JoJiPoJi
JF-Expert Member
- Aug 8, 2009
- 2,935
- 3,346
NA FARAJA MASINDE
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Bandari nchini (TPA), Mhandisi Deodatus Kakoko, amedai kuwa kampuni ya PMM Estates (2001) Ltd, inashiriki katika vitendo visivyofaa vya kuficha makontena.
Mhandisi Kakoko alitoa hayo wiki iliyopita katika mahojiano maalum na RAI, ambapo alisema kampuni hiyo imeendesha vitendo visivyo vya kiaminifu kwa wateja na bandari kwa muda mrefu.
Alisema hatua hiyo imechangia kuwakimbiza baadhi ya wateja, jambo ambalo limemlazimu kupambana na kampuni hiyo ikiwa ni pamoja na kutaka kuifutia kibali.
Kampuni hiyo ina miliki bandari kavu iliyopo eneo la Vingunguti, jijini Dar es Salaam. Katika mazungumzo yake hayo Mhandisi Kakoko alisema, PMM anatajwa kuwa ICD asiye na uaminifu kwa wateja na bandari.
“Wizi mkubwa ulikuwa kwenye ICD, kuna huyu mtu anaitwa PMM, huyu hata ukimwandika na huyu nataka kumfukia na ICD yake ‘completely’, kwa sababu nina ushahidi wa kutosha ameiba vitenge mpaka Kongo na bado anachukua Kontena ili aendelee kuibia watu.
“ Ushahidi wa madai haya ninao na si yeye tu, wako wengi na tayari nimeshazuia baadhi ya ICD’s,”alisema.
Mhandisi Kakoko alisema katika kuhakikisha wizi huo haujitokezi tena, amehakikisha anaimarisha ulinzi kwa kuweka maofisa usalama wa Taifa, polisi na Wanajeshi ambao watavaa kiraia kwani haihitaji kuona hata sindano ikitoka.
“Kwasa tumefanikiwa kudhibiti kabisa mianya hii kwani tumeimarisha usalama ikiwamo kutumia maofisa wa usalama wa Taifa na pia tunafikiria kuwatumia wanajeshi lengo likiwa ni kudhibiti upoteaji na udokozi holela wa mizigo na vitu vya wateja.
“Tunataka kurejesha imani ya wateja wetu ambao wamepungua kwa wastani na kwamba mbali na PMM pia kumekuwa na wafanyabiashara wanaomiliki bandari kavu (ICDs) ambao wamekuwa wakipitisha makontena kwa magendo jambo lililosababisha bandari ya Dar es Salaam kuzuia baadhi ya ICDs hizo kupata makontena.
“Kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaomiliki ICDs ambao wamekuwa siyo waaminifu kutokana na kuiingizia serikali hasara na hivyo kusababisha baadhi ya wafanyabiashara wa nje kushindwa kutumia bandari yetu.
Katika hatua nyingine Kakoko, aliweka wazi kuwa kumekuwapo na baadhi ya watendaji wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini kwenye eneo la kodi ambao wamekuwa wakihusika kuwafukuza wafanyabiashara wanaotumia Bandari ya Dar es Salaam.
“Ili kuhakikisha kuwa Bandari yetu inaimarika nimefanikiwa kukutana na wafanyabiashara wakubwa wa Kongo wasiopungua 100 ambao wamenihakikishia kurejea kwenye bandari yetu ya, Dar es Salaam iwapo tu ataondolewa Ofisa aliyeko kwenye Idara ya Kodi ya Kongo hapa nchini anayefahamika kwa jina la, Peter Mrisho, ambaye amekuwa akituhumiwa kuwatoza wafanyabiashara hao kiasi cha dola 1,000 mpaka 3,000 kwa kila ‘Kontena’ kama hongo ya kupitisha mizigo yao kirahisi.
“Hivyo wamehaidi kuwa watarejea mara tu baada ya kuondolewa kwa Ofisa huyo, kuna akinamama ambao nilikutana nao, Bukavu, Kongo ambao awali walikuwa wakishusha kontena zisizopungua 50 kila mwezi kwenye Bandari ya Dar es Salaam lakini wameamua kuhamishia kwenye bandari ya Mombasa kutokana na kusumbuliwa na, Mrisho kwa hiyo amesema kuwa akiondolewa tu huyo amenihakikishia kuwa atarejea,” alisema Mhandishi Kakoko.
RAI liliutafuta uongozi wa kampuni hiyo ili kutolea ufafanuzi madai hayo ya Mhandinsi Kakoko, hata hivyo haukuwa tayari kutoa ushirikiano baada ya Katibu Muhtasi kudai kuwa uongozi hauna muda wa kuzungumza kutokana na kutingwa na majukumu ya ofisi.
Katika hatua nyingine, Mhandisi Kakoko alisema katika kipindi chote cha ufisadi uliochangia kuwakimbiza wafanyabiashara wengi, bandari ilipoteza mizigo tani laki nane kwa katika kipindi cha miezi tisa, ambapo awali kiwango cha mizigo kilikuwa ni kufikia tani milioni 14.8, hata hivyo ilishuka na kuwa milioni 14 pekee.
Alisema ni lazima Watanzania wakubali kuwa na uzalendo kwa ajili ya nchi yao ili waweze kutambua kuwa kilicho cha kwao ni bora zaidi.
“Hapa nazungumzia pia mawakala wa Forodha na ICDs ni lazima watambue kuwa muda wa kufanya biashara ya faida ya kuiba umepita , hivyo ni bora tukafuata taratibu kwa kujitolea kufanya kazi kwa kutambua kuwa tunafanya kwa masilahi ya taifa.
“Pia wafanyakazi wa umma ni vyema wakajitolea zaidi kuliko kuendelea kuidai serikali ili tuweze kutengeneza ziada kwaajili ya maendeleo ya serikali, hata upande wetu TPA matumizi yake yalikuwa ni bilioni 450 kwa mwaka, sasa nataka tusizidi bilioni 300 ili tuweze kutunza zaidi ya bilioni 100.
“Ni lazima tupunguze posho na marupurupu ambayo yataturudisha nyuma, kama TPA tunajitahidi kuhakikisha kuwa tunarejesha wafanyabiashara wote waliokuwa wamekimbia bandari yetu,” alisema.
Alisema nchi kama Rwanda, Uganda, Kongo na nyingine zimehaidi kurejea kutumia bandari hiyo ambapo pia TPA imetangaza kuondoa vikwazo kwa wafanyabiashara hao kutoka siku 15 za kutoa mzigo mpaka 30.
Chanzo: RAI- October 20, 2016