Mkumbuke mwalimu wako.

Mwalimu Philipo Mulugo kwa sasa anafundisha Zimbabwe Ireland, alinifundisha formular ya kuchochea kuni mbichi na zikaivisha .
Judgement hufai kabisa wewe!yani sijui ilikuwaje sikona hii post yako toka jumapili!yani nimechekaaaje!mpka watu wananishangaa hapa!
 
Last edited by a moderator:
Kulikuwa na mkali wa Hesabu Mwl Sendama enzi za primary , kwenye test zake za Hesabu ukipata 49/50 bora kesho yake usiende shule manake kipigo utakachokipata balaa anakwambia ni uzembe kukosa swali moja bora upate 0/50 anakusamehe..
Ila nashukuru alinijengea misingi mizuri sana ya Hesabu...
 
Mwalimu Ng'abi...sijui mzima?Mwadui A miaka hyo makaburu hawajapewa mgodi...Mwalimu Tanturu,muha fulani wa Kg...Mr and Mrs Toto pamoja na Mrs.Chubwa....hapo una mfuko umeweka vitumbua na tambi za Mama Spensi..kuenda kuiba miwa na mapera kwa Abrahaman...!dah enzi hzo za Mwadui kwelikweli!shulen mnaenda na Basi!wapi KK wa MWASECO?Dah
 
pole sana, duh mwl sheba na maisori nawakumbuka sana. ila umemsahau mwalimu rugumba chekechea duh nakumbuka uji ulikuwa unapikiwa kwa mwl mkuu maduka!

Wewe mtoto wewe!! halafu hujamsema Mwalimu hivi alikuwa anatoka Morogoro lakini alirudi kwao baada ya kushindwa vurugu za Wakurya.
Halafu hata Maisori alikuwa anauza mandazi na barafu. Ujanja kuruka madirisha na kwenda kwenye mashamba ya mapera na miwa kuiba.

Mwalimu mkora Kiganja na fimbo zake aisee.......hivi uliimba kwaya? Manake nakumbuka alikuwa ............
 
madame SIRILO.....MR.CHARLES MAZINGE(R.I.P),MR.CHARLES MANALA....MADAME NYANDA(R.I.P),MADAME WILKISTER.....WOTE HAWA KUTOKA SHULE YA MSINGI MWABASABI-LAMADI,MAGU-MWANZA!....
 
mwanza buzuruga pr xkul.,kitu Super mwl karuta. mwanza one kwa hisabati enzi zilee za miaka ya ticn vile...daaah ilikuwa balaaa kweli aisee
 

Hahahahaaa.. snochet umenikumbusha mbaali sana Lobilo alikuwa kiboko na wanafunzi walikuwa wakimwita hivyo anajibu Lobilo Baba yako...infwact sijui siku hizi yuko wapi na maana ya jina hilo ninini??

 
Last edited by a moderator:
Wapo wengi, leo nitaanza na Ignas Kiolanyorha...Anatoka Legho Kirua Vunjo na alifundisha chekechea ya kanisa pale Iwa...alikuwa mwalimu kweli kweli na hadi leo nakumbuka alivyokuwa akifundisha kwa moyo...
 
platozoom me niliimba kwaya tena sauti ya pili. namkumbuka sana mwl kiganja. unamzungumzia mwl makinda? nayakumbuka maandazi na barafu za mwl maisori. vp unakumbuka vibalagara vya mwl sheba?
mwl sapa pia unamkumbuka na mwl zakaria kwny somo la kilimo?
 
Last edited by a moderator:

Vibaragala aisee nimecheka sana dah! una kumbukumbu kali sana!! hilo neno nina miaka zaidi ya 15 sijalisikia!
Ni kweli nilikuwa namzungumzia mwalimu Makinda, hata sijui yuko wapi. Barafu pia nimekumbuka siku hizi watoto wanaita "ice cream". Nakumbuka alikuwa akinunua mmoja mnapanga msururu kupata japo kipande.

Mwalimu Sapa (nafikiri jina la utani baada ya kushindwa kutamka saba)......................Mwalimu Zakaria nafikiri atakuwa amezeeka sasa kwa sababu kama miaka ya mwanzo ya '90 alikuwa mtu mzima sasa je?

