GodfreyTajiri
JF-Expert Member
- Sep 26, 2010
- 1,001
- 704
I am interested to know who are economic advisers of our President kwasababu watakuwa wanaishi labda nchi tofauti na hii tunayoishi. Nauliza hivi kwasababu economic advisers wa rais ndio wana sauti ya mwisho kwa rais na wao ndio wanatoa independent view ya ishu muhimu ambazo rais anapelekewa na waziri na gavana wake. Vile vile wao ndio wanatengeneza mbadala wa mapendekezo ya waziri au gavana wakiona ni bomu. Hivyo tujiulize washauri wa rais akina nani tutapata kujua tatizo liko wapi.
naamini ni dr philip mpango, dr khamisi mwinyimvua and mrs elsie kanza.
kama sikosei dr. mwinyimvua alifundishwa na prof. ndulu udsm
Nashukuru Juma contena. Kuhusu magazeti, hakuna lililo bora kuliko mtandao wa JF - mengi ni aidha uchwara au yamenunuliwa na mafisadii. Kinachosubiriwa kwa hamu na wananchi ni teknolojia rahisi ya wao kuweza kuwa sehemu ya JF. Siku hiyo inakuja kwani teknolojia haimtupi mja wake.
Una CV zao mkuu utusaidie maana itaweza kutoa mwangaza wa kitu wanachokishauri. Mfano kama ni watu wa labour economics watakuwa wanapenda serikali itoe misaada kwa makampuni na wafanyakazi. Kama ni watu wa financial economics watakuwa wanapendelea kusaidiwa kwa sekta za mabenki na kadhalika. Kama unayo CV utusaidie. Vile vile kama sio wachumi tufahamu kama hilo nalo tatizo.
Una CV zao mkuu utusaidie maana itaweza kutoa mwangaza wa kitu wanachokishauri. Mfano kama ni watu wa labour economics watakuwa wanapenda serikali itoe misaada kwa makampuni na wafanyakazi. Kama ni watu wa financial economics watakuwa wanapendelea kusaidiwa kwa sekta za mabenki na kadhalika. Kama unayo CV utusaidie. Vile vile kama sio wachumi tufahamu kama hilo nalo tatizo.
Mkuu,
Kwanza kuhusu SME sio kweli kwamba sasa hivi wapo chini it is among the key booming financial sector in our country with an estimate portfolio around $2 Billion. SME ndio wamesababisha NMB kuwa benki iliyoongoza kwa kupata faida nchini. CRDB na NBC ambazo zimekijika katika corporate lending wameachwa mbali na NMB. Hivyo kusema SME ni sekta ndogo I do not think you are correct anyway hilo sio la msingi.
Pengine tuassume kweli construction, trade (which I suspect you are also mixing with manufacturing) are the leading lending sector in the country. Wakisema waongeze interest rate na kupunguza money available for lending what will happen? Kwanza sekta ya ujenzi gharama za ujenzi zitapanda na serikali ambayo some of the construction projects wana guarantee wataend up kulipa zaidi. Vile vile constructions projects involves large corporate investment na gharama zikipanda eventually mtumiaji wa huduma hizo ndio atakayeishia kulipa gharama hizo kwasababu bei za vitu zitaongezeka na serikali haitakuwa na budi bali kuongeza kodi iweze kumudu gharama hizo.
Tukihamia corporate lending especially kwa wafanyabiashara kama Bakhressa, Mohamed Enterprises etc wakipandishiwa interest ya mkopo ni mtumiaji wa unga wa Bakhressa au Mchele wa Mohamed Enterprises ndie atakayeishia kulipia gharama ya ziada. Hivyo utaona the multiplier effect ya kupanda interest on credit itahamishiwa kwa mtumiaji wa kawaida ambaye ni mlalahoi.
!
| Year | Percentage |
| 1990 | 34% |
| 1991 | 29% |
| 1992 | 29% |
| 1993 | 32% |
| 1994 | 27% |
| Year | Capital Inflows (%) | GDP Growth (%) |
| 2009 | 1.9 | 6.7 |
| 2008 | 1.9 | 7.4 |
| 2007 | 3.5 | 7.1 |
| 2006 | 2.8 | 6.7 |
| 2005 | 6.6 | 7.3 |
| 2004 | 3.4 | 7.8 |
| 2003 | 3.7 | 6.9 |
| 2002 | 3.8 | 7.1 |
| 2001 | 3.7 | 6.0 |
| 2000 | 4.5 | 5 |
| | 2002 | 2003 | 2004 | 2005 | 2006 | 2007 | 2008 | 2009 | 2010 |
| Agriculture | 28.6 | 28.7 | 29.5 | 27.6 | 26.2 | 25.7% | 24.6% | 25.5% | 26.5 |
| Mining | 2.1 | 2.4 | 2.6 | 2.9 | 3.2 | 3.5 | 3.3 | 3.5 | 3.7 |
| Manufacturing | 8.3 | 8.3 | 8.1 | 7.9 | 7.8 | 7.8 | 8.3 | 9.4 | 10.2 |
| Electricity | 2 | 1.9 | 1.8 | 1.7 | 1.5 | 1.6 | 1.7 | 1.8 | 2.0 |
| Water Supply | 0.5 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.5 |
| Construction | 6.8 | 8 | 7.9 | 7.8 | 7.8 | 7.8 | 7.9 | 8.6 | 9.4 |
| Trade and Repair | 12.4 | 12 | 11.4 | 11 | 11.4 | 11.5 | 11.8 | 12.7 | 13.8 |
| Hotel and Restaurants | 2.6 | 2.4 | 2.3 | 2.5 | 2.6 | 2.7 | 2.3 | 2.4 | 2.3 |
| Transport | 5 | 4.8 | 4.6 | 4.4 | 4.3 | 4.2 | 5 | 5.3 | 5.7 |
| Communication | 1.2 | 1.3 | 1.5 | 1.7 | 1.7 | 2.3 | 2.1 | 2.6 | 3.2 |
| Financial Services | 1.7 | 1.7 | 1.6 | 1.7 | 1.7 | 1.6 | 1.7 | 1.8 | 2.0 |
| Real estate | 9.7 | 9.4 | 9.1 | 8 | 9.6 | 9.5 | 9 | 9.7 | 10.3 |
| Public administration | 7.2 | 7.2 | 7.7 | 7.7 | 8 | 8 | 8.1 | 8.7 | 9.3 |
| Year | Annual Growth | (% of GDP) | Value added per worker in dollars |
| 2009 | 3.2 | 28 | $283 |
| 2008 | 4.5 | 29 | $281 |
| 2007 | 4 | 29 | $275 |
| 2006 | 3.8 | 30 | $270 |
| 2005 | 4 | 31 | $266 |
| 2004 | 5.9 | 33 | $261 |
Mdondoaji,
Thanks for the data on SMEs and the $2 billion figure ya credit to the sector. Sijui nilisoma wapi lakini kwamba leading sectors zinazopata mikopo Tanzania ni Construction (ujenzi wa barabara, majengo makubwa na real estate) ikifuatiwa na trade; nitaendelea kuzitafuta ili nizichunguze zaidi, otherwise you have a point.
Kuhusu NMB kupata faida kutokana na credit to SMEs, I can understand that ila tujue kwamba mikopo mingi sana to SMEs ni government guaranteed, sio mikopo ambayo benki zenyewe zinafanya maamuzi yake ya ndani based on credit scores etc; kwa mfano, in 2006 – 2007, the government set aside Tsh 21 billion for soft loans to micro and small enterprise in Tanzania wakati Zhakia Meghji akiwa Waziri wa fedha. Ninachofahamu ni kwamba watu wengi walichukua mikopo hii, some kwa njia sahihi, some kwa njia ya upendeleo na mrejesho wake hatuujui. Inawezekana zimerudi, inawezekana mrejesho wake unasua sua Kwahiyo kuzidi kuchangia inflation. But the bottom line is, kwa fedha kama hizi kutoka serikalini kwenda into the public hands (via soft loans to SMEs), serikali yoyote makini itazipeleka kwenye benki zake, sio benki za nje, ndio maana banks kama NMB wakawa wa kwanza katika list kusaidia serikali kuzisukuma fedha hizi kwa SMEs.
Kitu ambacho bado kinanitatiza kuelewa ni kwamba je:
Hizi government guaranteed loans to SMEs, are these part of the domestic credit provided by the banking sector?
Are these included katika figures telling us the percentage of firms using banks to finance investment?
