Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filbeto Sanga, amewataka walimu kutowatoza michango ya aina yoyote wanafunzi ambao wanaoanza shule.
Sanga aliyasema hayo jana katika kikao maalumu cha Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, kilichoitishwa kubadilisha matumizi ya fedha ili ziende kutumika katika ujenzi wa vyumba vya madarasa kwenye shule 10.
Ujenzi wa madarasa hayo utawawezesha wanafunzi 3,627 ambao mwaka huu walichaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza, lakini wakabakizwa kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa, kuanza masomo.