Mwanantogakulya
Senior Member
- Mar 18, 2025
- 157
- 155
Mwanaharakati mashuhuri Kanda ya ziwa,Thomas Nkola maarufu kwa jina la Mkulima, amechukua fomu ya kuomba kuteuliwa na chama cha ACT Wazalendo kugombea ubunge katika Jimbo la Maswa Magharibi wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu.
Amekabidhiwa fomu hiyo leo na Katibu wa chama hicho jimbo la Maswa Magharibi,Emanuel Numbili katika mji wa Malampaka uliopo wilaya ya Maswa.
Akizungumza baada ya kuchukua fomu hiyo amesema dhamira yake kuu ni kutetea maslahi ya wakulima wa pamba ambao kwa muda mrefu, wamekuwa wakikandamizwa kwa kupata bei ndogo ya zao hilo licha ya juhudi kubwa wanazoweka.
Pia soma Pre GE2025 Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema kuwa amekuwa mwanaharakati kwa kupambania wananchi hasa wafugaji na wakulima na sasa ameamua mapambano hayo ayapeleke bungeni ili sauti ya wananchi iweze kusikika na serikali kuchukua hatua kwa vitendo vyote vya ubadhirifu vinavyofanywa na viongozi wa serikali.
Nkola amehoji uhalali wa viongozi waliopo sasa, hasa wabunge wanaotoka kwenye maeneo yanayolima pamba, kuendelea kuwa sehemu ya wafanyabiashara wa zao hilo, jambo alilolieleza kuwa ni mgongano wa maslahi unaowazuia kutetea wakulima ipasavyo.
“Haiwezekani mbunge awe mnunuzi wa pamba, halafu tumtarajie atang’ang’anie bei nzuri kwa wakulima,kwa sababu hiyo, wakulima hawawezi kupata haki yao kwenye soko la pamba,”
“Nimechukua fomu si kwamba nataka kugombana na mbunge aliyepo sasa,siasa zangu si za ugomvi,najua mbunge wetu hawezi kulisemea zao la pamba kutokana na wabunge walio wengi na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika kanda ya ziwa na mkoa wa Simiyu wakiwemo, kujihusisha na biashara ya ununuzi wa zao hilo,”amesema.
Amesema kuwa na hivi karibuni atakwenda katika mahakama ya mkoa wa Simiyu kuwashtaki wabunge wote wa mkoa huo ambao wanajihusisha na biashara ya ununuzi wa zao la pamba kwani amegundua ya kuwa hao ndiyo wanaosababisha anguko la zao la pamba na kusababisha mkulima kutopata bei nzuri.
Ameongeza kusema kuwa mfumo wa sasa wa ununuzi wa pamba unawanyima wakulima nguvu ya kujadiliana kuhusu bei, huku baadhi ya viongozi wakitumia nafasi zao kunufaika binafsi.
Uchukuaji na urejeshaji wa fomu kwa nafasi za udiwani,ubunge na urais ndani ya ACT-Wazalendo utafungwa rasmi mei 28,2025.