Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, John Kayombo, ameibuka na majibu makali kufuatia madai yaliyotolewa na Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Kaskazini, Godbless Lema, kuhusu kasoro katika zoezi la uandikishaji wa wapiga kura kwenye daftari la mkazi linaloendelea nchini.
Akizungumza na Jambo TV, Kayombo amekanusha vikali madai ya Lema, akisisitiza kuwa zoezi la uandikishaji linaendelea vyema bila changamoto yoyote.
"Hakuna changamoto yeyote kwenye zoezi hili na ujue tuna vyama 19 vya siasa vilivyosajiliwa kamili, lakini ni chama kimoja tu kinacholalamika. Mjiulize shida iko kwa nani? Upande wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, hatuna shida kwenye zoezi hili. Tunakwenda vyema, na zoezi la uandikishaji litakwisha salama kabisa." Ameeleza.
Kuhusu madai ya baadhi ya mawakala kuzuiwa kuapishwa, Mkurugenzi huyo amesema hakuna jambo kama hilo, isipokuwa CHADEMA na viongozi wake wanapaswa kufahamu ni nani wa kuwaapisha na kwa wakati gani, kwa kurejea kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambazo zinaeleza kuwa kama chama kimekosa hakimu wa kuwaapisha mawakala wake basi Mkurugenzi ambaye ndiye msimamizi wa uchaguzi au wasaidizi wake watawaapisha badala ya hakimu.
Soma Pia:
“Hao CHADEMA sijawaona kwangu kwa lolote na mie siwezi kuwapigia simu kuwaita, ila hakuna shida yeyote ile kwenye uandikishaji hadi sasa”, amesema Kayombo na kuongeza kuwa hajawahi kumuona Lema ofisini kwake kuleta malalamiko yoyote.