TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

TANZIA Mkurugenzi Mkuu Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa, Apson Mwang’onda afariki Dunia nchini Afrika Kusini

Moja ya watu wenye akili kubwa sana na unapoongea naye inabidi uwe makini na unachoongea. Wengi mnasimuliwa historia yake ila kwa tuliokutana naye na kubadilishana mawazo mawili maratu Tunamfahamu uwezo wake wa kupambanua mambo. Hii ilikuwa moja ya dhahabu iliyosafishwa na Nyerere.
 
Na ' Obey ' ya enzi hizo ndiyo ilikuwa ' Obey ' hasa siyo hii sasa ambayo imejaza ' Wakuja ' tupu halafu wanajifanya Wajanja.
Kwa hiyo Mwang'ondas,Mihayos,Kimarios,Lubuvas sio wakuja?
 
Pale Bongoyo, cross streets ni Mkwawa na Winding Ave. Viwanja vya wazee vile.

Kwa Mzee Lubuva mbele kidogo.

Mzee Kimario mpaka amefariki alikuwa anaandika kitabu cha "War Stories" nilikuwa namsihi Mfaume kitabu kichapishwe watu wapate habari.

Umenikumbusha mbali sana kwenye kiduka kile.

Kuna siku nimekaa na kichaa wangu Alpha Opanga pale, ananiambia ana bonge la project la kuweka vyoo vya kulipia Dar. Nikasema Alpha acha stories zako, hakuna kitu kama hicho. Baadaye kidogo, nakuja kukuta Dar kuna vyoo vile vile alivyovisema Alpha!

The sad thing was Alpha had nothing to do with that.
Mkuu Kiranga,naomba ikikupendeza na ikiwezekana,andika kitabu kuhusu Oysterbay ya zamani. Mimi nipo kwenye mchakato wa kuandika kitabu kuhusu UDSM ya 1970s mpaka 1990s.
Pia kama hutumiki serikalini,basi Tanzania hatufaidiki na "vipaji" vyako.
Ubarikiwe.
 
Mbona umemsahau pia na Mzee mwingine aliyekuwa na Historia yake nzuri tu hapa Tanzania Kipindi cha Hayati Baba wa Taifa Mzee Kitundu ambaye alikuwa anakaa Mita chache tu kutoka Nyumba aliyokuwa akiishi Jaji Mstaafu Mzee Damian Lubuva?
Nilimkumbuka ila jina lilinitoka kidogo. Miaka imesogea sana.

Hawa wazee kama bado wapo miaka itakuwa inafikia jioni ya maisha yao sasa.
 
Naam kaaa sana kidukani pale ,jioni unaingia kwenye court ya Mzee kimario kudunda kikapu

Ile mitaa siku hz watu hkn kabisa wote wamehama
Nilirudi likizo, mimi ndiye nikaonekana mgeni viwanja vyangu.

Mzee Kimario alikuwa na basketball court, halafu ana bendi watu waliozibukia muziki wanapiga muziki.

Mzee poa sana.

The guy was an institution.
 
Kina nafsi itaonja mauti...huwa ni suala la muda tu.

Kinachotakiwa kwenye haya maisha mafupi ya duniani ni kutenda haki ili wakati wa kuhesabiwa usipitwe.

Nafsi yake ilipo kwa sasa wote hatujui kama ni peponi ama jehanam maana hiyo inategemeana na matendo yake yalikuwake wakati wa uhai wake.

Tumebaki mimi na wewe, tujitafakari matendo yetu...!!
 
Mav matupu, ndo nini hicho umeandika we kiazi mbatata na selule uliyekubuhu?

Kiongozi,
Hasira za nini Mkuu. Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa mstaafu tanzia yake ilitakiwa iwe na urefu wa angalau hata page / kurasa 3. Fursa ya mwanzisha uzi thread yake kuwa edited inatoa nafasi zoezi hilo kufanyika.

Historia / habari hizi za utumishi mrefu wa umma / ktk fani mbalimbali husaidia chombo kama JamiiForums kuwa mkataba / kisima / archive kubwa ya info kuliko zote.
 
Naona sahv anaishi pia nyuma ya laibon Street zamani us embassy..... Mtoto wake Sam yule anayemiliki agies record ni mwanangu kitambo Sana since udogoni

Ova

Hivi Sam ( Yule Jamaa Mrefu ) sana aliyekuwa ' Komandoo ' ila walimtoa huko baada ya ' Kuvunjika ' vibaya Miguu yake wakati akiruka kutoka katika Ndege Angani na akatua vibaya wakiwa Mazoezini, ila alitibiwa na sasa amepona japo akitembea ' anachechemea ' na ni ' Brazameni ' sana ni Mtoto wa Marehemu Mzee Apson au amemuolea Binti yake? Nitashukuru ukinipa ufafanuzi wa Kutosha juu ya hili Ndugu. Huyo Sam japo kwa sasa ana ' Ukilema ' kutokana na hiyo Ajali ya Kijeshi ( Kikomandoo ) aliyoipata, ila Jamaa anapiga ' Combat Kung Fu ' utadhani alizaliwa baada ya Hayati Jun Fan ( wengi wenu mnamjua kwa Jina lake maarufu la Bruce Lee ) Kuna Siku moja alitoa ' Demo ' fupi tu mitaa ya Mikocheni na ndani ya muda mchache hiyo sehemu ilitulia huku DJ akiacha Muziki wake na Wahudumu nao wakiacha Kutuhudumia halafu akina An Eagle tukitafuta ' Vichochoro ' vya kutokea barabara Kuu ili tudadindie ' DalaDala ' tuje Kupumzisha Akili na Presha. Ni Jamaa Mmoja mpole sana halafu Mstaarabu mno ila ' ukijichanganya ' tu Kwake ndipo utajua ni kwanini Wimbo wa Taifa huwa hauna ' Video ' yake tokea nchi hii ipate Uhuru wake hadi hivi leo.
 
Watu wanaijua obay tokea Enzi za John bichwa mzungu

Ova

Ni kweli Ndugu na nakumbuka huyo Mzungu Mgiriki John Bichwa Kipindi hicho alikuwa na Pikipiki moja Kubwa halafu Matata sana na alikuwa akipenda sana Kupita nayo ' Baru / Mbio ' katika Barabara za Oysterbay na Masaki huku Mimi nikiwa namfaidi zaidi kwakuwa ili aweze kwenda Kwake ilimlazimu awe anapita Chole Road kwenda Kwake kule juu jirani kabisa na zilipokuwa Ghorofa za ATC Kipindi hicho na pia siyo mbali na Nyumba anayoishi hadi sasa Mwanadiplomasia Mwandamizi, Balozi na aliyekuwa kuwa Katibu Mkuu wa OAU Mzee Salim Ahmed Salim..

Nakumbuka kuna Siku Kaka zangu ambao walikuwa ni ' Watundu ' mno na hata Shuleni Oysterbay Primary hadi Shabaan Robert Secondary walijulikana kwa hilo waliyoka nje ya Geti na walipoisikia tu Pikipiki ya John Bichwa inakuja wakatoka na Kuanza Kumchokoza na Kumdhihaki ndipo Jamaa akawapita kisha akaenda mbele kidogo na Kugeuka ' mazima mazima ' na Pikipiki yake ambapo aliwarudia kwa Kasi ya Ajabu ambapo kama isingekuwa uimara kwa Kaka zangu wa Kutoka ' Mbio / Baru ' na Kuzijua vyema ' Chochoro ' za Nyumbani basi Siku hiyo Jamaa angewaua kwani John Bichwa aliingiza Pikipiki hadi ndani ya Nyumba huku akiwasaka na alipowakosa alitoka na Spidi ile ile Kubwa Getini na Kutokomea zake na tokea Siku hiyo Kaka zangu hao walikoma na sikumbuki kama walirudia tena Kumdhihaki.

