Mkurugenzi Karatu: Dkt. Samia Suluhu Hassan ni chachu ya maendeleo kwa wanawake wa wilaya ya Karatu

Mkurugenzi Karatu: Dkt. Samia Suluhu Hassan ni chachu ya maendeleo kwa wanawake wa wilaya ya Karatu

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu mkoani Arusha, Juma Hokororo, amemtaja Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama chachu ya maendeleo kwa wanawake wa wilaya ya Karatu kutokana na uwezeshaji wake mkubwa wa kiuchumi na kijamii, kwa kufanikisha utoaji wa zaidi ya Shilingi bilioni moja za mkopo wa asilimia 10.

Hokororo mara baada ya kutembelea mabanda ya maonesho ya wanawake wajasiriamali kutoka Karatu, wanaoonesha na kuuza bidhaa zao mbalimbali, amesema Serikali ya awamu ya sita imewezesha takribani bilioni 1.2 za mikopo ambapo wanawake walipata milioni 440, vijana milioni 440 na wenye ulemavu shilingi milioni 200, suala ambalo limewezesha wanawake kujiajiri na kuwa na mchango katika uchumi wa familia na jamii nzima ya wilaya ya Karatu.

Hokororo ametumia fursa hiyo pia kutoa wito kwa wananchi wa Karatu kujitokeza kwa wingi kumlaki na kumsikiliza Rais Samia hapo siku ya Jumamosi, atakapokuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Wanawake kitaifa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha, kama sehemu ya ahsante kwa miradi mingi ya maendeleo iliyotekelezwa wilayani Karatu kwa kipindi cha miaka minne ya uongozi wake akiwa Rais wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom