KERO Mkurugenzi Korogwe DC tupia jicho shule ya msingi Makole iliyopo KIJIJI Cha MAKOLE kata ya Magamba Kwalukonge

KERO Mkurugenzi Korogwe DC tupia jicho shule ya msingi Makole iliyopo KIJIJI Cha MAKOLE kata ya Magamba Kwalukonge

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Jantisa

Member
Joined
Feb 13, 2023
Posts
59
Reaction score
51
Habari wakuu mimi ni mdau wa elimu kutoka mkoa wa Tanga nimekuwa nikifuatilia maendeleo ya elimu katika shule ya msingi Makole iliyopo katika halmashauri ya WILAYA Korogwe DC katika kata ya Magamba KWALUKONGE Kijiji Cha Makole.

Kwa kipindi kirefu shule hiyo imekuwa ikipoteza thamani yake ya zamani ambapo shule hii imekuwa na matokeo mabaya sana katika ngazi ya kitaifa Hali inayotishia mustakabali wa kesho ya vijana wetu

Mfano matokeo ya darasa la saba na la nne katika kipindi Cha miaka minne mfufulizo yamekuwa yakishuka

Katika kufuatilia nimegundua Kuna upungufu mkubwa wa walimu ambapo kwasasa shule hiyo Ina walimu watano ambao wanafundisha wanafunzi katika madarasa yote

Ombi kwa mkurugenzi na ofisi ya waziri mkuu Tamisemi kufuatilia na kutatua changamoto katika shule hiyo Ili kuchelea utekelezaji wa dira ya Taifa 2050 na kuchochea maendeleo ya Vijana wetu kwani ELIMU ndio ufunguo wa maisha
 
Back
Top Bottom