GE2025 Mkulima auza tani 11 za mbaazi, kuzunguka kwenye kampeni za Samia

GE2025 Mkulima auza tani 11 za mbaazi, kuzunguka kwenye kampeni za Samia

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mkulima na pia Balozi wa Shina namba 2, Kitongoji cha Mkwajuni, Kijiji na Kata ya Mwenge Mtapika, Wilaya ya Masasi, Nickson Amlima, ametangaza kutumia fedha alizopata kutokana na mauzo ya zao la mbaazi tani 11, kufadhili safari yake ya kuzunguka nchi nzima na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kampeni za uchaguzi mkuu.

Amlima amesema hatua hiyo ni ishara ya kuthamini mchango mkubwa wa Dk. Samia kwa wakulima kupitia upatikanaji wa mbolea na pembejeo za ruzuku ambazo zimewawezesha wakulima kuongeza tija na kipato pia amepongeza uamuzi wa Mwenyekiti huyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwapa baiskeli mabalozi ili kuendesha shughuli zao za kichama kiwepesi.

Kwa nafasi yake ya balozi wa shina, Amlima amesema anaona ni wajibu wake kuwawakilisha mabalozi na wakulima wengine, kuonesha mshikamano na shukrani kwa kiongozi huyo anayewania urais kupitia CCM.

Amesisitiza kuwa uamuzi wake pia ni mfano wa namna wakulima na mabalozi wanavyohusisha mafanikio yao ya kila siku na sera za chama, na ndiyo maana amejitolea kuwa sehemu ya safari ya ushindi kuelekea Oktoba 29, 2025.

 
Back
Top Bottom