Mkurugenzi Catherine Mashala alitumbuliwa kwa kesi ya Ufisadi wa Tsh. Bilioni 1.245,989,000?

Mkurugenzi Catherine Mashala alitumbuliwa kwa kesi ya Ufisadi wa Tsh. Bilioni 1.245,989,000?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Screen Shot 2024-04-05 at 08.33.38.png


xxx.jpeg


Mkurugenzi wa Katavi aliyetumbuliwa jana na Mh. Samia Suluhu bibi Catherine Mashalla haikutolewa sababu, lakini kumbe ana kesi ya uhujumu uchumi na alikuwa sero mpaka wiki iliyopita ndio amepata dhamana kwenye hii kesi niliyoambatanisha. Kiasi halisi alichotuhumiwa kupiga ni (TZS-1,232,408,689.0] Bilioni na ushee bibie Cathy unapeleka wapi?

Yeye ndio huyo mshitaki wa Kwanza. Vyombo vyetu vya habari havia habari za kichunguzi, hakuna hata kimoja na ndio maana kila uchao namuomba sana kaka Pascal Mayalla arudi kwenye habari, atuletee za kichunguzi. Naamini, mtu kama Mayala[Njaa] angeweza kutuambia sababu ya Pauli kushushwa Cheo, Sababu ya Jokate kushushwa cheo of which mtaani zimebaki sababu za kuhisia kwamba akina mama walilalamika hawawezi kuongozwa na mtu asiye na ndoa, asiyejua unyenyekevu kwa mume, mtu ambaye picha zake mtandaoni hata uki google hazifai hata kama ametubu nk.

Kwenye Picha Catherine ameva nguo ya Draft Draft, sijataja chama chake, ila nafikiri hana chama!


25 August 2023, 10:25 am

KATAVI

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU mkoa wa Katavi imewafikisha mahakamani watumishi wa serikali 7 kwa makosa matatu ikiwemo wizi wa fedha zaidi ya bilioni 1.2.

Kelvin Mwaja ni mwanasheria kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru mkoa wa Katavi amesema kuwa watuhumiwa walitenda makosa hayo mwaka 2022 na 2023.

Wakisomewa mashtaka yao Mara baada ya kufikishwa mahakamani, hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumayi ambapo ni Canuthe Hipolite Matsindiko (muhasibu) ,Michael Mathew Katanga (muhasibu), Masami Andrew Mashauri (muhasibu), tumaini Richard Misese Maira Samson Oluomba muhasibu, Emmanuel Damas Salanga (muhasibu) na Laurent William Sunga.

Watuhumiwa wote wanakabiliwa na mashtaka ya kuunda genge la kiarifu,wizi wa fedha Zaidi ya bilioni 1.2 na utakatishaji wa fedha za serikali katika halmashauri ya Mpimbwe wilaya ya Mlele mkoani Katavi.

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Katavi Gway Sumayi amesema kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kutoa dhamana au kusikiliza kesi hiyo hivyo imepelekwa katika mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Kesi hiyo imesikilizwa tarehe 21 mwezi huu ambapo inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 04 mwezi 9 mwaka huu katika mahakama kuu ya kanda ya Sumbawanga mkoani Rukwa na wala rushwa hao wamepewa dhamana.
 

Attachments

Kesi nyingi za ufisadi zipo mahakamani. Tatizo Sasa hivi kuna waandishi wa hovyo hazisikiki na Wala hawana habari wao kazi Yao ni kuandika habari za Zuchu na Diamonds,alafu hao hao waandishi ndio wanalalama kuwa serikali haichukui hatua
 
Itakuwa umekosea kuandika hiyo hela, bilioni 1, 245,989,000 hata ukikusanya zote za hazina hazifiki.

Labda ulipaswa kusema Tshs: bilioni moja, milioni 245, laki 9 na 89 elfu).
ewaa, ni bilioni moja na milioni 200. Hawa ndio wanasababisha vijana wapambanaji wanakata tamaa, mtu unafanya kazi miaka na miaka huwezi kununua kiwanja alafu unambiwa mbona fulani kafanya kazi mwaka mmoja ytu kajengea wazazi wake nyumba, ana gari , ameoa!
 
Ila na nyie wenzetu sijui mnajiaminije
Maana mkipiga mnapiga haswa kama ni hela za mradi mnazichukua zote
Huo sio wizi sasa ila mnapeana madili tu ya kupiga
Halafu wanawekwa pembeni wanachaguliwa wapya wa kipiga tena

Hivi kwanini huwa wanaapishwa kwa vitabu vya dini wakati hawana dini na hofu ya Mungu?

Tunaomba badala ya kuapishwa wawe wanaambiwa Ukiiba miaka 40 jela badala ya kuapishwa kinafiki
 
ewaa, ni bilioni moja na milioni 200. Hawa ndio wanasababisha vijana wapambanaji wanakata tamaa, mtu unafanya kazi miaka na miaka huwezi kununua kiwanja alafu unambiwa mbona fulani kafanya kazi mwaka mmoja ytu kajengea wazazi wake nyumba, ana gari , ameoa!
Mwisho wa siku kijana ambaye hajafanywa ufisadi anaonekana boya tu.

Wizi unapogiwa promo sana na jamii kwasabb ya ufisadi wa baadhi ya watu.
 
ccm ni genge la wezi. Kila sehemu watu wanapiga tu. Baadaye wanajifanya kufikishana mahakamani, halafu mwisho wa siku kesi inafutwa! Huku hela za walipa kodi nazo zikiwa zimeliwa.
Ndiyo maana mimi mtu akiniletea habari za kulipa kodi huwa namuangaliaa kisha natikisa kichwa naondoka.

Bado zile wanazolipana wakiingia kwenye vikao vyao wenyewe wamezipa jina la posho,wizi mtupu!
 
Kesi nyini za ufisadi zipo mahakamani. Tatizo Sasa hivi kuna waandishi wa hovyo hazisikiki na Wala hawana habari wao kazi Yao ni kuandika habari za Zuchu na Diamonds,alafu hao hao waandishi ndio wanalalama kuwa serikali haichukui hatua
Mbona Watz tunakuwa wasahaulifu?? Waandishi wa habari waliokuwa wakifichua uozo wa Watendaji mbali mbali wa Serikali Walsingham kwenye misukosuko na hata wengine kupotezwa hadi leo mf Anzori Gwanda. Ni nani asiyependa kuishi??
 
Back
Top Bottom