huyu alikuwa akitaka mambo ya halali, sio kama alivyokuwa akitaka baba yake, kwahiyo walikuwa hawapatani kabisa, sasa iweje yeye apewe majukumu ya kifamilia, majukumu ambayo ndani yake kuna magumashi mengi.

Sasa maswali mengi nahisi hapa polisi watakuwa wakijiuliza sana, huyu aliyetarajiw akwua kinaraka kwanini hata kwenye mirathi awe ni mtu wa tatu…ujue huyu mtu kiukweli hata ndani ya familia alikuwa hajulikani sana zaidi ya kujuliana na baba yake…. Na ukumbuke huyo ni mtoto wa nje tu wa Makabrasha, hakuzaliwa kwa mke anayejulikana, alizaliwa na mwanamke wa nje tu..Hapa kuna jambo,…sijaweza kuliweka sawa, mtanisaidia..

***********

Mipango ilipokamilika na mikataba halali iliyokuwemo kabla ikaharibiwa, na kuwekwa mikataba iliyogushiwa, na kilichobakia ulikuwa mkataba mpya ambao ulionyesha dhamira ya Makabrasha, na huo ulileta sintofahamu, lakini kwa vile Makabrasha alishajiandaa kwa hilo, akatoa vitisho vyake, na mume wa familia akasalimu amri. Na kila kitu kikawa kimekamilika

Kilichokuja kuharibu sasa ni huo utaratibu wa nakala kuhifadhiwa kwenye mtandao, sijui kwanini Makabrasha hakulifikiria hilo mapema, sijui kwanini hata huyo mtu wa masijala hakuwahi kumuambia Makabrasha kuhusu hilo, kama angelifikira hilo mapema, isingelikuwa kazi nguku kwa huyu mtu.

Kwa Makabrasha mambo ya mitandao anaifahamu sana , na ana watu wake wanaoweza kufanya zaidi ya hapo,..na hadi hapo kila mtu anayehitajika alishakuwa mikononi mwake. Nakumbuka siku zoezi hilo lilipokamilika, alifanya shereeh fupi y akujipongeza na kujinadi kuwa sasa yeye ni kaam yule mtaalamu wa kile kisa cha dunia yangu

Hadi hapo alikuwa ameshawaweka matajiri wengi mkononi, alikuwa na hisa karibu kwenye makampuni mwengi makubwa, alikuwa akila sahani moja na wanasiasa wakubwa, aliyekuwa amebakia ndio huyu mkwe wa mume wa familia. Sasa aktika kuongea ndio nikagundua jambo

‘Sasa hata mkuu wangu hataniweza…’akasema

‘Mkuu wako!!! , kumbe kuna mtu yupo juu yako..?’ nikamuuliza

‘Hahaha, hivi ningelipatia wapi pesa nyingi ya kufanikisha haya yote..yupo mkuu, na sio yupo, wapo, wakuu, wafadhili wangu…ila muhimu ndio huyo mpinzani wa ..baba mkwe,…, lakini yeye hawezi kuniingilia kwenye mali zangu, ana yake na mimi ninayangu, ila mimi nitamwezesha kufika juu, akifanikiwa yeye, na mimi nimefanikiwa…’akasema na kucheka kicheko cha kishetani..

Tamaa ya Makabrasha sasa ilionekana wazi, kwani baada ya hapo, akatayarisha mkataba wa makubaliano kati yake na wamiliki wa makapuni na yakimuweka yeye kuwa kama mumiliki wa hisa nyingi kwenye kampuni ya mume wa familia,kama alivyozoanisha kwenye huo mkataba.

Yeye hakuishia hapo,akatayarishwa mkataba mwingine ambao mali yangu ikiwemo hospitali ya mume wangu yeye pia awe na hisa na nayo yalishafikia hatua ya mwisho, na kama kikao kile cha kusaini huo mkataba kingelipita basi ungelisikia makali yake, lakini hakikufanikiwa kwani ndio siku Makabrasha aliuwawa...’akasema na kutulia, mwenyekiti alipoona mungumzaji katulia akamuuliza.

‘Kwahiyo kutokana na maelezo yako wewe, inavyoonekana kabisa ni wewe mlishirikiana na mpenzi wako, yaani mume wa familia kumzimisha huyo mtu au sio..hatuingilii mambo ya polisi, ila hadi hapo inavyoonekana ni hivyo, mengine ni kazi ya polisi, au sio, ? akauliza mwenyekiti akiangalia saa yake.

