Mkurugenzi aliyefariki kwenye ajali Mbeya alionywa asiendelee na safari akadai ana haraka

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema Askari waliokuwepo eneo la Inyala Mbeya waliwashauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga Fatma Omary na Dereva wake kutoondoa gari leo eneo hilo kusubiria Malori yapite ili magari madogo yaruhusiwe kama utaratibu unavyotaka lakini wawili hao walisema wana haraka hivyo wakaondoa gari hilo.

"Baada ya magari makubwa kuruhusiwa kupita magari madogo pia yaliruhusiwa ambapo Mkurugenzi alipofika mbele alihitaji kununua mahitaji hivyo akashuka na aliporudi kwenye gari akakuta muda wa kupita magari madogo umeshapita ikawa ni zamu ya magari makubwa, walipoingia katikati gari lilifeli breki likagonga gari la DED na mengine na kusababisha kifo cha DED, Dereva na Mtu mwingine mmoja"

"Wakati ameshuka Askari walimzuia wakamwambia ni muda wa malori lakini wakasema wanawahi, tunatoa wito mnapoambiwa msipite msubiri msipite mpaka Malori yamalizike, pale ni lazima tupite kwa kupishana kwasababu malori asilimia kubwa yanafeli breki ndio maana tunawasubirisha wanapita kwa awamu, natoa wito Askari wakikuzuia usijiingize kwenye changamoto, chanzo ni gari aina ya lori kufeli breki na kugonga magari mawili, gari la Mkurugenzi na jingine la Watu wengine"

Amesema RC Homera

IMG_1198.jpg

Amesema RC HomeraView attachment 2357256
Kweli haraka haraka haina baraka. Yamekuwa yaliyomkuta, kilichobaki ni kumwombea kwa Mungu amlaze mahali pema peponi. Ameen.

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema Askari waliokuwepo eneo la Inyala Mbeya waliwashauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga Fatma Omary na Dereva wake kutoondoa gari leo eneo hilo kusubiria Malori yapite ili magari madogo yaruhusiwe kama utaratibu unavyotaka lakini wawili hao walisema wana haraka hivyo wakaondoa gari hilo.
RIP ndugu zetu
Wahenga walisema "...better late in this world than early in the next"
 
Hapo atakua aliwaambia polisi kasemeni popote, hamjui Mimi Ni mkurugenzi?
Angekua raia wa kawaida akakaidi amri halali ya polisi angechukuliwa hatua. Lakini wakubwa hawaogopi polisi, njiani hawaogopi tochi za spidi Kali, wasichojua breki za malori hazijui kwamba baadhi yetu tuna vyeo vikubwa.
 
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Zuberi Homera amesema Askari waliokuwepo eneo la Inyala Mbeya waliwashauri Mkurugenzi wa Halmashauri ya Igunga Fatma Omary na Dereva wake kutoondoa gari leo eneo hilo kusubiria Malori yapite ili magari madogo yaruhusiwe kama utaratibu unavyotaka lakini wawili hao walisema wana haraka hivyo wakaondoa gari hilo.

"Baada ya magari makubwa kuruhusiwa kupita magari madogo pia yaliruhusiwa ambapo Mkurugenzi alipofika mbele alihitaji kununua mahitaji hivyo akashuka na aliporudi kwenye gari akakuta muda wa kupita magari madogo umeshapita ikawa ni zamu ya magari makubwa, walipoingia katikati gari lilifeli breki likagonga gari la DED na mengine na kusababisha kifo cha DED, Dereva na Mtu mwingine mmoja"

"Wakati ameshuka Askari walimzuia wakamwambia ni muda wa malori lakini wakasema wanawahi, tunatoa wito mnapoambiwa msipite msubiri msipite mpaka Malori yamalizike, pale ni lazima tupite kwa kupishana kwasababu malori asilimia kubwa yanafeli breki ndio maana tunawasubirisha wanapita kwa awamu, natoa wito Askari wakikuzuia usijiingize kwenye changamoto, chanzo ni gari aina ya lori kufeli breki na kugonga magari mawili, gari la Mkurugenzi na jingine la Watu wengine"

Amesema RC HomeraView attachment 2357256
Malori yana hitilafu za breki, mbele ya macho ya polisi! Hamna rushwa hapo?
 
Kuna vifo vingine vinatengenezwa mpaka uje kugundua baadae saaana...

R.I.P Marehemu wote
 
Madereva wa serikali wanajiona wako juu ya sheria
Hasa akiwa kambeba boss wake,anajiona yuko juu ya Sheria,na ukute boss na dereva wote vichwa Maji hakuna hata wakumkumbusha mwenzie Sheria za usalama barabarani,basi ndiyo kama hivyo wote wanaangamia kwa kukosa busara ndogo tu ya utii wa Sheria bila shuruti!!
 
Hapo dere unamuonea tu, ishu ni bosi wake
Mi bado namlaumu dereva kwa uzembe wa kuamrishwa kuendesha gari kwenye Mazingira hatari,ambayo Jeshi la Police limesha kuonya lakini bado ukakaidi kisa boss kasema!!
 
Ile Inyala pass inahitaji ufumbuzi wa kisayansi,kile kipande kiboreshwe na pia ni lazima kuwe na STOP ya LAZIMA kwa all heavy-duty vehicles na lazima tujenge ARRESTER pale, Zambia wanazo hasa ile pass inayoelekea kwenye border yake na Zimbabwe
 
Hapo atakua aliwaambia polisi kasemeni popote, hamjui Mimi Ni mkurugenzi?
Angekua raia wa kawaida akakaidi amri halali ya polisi angechukuliwa hatua. Lakini wakubwa hawaogopi polisi, njiani hawaogopi tochi za spidi Kali, wasichojua breki za malori hazijui kwamba baadhi yetu tuna vyeo vikubwa.

Sheria haziwahusu walamba asali. Si barabarani tu, bali hata kodi na tozo.
 
Back
Top Bottom