DAR si LAMU
JF-Expert Member
- Mar 31, 2007
- 2,928
- 551
...Mchambuzi, naomba urudie kusoma ulichokiandika, kama vile kaandika mtu mwingine. Utagundua kuwa, majibu yako kwenye hizo para mbili. Soma -between the lines- ya ulichokiandika.Ulikuwa na bado upo sahihi; cha kushangaza ni kwamba Ndullu ni mmoja wa wachumi wa hali ya juu kabisa kimataifa na ameandika mambo mazuri mengi sana miaka ya nyuma covering uchumi chini ya Nyerere hadi Mkapa lakini hatuoni akiyatekeleza kwa vitendo; Lipumba ambae ni mwenzake as World Class Economists toka IV League nae anasema mengi sana sasahivi on the root cause of the problem and how we can get out of it; Kinachoonekana ni kwamba walimu ni wazuri kwa maneno yao, sio matendo yao. Kuhusu washauri wa Rais katika masuala ya uchumi, ni dhahiri amezungukwa na wataalamu wengi sana, tatizo labda wanamwogopa na wanajitahidi kumweleza yale tu ambayo wanadhani atapenda kuyasikia wakati ukweli ni kwamba JK ni msikilizaji mzuri. Kama mnavyokumbuka enzi za iddi amin - true story - alitembelea siku moja Central Bank of Uganda ghafla after uchumi kuanza kuporomoka na kukutana na gavana, wakiwa kwenye corridor akauliza "Mr Gavana, tatizo ni nini"? Gavana akajibu, 'it is inflation your excellency', Amin akasimama na kuhamaki na kumwangalia usoni , "the problem is inflation?????, who is this inflation individual?" Gavana kuona hali ngumu na kwamba ni tatizo kumkosoa Rais, akamwonyeshea afisa mmoja aliekuwa karibu yao na kusema 'that's him sir'; iddi Amin akatoa amri - "Give him V.I.P treatment right away' meaning auliwe, walinzi wakatekeleza hayo.
...Asante kwa majibu.