informer 06
Member
- May 11, 2024
- 66
- 49
Mkurugenzi wa Boston Consulting Group,Edward Lupasa ambao wanajihusisha na ushauri wa masuala ya kibiashara hususani kodi na kufanya uchechemuzi kwa vijana na Wanawake katika nyanja ya maendeleo, amesema kwamba suala la elimu ya fedha linatakiwa kupewa kipaumbele katika kuwasaidia wanufaika wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Serikali.
Pichani: Mkurugenzi wa Boston Consulting Group,Edward Lupasa akizungumza na wadau masuala mbalimbali ya kibiashara
Amesema kwamba pesa ina kanuni muhimu ambazo bila kuzizingatia ni ngumu kufanikiwa kwenye suala husika ambalo limekusudiwa.
Akizungumza na wadau mbalimbali ambao walifika kwenye Ofisi za Boston Posta Jijini Dar es Salaam, amesema kwamba Wanawake na Vijana ni kati ya makundi ambayo yamelengwa na Serikali kwenye mkopo wa asilimia 10, lakini anadai kwamba fursa hiyo inapowakuta wanufaika hawana elimu ya fedha inaweza kuwa changamoto.
Ameshauri vijana, Wanawake ambao wananufaika na mikopo hiyo kujipatia elimu ya fedha ambayo itawasaidia kuelewa kanuni za msingi katika kunufaika na pesa hizo, amesema kwamba Boston Consulting Group imekuwa ikifanya jitihada za kukuza elimu hiyo ikiwemo kwenye masuala ya kikodi.
"Tumekuwa tukisaidia kutoa elimu kwa Vijana na Wanawake ambao wananufaika na mkopo wa asilimia kumi kwenye Halmashauri, lakini jambo unagundua kuwa watu wengi tunakwama kwa kuchukua fedha bila kuwa na kanuni za fedha, ukichukua fedha bila kuzingatia kanuni zake muhimu unapotea mapema"amesema Edward Lupasa
Ametoa wito kwa Vijana na makundi mengine kuwasiliana na Boston Consulting Group ili kunufaika na elimu ambayo wamekuwa wakitoa hususani kupitia kurasa zao za Mitandao ya kijamii, ambapo amesema kwamba hivi karibuni wanatarajia kuendelea kutoa maudhui kupitia chaneli yao ya YouTube ili kuwawezesha wananchi kuongeza uelewa kwenye mamabo mbalimbali.
Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara mbalimbali nchini kwamba wanaweza kuepuka changamoto za kikodi, ambapo amesema Boston wanaweza kuwasaidia kushughulikia masuala yote kwa gharama nafuu bila wao kuanza kuangaika.
"Sisi (Boston Consulting Group) tupo kwa ajili kuwasaidia wafanyabiashara kuondokana na usumbufu wa masuala ya kikodi, mfanyabiashira tunaweza kuingia makubaliano tukawa tunamsaidia kwenye masuala yote kikodi akaondokana na zile changamoto mfano malimbikizo, lakini wengi wanaweza kuwa na hofu kwamba gharama ni kubwa, niwaambie kuwa gharama zetu ni nafuu sana"amesema Edward lupasa
Ameongeza " Kwa Dar es Salaam ofisi zetu zipo Salamander Tower gorofa ya nane mfanyabiashira wa aina yeyote tunamkaribisha, lakini pia tumekuwa na utaratibu wa kuwatembelea wafanyabiashara wetu ambao tayari tumeingia makubaliano au ambao tumewapa ushauri kwenye masuala ya biashara"