Hata hivyo nasikia kuwa Jamaa ( John Bichwa ) aliporudi tu Kwao hakukaa muda mrefu sana alifariki dunia. Alikuwa balaa!
 
Nilimkumbuka ila jina lilinitoka kidogo. Miaka imesogea sana.

Hawa wazee kama bado wapo miaka itakuwa inafikia jioni ya maisha yao sasa.

Mzee Kitundu alishafariki Kitambo sana Ndugu nadhani pamoja na Mama yao ( naomba Radhi mno kama atakuwa bado yupo hai ) ila sasa hivi Watoto wake wanaishi Mbezi Beach ambapo Marehemu Baba yao alinunua eneo Kubwa sana. Ukitaka kuwapata Kirahisi Watoto wake fika tu pale Mbezi Beach Tangi Bovu kisha pandisha na ile barabara ya kwenda Goba mbele kuna Baa Moja hivi maarufu iitwayo ' Kona Baa ' ukiwaulizia tu hapo utawapata Mmoja Mmoja kwani kuna Mmoja wao Yeye Maisha yake tayari ameshayabidhisha kama siyo kuyarathimisha rasmi na Unywaji wa Pombe Kupindukia na ukimkosa hapo njoo uninyonge An Eagle Mimi.
 
Magu amekua akihudhuria kusaini mahudhurio yadaftari LA wagonjwa ,nabahati zuri hawaponi ,yeye anajifunza nn
 
Magu amekua akihudhuria kusaini mahudhurio yadaftari LA wagonjwa ,nabahati zuri hawaponi ,yeye anajifunza nn

Sidhani kama ulichokiandika hapa kina ' Mantiki ' sana sana umendika tu kwa Chuki yako iliyokubuhu Kwake Rais JPM, Serikali yake hii ya Awamu ya Tano na hata Chama chake cha Mapinduzi kwani haitakiwi ' Akili ' kubwa kuweza Kung'amua / Kujua kama Wewe ni Mpinzani ambaye umeshashibishwa ' Propaganda ' za Roho Mbaya dhidi ya Mheshimiwa Rais.

Kama ni Marais kutembelea Wagonjwa na hata Kusaini Vitabu vya Mahudhurio hakuanza Yeye Rais JPM ila imekuwa ni desturi ya Marais karibia wote wa nchi hii na pia ni takwa la ' Kiitifaki ' kwa Wao ( Marais ) kufanya hivyo hasa ukizingatia kuwa Wote hao ( Wagonjwa ) walikuwa ni Viongozi ' Waandamizi ' wa Taifa hili la Tanzania na Serikali zinawatambua vile vile.

Rais Dkt. Magufuli kama Binadamu ana Mapungufu yake kama vile ambavyo Mimi na Wewe tunayo ila tujitahidi Kupunguza Chuki zetu Kwake zinatokana na Maisha yetu Magumu tuliyonayo hasa baada ya Yeye Kutuzibia ' Ulaji ' Wetu ambao haukuwa wa ' Kihalali ' na badala yake leo hii Maisha yanatupiga hivi na badala sasa ya Sisi kukaa chini tujiulize wapi tulikosea, tujirekebishe na tupambane na Maisha yetu kwa Kufanya Kazi / Kuwajibika muda wetu mwingi tunaumaliza katika Kumpiga ' Majungu ' Baba wa Watu wakati ukweli ni kwamba wala hausiki na Vyuma vyetu Kubana hivi bali tulijengewa Maisha ya Kuponda Raha, Kupata Pesa Kiuwepesi ( Kimagumashi ) na Kudekezwa hovyo na leo cha Moto tunakiona.

Tubadilike kwani bado hatujachelewa na tumwache Rais JPM atujengee Tanzania yetu ili baadae Vizazi vije Kumkumbuka.
 
Back
Top Bottom