Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mkoa wa Mbeya, imeweka msisitizo kwa Hospitali za Serikali wilayani humo, kuhudumia wagonjwa kabla ya malipo ili kuokoa maisha na kupunguza malalamiko.
Hatua hiyo imetajwa ni kutekeleza maagizo ya Serikali katika kusimamia sera ya afya kwa vitendo kwa lengo la kuwezesha Watanzania kunufaika kwa kuboreshwa upatikanaji wa huduma za matibabu kwa wakati pasipo vikwazo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali Mkoa wa Mbeya, Raymond Mweli ameliambia chombo cha habari Mwananchi leo Jumatano Januari 21, 2026, wakati akizungumzia mikakati ya kuboresha upatikanaji wa huduma muhimu kwa jamii.
"Hilo halina mjadala mikakati yetu kama halmashauri ni kuona wananchi wanapofika kupata matibabu wahudumiwe kwanza ndipo taratibu za malipo zifuate lengo ni kuondoa malalamiko na kuokoa maisha ya wagonjwa hususani wa dharura," amesema.
Mweli amesema suala hilo lazima lipewe kipaumbele cha hali ya juu ambalo viongozi wakuu wa nchi wametolea maelekezo mara kadhaa akiwepo Rais Samia Suluhu Hassan lengo kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya.