PreGE2025 Mkulima Tinson Nzunda atangaza kugombea Ubunge jimbo la Vwawa

PreGE2025 Mkulima Tinson Nzunda atangaza kugombea Ubunge jimbo la Vwawa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Aliyekuwa Diwani wa Kata ya Nyimbili, Tinson Nzunda, ametangaza rasmi nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Vwawa, akiahidi kuleta mabadiliko ya maendeleo endelevu kwa wananchi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Vwawa, Nzunda amesema ameamua kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho baada ya ushawishi mkubwa kutoka kwa wananchi waliomtaka awatumikie katika ngazi ya kitaifa.

“Nina uzoefu, dira na dhamira ya dhati kushughulikia changamoto za Vwawa kama vile miundombinu, kilimo, ajira kwa vijana na huduma bora za kijamii,” alisema Nzunda.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Tangazo hilo limetolewa siku moja kabla ya Bunge kuvunjwa rasmi tarehe 27 Juni 2025, na kumaliza kipindi cha Mbunge aliyepo, Japhet Hasunga ambae ametumikia kwa vipindi viwili miaka 10.

Nzunda amesema kampeni yake haitahusisha matusi wala siasa za chuki, bali itajikita kwenye hoja na vipaumbele vya wananchi. Ametaja sekta ya kilimo, ujasiriamali na ushiriki wa vijana kama nguzo kuu za ajenda yake ya maendeleo.

“Mimi si mgombea wa maneno, bali wa vitendo. Nimeishi na watu wa Vwawa, najua changamoto zao, na nina mipango ya kuzitatua,” alisisitiza.

Screenshot 2025-06-26 190621.png
 
Back
Top Bottom