Mkurugenzi mkuu LATRA Habibu Suluo hizi namba zenu 0800 11 0019 na 0800 11 0020 hazina msaada, toa namba zako mwenyewe

Mmm umechafukwa
 
Watanzania hatuna mtetezi.

Mtetezi wetu Alisha kufa pale chato. SASA hivi ni kilio kila Kona.

Anyway tutafika tuu
Wakati wenzetu wana chama.cha wamilikI wa mabasi Ila serikali inaona Sawa tuu kwasababu zao za kujilinda kisiasa kwa abiria kukosa chama.cha kuwatetea
 
Sijui hizi namba huwa za nini? Utashangaa jitu lina simu, ila limezima. Wale LATRA enzi zile wakiwa SUMATRA, walikuwa na zamu ya kushika simu baada ya mida ya kazi. Sijui utaratibu wa sasa umekaaje.
Mwaka jana mwanzoni nilikuwa naenda Mpanda mkoani Katavi na kampuni moja ya Bus. Kufika Sikonge, Tabora, saa 3 usiku tukazuiwa eti hakuna kuendelea na safari mpaka asubuhi. Traffic anayetuzuia tukitaka kujua sababu hana maelezo, eti ni maagizo toka juu. Abiria tukapeana zamu kupiga hizo namba, kumpigia RPC Tabora, RC Tabora nk hao jamaa kiukweli ni wasumbufu sana maana hawapokei simu na wakipokea hawana msaada. Inatakiwa hizi namba ziwe na mfumo wa ku record taarifa na kujua ni hatua gani zimechukuliwa. Nimeona Tanesco Morogoro, pamoja na changamoto zao, wana huu mfumo, yaani ukipiga simu kuelezea tatizo, muda mfupi baadaye unapata msg ya kumbukumbu. Then wataendelea kukupigia mpaka useme kero imefanyiwa kazi au laa. This is something good Kwa wengine kuiga.
 
[emoji1666][emoji1666][emoji1666][emoji122][emoji122][emoji122]
 
I agree with you... Kwa kumbukumbu zangu mifumo ilijifia rasmi awamu ya tano. Hii ni kwa sababu huko nyuma maafisa wa ngazi husika ndiyo walikuwa wanasukumwa kutoa huduma kwa jamii. Unakuta afisa afya wa kata, afisa maendeleo wa kata, afisa mifugo, afisa biashara, kilimo nk wako bize huko mitaani na mabosi wao wanawafuatilia. Baadae ikawa mara DC anakagua soko, mara RC anakagua ujenzi wa shule au barabara, mara waziri from Wizarani hukoo kaja kukagua mradi wa maji au kufuatia upungufu wa sukari. Hao viongozi wa juu imefikia sasa wao ndiyo kama watendaji wa day to day activities huko kwenye halmashauri na manispaa. Nimeona juzi clip mitandaoni huko Handeni wafanyabiashara hawamtaki afisa wa TRA wa eneo lao na amekuja DC kutatua. Sasa unajiuliza wapi afisa biashara na DED wa eneo hilo ambao ndiyo wataalamu zaidi ya DC? Hali hii imefanya watendaji huko chini, kwanza kupoteza kujiamini kwenye kazi zao lakini pili kuona kwamba wanaingiliwa na hivyo hawajitumi tena. Hatuwezi kuendesha nchi kubwa kama Tanzania kwa kutegemea watu wachache kutoka Dodoma au Dar au RC/DC... Lazima turudishe mifumo ambapo DED atamuagiza mkuu wa idara, naye mkuu wa idara ataishusha mpaka kwa msaidizi wake ngazi ya kata na vijiji.
 
Customer service Tanzania Ni rubbish.
Nenda wizara yoyote, Kama umekula kongoro unaweza kuwatapikia. Nenda kampuni za simu utajibiwa na mitambo Hadi uite maji nya. Sasa njoo DSTV.
CUSTOMER SERVICE YA DSTV NI NONSENSE.
Mkuu acha kuzarau kongoro,pale Wallet Pub, Kihonda Morogoro Kuna kongoro matata sana inauzwa na ndizi ya kuchemsha..
 
safi atasoma
 
Mkuu acha kuzarau kongoro,pale Wallet Pub, Kihonda Morogoro Kuna kongoro matata sana inauzwa na ndizi ya kuchemsha..
Kama unafuatilia michango yangu mingi utaona kongoro Ni sehemu ya maisha yangu Kama ilivyo supu ya utumbo, safari baridi, mbuzi choma, kunawa na nyimbo za OTTU.
 
Duuuh kumbe.. Sasa kapelekwa aliyewahi kuwa DG wa TTCL, yaani hii DART ni fupa la nyati mzee maana hata waje fisi hawaliwezi...
Kwa maneno mengine aliyefeli TTCL ndio anakuja kuiinua UDART?
Hii udart kwanini isipewe MTU aliye prove kwamba ana ujuzi kwenye usafirishaji? Mtu Kama Shabiby, Aboud, Rahaleo, Burdan etc???
Kihameo wamemuona hafai ndani ya exactly two months. Lini hii try and error itaisha? Barabara ya Mbagala imekamilika mwaka wa tatu huu hakuna Basi, Cha kushangaza wanajenga Basi ziende Hadi Pugu.
I am confused. What does the government want us to think?
 
Mimi naona umeandika kwa hisia tuu na sio hoja, mambo ya uzanzibari na ubara yanahusikaje?? Halafu pili hizo Namba ukipiga unapata msaada moja kwa moja, mfano Mimi nilikuwa nasafiri from Mbeya to Sumbawanga nauli ilkuwa juu, nlivyowapigia tulikuwa hatujaanza safari bado so ilimchukua Afisa wa LATRA kama DK 10 tuu kufika pale na nauli zetu zilirudishwa..

Pia Ni wajibu wetu kutoa taarifa kuliwa na matukio Maovu kuliko kulalamika, hizo Namba zinapatikana Hadi usiku wa manane
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…