‘Ndugu mwenyekiti umenionya nisiingilie huko, lakini nikifanya hivyo, ina maana kuwa ukweli halisi wa kifo hicho hautweza kujulikana …’akasema mzungumzaji.

‘Kwahiyo unataka uendelee, natamani ufanye hivyo, ila uwe makini..maana wahusika wenyewe wapo huko nje wanasikiliza..’akasema na wajumbe wakatizama nje, hawakuona mtu, na mzungumzaji yeye akaendelea kuongea…

‘Kifo cha Makabrasha ni tukio ambalo halikutarajiwa…japokuwa huyu mtu alikuwa na maadui wengi sana, lakini kutokana na jinsi alivyokuwa amejiweka ulinzi wa kila namna kutoka ofisini kwake hadi nyumbani, alikuwa na albi,..uhakikisho wa kujilinda kuwa hana kosa,

Kwa namna hiyo maadui zake, au yoyote aliyeathirika na mambo yake alikuwa na kisasi naye, …tatizo ikawa ni nani wa kumvika paka kengele,..na watu hujiuliza ni kwanini hakikutokea mapema, kwanini kifo chake kije kutokea muda huo. Muda ambao kampeni zinaanza..muda ambao watu wake wangemuhitajia sana, kwa mantiki hii polisi wanawaondoa watu wake kama washukiwa au sio…!!

‘Kumbuka kauli yake, ..sasa hivi hawataniweza tena, hata hao mabosi wangu, ..kauli hii imeficha siri kubwa sana, kuwa kwa kusema hata mabosi zangu ina maana kulikuwa na msigishano mwingien kati yake na mabosi zake walishafikia sehemu wanamuogopa, lakini kwa polis hilo halina nguvu, kwanini, jiulizeni sana hapo…’akatulia.

‘Lakini angalia haya aliyoyafanya, ina maana kama siku ile ule mkataba ungeliwekwa sahihi na mume wa familia, basi…mume wa familia angelikuwa hana chake, docta, na wengineo wengi, ambao walitegwa na huyu jamaa, na kwa mtaji huo wangalipoteza hisa za makampuni yao, na wengine huenda ingekuwa ndio mwisho wa utajiri wao, je hawa wanaweza kuwa washukiwa wakubwa, kwa mtizamo wa polisi ndio…ndio maana hapa tunashukiwa, hapa ndio kutapatokana muaaji kwa mtizamo wa polisi...

Mkataba ule ulikuwa na mambo mengi sana..iliyokuwa imebakia ni sahihi moja ya mume wa familia, wengine kwa namna moja walisharubuniwa, kuacha mume wangu ambaye bado alikuwa anasua sua, lakini hata yeye alishawekwa sawa, anajua kwa vipi..

Hadi hapo swali la kujiuliza huo mkataba mkubwa ambao, uliwajumuisha watu wengi, upo wapi…’akawa kama anauliza

Japokuwa kila mmoja alikuwa na mkataba wake wa kukubaliana ambao ulikuwa ni siri kati yake na hao watu, ama kuuziana hisa au wanajua wenyewe, lakini kulikuwa mkataba mkuu,…

Siku ile mume wa familia naye alitakiwa kufika, kukubali kuwa madeni yake yatalipwa kwa kuuza hisa zaidi ya asilimia hamsini kwa Makabrasha, na ilitakiwa siki hiyo kila kitu kikamilike, kwani akitoka hapo anakwenda kusajili hiyo mikataba yake kwa wahusika.

‘Ina maana kulikuwa na mkataba mwingine ambao ni mkubwa zaidi..?’ akauliza mwenyekiti.

‘Ndio…huo ndio ulikuwa funga kazi, docta na wengineo walishaweka sahihi zao, au sio docta,…? ‘ akamuuliza docta

Docta akaduwaa, halafu akatikisa kichwa kukubali, lakini sio ile ya kukubali kabisa kabisa.

Siku ile aliyekuwa amebakia ni mume wa familia, yeye si mgonjwa, yupo hospitalini,lakini hiyo hali indewe kwa makini, au sio…lakini pia ni lazima na yeye aweke sahihi yake, ili nakala zote za mikataba zifikishwe kwa wahusika, mume wa familia anauza kampuni yake kwa mtu mwingine kwa hasara…au sio mume wa familia..’ akauliza muongeaji .

