Mdondoaji,
Thanks for the data on SMEs and the $2 billion figure ya credit to the sector. Sijui nilisoma wapi lakini kwamba leading sectors zinazopata mikopo Tanzania ni Construction (ujenzi wa barabara, majengo makubwa na real estate) ikifuatiwa na trade; nitaendelea kuzitafuta ili nizichunguze zaidi, otherwise you have a point.
Kuhusu NMB kupata faida kutokana na credit to SMEs, I can understand that ila tujue kwamba mikopo mingi sana to SMEs ni government guaranteed, sio mikopo ambayo benki zenyewe zinafanya maamuzi yake ya ndani based on credit scores etc; kwa mfano,
in 2006 – 2007, the government set aside Tsh 21 billion for soft loans to micro and small enterprise in Tanzania wakati Zhakia Meghji akiwa Waziri wa fedha. Ninachofahamu ni kwamba watu wengi walichukua mikopo hii, some kwa njia sahihi, some kwa njia ya upendeleo na mrejesho wake hatuujui. Inawezekana zimerudi, inawezekana mrejesho wake unasua sua Kwahiyo kuzidi kuchangia inflation. But the bottom line is, kwa fedha kama hizi kutoka serikalini kwenda into the public hands (via soft loans to SMEs), serikali yoyote makini itazipeleka kwenye benki zake, sio benki za nje, ndio maana banks kama NMB wakawa wa kwanza katika list kusaidia serikali kuzisukuma fedha hizi kwa SMEs.
Kitu ambacho bado kinanitatiza kuelewa ni kwamba je:
Hizi government guaranteed loans to SMEs, are these part of the domestic credit provided by the banking sector?
Are these included katika figures telling us the percentage of firms using banks to finance investment?
Sina majibu but I can try to shed light into this – according to the latest figures, domestic credit provided by the banking sector is only 18%; swali la kujiuliza, nani ndio wanapata hizi and where is rest of the 82% of the domestic credit come from? Is it from outside the country? Vinginevyo, one doesn't need to be Albert Einstein to realize kwamba kama 18% is the total domestic credit provided by the banking sector ambayo hiyo hiyo ndio Mkullo anaenda kuomba Stanbic, Standard Chattered kujalizia kwenye bajeti yake; na kama ni hizo hizo mining companies and other Multi nationals wanaziwinda, then ushindani hapo ni mkubwa sana na hivyo SMEs za Tanzania katika ushindani huu watakuwa marginalized; na hivyo kuchochea uwepo wa uchumi uchwara to the majority of Tanzanians (over 70%).
Food for thought
Miaka ya 1990 – 1994, Tanzania ilikuwa ranked as the 3[SUP]rd[/SUP] poorest country in the world only ahead of Somalia and Afghanistan. Lakini takwimu on domestic credit provided by the banking sector katika miaka hiyo zinaonyesha hii figure ilikuwa record breaking, swali la kujiuliza ni je, nani alikuwa anapewa fedha hizi na zilikuwa zinafanya nini kwenye uchumi?
Jedwali: Domestic Credit provided by the bang sector
| Year | Percentage |
| 1990 | 34% |
| 1991 | 29% |
| 1992 | 29% |
| 1993 | 32% |
| 1994 | 27% |
Source: World Bank Tables…
Kwanini domestic credit provided by the banking sector ikiwa juu, watanzania ndio wanazidi kuwa chini zaidi? Something is Fundamentally Wrong, na ndio Uchumi Uchwara ninao uongelea.
Let us look at another set of figures
Tuangalie takwimu on firms using banks to finance investments (out of all firms in Tanzania). In 2001, about 24% of all registered firms in Tanzania obtained their sources of investments from banks. Cha ajabu ni kwamba, by 2003, that figure had dropped to 6%. Tukumbuke pia kwamba Tanzania started to record impressive economic growth from the 2000-2001 financial year (over 6%) and we haven't gone below that since then; Kulikoni wakati uchumi unazidi kushika kasi, domestic credit to domestic firms inashuka from 24% to 6%? Mind you, GDP growth katika kipindi hicho was as follows:
2001 = 6.1%; 2002 = 2002%; 2003 = 7.0%; and 2004 = 7.8%;
Sasa this impressive growth was for who? Kwani hata marekani sasahivi, an increase in GDP growth by even 0.05% will put Obama back on track to win back the white house; Sasa kwetu sisi uchumi huu ulikuwa na unakua for who? For the elite? For wawekezaji who then wanabeba faida zao zote na kukimbiza nje? Katika bahati kama hii ya kukua uchimi kwa kasi hivi, tunakusanya kodi?
