Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Mazingira Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph, amefafanua kuwa uvujaji na kupasuka kwa mabomba ya maji yanayotokea kabla ya mita ya mteja ni hasara inayobebwa kikamilifu na mamlaka hiyo na wala si mwananchi.
Akizungumza leo Oktoba 2, 2026 kwenye mahojiano na Clouds Media, Mhandisi Aron ameeleza kuwa wateja wanapaswa kulipia tu kiasi cha maji kinachopita na kusomwa na mita zao, huku akisisitiza kuwa mfumo wowote wa mabomba unaoharibika baada ya mita unakuwa chini ya uwajibikaji wa mwananchi mwenyewe.
Mhandisi Aron ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa za haraka mara wanapoona uvujaji wowote wa maji mtaani ili kuisaidia mamlaka hiyo kudhibiti upotevu wa maji. Pia, amewasihi wakazi wa Dodoma kutumia vifaa vya plumbing vilivyo na viwango bora pamoja na kukagua mifumo yao ya ndani ili kuepuka bili kubwa zinazotokana na uvujaji usioonekana chini ya udongo au kwenye vyoo.
Aidha, aliongeza kuwa kutokana na maji ya Dodoma kuwa na chumvi, matenki ya vyoo vya ku-flush yamekuwa na tabia ya kukwama (stack), na hivyo kusababisha maji kumwagika siku nzima bila mteja kutambua. Amewashauri wananchi kuwa makini na kuchezesha vifungo vya vyoo hivyo mara baada ya kutumia ili kuhakikisha mpira umeziba na kuzuia upotevu huo wa maji.