Sina majibu but I can try to shed light into this – according to the latest figures, domestic credit provided by the banking sector is only 18%; swali la kujiuliza, nani ndio wanapata hizi and where is rest of the 82% of the domestic credit come from? Is it from outside the country? Vinginevyo, one doesn't need to be Albert Einstein to realize kwamba kama 18% is the total domestic credit provided by the banking sector ambayo hiyo hiyo ndio Mkullo anaenda kuomba Stanbic, Standard Chattered kujalizia kwenye bajeti yake; na kama ni hizo hizo mining companies and other Multi nationals wanaziwinda, then ushindani hapo ni mkubwa sana na hivyo SMEs za Tanzania katika ushindani huu watakuwa marginalized; na hivyo kuchochea uwepo wa uchumi uchwara to the majority of Tanzanians (over 70%).
Food for thought
Miaka ya 1990 – 1994, Tanzania ilikuwa ranked as the 3[SUP]rd[/SUP] poorest country in the world only ahead of Somalia and Afghanistan. Lakini takwimu on domestic credit provided by the banking sector katika miaka hiyo zinaonyesha hii figure ilikuwa record breaking, swali la kujiuliza ni je, nani alikuwa anapewa fedha hizi na zilikuwa zinafanya nini kwenye uchumi?
Jedwali: Domestic Credit provided by the bang sector
Year Percentage 1990 34% 1991 29% 1992 29% 1993 32% 1994 27%
Source: World Bank Tables…
Kwanini domestic credit provided by the banking sector ikiwa juu, watanzania ndio wanazidi kuwa chini zaidi? Something is Fundamentally Wrong, na ndio Uchumi Uchwara ninao uongelea.
Let us look at another set of figures
Tuangalie takwimu on firms using banks to finance investments (out of all firms in Tanzania). In 2001, about 24% of all registered firms in Tanzania obtained their sources of investments from banks. Cha ajabu ni kwamba, by 2003, that figure had dropped to 6%. Tukumbuke pia kwamba Tanzania started to record impressive economic growth from the 2000-2001 financial year (over 6%) and we haven't gone below that since then; Kulikoni wakati uchumi unazidi kushika kasi, domestic credit to domestic firms inashuka from 24% to 6%? Mind you, GDP growth katika kipindi hicho was as follows:
2001 = 6.1%; 2002 = 2002%; 2003 = 7.0%; and 2004 = 7.8%;
Sasa this impressive growth was for who? Kwani hata marekani sasahivi, an increase in GDP growth by even 0.05% will put Obama back on track to win back the white house; Sasa kwetu sisi uchumi huu ulikuwa na unakua for who? For the elite? For wawekezaji who then wanabeba faida zao zote na kukimbiza nje? Katika bahati kama hii ya kukua uchimi kwa kasi hivi, tunakusanya kodi?
Something is fundamentally wrong here, the impressive growth we have been experiencing is not pro – poor growth bali uchumi ni uchwara wa Mkullo na Ndullu. Pia kuna an indication kwamba, ile figure yako ya $2billion as credit that went to SMEs usikute ilienda to only a handful of SMEs, tunaweza shikwa na butwaa kama tutapata data on who and how many SMEs provided with that credit. Waliopo bungeni watusaidie majibu ya hili, lakini tusisahau kwamba mpaka kikao cha mwisho cha Bunge kilipokuwa kinamalizika, Mkullo alikuwa anabania list aliyoamriwa na Spika aitoe juu ya masuala ambayo yanafanania na haya tunayozungumza.
SMEs have been extended with credit as you put it rightly, but we don't know the quantity and quality of it (in terms of SMEs); and this still makes many of us believe kwamba access ya SMEs to credit in large part bado ni tatizo. Based on the figure ya 2003 telling us kwamba it was only 6% of the firms in Tanzania that relied on domestic banks as source of capital/investment, ingawa hatuna figure za leo, I doubt kama things have gotten better. Na tusisahau kwmba domestic credit provided by the banking sector was juu sana in early to mid 1990s but still Tanzanians walitumbukia into extreme poverty kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya nchi yao.
Sasa kama banking sector in Tanzania inachangia kiasi kidogo hivyo to firms' credit, then what are their other sources?
An obvious answer is fedha za nje, unless kama mtu ana taarifa ya uwepo wa unofficial source of capital. Otherwise data on fedha za nje (official) zipo, so les try make sense of them: Below ni takwimu on private inflows toka nje ambazo zinakuja kama investment capital kwenye uchumi wetu Tanzania. It is obvious kwamba majority of foreign capital inflows zinaenda katika uwekezaji kwenye miradi aidha foreign owned by 100%, au yenye ubia na government au yenye ubia na wazawa (wenye bahati hiyo). Ni chenji ndogo sana ambazo zinaenda kwenye Dar stock market as portfolio investments kwani DSE is still at a very infant stage. Mfano, Portifolio inflows (DSE) in 2009 was only about USD 3 million.