Namkumbuka Mwalimu "Madomo" alitufundisha jiografia na kwa kweli somo lake sikuwahi kupata chini ya 80% na alikuwa anaijua vizuri sana.

Kuna wakati na mimi niliimba sauti ya tatu kwa muda fulani, infact alikuwa anapenda pia wenye vichwa vizuri darasani kwa sababu hata kina somebody Amani pia waliimba!!!! Nakumbuka pia nunda Nyamanda aliimba pia. Bila kumsahau Eva as choir master!!
 
yeah, namkumbuka mwl madomo. unamkumbuka mwl flan hivi alikuwa anakaa starehe tulimtungia jina kinjekitile ngwale alikuwa anakimbia kweli tena alikuwa mwl wa riadha. vp mwl onyango mzee wa kwiliii. . . . platozoom
 
Last edited by a moderator:
yeah, namkumbuka mwl madomo. unamkumbuka mwl flan hivi alikuwa anakaa starehe tulimtungia jina kinjekitile ngwale alikuwa anakimbia kweli tena alikuwa mwl wa riadha. vp mwl onyango mzee wa kwiliii. . . . platozoom

Tena nilitaka nikuulize huyo Ngwale jina lake.......halafu nasikia alikuwa anapiga msuba si mchezo na akili zake kama zimepinda flani hivi........Na niliskia walishawahi kuzichapa na Kiganja.Mwalimu Onyango kanifundisha English pia.

Yupo pia Mwalimu Misana alikuwa na mtoto wake anaitwa Eda unamkumbuka?
 

duh,ngwale hata jina lake cmkumbuki ni kwel alikuwa anapiga ms. misana si alikuwa mwl mkuu msaidizi enzi za maduka. afu wakazusha et misana na maduka walikuwa wpnz lol!
 
duh,ngwale hata jina lake cmkumbuki ni kwel alikuwa anapiga ms. misana si alikuwa mwl mkuu msaidizi enzi za maduka. afu wakazusha et misana na maduka walikuwa wpnz lol!

Na walioleta huo umbea ni ninyi hapo!
Ila kiukweli Maduka alikuwa wembe wa Topaz lakini si kwa wanafunzi wake........Tembelea Chuo cha ualimu weeeee
 
nimemkumbuka Mwalimu Ndabila-Tambaza
Hahahahaaa.. snochet umenikumbusha mbaali sana Lobilo alikuwa kiboko na wanafunzi walikuwa wakimwita hivyo anajibu Lobilo Baba yako...infwact sijui siku hizi yuko wapi na maana ya jina hilo ninini??

 
Mwalimu MJ shule ya msingi Mabatini-Tandika magorofani, kwa hesabu jamaa alikuwa balaa! alinisaidia sana kupenda na kufaulu hesabu. alinipenda sana maana nilikuwa ni mmoja wa wasichana wachache walokuwa wanafaulu somo lake! saa 12;30 asubuhi test ya hesabu, baada ya hapo mchakamchaka! weee bwana wee na lile joto la dar sasa.... na Mwalimu Senzigye-korogwe girls high schoo! mama alikuwa mkali yuleeeeee! akikuita unaanza kujikojolea, alikuwaga na swaga zake anasema SHIIIIIIIIIII MWANANGU HUNA ADABU.
 
Mwalimu MJ shule ya msingi Mabatini-Tandika magorofani, kwa hesabu jamaa alikuwa balaa! alinisaidia sana kupenda na kufaulu hesabu. alinipenda sana maana nilikuwa ni mmoja wa wasichana wachache walokuwa wanafaulu somo lake! saa 12;30 asubuhi test ya hesabu, baada ya hapo mchakamchaka! weee bwana wee na lile joto la dar sasa.... na Mwalimu Senzigye-korogwe girls high schoo! mama alikuwa mkali yuleeeeee! akikuita unaanza kujikojolea, alikuwaga na swaga zake anasema SHIIIIIIIIIII MWANANGU HUNA ADABU. Hapo ujuwe kimenukaaaaa...
 
Mwalimu Gembe pale Mzumbe sec,mkali wa Physics miss you sana!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…