Something is fundamentally wrong here,
the impressive growth we have been experiencing is not pro – poor growth bali uchumi ni uchwara wa Mkullo na Ndullu. Pia kuna an indication kwamba, ile figure yako ya $2billion as credit that went to SMEs usikute ilienda to only a handful of SMEs, tunaweza shikwa na butwaa kama tutapata data on who and how many SMEs provided with that credit. Waliopo bungeni watusaidie majibu ya hili, lakini tusisahau kwamba mpaka kikao cha mwisho cha Bunge kilipokuwa kinamalizika, Mkullo alikuwa anabania list aliyoamriwa na Spika aitoe juu ya masuala ambayo yanafanania na haya tunayozungumza.
SMEs have been extended with credit as you put it rightly, but we don't know the quantity and quality of it (in terms of SMEs); and this still makes many of us believe kwamba access ya SMEs to credit in large part bado ni tatizo. Based on the figure ya 2003 telling us kwamba it was only 6% of the firms in Tanzania that relied on domestic banks as source of capital/investment, ingawa hatuna figure za leo, I doubt kama things have gotten better. Na tusisahau kwmba domestic credit provided by the banking sector was juu sana in early to mid 1990s but still Tanzanians walitumbukia into extreme poverty kuliko kipindi kingine chochote katika historia ya nchi yao.
Sasa kama banking sector in Tanzania inachangia kiasi kidogo hivyo to firms' credit, then what are their other sources?
An obvious answer is fedha za nje, unless kama mtu ana taarifa ya uwepo wa unofficial source of capital. Otherwise data on fedha za nje (official) zipo, so les try make sense of them: Below ni takwimu on private inflows toka nje ambazo zinakuja kama investment capital kwenye uchumi wetu Tanzania. It is obvious kwamba majority of foreign capital inflows zinaenda katika uwekezaji kwenye miradi aidha foreign owned by 100%, au yenye ubia na government au yenye ubia na wazawa (wenye bahati hiyo). Ni chenji ndogo sana ambazo zinaenda kwenye Dar stock market as portfolio investments kwani DSE is still at a very infant stage. Mfano, Portifolio inflows (DSE) in 2009 was only about USD 3 million.
Now figures below za private capital flows ni pamoja na zile wenzetu ‘wazawa' wenye bahati ya kuwa na heka zao kadhaa na kufanikiwa kumpata mwekezaji toka nje aje alime nae mazao, au mzawa mwenye kiwanja chenye thamani kwahivyo mwekezaji anakuja kujenga hoteli, apartments etc.
Jedwali: Private capital inflows into Tanzania (2001 – 2009)
| Year | Capital Inflows (%) | GDP Growth (%) |
| 2009 | 1.9 | 6.7 |
| 2008 | 1.9 | 7.4 |
| 2007 | 3.5 | 7.1 |
| 2006 | 2.8 | 6.7 |
| 2005 | 6.6 | 7.3 |
| 2004 | 3.4 | 7.8 |
| 2003 | 3.7 | 6.9 |
| 2002 | 3.8 | 7.1 |
| 2001 | 3.7 | 6.0 |
| 2000 | 4.5 | 5 |
Source: World Bank
Tunagundua haraka kwamba by 2009, we were at the lowest point in terms of foreign capital inflows i.e at 1.9% katika kipindi cha miaka kumi (2000 – 2009) na pia tunagundua kumbe ule uchumi ulioanza kukua kwa kasi ya ajabu ulitokana na mitaji toka nje, sio za ndani which is understandable.
Cha kuangalia kwa ukaribu hapa ni: Kwanini hapo awali tuliona domestic credit provided by the banking sector (ambayo ofcoz ndio source kubwa kwa SMEs) ilikuwa inazidi kuteremka huku GDP ikipaa na foreign capital entry nayo ikipaa? Hii inaonyesha kwamba huu sio uchumi wetu, ni uchumi wa ‘wenyewe';
Tumalizie kwa kuangalia, je hizi capital inflows from nje zilienda ku stimulate what economic activities na hizi activities zina real value ya namna gani kwa the 70% of Tanzanians. Tunachojaribu ni kuangalia ule uchumi ulioanza kupaa from the year 2000 ambao uliambatana na kushuka kwa domestic credit from banks to firms in Tanzania sambamba na an increase in foreign capital flows kwenda kuwekezwa kwenye various sector, nani ametajirika na nani amezidi kuwa maskini, na kwanini maskini kawa maskini na tajiri kawa tajiri?
