Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mkuranga, Juma Abeid, anasema kuna jumla ya wakazi zaidi ya laki mbili kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2012, ina kata 25, vijiji 125 na vitongoji 475, zao lao kuu la biashara ni korosho.
Pia, anataja mazao mengine wilayani ni pamoja na nanasi, mihogo, korosho na maembe.
Abeid anasema, korosho inayolimwa na jumla ya wakulima 15,496 mpaka sasa. Idadi ya kilo zilizokusanywa za korosho katika msimu uliopita zaidi ya kilo milioni tisa.
Pia, anasema matarajio katika kilimo hicho cha korosho ambacho kazi ya maandalizi inaendelea, ni kuvuka zaidi makusanyo yaliyopita, kwa kuwa na jumla ya kilo milioni 10 za korosho na halmashauri imejipanga kuhakikisha lengo linafikiwa vizuri.
Anatoa angalizo kwa wote watakaothubutu kwenda kinyume na malengo, hatua kali zitachukuliwa na anafafanua: "Tumejipanga kuhakikisha kila mkulima ananufaika na alichovuna, lakini mtu yoyote akijaribu kuharibu mfumo huu, hatua kali za kisheria dhidi yake zitachukuliwa."
Aidha, kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Philiberto Sanga, amewataka viongozi wa Vyama vya Msingi (AMCOC) kuzingatia mwongozo wa utekelezaji wa Mfumo wa Stakabadhi Ghalani, ili kuepuka sintofahamu kwa wakulima wa korosho, kama ilivyokea katika msimu uliopita.
Akifungua mafunzo kwa vyama hivyo, aliwataka washiriki kuwa makini na mafunzo hayo na akawataka kuyafanyia kazi, hatimaye uwe mwarobaini wa kumaliza changamoto mbalimbali kwa wakulima.
Sanga, aliyewakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Mshamu Munde, alitumia fursa hiyo kuwaonya viongozi hao kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atayekwamisha malipo ya korosho kwa wakulima katika msimu wa sasa.
Ni agizo alilolielekeza pia kwa walanguzi wa korosho wa kupitia ‘Kangomba’ anawatangazia kwa kauli “watafute kazi nyingine ya kufanya’ ili kuepuka mkono sheria katika enedo hilo la ununuzi wa korosho.
Mkuu wa Wilaya anaviambia vyama vya ushirika, ambavyo kimsingi ni wateja wa mazao yao kutoka shambani, kwamba wakulima wao wananufaika na zao hilo waweze kuinua kipato chao.
" Vyama vya ushirika vinatakiwa kuhakikisha wakulima wananufaika Kwa kuinuka kiuchumi kutokana na wao kuwatambua wakulima," anasema.
Anaongeza kwamba, wakulima wanatumia muda mwingi katika kuzihudumia korosho mpaka hatua ya uvunaji na atakayehujumu mfumo huo, ajiandae kuchukuliwa hatua za kisheria.
Pia, Munde anawataka wakulima kutokuwa tayari kurubuniwa na wajanja wachache, cha msingi kwao ni kuwa wepesi na weledi kufuata taratibu zilizowekwa kwa ajili ya kunufaika na zao hili.
“Nitashangaa kuona pale mlipohangaika kutunza mashamba na hatimaye mkafanikiwa kuvuna korosho, lakini mwisho wa siku mkazipeleka kwa walanguzi,” anasema.
Chanzo: Nipashe