Kwa hali kama hiyo lolote lingeliweza kutokea, kwa hali kaam hiyo watu wengi walikuwa na hasira na mtu huyo,….na walishajua kuwa siku hiyo ndio siku ya hitimisho, wakichelewa …hawatakuwa na cha kwao…mauaji yakafanyika, na mikataba ikatoweka, iliyobakia ilikuwa na mume wa familia, jiulizeni kwanini ikawa hivyo..!

Ina maana huyo aliyefanya hiyo kazi, ya kummaliza Makabrsha aliutaka huo mkataba mkuu..mkataba uliobeba mambo mengi, ambao ungempa mamlaka Makabrsha, na mikataba mingine ya watu mbali mbali pia haikuonekana tena..ukabakia wa mume wa familia..polisi waliwafuatilia wale wote waliowahi kuandikishana na marehemu, lakini wote hawana habari…hawajui, ..ni kwanini.

Swali kwanini polis waendelee kuwaona watu kadhaa ndio wauaji, wakati hali kama hiyo wauaji wanaweza wakawa mapapa makubwa tu…mumeona hapo ilivyo..ni kwanini, hivi mnanielewa lakini, kwanini …washukiwa wawe akina sisi, ambao, hatuna kitu …ni kwanini..

‘Ndugu mwenyekiti nahis hapo wewe una jibu zaidi ya sisi, ambao, tunajikuta kama nyasi zinazoumia baada ya mafahali kupigana, lakini ni lazima iwe hivyo…au sio mwenyekiti..’akasema shahidi na mwenyekiti akatabasamu na tabasamu lake likakatishwa na simu

Simu ya mwenyekiti ikalia…na mwenyekiti akapokea akawa anasikiliza kwa muda tu, na alipomaliza akasema

‘Mpaka hapo, tunaweza kusema kuwa ..wewe na mume wa familia mtakuwa mnafahamu ni nani muuaji, kama sio nyie wawili, kweli si kweli,…?’ akauliza mwenyekiti

‘Hahaha, mzee usiwe na pupa, subiria usikilize zaidi utaharibu kila kitu, kama utawasikiliza hao watu … je mzee haupo tayari kusikiliza sehemu ambayo itakusaidia hata wewe kwenye kupambana na huyo adui yako,…’akasema kama anauliza

‘Ninahamu sana ya kusikia hilo, lakini polisi hawataki …’akasema

‘Unajua kwanini hawataki, ..?’ akauliza muongeaji.

‘Mimi sijui, lakini ni muhimu kufuata sheria, au sio..?’ akauliza wajumbe

‘Lakini mwenyekiti, ngoja muongeaji aendelee ili tuone ukweli ulipo, kwasababu huenda haki isitendeke hapo, nahisi kama siasa inataka kuingilia haki…kwanini na sisi kama wanafamilia, tusifahamu ukweli,…’akasema mke wake

‘Sawa ngoja tuvunje sheria kidogo, ili tusikie zaidi, ..sawa shahidi unaweza kuendelea japokua tunakiuka sheria..’akasema mwenyekiti.

‘Sawa ndugu mwenyekiti, ila…kabla sijaingia sehemu hiyo ya pili, nawaombeni kitu kimoja...’akasita kidogo, na kuchukau leso kufuta jasho.

Mwenyekiti hapo akashikwa na butwaa huku akiangalia saa yake na simu ikawa analia kuashiria ujumbe wa sauti, yeye akazarau kuusoma huo ujumbe akasema;

‘Kitu gani unachotuomba, ..?’ akauliza mwenyekiti akiwa kashikilia simu tu, huku anamuangalia huyo shahidi kwa macho ya shauku, na mashaka fulani

‘Ni hivi ndugu mwenyekiti...’akaanza hivyo shahidi , huku simu ya mwenyekiti ikianza kuita…

NB: Je itakuwaje, ndio hitimisho au?


WAZO LA LEO:Kila mtu ana ndoto zake, na ndoto nyingine ni za kufikirika tu, hatuwezi kupanga kununua gari , kujenga nyumba, au kufanya jambo kubwa wakati uwezo huo hatuna. Tunaweza kuweka malengo hayo, kwa mipangilio ya kimaisha, lakini hatuwezi kulazimisha yale yaliyo juu ya uweze wetu, tupange kutokana na uwezo na kipato chetu. Zaidi ya hapo tutaingiwa na tamaa mbaya, ambayo mwisho wake ni kutenda dhuluma.
 
Back
Top Bottom