Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,872
- 34,363
KWA UFUPI
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Dk Ndumbaro alitaja sababu za
Tazara kuporomoka kuwa ni pamoja na Serikali ya Zambia na Tanzania kutegeana katika uwekezaji
wa mtaji ndani ya mamlaka hiyo.
Dar es Salaam. Kaimu Mkurugenzi aliyemaliza muda wake wa kufanya kazi katika Mamlaka ya Reli Tanzania na Zambia(Tazara), Dk Damas Ndumaro ametoboa siri zinazofanya mamlaka hiyo kukabiliwa na changamoto nyingi hata kuporomoka.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi Jumapili, Dk Ndumbaro alitaja sababu za Tazara kuporomoka kuwa ni pamoja na Serikali ya Zambia na Tanzania kutegeana katika uwekezaji wa mtaji ndani ya mamlaka hiyo.
Katika miaka ya hivi karibuni Tazara imekuwa ikisuasua katika utoaji wa huduma zake, huku ikikumbwa na migogoro mbalimbali ikiwamo migomo ya wafanyakazi na wafanyakazi kukosa mishahara kwa unaostahili.
"Tazara inaonekana kuwa ni cha wote, kila mmoja ana mwangalia mwenzake afanye nini, hiyo ni changamoto kubwa sana. Lakini pia Serikali za Tanzania na Zambia hazijaamua kutoa kipaumbele. Mfano; hapa Tanzania bajeti inayotengwa ni kidogo sana ukilinganisha na barabara," alisema Dk Ndumbaro.
Alisema kuwa sababu hizo zimeifanya Tazara kushindwa kuongeza uzalishaji kutokana na idadi ndogo ya vichwa vya treni, miundombinu chakavu na mazingira magumu ya kufanyia kazi.
Dk Ndumbaro alisema kuwa usafiri wa treni una mchango mkubwa zaidi katika kuchochea ukuaji uchumi wa taifa ukilinganisha na miundombinu ya barabara.
"Serikali hizi zikiamua kuwekeza kikamilifu itakuwa faida kubwa, "alisema Dk Ndumbaro.
Aliongeza kuwa endapo Serikali zitawekeza itasaidia kupunguza gharama za usafirishaji na kuongeza mzunguko wa shughuli za kiuchumi. Utendaji wa mamlaka hiyo umeshuka tangu bajeti ya mwaka 1986/87 ambapo Tazara ilikuwa ikisafirisha tani za mizigo 1.2milioni na abiria wasiopungua 1 milioni, lakini hadi kufikia mwaka wa fedha wa 2011/12 utendaji umeshuka kufikia tani za mizigo 340,000 na abiria wasiozidi 900,000.
Kuhusu sakata la mafao ya wastaafu, Dk Ndumbaro aliweka wazi kuwa linatokana na udhaifu uliofanywa na menejimenti iliyomaliza muda wake miaka ya 1990.
"Mwaka 1992/93 mamlaka iliweka rekodi ya kuzalisha mizigo, menejimenti ikaongeza mishahara kwa wafanyakazi wote kwa asilimia 100, mwaka uliofuata uzalishaji ukashuka sana," alisema Dk Ndumbaro akiongeza hapo Tazara ikaanza kuzidiwa mzigo mishahara hadi kipindi hiki.Mkurugenzi atoboa matatizo ya Tazara - Biashara - mwananchi.co.tz