SoC02 Mkulima na nguvu zake

SoC02 Mkulima na nguvu zake

Stories of Change - 2022 Competition

Grace charles nzowa

New Member
Joined
Sep 2, 2022
Posts
1
Reaction score
0
Utangulizi
Mkulima ni nani? Mkulima ni mtu yeyote anaye jihusisha na shunguli za kilimo.
Aina za mkulima, mkulima mdogo, mkulima wa kati, mkulima mkubwa.

Uelewa juu ya kilimo
Wengi wetu hawajui nini maana ya kilimo, wakati kilimo ni uti wa mgongo kutokana na elimu ya kilimo kutokufika katika baadhi ya maemeo hasa vijijini.

Bwana matata ni mkulima kutoka katika kijiji cha buga yeye anajishughulisha na kilimo lakini yeye mwenyewe hajui anafanya aina gani ya kilimo kwasababu hana elimu ya kilimo bora hivyo yeye hulima kwa kutumia nguvu nyingi bila mafanikio.

Msimu uliopita amelima zaidi ya ekari tano na kutokana na ukosefu wa elimu ya kilimo na mabadiliko ya tabia ya nchi amejikuta kuangukia pua kwa kupata mazao machache kupita kiasi hivyo basi, serikali ingetoa mafunzo juu ya kilimo bora ili mkulima aweze kunufaika na kilimo hicho.

Serikali imetoa mbolea ya ruzuku kwa wakulima hilo tunalishkuru lakini elimu juu ya hiyo mbolea iliyotolewa ruzuku haijafika kwa wananchi. Mwananchi anajua baada ya kujiandikisha kwenye mbolea ya ruzuku yeye nafikiri kuwa hiyo mbolea anaipata bure au baada ya kuvuna mazao yake hivyo wananchi wanatakiwa kupewa elimu ya hiyo mbolea iliyotolewa.

Pia mkulima anatakiwa kupewa elimu juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na hii ni baada ya bwana matata kutoipata elimu juu ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kulima kwa kutumia uzorfu ameshindwa kupata mazao ya kutosha ambayo hata hayatoshi chakula cha familia yake.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom