Mkurugenzi Catherine Mashala alitumbuliwa kwa kesi ya Ufisadi wa Tsh. Bilioni 1.245,989,000?

DEDs wanawekwa pale kupiga hela na kuwapa waliowapigia debe kwa bi mkubwa. Toka aondolewe yule mwamba wa CCM tutarajie kusikia DEDs wengi wakiwa mahakamani
 
Mbona kuna wengine walioripotiwa wanasubiri kujadiliwa na bunge? Why?
Kamateni watoe maelezo haraka. Mnapo waacha wanaweza kushawishi wabunge wawili wenye ushawishi wakavuruga mjadala.
 
ccm ni genge la wezi. Kila sehemu watu wanapiga tu. Baadaye wanajifanya kufikishana mahakamani, halafu mwisho wa siku kesi inafutwa! Huku hela za walipa kodi nazo zikiwa zimeliwa.
Wizi wa timu Mara umerudi tena.Polisi wahangaike na hao waliopo wenye majina ya Mara hao.Kuna kipindi wizi ukitokea ofisi yeyote ya umma polisi walikuwa wanauliza hata kabla kuanza uchunguzi kuwa kuna watu wa Mara eneo la ofisi hiyo wizi ulipotokea au kitengo ulipotokea? Wakisema wapo wanaanzia kwao hao hao na walikuwa hawakosei wanawadala walikuwa wachongaji.michongo hasa ya kuibia serikali na Taasisi naona wameanza tena

Humo kwenye mashtaka naona kuna majina ya Mara kwenye hao washtakiwa wajikite hapo polisi
Kama huyo Mama kaiba atakuwa kasomeshwa na hao timu ya Mara.Walitulia muda naona wameibuka tena.
 
Andika jumla ya pesa vizuri. Ondoa neno bilioni au andika kwa maneno tu bila tarakimu.
 
Itakuwa umekosea kuandika hiyo hela, bilioni 1, 245,989,000 hata ukikusanya zote za hazina hazifiki.

Labda ulipaswa kusema Tshs: bilioni moja, milioni 245, laki 9 na 89 elfu).
Hata taifa tajiri la Marekani halina pesa kama hiyo! Hisabati ni mtihani mgumu kwa wengi ambao hawawezi kuandika kwa tarakimu au kwa maneno.
 
Reactions: G4N
Hela ya kujenga Dispensary, nyumba za madaktari na wauguzi mtu Katia mfukoni.
Asante Mama kwa kuteua na kutengua.
Wezi kama hao ingebidi watembezwe kwenye majiji makubwa kwa magari ya wazi walipakodi wawaone.
 
Ni kweli huwa hawafungwi.

Huyo mama baada ya upigaji alihamishiwa Sumbawanga, alipishana na mtangulizi wake aliyetumbuliwa kwa upigaji vile vile.... ila cha ajabu Mtalitinya anadunda tena kapangiwa kazi nyingine.
Yupo wapi Mtalitinya? Mjanja-mjanja sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…