Jedwali: Sectoral contribution to real GDP by economic activities (%)
| 2002 | 2003 | 2004 | 2005 | 2006 | 2007 | 2008 | 2009 | 2010 |
| Agriculture | 28.6 | 28.7 | 29.5 | 27.6 | 26.2 | 25.7% | 24.6% | 25.5% | 26.5 |
| Mining | 2.1 | 2.4 | 2.6 | 2.9 | 3.2 | 3.5 | 3.3 | 3.5 | 3.7 |
| Manufacturing | 8.3 | 8.3 | 8.1 | 7.9 | 7.8 | 7.8 | 8.3 | 9.4 | 10.2 |
| Electricity | 2 | 1.9 | 1.8 | 1.7 | 1.5 | 1.6 | 1.7 | 1.8 | 2.0 |
| Water Supply | 0.5 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.4 | 0.5 |
| Construction | 6.8 | 8 | 7.9 | 7.8 | 7.8 | 7.8 | 7.9 | 8.6 | 9.4 |
| Trade and Repair | 12.4 | 12 | 11.4 | 11 | 11.4 | 11.5 | 11.8 | 12.7 | 13.8 |
| Hotel and Restaurants | 2.6 | 2.4 | 2.3 | 2.5 | 2.6 | 2.7 | 2.3 | 2.4 | 2.3 |
| Transport | 5 | 4.8 | 4.6 | 4.4 | 4.3 | 4.2 | 5 | 5.3 | 5.7 |
| Communication | 1.2 | 1.3 | 1.5 | 1.7 | 1.7 | 2.3 | 2.1 | 2.6 | 3.2 |
| Financial Services | 1.7 | 1.7 | 1.6 | 1.7 | 1.7 | 1.6 | 1.7 | 1.8 | 2.0 |
| Real estate | 9.7 | 9.4 | 9.1 | 8 | 9.6 | 9.5 | 9 | 9.7 | 10.3 |
| Public administration | 7.2 | 7.2 | 7.7 | 7.7 | 8 | 8 | 8.1 | 8.7 | 9.3 |
Source: Delloitte
- Tunaona kwamba GDP inachangiwa sana na activities za kilimo.
Maswali:
- Je, how much investment goes to Kilimo?
- Je, mchango wa kilimo unatokana na quality of investment or quantity of peasants (70% of the labour force)?
- Jibu ni kwamba takwimu hizi strongly suggest kwamba kilimo hakipati much credit flows na ingawa huko ndio majority of labour force ipo. Huo ndio uchumi uchwara wa Mkullo. The real quality ya contribution of sekta ya kilimo can be seen from value added figures below.
Jedwali: Agriculture Value Added
| Year | Annual Growth | (% of GDP) | Value added per worker in dollars |
| 2009 | 3.2 | 28 | $283 |
| 2008 | 4.5 | 29 | $281 |
| 2007 | 4 | 29 | $275 |
| 2006 | 3.8 | 30 | $270 |
| 2005 | 4 | 31 | $266 |
| 2004 | 5.9 | 33 | $261 |
Source: World Bank
Note: Value added per worker in 1990 was $219, so only a change of $83 in 20 years.
- Nadhani tayari tunapata picha halisi ya uchumi uchwara wa Mkullo in the context of "KILIMO KWANZA" kwani hapo juu we see kwamba value added kwenye sekta ya kilimo is actually declining.
Je tukirudi kwenye Jedwali letu la awali on:
Sectoral Contribution to real GDP by economic activities (hapo juu):Je, ni sekta gani nje ya kilimo zina intense economic activities? Je zina linkages zipi na majority of Tanzanians (70%) vijijini? Tumeshaona kilimo kina mchango ingawa wakulima hawapati mikopo yoyote ya maana; je watanzania wengi (out of the 70%) wapo katika sekta nyingine zipi ili tujue wanafaidika vipi? kwani kwa kwaida, the more economically active the sector, the more attractive it becomes to the banking sector, thereby faidisha wazawa. I have figures ‘valued added' figures za manufacturing sector (chemicals, food beverages, textiles and clothing, machinery and transport equipments), kwa kweli ni za kusikitisha, san asana kutokana na matatizo ya umeme lakini pia low productivity ya the manufacturing sector in general, sasa sijui tatizo ni access to credit? Small domestic market? Inferior technology to compete with foreign goods nje as well as imported goods? Lack of innovation? Poor sectoral policies, atleast from the implementation perspective? I don't know, but all I know is Uchumi wa Mkullo na Ndullu ni Uchwara.