Mkuu pole sana, kwenye kada ya ualimu kuna unafiki makubwa sana ,usipokuwa makini unakuwa mtu wa majungu majungu hadi unastaafu huna hata bati moja.kwa mwalimu anayejitambua kamwe hawezi kulilia ukuu wa shule.
Nimekuwa kwenye hii kada kuwa miaka sasa lakini nilichojifunza, walimu sisi ni watu wanafiki sana,mwalimu yuko radhi kumsema vibaya mwalimu mwenzake kwa mkuu wa shule au maafsa wa elimu ili tu apate ofa ya kusimamia mitihani ya taifa na ikiwezekana ateuliwe awe mkuu wa shule au afsa elimu kata.
Usipojipendekeza kwa mkuu wa shule, kusimamia mitihani utakusikia tu,mfano mzuri ni hapa kituoni kwangu,mkuu wangu ni Mungu mtu,usipomuanza kumsalimia hana taimu na wewe atakupita kama hakuoni,mkiwa kwenye vikao kazi yake ni kutishia walimu eti atawapa barua ya onyo kwa wale wote wenye kwenda kinyume na yeye vile anaamini,huu ni upuuzi makubwa.
Nilichojifunza walimu hatuna kazi mbadala ndio maana kila siku tunajipendekeza kwa matumaini ya kupata ofa,
Pole sana walimu,ila kikubwa tujitahidi tuwe na vipato mbadala hii itasaidia kuondoa majungu na chuki zisizo tija.
Mimi huwa hainiingia akilini mwanamme mzima kuuza sura kwa mwanamme mwenzangu ili tu nipewe ofa, huu ni upuuzi walimu tushituke,tutumie mishahara yetu ili kujipatia vipato mbadala