Now figures below za private capital flows ni pamoja na zile wenzetu ‘wazawa' wenye bahati ya kuwa na heka zao kadhaa na kufanikiwa kumpata mwekezaji toka nje aje alime nae mazao, au mzawa mwenye kiwanja chenye thamani kwahivyo mwekezaji anakuja kujenga hoteli, apartments etc.
Jedwali: Private capital inflows into Tanzania (2001 – 2009)
Year Capital Inflows (%) GDP Growth (%) 2009 1.9 6.7 2008 1.9 7.4 2007 3.5 7.1 2006 2.8 6.7 2005 6.6 7.3 2004 3.4 7.8 2003 3.7 6.9 2002 3.8 7.1 2001 3.7 6.0 2000 4.5 5
Source: World Bank
Tunagundua haraka kwamba by 2009, we were at the lowest point in terms of foreign capital inflows i.e at 1.9% katika kipindi cha miaka kumi (2000 – 2009) na pia tunagundua kumbe ule uchumi ulioanza kukua kwa kasi ya ajabu ulitokana na mitaji toka nje, sio za ndani which is understandable. Cha kuangalia kwa ukaribu hapa ni: Kwanini hapo awali tuliona domestic credit provided by the banking sector (ambayo ofcoz ndio source kubwa kwa SMEs) ilikuwa inazidi kuteremka huku GDP ikipaa na foreign capital entry nayo ikipaa? Hii inaonyesha kwamba huu sio uchumi wetu, ni uchumi wa ‘wenyewe';
Tumalizie kwa kuangalia, je hizi capital inflows from nje zilienda ku stimulate what economic activities na hizi activities zina real value ya namna gani kwa the 70% of Tanzanians. Tunachojaribu ni kuangalia ule uchumi ulioanza kupaa from the year 2000 ambao uliambatana na kushuka kwa domestic credit from banks to firms in Tanzania sambamba na an increase in foreign capital flows kwenda kuwekezwa kwenye various sector, nani ametajirika na nani amezidi kuwa maskini, na kwanini maskini kawa maskini na tajiri kawa tajiri?
Jedwali: Sectoral contribution to real GDP by economic activities (%)
2002 2003 2004 2005 2006 2007 2008 2009 2010 Agriculture 28.6 28.7 29.5 27.6 26.2 25.7% 24.6% 25.5% 26.5 Mining 2.1 2.4 2.6 2.9 3.2 3.5 3.3 3.5 3.7 Manufacturing 8.3 8.3 8.1 7.9 7.8 7.8 8.3 9.4 10.2 Electricity 2 1.9 1.8 1.7 1.5 1.6 1.7 1.8 2.0 Water Supply 0.5 0.4 0.4 0.4 0.4 0.4 0.4 0.4 0.5 Construction 6.8 8 7.9 7.8 7.8 7.8 7.9 8.6 9.4 Trade and Repair 12.4 12 11.4 11 11.4 11.5 11.8 12.7 13.8 Hotel and Restaurants 2.6 2.4 2.3 2.5 2.6 2.7 2.3 2.4 2.3 Transport 5 4.8 4.6 4.4 4.3 4.2 5 5.3 5.7 Communication 1.2 1.3 1.5 1.7 1.7 2.3 2.1 2.6 3.2 Financial Services 1.7 1.7 1.6 1.7 1.7 1.6 1.7 1.8 2.0 Real estate 9.7 9.4 9.1 8 9.6 9.5 9 9.7 10.3 Public administration 7.2 7.2 7.7 7.7 8 8 8.1 8.7 9.3
Source: Delloitte
Maswali:
- Tunaona kwamba GDP inachangiwa sana na activities za kilimo.
Jedwali: Agriculture Value Added
- Je, how much investment goes to Kilimo?
- Je, mchango wa kilimo unatokana na quality of investment or quantity of peasants (70% of the labour force)?
- Jibu ni kwamba takwimu hizi strongly suggest kwamba kilimo hakipati much credit flows na ingawa huko ndio majority of labour force ipo. Huo ndio uchumi uchwara wa Mkullo. The real quality ya contribution of sekta ya kilimo can be seen from value added figures below.
Year Annual Growth (% of GDP) Value added per worker in dollars 2009 3.2 28 $283 2008 4.5 29 $281 2007 4 29 $275 2006 3.8 30 $270 2005 4 31 $266 2004 5.9 33 $261
Source: World Bank
Note: Value added per worker in 1990 was $219, so only a change of $83 in 20 years.
Je tukirudi kwenye Jedwali letu la awali on: Sectoral Contribution to real GDP by economic activities (hapo juu):Je, ni sekta gani nje ya kilimo zina intense economic activities? Je zina linkages zipi na majority of Tanzanians (70%) vijijini? Tumeshaona kilimo kina mchango ingawa wakulima hawapati mikopo yoyote ya maana; je watanzania wengi (out of the 70%) wapo katika sekta nyingine zipi ili tujue wanafaidika vipi? kwani kwa kwaida, the more economically active the sector, the more attractive it becomes to the banking sector, thereby faidisha wazawa. I have figures ‘valued added' figures za manufacturing sector (chemicals, food beverages, textiles and clothing, machinery and transport equipments), kwa kweli ni za kusikitisha, san asana kutokana na matatizo ya umeme lakini pia low productivity ya the manufacturing sector in general, sasa sijui tatizo ni access to credit? Small domestic market? Inferior technology to compete with foreign goods nje as well as imported goods? Lack of innovation? Poor sectoral policies, atleast from the implementation perspective? I don't know, but all I know is Uchumi wa Mkullo na Ndullu ni Uchwara.
- Nadhani tayari tunapata picha halisi ya uchumi uchwara wa Mkullo in the context of "KILIMO KWANZA" kwani hapo juu we see kwamba value added kwenye sekta ya kilimo is actually declining.
Sijakuelewa Dar si Lamu....
Godwine,
Wewe sio uliyesema unapendelea Shillingi ishuke zaidi. Halafu huu ushauri la viwanda unaweza kutuambia viwanda bila ya watu hela mifukoni hivyo viwanda vitamuuzia nani bidhaa??? Viwanda bila ya umeme vitazalisha nini? Ushauri wako nadhani umekaa kisiasa zaidi ya kitaaluma i suggest fikiria vizuri zaidi kwani viwanda haviwezi kuokoa uchumi wa Tanzania kwasasa.
Mkulo na Ndulu have themselves to blame for this disaster kwasababu walikuwa wanaopportunity kuavert hii crisis kabla haijakuwa worse off. Hakuna mtu ana chuki binafsi (kama kawaida yetu kila kitu tunachukulia siasa tu) ila tunasemea kwamba wanatakiwa waact in the interest of the nation na sio kufanya maamuzi ya kisiasa. Umeme limekuwa tatizo tangu 2009 kwanini waziri wa fedha asimshinikize waziri mwenzie wa nishati kulitafutia ufumbuzi wa kudum
u? Kwanini waziri wa fedha asitenge budget (emergency budget to save the nation from the brink of economic collapse)? Kwanini waziri asiwe na alternative plan ya kuongeza vyanzo vya kodi ikiwa sekta ya uzalishaji na huduma itazorota baada ya matatizo ya umeme?
Wanalaumika kwa kuwa tu wameachia mzunguko mkubwa wa fedha katika uchumi uliotokana na kuingiza fedha mpya na zamani. Matokeo yakawa kuongezeka kwa purchasing power na inflationary pressures.
Hakuna mtu ana chuki binafsi na mtu
Mchambuzi ,
Narrowness of the credit sector inatokana na factors nyingi na wewe umeangalia upande mmoja tu wa serikali na priorities zake but among other factors is tabia ya mabenki ya nchini kuwa tabia ya kuogopa kukopesha watu wa kawaida. Hivyo badala ya kulaumu serikali pekee na sisi watanzania we share the part of the blame kwa kutokuwa waaminifu na matapeli katika mahusiano yetu na mabenki. Kuhusu government guarantee loans to SMEs niliwahi kusema mwaka 2009 kuwa hilo ni another EPA in the making since no one knows who needs the money to borrow and what agricultural sectors needs the loan.
Labda nikuulize Mchambuzi wewe unashaurije akina Mkulo na Ndulu nini wafanye kuokoa hali iliyopo?
