Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Kusoma hoja ya Mdau bofya hapa ~ Majengo ya Hospitali (Mkuranga) yametelekezwa huu Mwaka wa 10 sasa, Wananchi tunaseka kupata huduma mbali
UFAFANUZI WA MKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Khadija Nassir Ally anasema: Sikuwa najua kuna hiyo hospitali kama alivyosema, naamini kama ipo basi haijajengwa na Serikali kwa kuwa hiyo ripoti haipo mezani kwangu.
Jambo la msingi nitafuatilia kujua kama ipo na nini kinaendelea, ikiwa ni Mdau au Wadau wameamua kujenga na kuishia njiani kisha Wananchi wakahitaji msaada wa Serikali ni jambo jema na linaweza kusaidia Serikali na Wananchi kwa jumla kama itahitajika Serikali kuendeleza mradi huo ulipoishia.
Nitafika katika Kijiji hicho kufuatilia hilo suala, kwa kuwa kwa sasa kuna mradi unaoendelea Kijiji cha Hoyoyo kujenga Zahanani na ujenzi unaendelea vizuri.
UFAFANUZI WA MKURUGENZI (DED)
Mkurugenzi wa Mkuranga, Waziri Kombo amesema “Mradi huo sio wa Serikali, ulijengwa na Taasisi ya WAMA (Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Tanzania), hivyo wao ndio wana majibu ya kwa nini mradi haujafunguliwa hadi leo kwa zaidi ya miaka 10.
Ungekuwa ni wa Serikali tungekuwa tumeshatoa fedha kuendeleza kituo hicho ambacho kwanza ni Zahanati na sio Hospitali kama inavyoelezwa, pia tungepeleka Watumishi, isingewezekana tukitelekeze kituo bila maelezo yoyote.
Suala lingine lolote zaidi ya maelezo hayo niliyoyasema waulizwe WAMA ndio wana majibu sahihi.
WAMA
JamiiForums imefanya jitihada za kutafuta uongozi wa WAMA lakini hilo halijafanikiwa, jitihada bado zinaendelea.