KATIKA hali isiyo ya kawaida, Mkurugenzi wa uchaguzi Moshi vijijini na Vujo Bw. Castory Msigala aliingia katika mgogoro na wanachama wa Chadema chanzo kikiwa ni fomu ya wagombea wa Chadema.
Mgogoro huo umesababisha mkurugenzi huyo kuondolewa katika nafasi hiyo ya kusimamia uchaguzi Moshi na hivyo mkurugenzi wa Moshi mjini amepokea fomu za CHADEMA.
CHADEMA imempongeza mkurugenzi wa uchaguzi Tume ya Taifa kwa kusikiliza kilio chao na kuwezesha fomu zao kupokelewa.