Nashukuru sana Ndinani kwa kunipa moyo kwani mimi nia yangu ni kutoa mchango wangu tu badala ya kulalamikia serikali vijiweni. Kuhusu Magazeti, aslimia ya watanzania wanaosoma magazeti sio zaidi ya 2% Ndinani, njia nzuri ya kuwafikia wengi ni kupitia mijadala ya kwenye Radio kwani vijana wengi hivi sasa wamekuwa na interest kubwa sana ya kusikia mijadala kuhusu maendeleo ya nchi; kwahiyo vijana kadhaa wakijipanga na mada zao watawaifikia wengi sana, hasa wa vijijini; ila kuhusu wabunge, kama unaona content yangu ina mambo mazuri for them to grasp, njia ya gazeti hapo itafaa kwa kweli, nashukuru sana kwa ushauri huo;
Kuhusu Lipumba, nilimtaja tu kama mwanasiasa ambae kabobea katika uchumi na huwa ana hoja nzuri sana, sasa ili apimwe, ushauri wangu ni kwamba Rais amteue mbunge na ampe nafasi katika kamati ya Kigoda ya uchumi na Fedha tuone mchango wake, vinginevyo upo sahihi kabisa kwamba kuna wachumi wazuri sana ambao hawapo in main stream thoughts. Kuhusu Rwegasira nimemsoma sana na nakubaliana na wewe juu ya uwezo wa mtu huyu, ila bado yupo huyu mtu? Kuna kitabu chake nilisoma, cha siku nyingi but still very useful alikiandika na wenzake - Green (from University of Sussex) and Brian Arkadie (from institute of Social Studies, the hague) - kitabu cha 1982 titled - Economic Schocks and National Policy Making: Tanzania in the 1970s; this is a very good read.
kwanza kabisa, naomba niseme hakuna anaetoa lawama hapa kwa serikali mdondoaji, at least not me, what i am doing is 'nina hoji', na natumia takwimu hizo hizo zinazotolewa na serikali, nimejaribu kukaa mbali kabisa na siasa, i am talking numbers and policy mzee;
Kuhusu credit to SMEs, kama umekuwa unanifuatilia, especially in the context of my original post, nimeongelea sana about the relationship between the banking sector and SMEs, independently from the role of the government in this mix; kwakifupi, what Ndullu did with the bank rate and the cash reserve requirement was to control the flow of credit from banks to domestic firms (SMEs included) and we had a discussion on that;
Kuna tatizo kama unavyosema kwa upande wa watanzania pia in terms of uaminifu and stuff when it comes to mikopo but kwa bahati mbaya, sababu hiyo hiyo imekuwa kichaka kwa taasisi zetu za fedha kukwepa watanzania wengine ambao they are credit worthy; ila tatizo hili linaanza kupungua ingawa safari bado ni ndefu sana; tatizo kubwa la watanzania wengi juu ya mikopo sio uaminifu, ni collateral, otherwise benki haitumii vigezo vya uaminifu kumpa mtu mkopo, labda marekani kwenye nchi yenye credit system whereby mtu au taasisi inaangaliwa credit history yake; miaka ya mwisho ya utawala wa mkapa alianzisha mkakati mzuri sana wa ku formalize assets za watanzania akisaidiwa na mchumi mmoja aliekuwa mshauri wake kutoka south america, someone 'desoto'; desoto argued kwamba kuna so much dead capital in Tanzania but just because haina hati na haijafanyiwa valuation, inaonekana useless; he even came up with a figure showing such assets to be in billions of dollars; upon completion, mradi huu ulikuwa usaidie watu sasa wawe na title deeds za viwanja vyao, mashamba yao, nyumba zao na ziwe na valuation so that mtu akitaka kwenda kuchukua mkopo benki asipate shida; serikali ya sasa sijui kama ili pick up from Mkapa on that; washauri wa mkapa kiuchumi kina Kwaku (mghana from the world bank), hernando desoto na wao wakayeyuka wakati administration nyingi huwa zinawabakiza wataalam kama hawa hata kama anaechukua nchi ni mtu kutoka chama kingine cha upinzani; mfano Obama ameacha watu wengi tu, hata Greespan alibakia;
Kuhusu swali lako je Mkullo na Ndullu wafanye nini kuokoa hali iliyopo, hiyo ndio sababu yangu ya kuleta hii mada ili tuijadili mzee; mimi siwezi kuwa na jibu, nachofanya ni kuchukua hoja mbalimbali humu na kuzifanyia kazi zaidi kwa kuzichambua then kurudisha mawazo yangu kama nimevyokuwa nafanya. Ni wajibu wetu wote interested in this thread kukubadilana na diagnosis then propose cure kwa pamoja na vile vile prevention; it is my belief kwamba we are doing great on that end so far na nashukuru sana for your valuable input;
naamini ni dr philip mpango, dr khamisi mwinyimvua and mrs elsie kanza.
kama sikosei dr. mwinyimvua alifundishwa na prof. ndulu udsm